JINSI YA KUENDELEA KATIKA NJIA YA WOKOVU.

 Françoise HABONAYO 

 

 

 

 

 

 

JINSI YA 

KUENDELEA KATIKA NJIA 

YA KRISTO 

………………… 

 

YALIYOMO

 

JINSI NILIVYOMPOKEA BWANA               ……………………………………….. III 

MUHTASARI            ……………………………………………………………………..  

UTANGULIZI            ……………………………………………………………………..   VIII 

 

SURA I: 

KUWA NA UHAKIKA NA NJIA YA KWELI:             ………………………      

          Mariam ni nani?                  ……………………………………………………         

          Ubatizo wa maji mengi        ………………………………………….        

          Ubatizo wa Roho Mtakatifu  ………………………………………….         12 

          Matunda ya Muongofu au matunda ya maisha mapya     ….      16 

 

SURA II: 

UBATIZO KATIKA ROHO MTAKATIFU                  ……………………………….         23 

          Karama za Roho Mtakatifu            …………………………………………          25 

          Tunda la Roho                             …………………………………………………. 30 

 

SURA III: 

UKARABATI WA ROHO                 ………………………………………………….. 32 

          Utulivu ndani ya Imani         ………………………………………….         35 

          Lugha                     …………………………………………………………….. 39 

          Kuwa na kiasi                    ……………………………………………………          44 

          Siri ndani ya mambo ya uchumi      ………………………………..        50 

 

SURA IV: 

MATATIZO YANAYOMKUTA MSAFIRI NJIANI       ……………………….       

          Bidii              ……………………………………………………………………….. 64 

          Thamani ya ushindi   …………………………………………………….         76 

 

SURA V: 

WEWE NI NANI?                ………………………………………………………………          83 

          Maombi                  …………………………………………………………….. 93 

 

SURA VI: 

WATU WA FAMILIA YANGU                    …………………………………………..        101 

          Umoja wa ndugu      …………………………………………………….         105 

          Tuondoe mipaka      …………………………………………………….         106 

 

SURA VII: 

MAHUSIANO YAHUSUYO MWENENDO WA KIKRISTO      ………………     110 

 

SURA VIII: 

SHUHUDA      ………………………………………………………………………….         119      

Ushuhuda wa kwanza                   …………………………………………….      119 

          Ushuhuda wa pili      ………………………………………………………       127 

          Ushuhuda wa tatu     ………………………………………………………       129 

          Ushuhuda wa nne; Mungu alivyoniita nimtumilkie            …….    129 

          Mtumishi mzuri wa Mungu    ……………………………………………       13 

HITIMISHO          ………………………………………………………………139  

 

JINSI NILIVYOMPOKEA BWANA

 

Nilimpokea Bwana Yesu kama mwokozi na Bwana wangu nikiwa na umri wa miaka 7 nilikuwa darasa la kwanza ambapo nilijiona kuwa mwenye dhambi. Nilikuwa na kiu ya kutakaswa na kuoshwa kwa damu ya Yesu.siku moja nikiwa katika ndoto, mtu mmoja aliniuliza; je unataka kujisafisha? Nikajibu, “ndiyo” akanichovya ndani ya ziwa ili nipate kuoshwa.Nilioga  ila Roho yangu hakuridhika kwani maji hayo ya ziwa hayakupenya mpaka rohoni ili kuniosha. Kuanzia hapo ndipo niligundua kuwa moyo wangu unahitaji kuoshwa na kuatakaswa kikamilifu, nikajiuliza swali hili, “Ni nani awezaye kunipa maji yanayoweza kuosha moyo wangu? Wapi naweza kupata maji yanayoweza kuosha mtu wa ndani (nafsi) kwa kuwa nilikuwa bado mdogosikuweza kuelewa maana ya ndoto hiyo Nilikasirika sana kwani sikuweza kupata maji ya kuniosha roho yangu .Ndugu msomaji, unaweza kufikiria kuwa mtoto wa miaka 7 hana dhambi? Mimi mwenyewe niligundua kuwa nilikuwa nahitajika kuoshwa moyoni mwangu. 

 

Wafudisheni watoto wenu maneno ya Mungu, kwani nao pia wanahitaji neno. Nilikiwa na dhambi za kitoto kama vile kudanganya, kuiba pesa kiasi cha F 5 au F 10 kwa kununulia pipi n.k. katika hayo yote pamoja na umri wangu kuwa mdogo nilihitaji wokovu wa Mungu. Usiseme kuwa huna dhambi bali sema kuwa ulisafishwa na maji yanayogusa mioyo. Maji hayo si kitu kingine chochote bali ni damu ya Yesu Kristo. 

 

Siku moja nilijikuta nasoma kitabu kiitwacho “woba warumvise…”maana yake ni (je,umeisha sikia…) Ndani ya kurasa za hicho kijitabu kidogo, nilikutana na hayo maji yaliyosafisha roho yangu: Mungu apewe sifa. Ndani ya kitabu hicho mwandishi anadhihirisha kuwa kati ya mwanadamu mwenye dhambi na Mungu Mtakatifu, kuna ufa mkubwa, lakini ili mwenye dhambi amfikie Mungu ni lazima apitie kwenye damu ya Yesu Kristo. Mwandishi wa kitabu hicho aliniongoza sala ya toba na nikampokea Yesu kuwa Bwana na mwolkozi wangu binafsi, sifa kwa Mungu. Tangu siku hiyo nilianza kwenda Kanisani. 

 

Siku nyingine katika ndoto, niliona mtu mmoja aliyefanana na mwalimu wangu wa shuleni akituomba  kuchora mtu na kuonyesha sehemu za miili yetu. Kichwa, mikono, miguu n.k. cha kushangaza ni kwamba, kabla sijaandika kichwa niligundua kuwa kitu kimeandikwa juu ya ile picha yangu na nikasoma “Quelle grace d’un petit enfant !” maana yake ni “NEEMA ILIYOJE JUU YA MTOTO MDOGO !” kwa kuwa sikujua badolugha ya kifaransa Mungu aliweka mhuri juu ya neno  hilo  likakaa moyoni. Baada ya muda,tulifundishwa lugha ya kifaransa ,ndipo nilielewa maana ya ujumbe huo wa Mungu.Namshukuru sana Bwana kwa neema yake kuu juu yangu. 

 

  Mama yangu mzazi aliniambia kwamba  baada ya kuzaliwa kwangu nilianza kuugua kiasi cha  kufa ,watu hospitalini walimukimbia akabaki peke yake huku akililia mototo wake.Watu walipeleka habali ya msiba nyumbani .wakati huo watu wakaandaa kaburi na wengine wakapeleka habari ya kifo changu kwa ndugu na jamaa wa mbali(mambo ya simu yalikuwa bado hayajafika kwetu)wakati mama yangu anatoka hospitalini na mtoto akielekea nyumbani ili wamzike mtoto,waliona naanza kutikisa kichwa na kufumbuwa macho yangu,  ndipo mama alianza kupiga kelele za furaha akisema; BwanaMungu huyu mtoto siyo wa kwangu bali ni wako! Mungu asifiwe. Wazazi wangu ambao wakati huo walikuwa wapagani walinikabidhi kwa Mungu. Bado naikumbuka  neema ya Mungu juu yangu!. 

 

 

 

 

 

  

 

UTANGULIZI

 

Ndugu msomaji, namshukuru sana Mungu kwa kunichagua kuwa mtumishi wake. Sio kwamba nina ujuzi wa hali ya juu wa neno la Mungu, ila naamini katika yeye Yesu anitiaye nguvu: Yesu alisema (Yohana 14:12) “Kweli nawaambieni, anayeniamini atafanya mambo ninayofanya mimi, naam, atafanya hata makuu zaidi, kwani ninakwenda kwa Baba”.

 

Katika kitabu hiki, utakutana na neno la Mungu litakalokusaidia kusonga mbele katika njia ya wokovu uliyoamua kuifuata. Bado tupo duniani ambapo shetani anazunguka na kubuni kila aina ya vishawishi ili tuiache njia na kumgeukia. Ila tunamshukuru Roho wa Mungu aliyefunua neno la kututia nguvu katika (Zaburi 119:105) “Neno lako ni taa ya kuniongoza, na mwanga katika njia yangu” Na kwa msaada wa Mungu tutamaliza mwendo. 

 

Pia  utapata kudhihirisha kwamba Yesu habadiriki kama alivyomgeuza mtume Paulo, anaweza kukubadilisha pia. Hata kama unajiona kuwa mbali na Mungu kama mwana mpotevu, basi sura mbalimbali za kitabu hiki zitakusogeza karibu na msaada wa Mungu. Fungua moyo wako ili Roho Mtakatifu akuongoze na kukufanya kuwa mwanamume, mwanamke au mtoto aliyekomaa kiimani. 

 

Mungu awabariki. 

 

Françoise HABONAYO. 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

MUHTASARI

 

Kitabu hiki ni matokeo ya kazi iliyofanywa na mama Françoise HABONAYO: ni Pentekoste aliyeokoka. Kitabu hiki kina lengo la kuwasaidia wakristo wapya kuendelea  na wokovu. Ndani yake kuna kutiwa moyo na shuhuda zitakazokufanya uendelee na wokovu.

 

Mungu asante kwa kumfungulia mama Françoise uzito wa pumziko ndani ya wokovu. Biblia inasema katika Yohana 15:4 Kaeni ndani yangu, nami ndani yenu kama vile tawi haliwezi peke yake kuzaa matunda lisipobaki katika mzabibu, halikadhalika nanyi hamuwezi kuzaa matunda msipokaa ndani yangu. Tumeitwa ili tuwe na matunda mazuri na ya kudumu, haiwezekani kuwa na matunda mazuri kama hatujazama ndani ya Bwana.

 

Tunajua kabisa kuwa matunda yanafaida sana kwa taifa.siku moja Yesu na wanafunzi wake walikuwa na njaa, na wakauona mtini ambao haukuwa na matunda na Yesu akaulaani kwani haukuwa na matunda, na kesho yake mtini ulikauka. Msidanganyike, matunda uliyonayo yanadhihirisha vile ulivyo. Yeyote anayejiita Mkristo ila hana wokovu ndani yake siyo wa Mungu, ndio maana ni muhimu kukaa ndani ya Bwana. Biblia inasema: “Mtu yeyote asipokaa ndani yangu hutupwa nje kama tawi litupwalo nje hata likakauka”. Yohana 15:6

 

Mungu alimfunulia mama Françoise kuandika kitabu kinachoitwa “Jinsi ya kuendelea katika njia ya wokovu”. Ilikuwa usiku wa tarehe 29/1/1996 alianza kuandika tarehe 30/1/1996 lakini miezi 10 baadaye alianza kukata tamaa ya kushindwa kuandika kitabu hiki. Baada ya miaka miwili, Mungu alijifunua kwake kwa mara ya pili na kumuhimiza kufanya haraka kazi hii.

 

Ni tarehe 22/7/1999 ndipo alipopata nguvu akaamua aenderee kuandika.  Ni Mungu anayetujalia akheri, bidii, nguvu na uwezo. Leo hii mmepata kitabu hiki sio ili kufahamiana kupitia ujumbe wa wazee wa maandishi, hapana, bali kukusaidia ushike wokovu usiuache,kwani ukienderea na wokovu wa Yesu utakuwa na amani,furaha ,utulivu na mengine mazuri.Bali ukiuacha,ni kama vile kutumbukia katika sehemu ya majonzi ya kila siku.Mungu atusaidie atujaze furaha yake.Amin.

 

 

 

 

 

 

 

SURA  

 

JIHAKIKISHIE NJIA SAHIHI 

 

Yesu anasema “Mimi ni njia, kweli na uzima. Mtu haji kwa baba ila kwa njia ya mimi (Yohana 14:6). Tunapoanza safari inabidi tuulizie kuhusu njia ya kufuata, kwani ikitokea tumekosea njia, siyo rahisi kufika. Watu wengi wanaamini kufika mbinguni ila wanakataa kutubu dhambi zao. Sasa tutaanzaje safari ya masafa? 

 

Inakubidi kumuamini Yesu katika maisha yako. Kabla ya kwenda kwa daktari, inabidi uwe na uhakika kuwa unaumwa, na inabidi umueleze jinsi unavyohisi maumivu mwilini mwako, na akupe dawa muhimu kwa ajili ya ugonjwa ulionao. Na ndivyo ilivyo pia katika swala la kuokoka (wokovu), inabidi kwanza ujitambue kuwa wewe ni mwenye dhambi, na kwamba unahitaji kufunguliwa (ukombozi) kutoka dhambi zako, alafu kumuomba Yesu aje ndani yako na kufukuza kila asichokitaka, na kuomba adumu maishani mwako. 

 

Kuingia kwa Yesu maishani mwako kunabadili utu wako. Kunaleta amani ya roho, utulivu, raha na furaha ndani ya moyo wako. Daima jinsi ya kuanza safari ni tofauti na jinsi ya kumariza safari kwa hiyo inabidi usonge mbele katika njia mpaka mwisho. Usisimame njiani kama wengi wafanyavyo, ila songa mbele, jipe moyo na Mungu yu pamoja nawe. Anakutaka ubaki na Yesu, utatoa matunda mema, kwani unachota uwezo ndani yake. Dumu ndani ya Bwana naye atadumu ndani yako. 

 

 

Katika Luka 10:25 – 33 tunasoma habari za msamaria alimsaidia mtu aliyekuwa akishuka kutoka Yerusalem kwenda Jeriko. Yule aliangukia mikononi mwa wanyang’anyi na wakampiga ,kuhani alipopita na hakumfanyia chochote, Msamaria akaja na akamtunza na kumponya yule mtu katika hatari. 

 

Tutende mema maadam tunaishi, matunda yetu yaonyeshe jinsi tulivyo. Matendo yetu yanaongea kuliko maneno yetu. Biblia inasema kuwa tutawatambua kwa matendo yao. Sifa kwa Mungu. 

 

Sasa macho yako yanaangaziwa na nuru ya kweli ambayo ni Yesu Kristo. Ukimpokea kama kiongozi wa maisha yako, utakuwa salama. Moyo wako utaona pumziko ndani ya Bwana. Ukiwa ulishampokea kama mwokozi wako, sifa kwa Mungu. Na ikiwa bado hujamkubali, hujachelewa sana, hata sasa, unaweza kumpokea. Yuko tayari kukujia ikiwa utafungua moyo wako. Atakutua mizigo yako, alikwenda msalabani kwa ajili ya upendo alionao kwa ajili yako. Usikatae wito wake, anataka kukuokoa, maisha yako yatapata heshima. Atakupa tumaini, utakuwa huru kutokana na kila laana. Utakuwa na maisha mapya ndani ya Yesu. Muombe aje ndani yako atakubadilisha kama alivyofanya kwangu na kwa wengine kama Paulo aliyekuwa muuwaji. Ukiwa unataka, nenda ndani ya chumba chako, muite Yesu kimya kimya, anakusikia na anakujibu. Mwambie kuwa u mwenye dhambi, taja dhambi zako unazozikumbuka, omba damu ya Yesu ikutakase, mwambie afute jina lako kwenye kitabu cha hukumu na kwandika jina lako kwenye kitabu cha uzima na atafanya hivyo mkalibishe yesu awe mwokozi na kiongozi wa maisha yako na uamini maneno hayo uliyo yasema na Mungu atasikiya .Amen ! Kwa ushauri wangu sasa  nenda kwa watumishi wa Mungu, watakupa ushauri  watakusaidia zaidi  ili uweze kukua katika imani. 

 

Hatua ya kwanza kwa safari ya kuelekea Mbinguni ni kumkalibisha Bwana Yesu moyoni mwako . Mengine tutayaongelea katika sura na kurasa zinazoendelea. Unaweza kuwa ndani ya familia ya Kikristo, wazazi wako, ndugu zako na dada zako wameokoka. Hilo haliwezi kukufanya uwe mwenye haki, kwani mtu anatambulika mbele za Mungu tu kwa ajili ya imani yake katika Yesu Kristo, na si kwa sababu anatii sheria ya Musa (Wagalatia 2:16). Baada ya Paulo kukutana na Yesu njiani Damaski, alitumwa kwa Anania ili ajifunze kitu kingine. Nawe pia inakubidi kuwaendea wana wa Mungu na watakusaidia. 

 

Sasa maisha yako yamebadilika kama umekubali kumpokea Bwana Yesu umetubu dhambi zako zote na kuomba kutakaswa na damu ya Yesu, kwa hio  wewe ni kiumbe kipya, wasiwasi kwako imekwisha Biblia inasema: sisi sote kama kondoo tumepotea kila mmoja amefuata njia yake ….; (Isaya 53:6) kwa ajili ya sadaka kama mtakatifu Petro anavyosema: “Kwa maana mlikuwa mnapotea kama kondoo; lakini sasa mmemrudia mchungaji na mwangalizi wa roho zenu” (1Petro 2:25) “Mwana wa Adam alikuja kutumikia na kutoa uhai wake uwe fidia ya wengi” (Marko 10:45) Biblia inasema kuwa mmenunuliwa si kwa vitu viharibikavyo kwa fedha au dhahabu; mpate kutoka katika mwenendo wenu usiofaa, bali kwa damu ya thamani ya Kristo (1Petro 1:18). 

 

Kama Mungu alivyookoa Waebrania waliokimbilia ndani ya nyumba zilizowekwa alama ya damu ya Kondoo asiye na hila, ndivyo anavyowaepusha na hukumu wale wote wanaotumaini ndani ya damu iliyobubujika kwa ajili yao msalabani. Yesu alibeba dhambi ya ulimwengu (Yohana 1:29) aliteseka kwa ajili ya wenye dhambi (Warumi 5:8) 

 

Yesu ni njia ya kweli, mtu haji kwa baba bila kupitia kwake. Tusidanganywe na fahari ya dini mbalimbali, tusome Biblia, tufuate njia sahihi ambayo ni Yesu Kristo. 

 

 

 

 

 

 

MARIAMU NI NANI? 

 

Biblia inatuambia baadhi ya wanawake mashujaa katika imani, tunaweza kumtaja Esta, Debora, Mariamu, Anna na wengine. Hapo tuseme tu juu ya Mariam mama mzazi wa Yesu. Mariamu alikuwa msichana mwenye kuwa na uzuri wa kuigwa. Alikuwa ameposwa na Yusufu na Biblia inasema alikuwa bikira. Siku moja malaika alimtokea na kumwambia kuwa atabeba mimba chini ya kivuli cha Roho Mtakatifu (Mathayo 1:18). Malaika akamwambia Yusufu asiogope kumchukua Mariam kwani mimba aliyonayo ni kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, na kwamba mtoto ataitwa “Yesu” kwa ni yeye atakaye waokoa watu wake na dhambi zao (Mathayo 1:20 – 21). Mungu hutusaidia katika mahitaji yetu yote. Malaika alimtokea Yusufu ili kumtia moyo. Kwa hakika Yusufu alikuwa na maswali mengi kwani alimwamini sana mchumba wake. Sio rahisi kuvumilia endapo utagundua kuwa mchumba wako ana ujauzito ambao wewe siyo mhusika. Kwa upande wake Mariamu ingelikuwa vigumu kwake kusema kuwa alikuwa hamjui mume, . Angalikuwa hana  neno la kusema ili watu wamuelewe ila ashukuriwe Mungu ambaye huingilia kati pale tunapokua na utata kutuliza nafsi zetu kabla mambo hayajazidi kuwa mabaya. Mungu wetu yuko makini anaona yote. 

 

 Siku moja kule Kana kulikuwa sherehe. Yesu na mama yake walikuwa wamealikwa. kwa sababu ya umati wa watu walioalikwa kuwa kubwa , mvinyo ilikwisha watu wakamjia Mariamu ili amwambie Yesu awape kinywaji. Lakini Yesu akajibu “Mwanamke ninanini nawe?” muda wangu haujafika (Yohana 2:4). Tangu hapo tunaona kuwa Mariamu hawezi kumuamrisha Yesu, wengi hujidanganya kuwa  kumuambia Mariamu awaombee. Msomaji mmpendwa tumeona jibu la Yesu hapo juu, » Mwanamke” Neno hili linadhihirisha kuwa ni mtu kama watu wengine. 

 

Sivyo ingeeleweka kama, akaendea, “tuna nini mimi na wewe?” swali hilo ni gumu! Hivyo inadhihirisha kuwa Mariamu ni mtu aliyeumbwa na Mungu, ila Yesu ni mwana wa Mungu sasa (mwenye dhambi na mtakatifu) kuna nini kati ya mwanadamu na Mungu mtakatifu?. Wakati wangu haujafika, Yesu aliendelea kusema, hayo yanaonyesha kuwa Yesu anatenda chini ya uongozi wa baba wa mbinguni,mtukufu, kwani yeye ametokana na Mungu. 

 

Anatii maagizo ya baba yake. Katika Yohana 5:30  “Mimi siwezi kufanya neno mwenyewe;kama nisikiavyo ndivyo nihukumuvyo;na hukumu yangu niya haki ,kwa sababu siyatafuti mapenzi yangu mimi ,bali mapenzi yake alienipeleka.” Yesu anasema, hawezi kutenda jambo lolote kwa ajili yake. Yesu anasema kuwa, kila anachokifanya ni pamoja na Mungu .Tena anafanya maagizo ya yule aliempeleka hapa duniani yani Mungu. Paulo yeye, anasisitiza kuwa hawezi kufanya lolote kwa uwezo wake,utoshelevu wake watoka kwa Mungu (2 Wakorintho 3 :5). Siku nyingine Yesu alikuwa na mitume wake,  Mariamu na ndugu zake Yesu walikuja kumtafuta. Watu wakamwambia kuwa mama na ndugu zako wako nje wanakuhitaji. Alijibu: mama na ndugu zangu ni nani? Mama ni nyie wote mnaomwamini Mungu, vivyo hivyo ndugu na dada zangu na mama yangu (Marko 3:32 – 35). Hayo yote yanaonyesha kuwa Yesu hausiki zaidi na uhusiano wa kifamilia ila anataka ulimwengu ujue kuwa yeye anatoka huko juu. Anawapenda wale wanaompenda Mungu na wanaofanya mapenzi yake. Nasi pia tuliokombolewa  tumezaliwa mala ya pili ,tumetokana na Mungu, Yesu alienda kutuandalia mahali mbinguni, sifa kwa Mungu urithi wetu ni makao ya wateule (Mbinguni). Tutakuwa na furaha, hakuna machozi, hakuna maombolezo. Oh jinsi ilivyo nzuri nchi ya kupendeza!! Kuna muimbaji aliyeandika: 

 “mimi najua nchi moja ambayo watu huishi kwa undugu, ni sherehe isiyo na kikomo. Maneno, » vita na kupigana » yametoka kwa kamusi ni sherehe isiyo na kikomo.” 

 

Katika Yohana 10:36 Yesu anasema: “je yeye ambaye Baba alimtakasa akamtuma ulimwenguni ,ninyi mnamwambia,unafukuru;kwa sababu nalisema ,mimi ni mwana wa Mungu?” aya 38 Yesu anahakikisha kuwa yu ndani ya Mungu na Mungu ndani yake. 

 

 

 Tunaweza kusema kuwa Yesu hakuwa mtii? Hakujua uhusiano aliokuwa nao na Mariamu? Hapana, Yesu ni mtii, ana adabu na hajawahi kutenda dhambi ni mtakatifu. Ila kinachomhusu ni wewe na mimi tunaohitaji maagizo yake. Kama unahitaji kuwa ndugu na dada wa Yesu tenda mapenzi yake Mungu. Jihusishe na ufalme wa Mungu. 

 Je katika zama hizi wapo wasichana ambao ni mabikira kama alivyokuwa Mariamu? Ndiyo kabisa. 

 Je kuna wasichana wanaotii neno la Mungu? Ndiyo kabisa. 

 Sasa kwa nini watu wanajikabidhi kwa Mariamu kuliko kwa Yesu aliyewafia msalabani? Shetani anao mpango wa kudanganya wana wa Mungu anataka watu wajidanganye kuhusu njia na kurithi hukumu. Hatari iliyopo ni kwamba watu hawataki kufahamu kweli. Wanadhani kuwa tayari wameshajua kweli kumbe shetani amewanasa. 

 

wakristo wengi wanampenda Mariamu kwa mioyo yao yote kiasi mpaka wanaelekeza maombi yao kwake! Ni hatari! Neno la Mungu linasema katika amri kumi (Kutoka 20: 4 – 6) “usijifanyie sanamu za kuchonga wala mfano wa kitu chochote kilicho juu mbinguni, wala kilicho duniani, wala kilicho majini chini ya dunia. Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi ni Bwana Mungu wako. Ninalazimisha kuwa Mungu wako wa pekee na ikiwa mtu yoyote atanipinga namhukumu, ……. Ila natenda wema ……. Kwao wanipendao na kutii amri zangu. 

 

Mungu anatukataza kujiundia miungu au vitu vinavyowakilisha kile kilicho mbinguni. Wakristo hawana miungu ila wana vitu vinavyomuwakilisha Yesu. Pia tunavyo vile vinavyowakilisha kile kilichopo juu ya nchi. Mfano; watu, wanyama wa kuchongwa kwa miti, n.k. yale yanayowakilisha vilivyoko chini ya dunia, mfano; sanamu za mamba, samaki wa kuchongwa kwa miti n.k. Mungu ametukataza kusujudia na kuinamia vitu vya aina hiyo. Ni Mungu pekee ambaye ni kwake tunaweza kusujudu na kuinama. 

 

Nyakati zilizopita kwetu tulikuwa tukiona watu wakiweka sanamu za Mariamu katika masinagogi ili kuabudu. Wakristo waliinamia na kusujudu mmoja baada ya mwingine wengine pia wanapo pita mbele ya Kanisa, wanainama na kupiga alama ya msalaba, kwa nini hayo? Mungu ametukataza kuinamia vitu kama hivyo. Na pia ametukataza kuviabudu au kuvitumikia. (Kotoka 20:3 – 6). Usiwe na miungu mingine ila mimi” Mungu anasema “ikiwa mtu atapingana na mimi nitamhukumu” nani anayeweza kustahimili hukumu ya Mungu? Hapa duniani watu huwainamia watu wanaowaheshimu. Wengine huinama na kuaga maiti kabla ya kufunga sanduku. Labda ni mila! 

 

Mungu anataka tumuabudu katika roho na kweli (Yohana 4:24). Tuwe kama Daniel aliyekataa kuabudu sanamu iliyowekwa na mfalme Nebukandeneza. Alikubali kufa kuliko kuvunja amri za Mungu wake (Daniel 3:17). Neno la Mungu ni nuru ya kweli, bila nuru giza litatuongoza upotevuni. Shetani anatupofusha ili tusitii maagizo ya Mungu. Sujuduni mbele za Mungu katika Roho, ila si mbele ya mtu au udongo wa mfinyanzi na si katika kitu chochote kinachowakilisha kilichotengenezwa kwa mikono ya wanadamu. Mungu alimaliza uumbaji na wala hakutuagiza tuendeleze au kumalizia (kukamilisha) jukumu lake. 

 Turudi kwenye aya yetu; “Yesu ni njia, kweli na uzima. Mtu haji kwa baba ila kwa njia ya mimi” Yohana 4:6. Yesu ndani yako atakuongoza katika njia hiyo nzuri. Wanaosema uongo wametokana na ibilisi kwani yeye ni baba wa uongo (Yohana 8:44) “ninyi ni wa baba yenu ibilisi, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzitenda. Yeye alikuwa muuaji tangu mwanzo na wala hakusimama katika kweli, kwa kuwa hamna kweli ndani yake, asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe; kwa sababu yeye ni muongo na baba wa huo ambaye hana Yesu ndani yake ni wa shetani, kwa sababu ni muongo na baba wa huo, Yesu ni uzima, aliyempokea ana uzima ndani yake. Tulikuwa tumekufa kwa dhambi zetu na damu ya Yesu ikatuokoa, sasa tuko hai sababu ya Yesu aliyetufufua pamoja naye Sifa kwa Mungu .Ambaye hana yesu, biblia inasema , hana uzima, amekufa hata kama anaishi. 

 

Mama wa Yesu alikuwa Mkristo na alimuamini mwanae, alikuwa na ushuhuda mzuri wa maisha ya Kikristo, alipenda kuwa ushuhuda. Msishangae, sikilizeni mashauri Yesu anayowapa kwani yana umuhimu mkubwa. Mariam alijua zilizomo ndani ya Yesu. Ndio maana anasema; fanyeni kila anachowaambia. 

 

 

 

UBATIZO NDANI YA MAJI 

 

Yesu mwenyewe alikuwa mfano kwetu katika Yordani, alibatizwa na Yohana mbatizaji. 

 

Sasa mpendwa Ubatizo ni nini? 

Ni alama ya unyenyekevu unaomaanisha kufa na kufufuka pamoja na Yesu, pia ni tendo la utii kwa Bwana, na pia ni ushahidi mbele za watu. 

 

Yohana mbatizaji anasema “kweli mimi nawabatiza kwa maji kwa ajili ya toba; bali yeye ajaye nyuma yangu ana nguvu kuliko mimi …. Yeye atawabatiza kwa roho mtakatifu” (Mathayo 3:11). Ubatizo ni tendo linalofanyika juu ya mwili wa mtu ila ubatizo wa roho mtakatifu, ni tendo la kiroho linalofanywa na Yesu mwenyewe. 

 

Ubatizo wa maji mengi uliwakilisha nini? 

 

 

Baada ya kutibu dhambi zao (Mathayo 3:6), waliokuja kubatizwa walijiingiza wazima wazima ndani ya Yordani, wakatoweka kwenye uso wa dunia: walikufa. Kwa nini walikufa? Myahudi aliyefundishwa na huyu mkufunzi ambaye ni torati ya Musa (Galatia 3:24) amezoea sadaka za kuteketezwa za Walawi, hakuwa na shida kuelewa ilipotolewa sadaka kwa ajili ya dhambi (Walawi 4), alijua kuwa mwana kondoo yule aliposwa kwa ajili ya dhambi zake alizokuja kutubia. Yohana mbatizaji aliwazika ndani ya kaburi ambalo ni maji mengi, mtu mwenye dhambi na waliofishwa kwa njia ya ubatizo, alifutika katika uso wa dunia hii. Yule ambaye kwa neema ya Mungu alichovywa kwa muda kadhaa katika yale maji, alipata kuwa mtu mpya, ambaye usubiri azae matunda tofauti na yale ya kabla ya kubatizwa. “timizeni matendo yanayodhihirisha kuwa mmebadirika  kutokana na tabia …”. Kipindi cha Pasaka huongeza nuru mpya na kuleta maana kamili. Bahati mbaya ubatizo wa maji hauwezi kuzalisha matukio ya kiroho yanayomaanisha kwa picha fulani; ila tu ubatizo wa roho mtakatifu unaweza. Tunagundua kuwa tunakuwa na namna nyingi za kubatiza. Yesu mwenyewe alituonyesha kielelezo pale alipokubali kubatizwa na Yohana mbatizaji katika Yordani. Yesu anawaambia wanafunzi wake kumi na mmoja (Marko 16:15 – 16) “enendeni duniani kote mkahubiri injili kwa watuwote. Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini atahukumiwa”. Yesu amesisitiza mambo matatu kwa mpangilio, 1. atakayeamini, 2. akabatizwa, 3. ataokoka. 

 

Kuhusu ubatizo, sehemu ya kwanza ni kuamini mwana wa Mungu. Ikiwa anabatizwa mtu asiyemuamini mwana wa Mungu ni bure haina maana. Kabla ya kumbatiza mtu, inabidi kwanza kumtangazia habari njema ya Yesu Kristo, akiliamini neno hilo ndipo abatizwe. 

 

 Siku moja nilimuuliza dada yangu wa kiroho “ulibatizwa lini?” akajibu, “hata mimi sijui lini kwani wazazi wangu ndio walionitafutia ubatizo nilipokuwa bado mdogo”. Je na wewe ulibatizwa tangu ulipokuwa mdogo? Biblia inatuonyesha maagizo ya Yesu mwenyewe, ila watu wamepindua ujumbe wa Yesu Kristo. Biblia inahukumu pia yule anayeongeza juu ya maneno ya unabii au kupunguza kitu chochote juu ya maneno ya unabii ya biblia takatifu (Ufunuo 22:18 – 19) 

 

Hatujaruhusiwa  kubadili  maneno ya unabii  ya Biblia kama tunavyotaka au tunavyopenda. Je watoto wadogo na wachanga wanauwezo wa kusikia maneno ya Mungu na kuamini kwa hayo? Tuliamini kuwa kwa umri Fulani, kabla ya kujua mema na mabaya, watoto hawana dhambi, kwani Yesu alisema kuwa anayetaka kuingia katika ufalme wa Mungu inambidi awe kama mtoto mdogo (Mathayo 19:14). 

 

Kwa nini Yesu anatoa mfano wa mtoto mdogo? Naamini mtoto hana dhambi,  kwangu mimi, mtoto hana haja ya kubatizwa . Tuwe kama watoto katika mabaya, na kama watu wazima katika ufahamu wa Bwana wetu. 

 

 Jinsi gani sasa tunavyoweza kubatizwa? Yesu alishuka Yordani ili abatizwe na Yohana mbatizaji. Yesu mwenyewe alikuwa akibatiza (Yohana 3:22). “Baada ya hayo Yesu na wanafunzi wake walikwenda mpaka nchi ya Uyahudi,akashinda huko pamoja nao akabatiza. »   (Yohana 3 :23) « Yohana naye alikuwa akibatiza huko Ainoni,karibu na Salimu,kwa sababu huko kulikuwa na maji tele. » 

 

Kwa nini Yohana aliwaongoza watu katika Uyahudi na hasa Ainoni? Biblia inajibu , kwa sababu kulikuwa na maji mengi. Kwa nini alibatiza katika Yordani? Kwa sababu kulikuwa  na maji mengi (Mathayo 3:16) “Naye Yesu alipokwisha kubatizwa, mara akapanda kutoka majini, na tazama mbingu zikamfunukia, akamwona roho wa Mungu akishuka kama hua, akija juu yake”. Kwa aya hii tunaona, Yesu alitoka ndani ya maji. Kwa hiyo kama Biblia inavyoonyesha, ubatizo unafanyika katika maji mengi. 

 

Yesu hakubatiza watoto ila aliwabariki. Tusome Mathayo 19:13 – 15 “Akaletewa watoto wadogo ili aweke mikono juu yao na kuwabariki, wanafunzi wake wakawakemea. Yesu akasema “waacheni watoto wadogo waje kwangu; kwani walio kama hao ufalme wa mbingu ni wao. Akaweka mikono juu yao akatoka huko” 

 

Hayo ni maneno machache ninayoweza kusema kuhusiana na jinsi ya kubatizwa.kubatizwa ni kiapo kinacho onyesha kwamba umekubali kuwa wa kwake.Ukibatizwa kwa jina la Yesu basi wewe umekubali kuwa wa kwake milele.Biblia ina sema (wagalatia 3:26-29) “Kwa kuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa Mungu kwa njia ya imani katika Kristo Yesu.Maana ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo Hapana Myahudi wala Myunani.Hapana mtumwa waka huru.Hapana mtu mume wala mtu mke.Maana ninyi nyote mmekuwa mmoja katika Kristo Yesu.Na kama ninyi ni wa Kristo,basi mmekuwa uzao wa Ibrahimu,na warithi sawasawa na ahadi.” 

 

 

 

 

 

 

 

 

UBATIZO WA ROHO MTAKATIFU 

 

 

Ikiwa tukija kwa Kristo kwa hamasa ya kuwa na toba ukilinganisha na ule wa Wayahudi waliokuja kwa Yohana mbatizaji, ubatizo wa roho mtakatifu unafusha na kutowesha kabisa “utu wa kale” mbele za macho ya Mungu. Wenye dhambi ambao tulikombolewa kwa ubatizo wa roho wake, ametuweka kwa faida ya kifo chake, anatushikamanisha kwake, mungu hutujali pamoja na mwana aliyekufa msalabani kwa ubatizo huo ambao mtume Paulo anasema kwa Warumi “Sisi tuliobatizwa katika Kristo Yesu, ni katika mauti yake ndipo tulipozamishwa. Tumefanyika pando lilelile pamoja naye kwa utimilifu wake katika mauti yake …. Utu wetu wa kale ulisulubiwa pamoja naye, ili mwili wa dhambi ubadilike ……… kwani yeye aliyekufa ameshahesabiwa haki mbali na dhambi” 

 

Ubatizo wa maji hauwezi kututambulisha kwa mauti ya Kristo, au kuondoa utu wetu wa kale, au kutokomeza miili yetu ya dhambi; labda kuufanya kwa mazingaombwe ambayo hauna. Yesu ananyoosha mikono na kusema: njooni nyote ! ila iweni waangalifu: kukumbatiwa huku kwanza ni mauti ….  kama mnakubali kujiachilia kabisa kwake, mtakufa kabisa kwani hakuna uzima “bila mwingine” kuwa maisha kupitia mauti. Tunaweza kuzaliwa upya kama tu tutakubali kufa “lakini mafarisayo na wanasheria walilipinga la Mungu juu yao, kwa kuwa wamekataa  kubatizwa na Yohana (Luka 7:30). 

 

Mtu anaweza kutubu  dhambi zake,  na kumgeukia Mungu, yaani kubadilika,.Anaweza kuja kwa Kristo, kuweka tumaini kwake, yaani kumuamini. Ni Mungu peke yake ndiye awezaye kufanya tendo la mabadiliko ndani ya mtu na kumfanya kiumbe kipya. Kabla ya kuumba mtu mpya Mungu kwanza hutowesha “utu wa kale ulio na udanganyifu na kuelemewa na dhambi.” 

 

Biblia inasema (1Korintho 11:31) “Kama tungejipambanua nafsi zetu tusingehukumiwa” Mungu anatupitisha kiroho na kwa kupitia dhamira inayopata hukumu. Biblia inasema: (Ezekiel 18:4) “Tazama roho zote ni mali yangu, kama vile roho ya baba ni mali yangu; roho ile itendayo dhambi itakufa” kwa aya hiyo, roho itendayo dhambi itakufa. Tunakufa kikamilifu kabla ya siku ya hukumu hivyo kuepuka hukumu. “Yeye alisikiaye neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka yu na uzima wa milele, wala haiingii hukumuni, bali amepita kutoka mautini kuingia uzimani” (Yohana 5:24, Wakolosai 2:11). 

 

Haistahili kusema narudi nyuma, inabidi nife, kwamba nimesulubiwa kama muasi ili kusikia neno lake la neema, hivyo unaweza kumwendea Kristo aliye mwana wake mpendwa. Kufa pamoja na Kristo ni jambo muhimu katika maisha ya Kikristo. Mauti yetu pamoja na Kristo inatupa msamaha wa dhambi zetu, hata katika vyombo vyetu vya sheria wafungwa wanaokufa hawahukumiwi tena. Mauti inamkomesha mashitaka na kuondoa hukumu zote. Vivyo hivyo Mungu pia husamehe wenye dhambi ambao kwa imani, wamekubali kufa pamoja na Kristo (Luka 24:47) Mungu pia huukumu (anadai haki) 

 

Hali nyingine ya ubatizo wa Roho Mtakatifu ni ufufuo wa Kiroho (Warumi 6:11 na katika Yohana 14: 17, 20, 23) “Kuzaliwa upya ni tendo linalotafsiriwa kwamba Yesu huingia ndani yetu na kufanya makao yake kama Bwana. Sifa kwa Mungu Bila roho mtakatifu hakuna hata mtu mmoja ambaye angeokoka. Yesu anawaambia mitume wake kuwa atakapokuja huyo mfariji atauhakikishia ulimwengu kwa habari ya dhambi, na haki (Yohana 16:8) ni roho mtakatifu peke yake awezaye kuhakikisha dhambi, ni yeye pekee pia ndiye awezaye kuweka ndani ya mtu kiu ya kuokoa. 

 Kulingana na Yohana 15:26 “Yule msaidizi atakuja kwenu, ni roho wa kweli atokaye kwa baba” bila kazi ya roho mtakatifu, kila injili, unabii wowote, ushuhuda wowote umebadilika, kwani mwanadamu mwenye mwili wa asili hawezi kujua mambo ya roho wa Mungu (1Korintho 2:14) mtu ambaye hana roho wa Mungu hawezi kupokea kweli inayotokana na roho huyo: ni wazimu kwako, hana uwezo wa kuelewa, kwani hawezi kuhukumiwa isipokuwa kwa roho mtakatifu. 

 

Hatua ya tatu ya ubatizo wa roho mtakatifu ni kutushikamanisha naye. Tusome  1Koritho 12:13 “Kwa maana katika roho mmoja sisi sote tuliobatizwa kuwa mwili mmoja, kwamba tu Wayahudi, au kwamba tu Wayunani, ikiwa tu watumwa au ikiwa tu huru; nasi sote tulinyweshwa Roho mmoja” Ubatizo wa roho mtakatifu, ambao utufisha na kutuzaa kwa maisha ya mbinguni, hutushikamanisha moja kwa moja kwa Kanisa la Kristo …… Paulo na ndugu yake Sostena, waliandika barua kwa wakristo wa Korintho: (1 Korinto 1:2) “Kwa Kanisa la Mungu lililo Korinto, wale waliotakaswa katika Kristo Yesu walioitwa wawe watakatifu, pamoja na wote wanaoliitia jina la Bwana wetu Yesu Kristo kila mahali, Bwana wao na wetu …… “Kwa andiko hilo, tunaona kwa Wakoritho wanamuita Yesu Kristo kuwa Bwana wao wameokolewa, wamezaliwa upya (1 Korintho 4:15) wamenunuliwa (1Korintho 7:23) “Mlinunuliwa kwa thamani msiwe watumwa wa wanadamu , waliooshwa, wametakaswa (1 Korintho 6:11) “Na baadhi yenu mlikuwa watu wa namna hii ; lakini mlioshwa, lakini mlitakaswa, mlihesabiwa haki katika jina la Bwana Yesu Kristo, na katika roho wa Mungu wetu” 

 wote waliookoka, kutakaswa na kuthibitishwa na Yesu Kristo, nao pia wamebatizwa kwa roho mtakatifu kama sisi tulivyohakikisha; 

 ubatizo wa maji hauwezi kumbadilisha mtu kwa hali ya kumthibitisha, kutakaswa, na kuokoka. 

 Ni huyo Roho mtakatifu ndiye anaye mhakikishia mtu kulingana na dhambi zake, ndiye anayempa hamu ya kuhitaji wokovu. 

 

Kuna hatua nyingine: ujazo wa Roho Mtakatifu. 

 

 Kabla ya Pentekoste, mitume wa Yesu walihubiri habari njema kwani walikuwa wameongoka na kubatizwa na Roho mtakatifu. Ila hatua ya pili ya ubatizo iliwapa ujasiri wa kutumika bila woga. Ubatizo huu uliwaletea karama tofauti na kuwa wakamilifu katika matendo ya Mungu. 

 

Roho mtakatifu humzamisha muamini katika mwili wa Kristo na kudhibiti utu wa kale (2 Korintho 4:10) siku zote twachukua katika mwili kuuwawa kwake Yesu, ili uzima wa Yesu udhihirishwe katika miili yetu. Roho ambaye kwake muamini amechovywa kama osheo lianavyochovywa ndani ya maji. Roho mmoja ni Mungu, ila kuna roho nyingine zilizo katika ulimwengu (1 Yohana 4:1 – 3) “Wapenzi msiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani. Katika hili mnajuwa wa Mungu; kila roho ikirivyo kwamba Yesu Kristo amekuja katika mwili yatokana na Mungu; na kila roho isiyomkiri Yesu haitokani na Mungu. Na hii ndiyo roho ya mpinga Kristo ambayo mmeisikia ya kwamba yaja; na sasa imekwisha kuwapo duniani”. 

 

Roho hizo hazimkiri Yesu Kristo, zinawapunguza watoto wa Mungu. Roho hizo zinapingana na ubatizo wa roho mtakatifu na kuendesha watu kwa matakwa yao. Korintho ilikuwa imejazwa na ibada nyingi za miungu. Mtume Paulo anawaandikia wakristo kwamba wasichangamane na wapagani (1 Korintho 10:20) anataka wajitunze chini ya uongozi pekee wa Roho (Roho wa Mungu) huwashikamanisha kutoka mauti kuingia ufufuo wa Bwana Yesu Kristo. Paulo anazungumzia roho mmoja sababu roho huyo mmoja anaweza kuwakusanya wote katika mwili mmoja. Kama kuna ubatizo wa roho unaotutenga na waumini wengine ambao nao ni watoto wa Mungu, tunaweza kweli kunfanya roho halisi ya Kristo ambayo inatusaidia kuungana na kuwa kitu kimoja? Sasa basi, kama roho mmoja yuko ndani yangu na ndani ya ndugu yangu tunaweza kutengana? Kwani lengo la roho mtakatifu katika kuwabatiza waumini ni kutengeneza mwili mmoja. Wakati mtoto anapozaliwa, anaingia ndani ya familia na mtu anapozaliwa upya, anaingia katika familia ya watoto wa Mungu. 

 

Mungu hapendi tuendelee kuwa kondoo wasio na muelekeo, kondoo wanakwenda kila mmoja katika njia yake  (Waefeso 2:19) alituingiza ndani ya familia yake, tunatakiwa “kuitwa watakatifu, watu wa nyumbani mwa Mungu” (Waefeso 2:20) “Mshirika wa mwili wa Kristo (1Kor 12). Iwe ubatizo wa maji; iwe ubatizo wa kawaida, iwe maungamo ya imani hayawezi kukufanya kuwa mshiriki wa mwili wa Kristo au kuwa mmoja wa familia ya watoto wa Mungu, ila tunaweza tukawa ndani ya familia ya wana wa Mungu kwa kubatizwa na roho mtakatifu. “Hivyo basi ni vizuri kuzaliwa upya” 

 

 

 

  

 

MATUNDA YA MWONGOFU AU MATUNDA YA MAISHA MAPYA 

 

 

Matunda ni alama inayotofautisha wakristo wa kweli na wasiomuamini; “mtawatambua kwa matunda yao” (Mathayo 7:16). Sawasawa na neno la Mungu; ni matunda gani ya maisha mapya? 

 

1.    Waliozaliwa upya wanauhakika wa wokovu ndani yao kwani Yesu asema (Katika Luka 5:20 “Mtu, dhambi zako zimesamehewa”.  Katika Luka 7:50 “Imani yako imekuponya, nenda kwa amani” kuwa na maisha ya umilele na imani. Siyo katika maisha yaliyopita, bali ya sasa “Yeye anaye mwamini ana maisha ya umilele” (Yohana 3:46). Tunaweza kuona sasa umuhimu wa kuokolewa. Mtume Yohana anasema wazi, aliye na mwana anao uzima. Niliwaandikia haya  ili mpate kujua kuwa mnaouzima wa milele. Ninyi mnaomwamini mwana wa Mungu” 1 Yohana 15:10 – 13 

 

Uhakika ndani ya wokovu, unaimarisha imani inayotegemea ahadi za Mungu. Yesu alisema, yule alisikiaye neno lake na kumwamini aliye mtuma ana 

a)  Uzima wa milele 

b)  kupitia kifo,ana uhai 

c)  Hata hukukumiwa 

 

Uhakika huo ndio unaoleta furaha, na upendo ndani ya   mioyo ijapo wakati mwingine kuna upinzani. Uhakika wa wokovu ni nguzo imara katika maisha ya muumini (2 Timotheo 1:12) “Nami nateseka kwa mambo haya kwa sababu hiyo lakini niko bado timamu kabisa kwani namjua yule niliyemwamini, tena nina uhakika kwamba yeye atakilinda salama kile alichonikabidhi mpaka siku ile. 

 

Hakuna mtu awezaye kuwa Mkristo wa kweli bila kuwa na uvuvio wa roho mtakatifu anayeweza kujaza amani ndani ya roho yetu, furaha upendo. 

 

Matunda ya ndani ya roho mtakatifu ni: Amani, furaha, imani ndani ya Mungu, kutoogopa kufa ,……………. Kwa kuhakikishiwa na imani tuna amani katika Mungu (Warumi 5:1) biblia inasema “Ufalme wa Mungu ni haki, amani na furaha iletwayo na roho mtakatifu (Warumi 14:17) 

    

2.    Aina nyingine ya tunda ni Hatua endelevu katika njia ya utakaso biblia inasema: yeyote anayeishi ndani yake hatendi dhambi, tena yeyote atendaye dhambi hakumuona na wala hakumjua, biblia inasema: aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu mbegu ya kiungu imo ndani yake. Na ndipo tunapoweza kujua yupi mtoto wa Mungu, na yupi wa shetani” 

 

Kuwa mwana wa Mungu hakuna kutokuwa na dhambi kabisa, kwani katika maandiko, mtume Yohana anasema, “Tukisema kwamba hakuna dhambi, tunajidanganya wenyewe, na ukweli haumo ndani yetu (1 Yohana 1:8). Katika agano jipya tunasoma kwamba kuzaliwa upya, ni lazima kuambatana na uamuzi wa matendo ya utakaso wa mwamini (Yohana 8:31, Warumi 6:19). Baada ya kusema kuwa: “mmekufa” (kwa dhambi, katika maisha yaliyopita) mtume Paulo anaongeza u basi na tuvuliwe  tamaa za kidunia …………. Tangazia vitu vyote …….. kwamba umeuvua wa kale na matendo yake na umeuvaa utu mpya (Wakolosai 3:3 – 10). Mungu anasema: jitahidini kuishi kwa amani na watu wote. Ishini maisha ya utakatifu kwa sababu hakuna atakayemuona Bwana bila ya maisha kama hayo. Utakatifu ni hatua mpya ambayo tunatakiwa kuingia ndani yake na kuendelea, ili tuweze kuwa na wokovu halisi uliokamilika. 

 

 

3.    Kuwa na tabia ya maombi. Roho anayekaa ndani ya mkristo anamuongoza kwa maombi  kwa sababu yeye mwenyewe anatuombea (Rum 8:26). Yesu akiwa ndani yetu, atatuwezesha kumsifu Mungu na kumwabudu, pia kutia watu moyo katika maisha yetu binafsi , maombi ya ndani kwa ndani yatajaza hatua kwa hatua nafasi zilizokuwa wazi kwa ajili ya mambo yasiyofaa. Udhihirisho mwingine kwa roho ya maombi ni maombi ya pamoja. 

 

 

4.    Aina nyingine: Hamu ya neno la Mungu. Tumegundua kuwa wakristo wengi wa agano la kale waliimba sana  juu ya upendo wa neno takatifu. “Nafungua kinywa kwa hamu kubwa, maana ninatamani sana amri zako … nafurahi kwa sababu ya neno lako, kama mtu aliyekuta kitu cha thamani kuu ………… sheria yako ndiyo furaha yangu”. (Zab 119:131, mstari wa 162 na 174). Yesu alisema kuwa kondoo wa mchungaji mwema anasikia sauti yake (Yoh 4:6) na mtume Yohana anasema, “mtu anayemjua Mungu hutusikiliza, mtu asiye wa Mungu hatusikilizi”. Basi kwa njia hiyo tuaweza kutambua tofauti kati ya roho wa ukweli na roho wa uongo(1yoh 4:6).Biblia ulikua unaisoma kama kubahatisha au kwa sababu ni amri tu,au urikua huisomi kabisa ,inageuka kuwa kitabu kizuri sana  na unathamani kukimariza kwa sababu kimegeuka kuwa chakula chako cha kila siku.Je,huoni kwambani barua aliyo kuandikia mpenzi wako, »neno la uzima »(1Petro 1:23)  ili azungumze nawe kila siku?. 

 

Ndipo upendo wa neno unatofauti na pendo   zingine ziiletazo ubinafsi. Mtume Petro aliandika kwa waongofu wapya, ushauri: “Kama vile watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa ,ili kwa hayo mpate kuukulia wokovu” (1 Petro 2:2) kupenda kusoma maneno ya Mungu ni uahirisho wa uwepo wa roho wa Mungu.ukiona maandiko ya Mungu huyataki tena iyo ni alama ya kurudi nyuma .Bibia tunaiamini kwa imani kwamba ni ufunuo wa Mungu kwa wanadamu. 

 

 

5.    Tunda lingine muhimu: Upendo wa Mungu na wa Kristo. Waongofu wapya wanakuwa na hamu ya kuwa karibu ya Kristo. Mara zote mwanadamu wa kawaida anaishi akiwa na woga wa kifo (Waebr. 2:15). Kristo anatuweka huru mbali na hofu hiyo. Ujio wa Kristo umekuwa sasa kitu cha kusubiri tena kwa furaha kuliko kuwa na hofu: u kwa sababu mnapokea wokovu wa roho zenu ambao ni lengo la imani” (1 Petro 1:9, Wafilipi 3:20). Upendo wa Mungu ni sababu ya uwepo wa roho wa Mungu ndani yetu. “Upendo wa Mungu uliweza kugawanywa kwetu na roho mtakatifu (Rum 5:5). Tunampenda kwa kuwa alitupenda kwanza. (Yoh 21:17). Ni upendo wa Mungu ndio unaotuweka mbali na hofu. Mwanafunzi mwema ni yule atakayesema kama Petro alivyomwambia Yesu “Bwana, wewe wajua yote, unajua nakupenda” Yoh 21:17). Petro aliandika kwa waliopotea: “Mlimpenda bila ya kumwona” (1 Petro 1:8). Neema ya Mungu na iwe juu ya wote wampendao Bwana Yesu Kristokwa upendo wa dhati” (Waefeso 6:24). Bwana ameandaa taji ya haki kwa wote wanaomtazamia kwa upendo kutokea kwake (2 Tim 4:8) « Kati ka hili tunafahamu ya kuwa tunakaa ndani yake ,naye ndani yetu ,kwakua ametushirikisha roho wake. »(1Yoh 4:13) 

 

 

6.    Hamu ya kumtumikia Mungu. Kuwa na nia hiyo ni tunda lingine muhimu la maisha mapya. Tunaona kuwa, mtu anampokea Yesu katika maisha yake anapenda mara kwa mara kuwashuhudia wengine juu ya upendo wa Kristo, ila na wao wampokee. Mwanafunzi wa kwanza alipokutana na Yesu, aliwaleta pia wazazi na marafiki zake. “Andrea alimkuta nduguye Petro na akawaleta kwa Yesu ……. Filipo akamwambia Natanael: tumempata masiya (Yoh. 1: 40 – 45)” kila akiriye ya kuwa yesu ni mwana wa Mungu,Mungu hukaa ndani yake ,naye ndani ya Mungu »(1Yoh 4:15) 

 

7.    Upendo wa ndugu: Upendo huu wa ndugu ni sababu ya karibu ya upendo wetu kwa Mungu. “Kila anayempenda mzazi humpenda pia mtoto wa huyo mzazi. (1 Yoh. 5:1) amchukiaye ndugu yake yuko gizani, anatembea katika giza na hajui aendako (1 Yoh 2:11). 

 

“Mtu asiye na upendo hamjui Mungu” (1 Yoh. 4:8). Kabla ya kutubu, shirika la kikristo lilionekana kama kitu fulani kisicho na msingi “Dunia inapenda aliye ndani yake” (Yoh. 15:19). Kwa sasa tunajisikia kuvutiwa na ndugu na dada katika Kristo, tunapenda kuhudhuria sehemu za maombi, au neno la Mungu na pia hata kutangaza kuwa tunatafuta mahali pa kuabudu. Yesu alisema: mkipendana, watu wote watajua kwamba ninyi ni wanafunzi wangu” (1 Yoh. 13:35). 

 

Mtume Yohana anahakikisha, kwa kusema kuwa upendo huu pia ni alama ya maisha mapya; “Tunaweza kujua kuwa tumepitia mauti na kuelekea uzima, iwapo tutakuwa na upendo wa ndugu (1 Yoh 3:14)”; “Kupenda kwa vitendo na kweli; hivyo ndivyo tuwezavyo kuwa na hakika kwamba sisi ni watu wa ukweli (1 Yoh 3:19). 

 

Aina nyingi zinaonekana baada ya kipindi kirefu, nyingine zinaonekana pale mabadiliko yanapoingia ndani ya moyo wa muumini kama roho wa Mungu anafanya kazi ndani yako, basi kutakuwa pia na matendo ya neema yako ndani yako. Endapo hakutakuwa na mabadiriko ndani ya yule anayejiita mwongofu, na kutokuwa na uhakika na wokovu wake, pia kukosa hamu ya kuomba wala kusoma biblia, kutopenda kushuhudia, kuacha kuwashiriki au kuwatembelea wakristo wenzake, tunakuwa na haki ya kuwa na mashaka na wokovu wake. Kuwa na mashaka sio “kuhukumu”. Biblia inatuonyesha alama za maisha mapya na kusema hukumu wale walio katika jamii yenu” (1 Kor 5:12) tunaweza kusema kwa mfano: kuwaambia watu kuwa ni lazima waombe sana, kudhuria ibada zote, kuwa wa kiroho sana, kutoa sana kwa ajili ya kazi za Mungu n.k. …… “Lakini kama tungewaambia kuwa ni lazima wazaliwe mara ya pili wangeanguka kama Nikodemu. Wangefunguka, na pia wangekasirika.    

 

   

        

 

   

   

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

SURA YA PILI 

 

 

UBATIZO KATIKA ROHO MTAKATIFU 

 

Tulionyesha ubatizo wa maji na ubatizo wa Roho Mtakatifu, na tukasema kwamba ubatizo wa maji ni alama ya unyenyekevu inayomaanisha kufa na kufufuka pamoja na Kristo. Lakini cha muhimu ni ubatizo katika Roho Mtakatifu inayokufanya kuona wewe ni mtenda dhambi na kwamba unamhitaji Kristo katika maisha yako. Bila ya Roho Mtakatifu wa Mungu, hakuna anayetambua madhambi yake. Lakini Roho hiyo inayo jukumu la kututhibitishia hali yetu ya kiroho na kutufunulia upendo wa Mungu kwa ajili yetu. Tukiwa katika ubatizo wa Roho hiyo, tunakuwa wakristo wapya, kwa hiyo tumezaliwa upya, kwani tumepita toka umauti hadi maisha kwa sababu ya Kristo aliye badilisha maisha yetu kupitia Roho hiyo. Tumetoka kuona baadhi ya alama zinazoonyesha kuwa mtu amezaliwa upya au hapana. 

 

Tutazame sasa hatuwa nyingine muhimu katika maisha ya myu anayesemekana amezaliwa upya au kaokoka. Kwa undani, Roho Mtakatifu ni kitu gani ? Ni nafsi mmoja katika Utatu Takatifu atupaye uwezo na nguvu ya kuishinda dhambi na kutoingia katika mitego ya Shetani. Ni vigumu sana kupingana na Shetani bila ya kuwa na uwezo hua ( Mndo 1 :8 ) ‘’ Lakini Roho Mtakatifu atashuka kwenu, atawapa nguvu na mtakuwa mashaidi  wangu huko Yerusalemu,……hadi pembe za dunia.’’  Roho Mtakatifu ni muhimu katika kazi ya Mungu. Aliwaahidi wanafunzi wake kuwa atawatumia Roho Mtakatifu ili awasaidie katika kufanya kazi bila woga (Yoh.14 :26) ‘’Yule anayepashwa kuwasaidia, Roho Mtakatifu atakayetumwa na Mungu kwa jina langu, atawafundisha kila kitu, na atawakumbusha yote niliyowaambia ‘’.  Roho Mtakatifu ana jukumu la kutusaidia katika ukuaji wa kiroho, kumtumikia Mungu kwa upendo, kutufundisha yote toka kwa Mungu na kutukumbusha yote aliyetwambia Yesu, n.k. 

 

Kwa haya ya Yohana 14 :26, tunaona kuwa Mungu ndiye anayemtuma Roho mtakatifu kwa waumini kwa jina la Yesu Kristo. Ni kazi ya Baba wala si ya myu mwingine yeyote. Anatoa baraka kwa wakristo wenye mioyo isiyo na dhambi.Yesu aliwaambia wanafunzi wake : ‘’ Nitamuomba Baba awape mtu mwingine ili awsaidie, Roho wa kweli, ili hatimaye awe pamoja nanyi siku zote.’’  ( Yoh. 14 :16).   

 

Jihadharini sana, kwa kuwa dunia haiwezi kumpokea wala kumfahamu                    ( Yoh.14 :17) . Tuchukue mfano wa Simoni  yule  Mchawi, alisikiliza Neno la Mungu lililosemwa na Filipo, akaamua kuacha dhambi na kumfuata Yesu Kristo. Lakini alipoona wanafunzi wakiwaombea waumini kwa ajili ya kupokea Roho Mtakatifu, akawaagiza wanafunzi hao wanunue kwa thamani ya fedha uwezo wa kupokea huyu Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu hanunuliwi kwa fedha. Katika moyo wa Simoni , kulikuwa na madhambi mengine , alikuwa bado hajazaliwa upya.Alikuwa mukristo bandia na alikuwa antowa ushuhuda wa Kristo kwa mdomo tu. Moyo wake haukutakaswa. Wasiyokuwa wayahudi, nao pia walimpokea Roho Mtakatifu. (Mndo 10 :44) ‘’Wakati Petro alikua akiendelea kuongea, Roho Mtakatifu alishuka juu ya wote waliyokuwa wakimsikiliza’’. Haya ya 46 ‘’ Basi walisikika wakiongea katika lugha zisizofahamika na kusifu utukufu wa Mungu’’. 

 

Sasa ni nani anayeweza kubatizwa katika Roho Mtakatifu ? Ni yeyote anayetaka kufanya hivyo.Bibliya inasema: ‘’Ombeni nanyi mtapewa, tafuteni mtapata, pigeni hodi nanyi mtafunguliwa’’. (Mt.7 :7). Mwenyezi Mungu aliyewabatiza wasiyo wayahudi na wayahudi bila ubaguzi ( uwe mkristo kutoka dhehebu yeyote, amioni ahadi yake Mungu tu na omba kwa Mungu akubatize naye atafanya hivyo). Katika makanisa mengi wakristo hawawezi kufanya zoezi hili. 

 

Ni Mungu peke yake ndiye anayefahamu mioyo ya waumini, ni yeye peke yake anayeweza kumtuma Roho Mtakatifu katika kila mmoja wetu. Mungu wetu apewe sifa. Kama umezaliwa upya na kama umebatizwa kwa maji, ni wakati wako sasa wa kutafuta kubatizwa kwa Roho mtakatifu. Yesu Kristo mwenyewe aliupata ubatizo huo wa Roho Mtakatifu wakati alipokuwa akibatizwa na Yohana katika mto wa Yorodani.Ubatizo wa Roho Mtakatifu unatafutwa namna gani ? Kama unataka kubatizwa kwa Roho Mtakatifu, basi omba kwa Mungu , kazana uombe usiku na mchana hadi upate kubatizwa. Ubatizo wa Roho Mtakatifu siyo jambo la kikundi  chochote cha watu ama kanisa lolote, bali ni ahadi ya Mungu mwenyewe kwa kwa ajili ya muumini yeyote. Yesu alibatizwa , wanafunzi wake pia pamoja na baadhi ya wakristo wa makanisa yetu, na wewe unaweza ukabatizwa, kwa nini usifanye hivyo ? 

 

 

                             VIPAJI VYA ROHO MTAKATIFU 

 

‘’Ndugu zangu, nataka mtambue ukweli kuhusu vipaji hivyo. Kuna aina mbali mbali za vipaji vya kiroho , lakini ni Roho Mtakatifu huyu huyu aneidhinisha. Kuna njia mbali mbali ya utumishi, lakini ni Bwana huyo huyo ndiye anaetumikiwa. Kuna shudghuli mbali mbali , lakini ni Mungu huyo huyo ndiye anayeyazalisha yote kwa wote. Roho Mtakatifu hufanya kazi kwa kipaji kwa manufaa ya wote’’ ( 1 Korintho 12 : 1-7).  

 

Mtume Paulo kawaambia wakorintho kuwa kuna aina mbali mbali ya vipaji vya kiroho vilivyotolewa na Roho Mtakatifu . Mungu wetu an utajiri wa vipaji. Kupiyia njia ya ubatizo katika Roho Mtakatifu, umepokea baadhi ya vipaji vitakatifu. Vipaji hivi vinatofautiyana kulingana na watu. Kwa vile kuna aina mbali mbali ya utumishi, ni sahihi kuwepo na vipaji vya aina mbali mbali.Kwa kila mmoja, Mungu katoa kipaji fulani kufuatana na kazi aliyopewa. Kwa mfano, watu walio na shughuli mbali mbali , mtu anayefanya kazi katika kanisa na yule anayefanya kazi katika tevisheni , yule anayewahubilia watoto wadogo na yule ambae anamtumikia Mungu katika kazi ya uinjilisti kwa nyimbo au kwa kongamono ama kwa vitabu, n.k. Kwa kila mmoja Mungu anampa vipaji ili kumsaidia kumtumikia vizuri zaidi. Kwa haya ifutao, inatupasa tuelewe kuwa shamba la Mungu ni kubwa na ni pana. (Zab. 24 :1) ‘’ Ni Bwana ndiye anayeweka mikononi mwake dunia hii pamoja na viumbe vyake vyote, na wakaazi wake wote’’.  Mungu anaweza kukutuma ukamtumikie popote anakotaka. Aidha kwa waislamu, wakatoliki, waanglikana, wapentekote, huko Burundi au Ulaya, kwa wahutu hali kadhalika kwa watutsi au kwa wazungu popote anapotaka, kwani dunia nzima ipo mikononi mwake. Kila mtu ni kiumbe chake. Mungu anapenda sana kila mtu. Je , uko tayari kwenda popote atakapo kutuma ? au bado unasema kwa jina la Bwana , nataka kubaki katika kanisa langu, na nchini mwangu  n.k. ? 

 

Mungu ni Baba na anmpenda kila mtu , sisi ni watoto katika malisho yake. Lazima tumtii kwa kila kitu na popote. Na tusisahau, vipaji tulivyopewa ni kwa manufaa ya wote.( 1 korin. 12 :7). 

 

Sasa tuvitazame hivi vipaji tofauti : 

 

(1korin.12 :8-11) ‘’Roho Mtakatifu anampa kila mmoja uwezo wa kuongea kwa busara……… kuongea kwa ufahamu…… imani…… kuponya wagonjwa….. kutenda miujiza….. kupeleka ujumbe toka kwa Mungu      uwezo wa kuongea katika lugha zisizofahamika….. uwezo wa kuzitafsiri hizo lugha. Ni Roho Mtakatifu peke yake ndiye anayetoa vitu vyote hivyo, Anampa kila mmoja kipaji tofauti jinsi anavyotaka’’. 

 

Siku hizi wakristo wengi huelekea kudhani kuwa yule asiyezungumza lugha ya kigeni hajabatizwa katika Roho Mtakatifu. Wanasahau kwamba kuzungumza kwa lugha ni mmoja ya vipaji. Mwingine an kipaji cha kuzungumza kwa busara ,na mwingine naye ana kipaji cha imani , mwingine an kipaji cha kutenda miujiza,  kufutia mipango ya Mungu kwa kila mmoja na utumishi wa kila mmoja. Vipaji tulivyopewa na Mungu ni kwa kutimiza kazi yake kwa ajili ya ujenzi wa kanisa lake. Kipaji ni kitu gani ? Ni upeo maalum usio wa kidunia wa kumtumikia Kristo. 

 

Kuna tofauti gani kati ya vipaji vya kiroho na tunda la kiroho ? 

 

Ikiwa vipaji vipo kwa ajili ya utumishi, tunda ni kwa ajili ya mwenendo. Vipaji vinakuwa katika mfumo wa kufanya kazi, lakini tunda ni hali ya maisha. Tunda huonyesha kiufasaha jinsi nilivyo. Wakristo wa Korintho walikuwa matajiri kwa vipaji, lakini , kwa bahati mbaya, walijiingiza sana katika mahusiyano ya kimwili. Vipaji vya kiroho vikageuka kuwa chanzo cha kutofautiyana , wivu, majivuno, na fujo hata katika huduma ya ibada. Kwa hakika , lazima tukiri kwamba mwenendo wa wakorintho bado umo katika makanisa yetu. Kuna wanaochanganya kitu kionekanacho na kukiita cha kiroho na wasitofautishe vipaji vya kiroho na tunda lake. 

 

Mtume Paulo alitoa maoni kuhusu vipaji, ( 1korin.14 :1)’’Basi tafuteni kwanza kuupokea upendo. Mvihitaji pia vya kiroho , hasa ya kupeleka ujumbe uliyopokelewa kutoka kwa Mungu’’. ( 1 korin.14 :5) ‘’Napenda kuwaona nyote mukiongea lugha zisizofahamika, lakini ningetaka tena zaidi mtoe ujumbe kutoka kwa Mungu. Kwa hio, anaetoa ujumbe aina hii ni muhimu kuliko yule anaeongea katrika lugha zisizofahamika , isipokuwa pale ambapo hakuna mtu awezae kufafanua yale anayeyasema ili kanisa nzima liimarishwe katika imani yake’’. 

 

(1 korin.14 :22) ‘’Kwa hiyo, kipaji cha kuongea katika lugha zisizofahamika ni alama kwa ajili ya wasio wauminmi , lakini siyo kwa ajili ya waumini, kinyume chake, kipaji cha kupeleka ujumbe wa Mungu ni alama kwa waumini, na siyo kwa wasio waumini’’. 

 

Tuibebe tunda mahsusi ya kutubu na wale wanaotutazama watapata kiu ya kubadili mwenendo. Tuwe mfano kwa watiifu kwa maneno na kwa vitendo. 

 

Tuzingatie pia vipaji vingine ambavyo Mungu anawapa watumishi wake. Kama tulivyosisitiza kuwa kuna njia mbali mbali za kumtumikia Mungu, sasa tuzungumzie utumishi katika semina ya kikristo kanisani au katika kikundi cha kikristo. 

 

Tuchukulie mfano wa kanisa . Paulo anaonyesha kuwa huenda katika kanisa moja tu kunakuwa na vipaji vingi, kwa kuwa kuna watu wengi. Vipaji vyote hivyo, ni kwa ajili ya kuwasaidia wa kristo kujiendeleza katika imani ( 1korin. 14: 27-28) ‘’Tukianza kuzungumza katika lugha zisizofahamika, inabidi wawili, watatu ama wengi wafanye hivyo, kila mmoja kwa zamu yake, na kuwe na mmoja ambae anatafsiri wanachozungumza. Asipopatikana mtu awezae kutoa maelezo ya aina hii, na kila mmoja wao aachane na kuongea kwa sauti ya juu hadharani, awe anaongea kwa ajili yake tu na kwa Mungu’’.  (1korin.14: 30) ‘’Na kama mwingine anapata maoni hadharani , lazima yule anayefundisha asimame kwa muda ilim maoni hayo yatolewe kanisani’’. 

 

( 1korin.14:40) ‘’ Lazima kila kitu kifanyike katika mipangiliyo’’. (Efe. 4:11) ‘’ Ni Mungu ndiye aliyetoa vipaji maalum kwa wanadamu. Kuna waliyopewa kipaji cha kuwa wafuasi, wengine mitume na wengine wainjilisti, wachungaji au waalimu ‘’. 

 

Kuwa mfuwasi wa Yesu Kristo ni kipaji kutoka kwa Mungu. Mungu amekitoa kwa wamoja na kwa wengine kufuatia mipango yake. Mfuwasi hana sehemu maalum, kwani anakomuelekeza Roho Mtakatifu, ndiko huko anakokwenda. Anazungumzia au kutoa ujumbe kamili. Mungu anamtuma ankotaka, na yeye ni tofauti na mtu aliyepokea kipaji cha kuwa mchungaji. Huyu ametulia, siku zote anakaa pamoja na wanachama wa kanisa. Ana kipaji cha kuongoza na kuwashughulikiya wakristo. Waumini waliopokea kipaji cha kuwa mchungaji huitwa viongozi. Yawezekana kuwa na kipaji cha uchungaji bila ya kuwa mchungaji wa kanisa fulani?  Jibu ni Ndiyo, kwani kuwa mchungaji au kuwa na kipaji cha uchungaji ni kipaji kitolewacho na Mungu kwa mtu anayemtaka. Naweza kuwa na kipaji cha kuongoza katika chama au kikundi fulani. Mungu amenipa kipaji hicho ili niongoze pale ambapo nipo. Kutokana na kipaji hicho cha uchungaji,mimi ni mchungaji katika kazi niliyopewa na Mungu. 

 

Yawezekana kuwa kiongozi wa kanisa bila ya kuwa Mchungaji? Jibu bila shaka ni Ndiyo. Kwani baadhi ya viongozi wa ma kanisa walipokea uchungaji kwa kuwekewa mikono na rafiki zao au wanadamu wa familiya yao. Kwa mfano, kama baba yangu ni kiongozi wa kanisa moja na akiwa ana mtoto mmoja aliyeponywa ambaye angetaka amsaidie katika kazi ya Mungu. Wakati anapoomba kwa ajili ya mtoto wake na kuweka mikono ili awe kiongozi wa kanisa fulani, huyu muumini , kwa kweli anacho kipaji cha kuwa Mchungaji ? Kwa sababu kipaji hiki hutolewa na Mungu tu peke yake wala si mwanadamu awye yote hata kama ni Askofu wa aina gani. 

 

Baadhi ya watumishi wa Mungu ni viongozi wa makanisa , lakini siyo wachungaji, kwa sababu kuwa Mchungaji ni kipaji cha Mungu kama kilivyo kipaji cha kufundisha , kuhubiri au kipaji cha mfuasi. Baadhi wanaonekana kudhani kuwa viongozi wana vipaji vyote, siyo kweli ! Kazi ya Mungu imegawanywa, na ndiyo maana waumini wote hushirikiana katika kanisa au katika kikundi cha kikristo. 

 

Kiongozi ( Mchungaji ) huhitaji muumini (Mfuasi) naye pia humuhitaji muumini (Mtume ) . Muumini anahitaji kipaji hicho cha Mchungaji ili atimize kazi ya Mungu kwa kufuatia Mungu mwenyewe. Ni bahati mbaya kuona siku hizi ni vigumu sana kutofautisha viongozi na wachungaji. Watu huonekana kudhani kuwa kiongozi yeyote wa kanisa au wa kikundi cha kikristo ni Mchungaji wa kweli. Baadhi huwa wachungaji kwa kupitia ndugu zao lakini siyo kwa kipaji cha Mungu.Baadhi huitwa wachungaji wakati ambapo wana kipaji cha kuwa wafuasi. Ni kikwazo kikubwa katika kazi ya Mungu, kwani wana kipaji walichopewa na Mungu, lakini wanafanya kazi wakitumia kipaji wasiyokuwa nacho, yaani katika kufanya kazi ya Mungu wanatumia kipaji ambacho Mungu hajawapa.Naomba Roho Mtakatifu aweze kuuangaza ujumbe huu, ili sote tuweze kuona vizuri nafasi zetu na vipaji tulivyopewa na Mungu. Kila mtu aweze kujichunguza na kuhakikisha kuwa anafanya kazi ya Mungu kulingana na kipaji Mungu alichompa kwa ajili ya kazi hiyo, ama la, na Mungu atatubariki. 

 

Kaika ushuuda wake, mwanamke mmoja aliwahi kutuambia hivi : ‘’ Mimi nampenda sana Bwana Yesu,  kanisani nahubiri habari njema na watu wengi wanatubu dhambi zao na kumpokea Yesu. Lakini nyumbani kwangu huko ninako kaa, mimi ni mwanamke mwenye hasira za ajabu , nyumba nzima wananijua na hata majirani wananijua’’. Hapa tunaona mfano wa mtu ambae ana kipaji cha kufundisha  vizuri tu, lakini pamoja na hayo, alikuwa na ushuhuda mbaya sana nyumabani kwake. Hakuwa na matunda mazuri. Mungu humpa vipaji kwa anayemtaka kufuatana na kazi ambayo Mungu mwenyewe anataka itimizwe kwa ajili ya ujenzi wa kanisa lake. 

 

 

                                      TUNDA LA ROHO 

 

Tunda la Roho ni nini ? Tusome Wagalatia 5 :22 ‘’ Tunda la Roho ni unyenyekevu, furaha, amani, upendo, utiifu, upole’’. 

 

Ikiwa tunasema kwamba tunaye Roho Mtakatifu ndani yetu, lazima wengine wachunguze tunda lake , na tunda lake lenyewe lionekane.Mtume Paulo anaonyesha wazi kwa wakorintho kwa kusema : ‘’Wakati nitakapozungumza lugha za kibinadamu na za malaika, nikiwa mnyenyekevu , nikiwa sina imani  sina kitu, mimi ni kama chombo kitowacho mngurumo. Nitakapopata kipaji cha unabii na nitakapofahamu maajabu yote, sayansi, na nitakapopata imani kamili ya kubeba milima , nikiwa sina upendo nitakuwa si kitu cho chote. Nitakapogawa mali zangu kwa ajili ya kuwahudumia masikini, nitakapotosa mwili wangu motoni, nikiwa sina imani, nitakuwa si kitu’’. 

 

Hapo tumeona kuwa vipaji hutoka kwa Mungu mwenyewe kwa matakwa yake, lakini tunda ni muhimu sana kwa maisha ya muumini . Mtume Paulo anasema kwamba vipaji hivyo vitakwisha ( Korin.13 :8) ‘’ Ujumbe zilizopokelewa kutoka kwa Mungu zitakwisha siku moja, kipaji cha kuzungumza kwa lugha zisizofahamika kitakwisha, ujuzi nao utatoweka’’. Tunda muhimu katika maisha ya muumini ni imani au upendo, kwani tunda hili huwezesha kumtumikia Mungu. Nikitenda miujiza, nikaponya wagonjwa, nikahubiri usiku na mchana, na kama nitatoa mali zangu nikawapa masikini, hata nikatoa mwili wangu ukachomwakwa moto, pamoja na vyote hivyo, kama sina upendo , Bibliya inaniambia kwamba mimi si kitu. 

 

Upendo ni muhimu sana. Upendo ni milele , upendo hutuepusha na dhambi za aina yote, kwani bila upendo hakuna kinachoendelea. Upendo ni mvumilivu, haujioni, hauna majivuno, upendo hautendi cho chote cha aibu, si mchoyo, haukasiriki wala kujijengea chuki. Upendo unafurahia ukweli. Unyenyekevu pia ni kipaji kutoka kwa Mungu. Paulo anawalika wakristo kwa kutafuta imani kuliko kipaji kingine cho chote, kwani vipaji vingine vyote vitakwisha siku moja. Imani ni kubwa kuliko kipaji kingine .( Imani na Tumaini, imani inachukuliwa kama lengo la kikristo). 

 

 

 

Mtume Yohana, yeye, anaweza kuunganisha upendo pamoja na na uwepo wa Mungu, ili kama tunapendana, Mungu hua pamoja nasi.( !Yoha.4 :8 na 21)’’ Asiyempenda ndugu yake hamfahamu Mungu, kwani Mungu ni upendo…….Ampendae Mungu, lazima ampende pia ndugu yake’’. 

 

Lakini moyo wenye Roho ya Mungu huonyesha furaha, amani, upole….. na tunda la upendo huonekana katika kila hali. Kwa hiyo, tunda ni watu wengine wa nje wanaoweza kuliona na kuthibitisha hilo kwa kuwa wanaona mwenenendo wako. 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

SURA YA III 

 

UKARABATI WA KIROHO 

 

Katika kurasa zilizopita, tumezungumzia mambo mengi, na sasa mmepata kujua ni mguu gani unaocheza vizuri tuliweza kuwaambia juu ya wokovukatika YesuKristo, ubatizo wa maji na ubatizo wa ndani ya roho mtakatifu. Kama sura inavyosema, ukarabati ni kitu kingine muhimu sana katika maisha yetu ya kila siku. Unaweza kuwa na nyumba nzuri lakini bila kuikarabati mara kwa mara itaharibika mapema. Hata kama ukiwa mrembo, pia unatakiwa kuoga kila siku, kwani uharabati ni wa siku zote. Hata katika mambo ya kiroho, ukarabati ni wa muhimu. Rafiki, ukristo ni hazina toka juu. Ukarabati wake unaitwamaombi kwani ibilisi anafanya kila njia ili tuweze ili tuweze kufuata njia sahihi ya Mungu. Tuwe macho, soma mara zote Biblia, itakusaidia kuyaelewa maandiko. Kama ibilisi aliweza kumjaribu Yesu, ambaye ni Mungu, je si zaidi kwetu? Kwa kuwa Yesu alimshinda shetani, atatusaidia pia kumshinda. 

 

Wokovu mlioupata ni kama dinari ndani ya mikono yenu. Pia ni chombo cha kazi ndani ya shamba la Mungu. Iwapo jembe jipya litakuwa bila kazi yoyote, litapata kutu na kuwa chombo kisicho na faida. Lakini kama kitaweza kutumika mara kwa mara, kitaanza kuwa kikali hatua kwa hatua. Kama unamtumikia Mungu kwa kuwashuhudia wengine juu ya kile ulichopokea, utakuwa zaidi kiroho. Usifiche talanta yako (Math 25:24 – 30) Wakati bwana aliporudi kutoka safari, alianza kukagua hesabu ya matumizi ya mapato ya fedha yake. Wakwanza aliyekabidhiwa tano alikuwa na talanta kumi, wa pili aliyekabidhiwa mbili alikuwa na nne, wa tatu aliyekabidhiwa talanta moja aliifukia ile ile moja ndani ya mchanga. 

 

Mungu hakukosea alipokukabidhi talanta tano (naweza kusema ni njia mbalimbali za kumtumikia Mungu) anajua kwa nini amempa kila mmoja kadiri awezavyo, Bwana atarudi kukagua kile tulichokifanya kupitia wokovu aliotupatia. Yawezekana ukawa na ujuzi wa kazi nyingine au ukawa ni mgonjwa, ambaye yupo kitandani siku zote umelala vyovyote ulivyo, Mungu ataomba ripoti ya kazi uliyotenda mahali alipokuweka. Mungu atusaidie kuwaleta wengine kwa Kristo. Kutokuwa na malipo mazuri kwa mtumishi mwaminifu. Mungu alisema Mathayo 25:21 “Nitakukabidhi makubwa njoo ufurahi pamoja na Bwana wako” 

 

Wakati bwana alipoomba ripoti kwa mtu wa tatu, hivyo alijibu “Bwana najuwa wewe ni mtu mgumu, wewe huvuna pale ambapo hukupanda, na hukusanya pale ambapo hukutawanya. Niliogopa, nikaficha fedha yako Katika ardhi chukua basi mali yako. Bwana alijuwa Kwanini amemkabidhi talanta moja mtumishi alimshitaki Bwana wake, pia kumtukana, japo yeye alikuwa mvivu ,alijuwa kile Bwana wake alichopenda afanye, lakini hakuweza kufanya, ndipo Bwana wake akasema “mtumishi mbaya na mvivu …! Mnyang’anyeni alichonacho….. mtupeni nnje’’ (Matayo 25:30). Tusiwe watumishi wabaya na wavivu, bali tuige mfano wa mtume Petro, yeye baada ya kukutana na Bwana  aliendelea kufanya shuguli zake za kila siku alikwenda mjini na vijijini kwa wasiomjua Mungu na kuwatangazia wokovu wa kweli Kwa muda mrefu alihubiri hata kwa machozi. Mdo 20:31 “kwa hiyo muwe macho mkikumbuka Kwamba kwa muda wa miaka mitatu usiku na mchana, Sikuchoka Kumwona kila mmoja wenu kwa machozi. Paulo hakuwa mvivu alitega muda mwingi kwa kuhubiri habari njema na pia alikuwa na muda wa kutafuta maitaji yake (Mdo:20:33 – 34). Tumegunduwa kwamba kuwa siku hizi waKristo wengi kwa njia hiyo wanakuwa wavivu, mtume Paulo alikuwa akifungwa mara kwa mara, lakini hakukata tamaa, hata ndani ya gereza bado alihubiri kwa waliokuwa Karibu naye na pia waliokuwa mbali. Aliandika kwa Timotheo “Hubiri huo ujumbe, sisitiza kuutangaza uwe ni wakati uliofaa na usiofaa. 2 Tm 4:2” 

 

Inabidi kujenga mazoea ya kukarabati utu wetu wa ndani mara kwa mara, bila ya kufanya hivyo twaweza kupoteza kila kitu. Angalia hata afya yako kama hujapata chakula kwa muda mrefu, ni wazi kuwa afya yako itakuwa na matatizo, na hata unaweza kufa kwa njaa. 

 

Mtume Petro alihakikisha ya kuwa, tunapovaa vazi la ukristo, ni lazima tuwe na kitu kingine cha kukufanya uwe timilifu, na pia kutafuta kutafuta kitu kingine chenye chenye uthamani wa hali ya juu. Kwa hiyo ni lazima kuweka bidii katika mambo yote. Tunaweza kujiuliza ni kwa nini tuwe na bidii? Biblia inasema “Mkiwa na sifa hizo zote kwa wingi, zitawawezesheni kuwa watendaji na kupata faida katika kumjua Bwana wetu Yesu Kristo. 

 

Mtume Paulo alikuwa na bidii ya neno la Mungu, hakuogopa kufa. Siku moja Roho Mtakatifu alimwonyesha vile atavyofungwa na wapagani Yerusalem. Wengi walimsihi asiende ili asiweze kukutana na matatizo hayo, akawajibu “Kwa nini mnalia na kutaka kunivunja moyo? Niko tayari, mimi, sio tu kwa kufungwa, lakini hata kufia Yerusalem kwa ajili ya Bwana Yesu” (Mdo 21:13). 

 

Wengi wanaweza kukuvunja moyo kwa kukuambia kuwa umezidi kuomba, kushuhudia, nk …….. lakini uwe na bidii kwa ajili ya Bwana Yesu Kristo, yeye atakayekuja kukagua kile unachofanya. Mungu awasaidie. 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

UTULIVU NDANI YA MOYO  

 

Utulivu ni jambo muhimu katika tabia ya mtu aliyeokoka. Siku moja Yesu aliwauliza wanafunzi wake “Watu wasema nini juu ya mwana wa Adamu?” wakajibu, “ “Wengine wanasema wewe ni Yohana mbatizaji, wengine wanasema wewe ni Eliya, wengine eti wewe ni Yeremia au mtume mwingine”. Yesu akauliza tena, “Je nanyi mwaniitaje? Simony Petro akajibu, “Wewe ni Masiya, mwana wa Mungu aliye hai”. Simoni Petro alimjua vizuri Bwana wake. Biblia haikuonyesha mawazo ya wanafunzi wengine (labda na wao walidhania Yesu alikuwa mmoja wa mitume. Huo ni mwono wangu binafsi). 

 

Yesu alimwambia Simoni Petro, “Unaheri …….. kwani kwani hukufunuliwa na mwanadamu ukweli huu, bali baba yangu aliye mbinguni”. Simony Petro alipata ufunuo kutoka juu kuhusu Yesu Kristo, Mungu asifiwe. Nawe unaweza kupata ufunuo huo. Yesu alisema “Wewe ni jiwe na juu ya jiwe hilo nitalijenga Kanisa”. Kanisa la Mungu lina msingi imara. Bwana anatukumbusha juu ya mtu mwenye hekima aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba ili iwe imara zaidi ya yule aliyejenga juu ya mchanga. 

 

Tunajua ya kwamba Kanisa la Mungu (Siyo majengo bali ni mhristo imara) atapitia matatizo, lakini tunaamini ndani ya Yesu kuwa tutashinda mpaka mwisho wa safari yetu ya mbinguni. Kanisa la Mungu limejengwa imara juu ya mwamba, ambaye ni Yesu Kristo. Mtume Petro aliandika (1 Petro 2:5) “Ninyi wenyewe, kama mawe yaliyo hai, mkajengeke na kuwa nyumba ya kiroho ambamo mtanitumikia. Kama nyumba imejengwa kwa mawe imara, nyumba hiyo itakuwa imara pia, lakini nyumba ikijengwa kwa mchanga haitakawia kuanguka. 

 

Muwe wakristo imara ambao hamtajali chochote cha kuwarudisha nyuma. Hata ule upepo unaoweza kujiita wa kiroho usiwapeperushe. Baada ya Petro kutubu, Yesu alianza kuwafunulia wanafunzi wake juu ya mateso atakayopitia kabla ya kuangukwa msalabani, na juu ya ufufuo wake. Petro baada ya kumsikiliza alimchukua kando na kusema “Isiwe hivyo Bwana, jambo hili halitakupata! Lakini Yesu akageuka na kusema “Ondoka mbele yangu shetani” Mathayo 16:22 – 23. 

 

Baada ya kuhakikisha kuwa mtume amepata ufunuo toka juu tena mzuri, Mungu anamfanya kuwa chombo cha kumpigia shetani. Katika mambo ya kiroho; tunashangazwa na vile Petro alivyoitwa shetani, wakati kabla ya hapo aliitwa mwema. Shetani alitaka kumtumia ili Yesu asiende msalabani. 

 

Bwana alitoa uamuzi papo kwa papo na kusema “Rudi nyuma yangu shetani”. Unaweza kuamini kwamba Petro yule yule aliyeambiwa na Yesu kwamba “Wewe ni jiwe na juu  yako nitalijenga Kanisa”, Petro yule yule anageuka kuwa chombo cha kutumiwa na ibilisi. Wakati huo huo anatakiwa kutumikia Kanisa kwa ajili ya utukufu wa Mungu? Simony Petro aliyeitwa kuifanya kazi ya Mungu alihitaji badiliko ndani na nje na ndicho kilichotokea. Sisi pia tunatakiwa kumpenda Bwana, ikiwezekana hata kuambatana naye hata msalabani. Ni lazima utu wetu wa ndani na kwa midomo yetu tukiri na kwa vitendo kuwa tutaendelea kuwa waaminifu kwa Bwana. Mungu aêwe sifa. 

 

Petro alimwambia Yesu, “Hata wengine wakuache, mimi sitokuacha kamwe”. Maana yake ni kwamba “Hata kama itabidi kufa pamoja nawe, sitakuacha”. Hapa Petro alikuwa anamaanisha kuwa alimpenda Bwana pia alitamani kumfuata popote bila mipaka. Tukichukulia mfano wa mambo aliyoyafanya Petro, tunaona vile alivyompenda Bwana kwa upendo wa dhati, lakini yeye mwenyewe hakuweza kujitambua yeye mwenyewe ni nani? Alitakiwa kulipa gharama kwa kumfuata Yesu. Biblia inatuambia; pale Yesu alipowachukua wawili kati ya wanafunzi na kwenda mlimani kuomba, Yesu alisema, “Roho yangu ina huzuni hata kufa, kaeni hapa mkeshe pamoja nanyi”. Yesu alikuwa akimpenda sana Petro, alikuwa mtu mwema, lakini alikuwa anajua udhaifu. Petro alikuwa mtu mwema lakini dhaifu! 

 

Tuwe imara katika imani ndani ya Yesu, narudia nyumba ya Mungu haiwezi kujengwa na watu waliojaa tamaa. Ili tumfuate Yesu popote, siwezi kujua ni gharama gani nitakayolipa katika kumfuata, ila ninachoamini ni kwamba mtapitia matatizo mbalimbali yatakayoimarisha na kuonyesha msimamo thabiti kwa Bwana Yesu. Mungu anataka ujitambue kuwa wewe ni mkristo wa aina gani. Tusiwe kama Petro aliyekuwa anabadirika nyakati mbalimbali hasa wakati wa matatizo. Tuwe kama Daniel ambaye hakukubali kuutoa uhai wake kwa vitu viharibikavyo, kutukanwa, matatizo, vilio nk. Vyaweza kututenga na Kristo? Endelea kumng’ang’ania  kwani bila yeye twaweza kupotea bila ya kupata msaada wa mtu mwingine. Kwa nini Petro alimkana Yesu mara tatu, japo alishuhudia mbele ya Yesu kuwa hata muacha? Inamaanisha kuwa alikuwa na tabia ya kutojiamini. Alikuwa akiongozwa na tamaa zake, mwenendo wake au kuwa na msimamo kamili, alikuwa kama watu wengine wanoongozwa na tamaa zao wenyewe. Inawezekana akapata ufunuo toka juu, lakinianaweza pia kuweka pingamizi. 

 

Wako tayari kusema na kuchukua maamuzi ya haraka bila kufikiria. Hali kama hiyo yaweza kuleta matatizo katika kazi ya Mungu. Petro alijiamini lakini alikuwa mtu mwenye maamuzi ya haraka. Tumuombe Yesu alete mabadiliko katika maisha yetu, ili tufanyike vyombo imara kwa kulijenga Kanisa, hivyo basi tuwe imara na kuendelea kufanya ukarabati ndani na nje ya miili yetu. Tusiwe kama Petro, ili tuweze kukamilisha kusudi la Mungu katika kazi yake. 

 

 

 

 

 

LUGHA 

Mungu alimuumba mwanadamu na kichwa ambacho juu yake kuna viungo 7, macho 2, mashavu 2, masiko 2 na kinywa. Hapa tutazungumzia yale yahusuyo kinywa, ulimi, midomo, mawaidha, maneno nk ….. sehemu ya utu wetu inayounganishwa moja kwa moja na maisha yetu ni “ulimi na siyo maneno” 

 

Siku moja mgeni alikuja nyumbani kwangu na kuanza kuhubiri neno la Mungu. Tulipokuwa tunaendelea na maongezi, nilianza kuelewa hali ya moyo wake, na ndipo nikamuuliza swali, “ni kitabu gani umepata maneno haya unayonifundisha? Kupitia swali hilo alijua kuwa nimeshamgundua 

 

Ni kupitia maneno yetu ndipo tunapojulikana wazi vile tulivyo kiroho. Biblia inasema, “Mathayo 12:35, mtu mwema hutoa mambo mema katika hazina yake njema; na mtu mbaya hutoa mambo mabaya katika hazina yake mbaya”. Tena Biblia inasema, “….mti unajulikana kwa matunda yake” Mathayo 12:31. maneno yatokayo vinywani mwetu hututambulisha vile hali yetu ya kiroho ilivyo. Yesu alisema, “Siku ya hukumu kila mmoja atatoa hesabu ya maneno yake. Mathayo 12:36 na anaendelea mstari wa 37 ……… maana kwa maneno yako utakubaliwa kuwa mwadilifu, na kwa maneno yako utahukumiwa kuwa na hatia”. 

 

Na katika ufunuo wa Yohana, tunasoma hivi “Uf 20:12 ….. kisha nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo wamesimama mbele ya kiti cha enzi na vitabu vikafunguliwa ……. Wafu wakahukumiwa kulingana na matendo yao kama ilivyoandikwa ndani ya vitabu hivyo”. Maneno yetu yote yatahukumiwa, tutahukumiwa sawa na maneno yetu. Mistari hii inatujulisha kwamba, mbinguni kuna anayeandika kila jambo tutendalo, iwe kwa maneno au kwa vitendo. Tuwe makini. 

 

Mtunzi wa mashaihiri alisema (Zab 34:11 – 13) “Njooni , enyi wana, mnisikilize,nami nitawafundisha kumcha Bwana .Ninani mtu yule apemdezwaye na uzima,apendaye siku nyingi apate kuona mema ?  Auzuiye ulimi wake na mabaya, na midomo yake kwa kusema hila”. 

 

Neno la Mungu  linatufundisha “kumcha Bwana” hili lina dhamana kubwa isiyo na mwisho. Ndipo mtunga mashahiri anasema “siku nyingi” na “kuana mema” vinaambatanishwa na «  kumcha Bwana ». Kipimo cha kumcha Bwana kina kamilisha kipimo «  chakuona mema »tunayopitiakila siku. Kumcha Mungu kunaanzia wapi? ……..” zuia ulimi wako kwa mabaya na midomo yako kwa kusema uongo”. Hakika kumcha Mungu kunaanzia ndani ya kinywa na midomo yetu. 

 

Hatuwezi kuwa na maisha yenye furaha kama hatutaweza kumiliki vinywa vyetu na midomo yetu. Meth 13:3 inasema “Achungaye mdomo wake huyahifadhi maisha yake, anaye ropoka hovyo hujiletea maangamizi” 

 

 

Nafsi yako ndiyo utu wako. Ni mahali ambapo udhaifu wote unadhihirishwa kwanza na pia shetani anapachezea. Sasa ukitaka kuitunza nafsi yako, ni lazima kuchunga midomo yako isiseme harakaharaka kwani unaweza kupatwa na matatizo. Katika Methali 21:23 imeandikwa; “Achungaye mdomo wake na ulimi wake, hujiepusha na matatizo”. 

 

Tunajua ya kwamba ulimi ni kiungo kidogo, lakini kazi yake ni pana. Yakobo 3:11 inasema; “Je chemchemi moja yaweza kutoa maji matamu na maji machungu kwa pamoja? Hilo ni swali la Yakobo, lakini Mungu akiweka ujumbe wake ndani ya vinywa vyetu, hatuna budi kuchunga vinywa vyetu kwa ajili ya kazi ya Mungu. Tumejitoa kamilifu, kwa hiyo tumtumikie na viungo vyetu vyote. 

 

Tusome Muhubiri 5:2 “Sauti ya mpumbavu ni maneno mengi” 

 

Oh ni mara ngapi tumejaribiwa katika utani, na hata kuongea mambo ya wengine! Na ndipo tunapopoteza nguvu zetu nyingi za kiroho. Maongezi haya yatadhihirisha vile tulivyo, watu hawataweza kukuamini kwani watakufananisha na maneno yako. Mathayo 5:37 “Ndiyo yenu na iwe ndiyo, chochote kinachozidi hayo hutoka kwa yule mwovu”. Mkristo  anayetaka kumpendeza Bwana wake, asiwe mtu aliyetawaliwa na ujanja, pia awe akijiuliza mara zote kitu gani kitaweza kuumbika ndani ya wale wamsikilizao kabla ya kunena. Mungu atusaidie kuyapima maneno yetu. Wakati mwingine Wafarisayo walikuwa wakimuuliza Yesu mambo mengi ya mtego, hali yake ilikuwa ya ukimya, wakati mwingine alikaa kimya bila kujibu neno. 

 

Mtume Paulo anawashauri Wakorinto; “Mtu asijidanganye mwenyewe;kama mtu akijiona kuwamwenye hekima miongoni mwenu katika dunia hii,na awe mpumbavu,ili apate kuwa mwenye hekima .» (1 Kor 3:18); Na kwa Warumi anasema “maana utii wenu umewafikilia watu wote ;basi nafurahi kwa ajili yenu,lakini nataka ninyi kuwa wenye hekima katika mambo mema na wajinga katika mambo mabaya. ‘Rum 16:19”. 

 

Utawezaje kutunza siri kama hujaweza kuuzuiya ulimi wako? Ndani ya Kristo ni lazima kusema kweli daima. Unaweza ukaulizwa swali, kama hutakuwa na uhakika, kaa kimya, sio lazima ujibu, na iwapo utakuwa na jibu sahihi, basi jibu kwa adabu na hekima. Tunapenda watu waamini ukweli na siyo uongo; Yoh 8:44”. Ninyi ni watoto wa Baba yenu ibilisi, ……….. yeye ni mwongo na baba wa uongo……..” 

 

Anayesema uongo ni mwana wa ibilisi. Mungu atusamehe na atufundishe kusema kweli katika kila jambo siku zote. 

 

Kama unataka kuwa mkristo safi na kupenda kumpendeza Bwana wako usiku na mchana, chunga ulimi wako na uongo, na kusema kwa kiasi, hepuka kitu chochote kinachofanana na ugomvi. 

 

(2 Tim 2:24) “Tena haimpasi mtumwa wa Bwana kuwa mgomvi;bali kuwa mwanana kwa watu wote,awezaye kufundisha,mvumilivu.”    

 

Tuenende mbele za Bwana kwa utakatifu aliotuachia. Kujichunguza mara kwa mara, na pia kujizuiya vinaweza kupunguza au kuondoa kabisa tabia ya masengenyo na utani usiofaa, na kufumbia tabia njema. Kujizuiya pia kutafagia kila tendo baya katika kumtumikia Yesu Kristo. 

 

“Ulimi una nguvu ya kufanya hai na kuua wanaopenda kuutumia watakula matunda yake. (Methali 18:21). 

 

Ni kufa, au kuishi, yote mawili yapo ndani ya uwezo wa ulimi, vyo vyote utakavyo utumia , lakini tunavuna matunda yake. Kama matunda yake ni matamu, tutakula matunda hayo matamu, lakini yakiwa machungu, tutakula pia hayo matunda japo ni machungu. Matunda yote haya yatatokana na hali ya ndani ya mioyo yetu. Roho yako ikiwa safi, basi utasema maneno mazuri, lakini ukiwa na roho chafu, basi utasema maneno mabaya. Yakobo alisema; “Kama mtu akijiona kuwa ni mtu mwenye dini, lakini hawezi kutawala ulimi wake, dini yake haifai kitu, na anajidanganya mwenyewe Yakobo 1:26”. 

 

Tunaweza kuwa washika dini, wafuasi wa ibada zote, kuimba tenzi na kutimiza mambo yote tunayosikia katika dini. 

 

Ndani yake, kila kitu ni kizuri: lakini lkama hatutaweza kuudhibiti ulimi, dini yetu haitakuwa na dhamana inayokubalika mbele za Mungu. Mungu anatusaidia kuchunga ndimi zetu! 

 

Inawezekana kufuga ulimi? Yakobo 3:7 – 9 imeandikwa: “Binadamu anaweza kuwafuga wanyama, na amefaulu kufuga viumbe vyote – wanyama wa mwituni, ndege, nyoka na viumbe vya baharini, lakini hakuna mtu aliefaulu kufuga ulimi. Ulimi ni kitu kiovu, hakitawaliki, na kimejaa sumu inayoiva”. Ni lazima ukubali kuwa yapo mambo ambayo huwezi kufuga wala kuyamiliki kwa ulimi wako mwenyewe. Lakini kuna nguvu moja inayoweza kuchunguza na kuudhibiti ulimi wako kwa mambo mema: nayo ni nguvu ya Mungu kupitia Roho Mtakatifu. 

 

Wakati naliposamehewa na kutakaswa, na kukatazwa kutoutumia ulimi kwa ajili ya dhambi, ni lazima kuambia dhambi: “Hutaweza kutumia ulimi wangu; nakukataa”. Ila mwambie Roho Mtakatifu kuwa tangu sasa nakuachia ulimi wangu uutawale, mimi siwezi”. Sasa mgeukie Mungu naku sema: “Bwana nakupa ulimi wangu; naunyenyekesha kwako, nakuomba uuchunguze pamoja na viungo vingine ambavyo nimeshindwa kuvichunguza”. 

 

Ndugu, dada, njia ambayo umeanza kuifuata, ina safari ndefu, ni lazima kufunga mikanda vizuri. Kama hutaweza kuyatawala maneno yako na kuamua kuacha kutoa siri za watu wengine, na ulimi wako umeutiisha kwa mambo ya kiroho, ni lazima utafanyika kuwa chombo cha Bwana. Tusimame katika zamu zetu ili tuweze kukata mawasiliano na kila neno baya linaloweza kuharibu kazi ya Mungu ndani yetu. Ulimi wako ni chombo kizuri kinachoweza kumtukuza Mungu kupitia nyimbo, na kutangaza ulimwengu habari njema, na siyo kwa uongo, ugomvi, maneno machafu, nk …….. 

 

 

 

KUWA NA KIASI  

Mnajuwa yakuwa miili yetu ni watumishi kwenu, na siyo Bwana zenu? Tunajua kwamba Mungu alitupatia nafsi, Roho na Mwili. Ni lazima vitu hivi vitatu viwe safi kwa Mkristo mwaminifu wa Yesu Kristo. Siku moja Yesu Kristo alikwenda kuomba katika bustani ya Getisemane na wanafunzi wawili. Ni kitu cha kawaida mtu kusinzia usiku. Lakini Yesu alisema, “Roho yangu ina huzuni hata kufa, kaeni hapa na mkeshe pamoja nami”. Yesu hakuwaomba kufanya jambo kubwa, bali kukesha tu! Lakini wanafunzi hao hawakukesha hata saa moja pamoja naye, huku walitakiwa kukaa pamoja na Yesu usiku mzima wakiomba. Ni lazima kuitiisha miili yetu. Yesu akawaonyeha ni jinsi gani hawakuwa na utii. “Roho I radhi, bali mwili ni dhaifu”. 

 

Itasaidia nini Roho ikiwa radhi kama mwili hauwezi kile ROHO INATAKA? Mwili ukiwa dhaifu, roho yenye utayari haiwezi kutuchangamsha. Kama mmeitwa kukesha pamoja na Bwana, ni lazima mwili na roho viwe na utayari. 

 

Mwili una pingamizi, lakini mtumishi mwema ni yule anayeufanyisha mwili wake mazoezi ili kumtumikia Mungu vizuri. Mazoezi haya yanatakiwa yawe ya kila wakati, iwe katika matatizo au la, ili uweze kuwa tayari kwa kazi iliyo mbele yako. Paulo anasema katika barua zake kwa Wakorinto, waweza kuitumia miili yao kwa nguvu, wakati mwingine alikuwa mgonjwa kwa sababu ya baridi, kwa kukosa chakula, kwa kuchoka nk ….. lakini katika hayo yote tunaona vile kazi ya Mungu ilivyoendelea kukua kwa mfano wa kuigwa. Mkristo mzuri ni yule anayetenga muda wake kwa ajili ya kuomba hasa nyakati za usiku. 

 

Tunaona jinsi Yesu mwenyewe alitenga muda mwingi kuomba. Tunatakiwa kutoa usingizi wetu kwa ajili ya Bwana  japo wakati mwingine miili yetu inahitaji kupumzishwa. Tukumbuke ya kwamba miili yetu inatutumikia na siyo kututawala. 

 

Inapofika saa sita mwili unakukumbusha kuwa huwezi kuendelea kufanya kazi huku una njaa. Kwa nini ukubali? Sema hapana, nitendelea kufanya kazi. Siyo mwili wako unaoweza kukulazimisha juu ya kitu unachoweza kufanya mwili, bali wewe ndiye unayetakiwa kuwa mkuu wa viungo vyako. Wakati mwingine unapomaliza kula, utaweza kusika mwili wako bado unadai, unataka chakula kingine, tena, tena na tena ……… kwa nini? Usilisikilize tumbo lako. (Angalisho). Sisemi usitengeneze mwili wako, nasisitiza kuwa, iwapo kazi ya Mungu itahitaji kupunguza tamaa za miili yetu na matakwa yake hatuna budi kutii. Tumekwishaona ya kwamba Roho na miili yetu vinatakiwa kuwa na utayari kwa kazi ya Mungu. 

 

Lakini wakati mwingine miili yetu inakuwa kikwazo kwa kazi ya Mungu. Katika Marko 3:20 tunasoma ya kwamba Yesu alifanya kazi mpaka kuisha muda wa kula chakula. Ikiwezekana, zoesha mwili wako kutokula. Kumbukeni Yesu na mwanamke Msamaria kando ya kisima cha Yakobo, ulikuwa wakati wa chakula cha mchana (saa sita). 

 

Yesu hakumuuliza mwanamke kwa nini hakuweza kuwa nyumbani kwake saa zile! Na watu wa nyumbani mwake au kwa nini hakupumzika kwani jua lilikuwa kali, bali Bwana alitaka kuiponya Roho yake kwani ndiyo iliyokuwa chanzo cha matatizo aliyokuwa nayo. Yesu alipenda kutangaza mara zotekuwa chakula chake ni kufanya kazi ya yule aliyemtuma. Tujifunze kuitiisha miili yetu kwa chakula, ili ifikapo wakati wa kufunga na kuomba tusiweze kupata matatizo yatokanayo na kukosa chakula. 

 

Wakristo wanatakiwa kufunga, kama kuna ulazima wa kufanya hivyo. Kuna tatizo ambalo linaweza kukulazimu kuomba na kufunga kwa kipindi kirefu. Paulo anasema: “Nimefanya kazi na kutaabika, nimekesha bila usingizi mara nyingi, nimekuwa na njaa na kiu mara nyingi, nimefunga na kukaa katika baridi bila nguo. (2 Kor. 11:27)”. Tuangalie kitu kingine hatari hapa. Wakati wa magonjwa, mwili unakuambia kuwa huwezi kufanya chochote, ila unatakiwa kulala tu kitandani tu. 

 

Uamuzi gani? Watumishi na wakristo wengi wanapunguza bidii katika kuifanya kazi ya Mungu. Siyo vizuri! Paulo angewezaje kukamilisha  iliyokuwa mbele yake endapo angeendelea kupumzika kila alipokuwa akijisikia kuumwa, pia Timotheo aliyekuwa na vikwazo mara nyingi? Ni wajibu wetu kufanya uamuzi wa busara pale miili yetu inapougua au wakati wa uzima, lakini pia haituzuii kutoitiisha, na kumsikiliza Bwana wetu kwa kile anachotuomba tukifanye. Tena kuitiisha katika amri tulizopewa na Bwana wetu Yesu Kristo, ili tumtumikie kwa kuwa sisi ni mali yake. Bwana ndiye aliyeumba miili yetu, na aliweza kuifanya itutumikie, sasa basi hatuwezi kumtukuza Mungu ipasavyo bila kuitiisha kwanza miili yetu. Hebu tuchangamshe akili zetu kwa kuangalia michezo ya mbio, “Kila mkimbiaji anaepuka kila aina ya kitu kitakachomfanya asiweze kukimbia inavyopasa”. Paulo anasisitiza juu ya kiasi kwa kila mtu anayepigania kupata thawabu ni lazima azoee kujichunguza yeye mwenyewe na kujinyima starehe wakati wa mazoezi ya michezo. 

 

Wakati mpiga mbio anapoanza kukimbia, ni lazima aheshimu kanuni za mbio ili aweze kukubalika. Ina maana gani? “Kuwa kinyume na uvivu?” labda mwili wako unasema: nataka hiki au kile, sawa, iwapo  umekwishaungana na wenzako kukimbia, ni lazima kulazimisha mwili wako kupenda kazi hiyo. Hapa mwili unatakiwa kuwa na uangalizi uliyo imara ili kuwa bidii. Uhuru wako ni lazima uwe na mipaka. Mkimbiaji hashiriki katika mbio ili kujitosheleza kimavazi, usingizi, katika kupumzika, katika kujifurahisha, nk ……… lakini amejiunga na michezo hiyo ili kutimiza kazi moja tu, ile ya kukimbia ili aweze kupata thawabu. Mungu asifiwe. Siyo mchezo wa kawaida, ila ni kazi kubwa! “Na yote hayo ni ili kupata taji ya ushindi”. 

 

Ili uweze kupata taji hiyo, ni lazima uwe na utii wa hali ya juu, kuwa upande wa Paulo yeye aliweka bidii katika utii kwani alitaka kutimiza lengo la kazi yake, alipiga mbio mpaka mwisho. Mtume Paulo alifaulu katika huduma yake kwa sababu alipenda kuutiisha mwili wake na njaa, kiu na mambo yasiyofaa nk …… 

 

Bwana wetu aliacha mbingu ili afe msalabani kwa ajili yetu, ni lazima miili yetu itutumikie ili na sisi tuwezekumtumikia bwana wetu Yesu Kristo. Tena kutumika wakati unaofaa na usiofaa …….. ndugu, dada, tuko katika shule ya Mungu, ni lazima tuwe na mzigo wa kumtumikia, kumfuata popote kuisimamia miili yetu kutatuweka huru ili tuweze kumfuata Bwana. Paulo aliandika kwa Timotheo kufanya mazoezi katika utakatifu kwani ni kitu muhimu katika maisha ya Mkristo. Kwa nini unautumia kwa nguvu mwili wako? Je kwa ajili ya taji iharibikayo au taji isiyoharibika? Kwa nini ujizuie kula au kunywa? 

 

Je ni kwa ajili ya Bwana? Upe mwili wako mazoezi kwa ajili ya Bwana ili uweze kupata taji isiyoharibika kama alivyotuonyesha Paulo. Biblia inatia mkazo juu ya mazoezi ya mwili mzima, lakini mazoezi yenye utakatifu ndiyo yenye thamani kubwa. 

 

Kwa Mkristo, nasisitiza kuwa mazoezi ya viungo (michezo) ni ya muhimu, pia inasaidia katika kazi ya Mungu, mfano, Yesu anaweza kukutuma ukahubiri milimani. Sasa itakuwa vigumu kama hukuwa na tabia ya kuupa mwili mazoezi ya kutembea kwa miguu, ila kwa Mkristo aliyezoea mazoezi hayo hataweza kupata taabu. Muombe Bwana Yesu Kristo aweze kuwabadilisha. Anza kuzoea kupunguza muda wako wa usingizi na utoe japo masaa mawili usiku kwa kuomba, kusifu na kuabudu Mungu. Wakati wa mchana punguza usingizi wa mchana ili usome Biblia na yote ambayo Roho wa Mungu atakayekuonyesha. Katika mwezi au wiki, tafuta siku moja ya kufunga  kwa ajili ya Bwana. Tafuta pia muda wa kukesha ukiomba, ni mazoezi mazuri yatakayoifurahisha mbingu. 

 

 

 

 

 

 

SIRI NDANI YA MAMBO YA UCHUMI 

 

Kama mtu wa kawaida katika dunia hii, pamoja na kuwa Mkristo, ni lazima mtumike ili muweze kumudu maisha. Tunaona tabia ambayo siyo nzuri kwa baadhi ya Wakristo wanaobisha hodi katika nyumba mbalimbali tangu asubuhi mpaka jioni kwa kisingizio cha kuhubiri habari njema. Ni lazima Mkristo awe na hekima katika kila atendalo. Tusisahau kuwa baada ya kufanya kile ambacho Mungu anatutuma kufanya, iwe kuhubiri au kushuhudia, lakini pia baada ya hayo tuwe na muda wa kufanya kazi. 

 

Fanya kazi, usiwe kama kahaba anaweza kulala popote atakapo. Una mahali unapoishi, hubiri injili na rudi nyumbani uendelee na shughuli zinazokupatia kipato ili uweze kuitunza familia yako. Tafuta muda mzuri na usimsumbue mtu. Andaa maisha ya baadaye kwa watoto wako ili wajitosheleze. 

 

Mahitaji yote yanaonyesha ni jinsi gani unatakiwa kutenga muda wako kwa kufanya kazi. 

 

Kuna baadhi ya Wakristo wanaokwenda kuhubiri nyumba kwa nyumba ili baada ya kaziyake aweze kupewa chochote (pesa, chakula, nguo, nk ……) Angalisho!!! Injili inatolewa bure, injili haibadilishwi na chakula, pesa …… kinyume chake ni lazima kutoa injili kwa tajiri na pia kwa masikini kwani ukifanya hivyo Mungu atakupa mahitaji yako. Baadhi ya Wakristo pia watumishi wanafuata njia ya Balama. Huyo alikuwa nabii aliyependa pesa na alikuwa akitoa unabii ili baadaye apewe mshahara. Alikuwa anafanyia biashara huduma ya kinabii. Mungu atusaidie tusimuige Balama! Mtume Paulo alisema; “Mimi nilihubiri kwenu habari njema ya Mungu bila kudai mshahara; nilijinyenyekeza ili nipate kuwakweza ninyi, je nilifanya vibaya? (2 Kor 11:7). Alisisitiza tena katika barua zake kwa Waefeso kwamba hakumkemea mtu. 

 

Anasema tena, “…… katika mambo yetu, nilijichunga ili nisiwe mzigo kwenu, na nitaendelea kujichunga”. Paulo alimjua Bwana wake kwamba ni mwenye nguvu na anaweza kumsaidia. Paulo alitakiwa kukubali msaada wa kiuchumi, kama tunavyoona katika ujumbe huu pale anaposema kuwa alipohitaji fedha, ndugu waliotoka Makedonia walimletea kila kitu alichohitaji. Pamoja na huduma Paulo aliyokuwa anafanya, bado alikuwa na kazi iliyomuingizia kipato ili asiweze kuwategemezi kwa watu wengine. Bali yeye mwenyewe alikuwa na moyo wa kuwasaidia wengine. Wakristo wote wanatakiwa kuwa watayarikutoa hata kama wana kipato kidogo. kupokea bila kutoa kunaleta kupungukiwa. Na kama hatutaweza kuwategemeza wengine  kwa mapato yetu, Mungu atatubariki kidogo tu. Tusome 2 Kor. 6:10 “…… Ingawa tu maskini, twatajirisha watu wengine”. Katika Luka 6:38 imeandikwa “Wapeni nanyi mtapewa ……..” ndiyo amri toka juu. Hiyo ndiyo siri ya Baraka katika mapato. 

 

Wekeza mali zako na vitu vyako katika kumtumikia Bwana. Mtapata baraka sasa na hata katika maisha yajayo. Weka hazina yako pale ambapo hakuna kutu. Usitafute faida yako binafsi, fanya bidii ili kazi ya Mungu ipate kukuwa. Usifanye kazi ya Mungu ili ulipewe, fanya kama Paulo alivyosema kuwa kazi ya Mungu inafanywa bure. Tumepata kwa neema tutoe bure. “Na Mungu wangu atawatosheleza kadiri ya utajiri wake na utukufu katika Yesu Kristo”. 

 

Mtu akiwa na kitu cha kuwapa wengine na afanye hivyo kwa furaha. Hata kama Mungu atakawia kumbariki, wewe endelea kutoa tu. Kupata kitu cha kuwapatia wengine nayo ni baraka. Nilikuwa na umri wa miaka kama 10. mnaona kabisa kwamba nilikuwa bado mtoto, lakini nilikuwa nimekwishampokea Yesu kama Bwana na mwokozi wangu. Katika umri huo nilimpenda sana Bwana, na watu pia. Karibu na nyumba yetu palikuwa na barabara kuu, ambapo walipita watu wengi sana wakitoka sokoni, wengine hospitalini ……. Upendo uliojaa moyoni ulinisukuma kuenda njia panda na kutafuta mtu mwenye njaa ili nimlete nyumbani, na tumpe chakula. Hamu yangu ilikuwa ya kuwatosheleza wengine. 

 

Siku nyingine nilikuwa na pesa za Burundi 50, nikampa mpita njia ili amnunulie mtoto wake mkate. Sikuwa na zaidi ya kiasi cha pesa, lakini nilimpa. Yote hayo niliyafanya ili kumpendeza Bwana wangu. Kila siku nilipenda kuwa muhimu kwa wengine. Neno la Mungu linasema kuwa hatuwezi kusema kwamba tunampenda Mungu huku tukiwachukia watu wa nyumbani mwetu. Upendo wa Mungu unadhihirika katika yale tunayofanya kila siku na majirani zetu au marafiki zetu. 

 

Sikuwa nikifanya hivyo kwa kumuinua mtu, bali kwa utukufu wa Mungu. Kutoa ilikuwa furaha yangu. Neno la Mungu linasema; Luka 6:38: “Wapeni wengine wanavyohitaji, nanyi mtapewa. Naam, mtapokea mikononi mwenu kipimo kilichojaa, kikashindiliwa na kusukwa sukwa hata kumwagika, kwa maana kipimo kile mnachotumia kwa wengine ndicho atakachotumia Mungu kwenu”. Kama ukitoa ni Mungu ndiye atakayekurudishia. 

 

Siku nyingine, kulikuwa na mkutano wa neno la Mungu jirani na kwetu. Wageni waalikwa walitoka sehemu mbalimbali za nchi yetu . Nikamuomba Mungu anipe kibali cha kuweza kuwaalika wageni nyumbani. Niliomba hivi: “Bwana nitumie wageni …… haijalishi watakuwa wangapi. Najua ukimtuma mtu mmoja, basi utaleta posho yahuyo mmoja ukileta watu mia moja utawatoshereza hao watu mia moja. Najua kwamba kila atakayebisha hodi mlangoni kwetu, ametumwa na wewe. Kwa jina lako nimeomba Amen”. Wazazi wangu bado walikuwa wapagani, ila walikuwa wakiona watoto wa Mungu wakija nyumbani kututembelea, waliwazoea wageni. 

 

Mwanzoni mwa mkutano tulipokea wageni wengi kutoka sehemu mbalimbali za nchi yetu. Nilipata ugumu kidogo kwani sikuwa na nafasi ya kuwalaza ndani ya nyumba yetu. Sasa mama akaniuliza swali, “Binti yangu, naona watu wengi bado wako hapa, wamechoka na safari na pia bado wana njaa. Sasa tufanyeje na hatuna chakula cha kuwatosheleza wote!” nikajibu, mama yangu, usihangaike. Nilimuomba Mungu atawatosheleza wote. Kama ameweza kuwaleta, basi atawatosheleza. Sasa usiwe na wasi wasi, tutauona mkono wa Mungu”. Mama aliondoka, nami nikapiga magoti ndani ya chumba changu na kuanza kuomba, kwani swali aliloniuliza mama lilikuwa muhimu. Nikasema Bwana fanya kitu, muda umepita. Watu wamechoka na wana njaa! 

 

Wakati huo huo nikasikia mlio wa gari (dogo) likipiga honi na nikafikiria labda ni wageni wengine wamekuja. Kwa mshangao mkubwa nikaona kumbe ni gari limebeba chakula (mifuko ya ngano, sukari, mihogo, nk …) nikawaomba wageni wanisaidie kunyanyua na kuingiza ndani. Mungu asante. Anasikia maombi yetu, wageni walikula vizuri bila matatizo. Mungu asifiwe, Mungu anajua mahitaji yetu na anajua wakati wake wa kutenda. Toeni mlichonacho na Mungu atajaza kapu lako kwa kipimo cha tele. 

 

Wakristo wengi ni maskini kwa sababu ya uchoyo. Siri ya baraka ni kuwapa wahitaji: toa pia kwa ajili ya kazi ya Mungu, kwa mfano kuwapa watumishi wa Mungu, toa sadaka na fungu la kumi na Mungu mwenyewe atawarudishia. Biblia inasema: Methali 11:24 atowaye kwa ukarimu huzidi kutajirika; lakini bahili huzidi kudidimia katika umasikini. Mstari wa 25 mtu mkarimu atafanikishwa, amnyweshaye mwingine naye atanyweshwa.      

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

SURA YA IV 

 

MATATIZO YANAYOMKUTA MSAFIRI NJIANI 

 

Msafiri ni mtu anayekwenda mahali  kwa sababu zake na kwa nia njema. Kwa maana hiyo sisi sote tu wasafiri tunaoelekea nchi nzuri kwenye makao mazuri tuliyoandaliwa na Bwana mbinguni (Yoh.14:2) “Nyumbani mwa baba yangu mna makao mengi; sasa nakwenda kuwatayarishieni nafasi ……….”. Ni kweli Yesu alikwenda kutuandalia makao, lakini ili tufike, inahitaji bidii, kwani ni safari ndefu. Siyo mchezo, umbali wake unachosha na utaumiza kipindi cha ukame na kipindi cha masika, yote yanamkuta msafiri njiani: jua kali, kiu, joto, njaa, mwanga na giza, baridi, nk ….. ni mambo mengi yanayompata msafiri. Lakini mara zote msafiri anatakiwa awe mwangalifu ili aweze kutimiza kusudi, na lengo. Lengo kubwa ni kufika kule anakotusubiri Bwana harusi. Bwana atusaidie kumaliza safari salama. 

 

Kutokana na matatizo yote hayo tunayokutana nayo, ni muhimu kuwa na msimamo thabiti ili tusiingie katika mitego. Unaweza kuchoka njiani na ukahitaji mtu wa kukusaidia. Nabii Elia, Mungu alimtumia kunguru ili aweze kumletea chakula. Malaika wa Bwana akamwambia: Elia, simama, kula na kunywa kwa sababu safari bado ni ndefu. Katika matatizo, kumbukeni kwamba Yesu anawajua, anaweza hata kukuita kwa jina lako kama alivyofanya kwa Elia. Yesu anawajua vizuri kondoo wake. Anajua sauti ya kila mmoja wetu. Elia alikuwa na njaa na kiu, akampa chakula na maji. Hakumpa pesa, nyumba au utajiri wowote, kwani alijua vizuri matatizo ya Elia. Allishiwa nguvu za kuendelea na safari na Mungu akampa (chakula kamili) ili kimtie nguvu za kuendelea mbele. 

 

Nina ushuhuda mfupi kuhusu jambo hili. Siku moja, ilikuwa siku ya kufungua shule, mimi na dada yangu tulikosa mahitaji muhimu ya shule. Tulikosa madaftari 10 yenye karatasi 100 (5 za mwandiko safi na 5 za hesabu). Niliomba kabla ya kwenda kupanda gariya kutupeleka  shule. Hata ada ya shule ilikuwa haitoshi. Ilikuwa vigumu kwenda shuleni bila ada wala madaftari kwani shule yetu ilikuwa mbali na mahali tulipokuwa tunaishi. Endapo tungechelewa kupata madaftari hayo baada ya wiki 2, tungekuwa nyuma ya wenzetu. Pia tulitakiwa kulipa ada pindi tunapoingia darasani. 

 

Niliamini ya kwamba, baba ametupatia kile alichokuwa nacho. Ndiyo maana sikuweza kulia mbele ya baba kwani nilijua ametoa kile alichokuwa nacho kama akiba. Na hakuwa na kitu tena. Ndipo nikaomba na kusema, “Bwana, naamini kabisa kwamba unaweza kuongeza pesa iliyopungua, pia na madaftari. Sielewi utafanyaje, ila naamini unaweza kutusaidia”. Jioni ya siku hiyo, akaja mtu mmoja, akawauliza; “Françoise yupo?” Dada zangu wakajibu kwamba “Amelala”, mtu huyo akaacha kiasi cha (pesa tulichopungukiwa kulipia ada) na akaagiza nipewe kama pesa za matumizi, na mtu huyo akaondoka. Nikaletewa pesa hizo chumbani nilipokuwa nikiomba. Ndipo tukaenda njia panda kusubiri gari.kituo kilikuwa karibu na nyumbani. Tulipofika kituoni nilisikia dereva mmoja akiniita akisema njoo haraka nina mambo mengi njoo upesi. “Chukua mfuko huu mdogo, ni wa kwako! Nisingekuona leo, ningeendelea na safari yangu . ” naye akaendelea na safari yake. 

 

Kwa upande wangu, nilikimbia na kufungua ule mfuko ili nione kilichokuwa ndani yake. Nikajiuliza swali kama alivyosema yule dereva: “Kama nisingekuona leo, ningeendelea na safari yangu.” Ndani ya yule mfuko nilikuta madaftari 10 tuliyohitaji. Mungu asifiwe. Anajua mahitaji yetu  na muda wa kutenda. Kwa nini Mungu hakunipa daftari 9 au 11 au madogo? Kwa nini madaftari yote yasilingane? Kwa nini gari lilipita muda ule ule ambao mimi nilikuwa kituoni? Kuna maswali mengi, lakini Mungu alinipatia kile nilichohitaji na ada  ile ile niliyomuomba. 

 

Mungu ni mwaminifu kama alivyofanya kwangu, anaweza na kufanya kwako pia. Yesu mwenyewe alisema ya kwamba anawajua kondoo wake, alijitoa kwa ajili yao (Yoh. 10:11 na mstari wa 15). Yesu anakujua, atakusaidia katika shida zako. Macho ya Mungu ambaye ni Baba yetu yako juu yako. Endelea kuwa mwaminifu kwa Bwana wako, hawezi kukuacha, maisha yako yamo mkononi mwake, usikate tamaa, na usiangalie ukubwa wa shida yako, bali angalia ukuu wa Mungu na upendo wake Kristo. Hakuna lisilowezekana kwake. Ana uwezo wa kubadilisha kila kitu. Kulikuwa na mwanamke mmoja ndani ya Biblia aliyeitwa Anna, mke wa Elkana. Alikuwa tasa, mume wake alimpenda sana (1 Sam. 1:5). Elkana alikuwa na mke wa pili aliyeitwa Penina, hivyo alikuwa na watoto. 

 

Penina hakuweza kumheshimu Anna kwa sababu hakuwa na watoto. Anna alikuwa akilia siku zote kwa sababu ya tabia ya dharau ya Penina. Mume wake alikuwa  akijiuliza :kwa nini Anna aliye mara kwa mara wakati yeye nampenda zaidi ya Penina na wanaye? Ndipo Anna akamuomba Mungu ampe mtoto, na akatoa ahadi ya kumtolea Mungu kama sadaka ya shukrani kwa Mungu. Mungu akasikia kilio cha Anna, akampa mtoto jina lake Samweli. Mungu asifiwe sana. Anna alionyesha moyo wa kumpenda Mungu. Nawewe , wakati wa matatizo, fungua moyo wako kwa Bwana, na umpe mizigo yako, yeye yuko tayari kukusaidia. Yeye ni mchungaji mwema. Alisikia sauti ya Anna, nawe anaweza kukujibu pia. 

 

Anna alitoa ahadi kwa Mungu (1 Sam. 1:11) “Bwana Mungu wa Israel, angalia unyonge wangu, usinisahau, nihurumie! Nipe mtoto, nami nitamtoa kwako kwa ajili ya kazi yako ……..”. ahadi ya Anna ilikuwa kwa Mungu, ilikuwa ni kumtolea mtoto kwa ajili yake, na Mungu asifiwe kwani Anna aliweza kutimiza nadhiri yake kwa Mungu. Kwa kuendelea tunaona Elkana na familia yake walienda Shilo na kumtolea Mungu dhabihu ya kila mwaka na kutimiza nadhiri. (1 Sam. 1:22). Alipomuachisha kunyonya alimpeleka pamoja na fahali wa miaka mitatu, gunia la unga na kiriba cha divai. Hana alimuingiza mtoto kwenye nyumba ya Mwenyezi Mungu huko Shilo, naye mtoto alikuwa mdogo bado. Walipokwisha kumchinja yule fahali, walimpeleka  mtoto kwa kuhani Eli. Hana akamwambia, “Nilimwomba Mungu anipe mtoto huyu, naye akanipa mtoto huyu. Kwa sababu hiyo nami nampa Mwenyezi Mungu mtoto huyo wakati wote atakapokuwa hai.  (1 Sam. 1:27 – 28) 

 

Ni ajabu! Huyu mwanamke alipata kibali machoni pa Mungu. Lakini alitimiza ahadi za Mungu .Mungu ni mwema  anasikia maombi ya watoto wake. Hakuna kisichowezekana kwa Mungu. Msafiri anakutana na matatizo mengi yanayoweza kumrudisha nyuma, kinachotakiwa ni kusonga mbele bila kuangalia matatizo. Yesu habadiliki, anaweza kukusaidia leo kesho na kesho kutwa. Kwa sababu wewe ni mmoja wa kondoo wake. Usilie sana Yesu alimshinda shetani alifufuka kutoka kwa wafu. Jina lake lisifiwe, anakupenda, aliyatoa maisha yake kwa ajili yako. Wewe ni mali yake, (1 Sam. 2:9), “Yeye atalinda miguu ya watakatifu wake ;bali waovu watanyamazishwa gizani,Maana kwa nguvu hakuna atakayeshinda ». 

 

Tuangalie Shadraki, Meshaki na Abedinego. Mfalme Nebukandeneza alitengeneza sanamu ya dhahabu ya mita 30 kwenda juu na mita 3 upana. Akaisimamisha katika sehemu tambarare ya Dura. Mkoani Babuloni, kisha mfalme akaamuru maliwali, wasimamizi, majaji, mahakimu ili wahudhurie sherehe ya sanamu aliyoisimamisha. Mpiga mbiu akatangaza kwa sauti kubwa: “Enyi watu wa makabila yote, mataifa yote na lugha zote, mnaamriwa kwamba, mkisikia sauti ya baragumu, filimbi  ……… na sauti zingine nyingi za muziki, lazima muiname chini na kuiabudu sanamu ya dhahabu aliyosimamisha mfalme. Na yeyote ambaye hatoinama kuiabudu, atatupwa katika tanuri ya moto mkali          (Daniel 3:40 – 6). 

 

Kutoka 20:3 – 5 imeandikwa: “Usiwe na Miungu wengine ila mimi. Usijifanyie sanamu ya miungu wa uongo, au kinyago chochote kilicho mbinguni, katika nchi au majini chini duniani. Usiisujudie wala kuitumikia; kwa kuwa mimi Mwenyezi Mungu ni Mungu wako ni Mungu mwenye wivu. Nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha hao wanichukiao”. Mstari wa 6 watu hawa watatu walimheshimu Mungu na kuendelea kuwa waaminifu, lakini kulikuwa pia mfalme aliyetaka kuwa na mamlaka juu ya maisha yao, kwa kuamuru watu wote kuiinamia sanamu na kuiabudu katika bonde tambarare la Dura. Aliahidi kumuadhibu mtu yeyote atakayekosa kutii amri yake. 

 

Watu wote walitii isipokuwa watu watatu wa Mungu. Walikataa kupinda migongo yao mbele ya sanamu la dhahabu. Walitii amri ya Mungu anayekataa kuinamia na kuziabudu sanamu. Bwana alimwambia Musa, atakayeinuka kinyume changu, nitamwadhibu, yeye na kizazi chake. Watu hawa watatu waliogopa kumkosea Mungu, kwani yeye akikuadhibu nani atakayekusaidia? Ni Mungu pekee mwenye uwezo juu ya kila kiumbe kilicho hai. Na unapotii amri zake, atakutendea mema wewe na kizazi chako. Watu hawa watatu walimjibu mfalme, lakini, hata kama haitafanyika hivyo, ujue wazi ee mfalme, kwamba, sisi hatutaitumikia miungu yako wala kuiabudu sanamu ya dhahabu uliyosimamisha (Daniel 3:18). Mfalme akajibu, Mungu gani atakayewaokoa mikononi mwangu? Mfalme hakujua kuwa kuna Mungu aliye zaidi ya miungu yake. 

 

Mungu wetu, aliyeumba ulimwengu anaweza kutuokoa na matatizo yote. Watu wa Mungu waliendelea kujibu, “Tambua ya kwamba Mungu wetu, Mungu tunaye mtumikia yuko tayari kutusaidia. (mstari wa 17). 

 

Mfalme, akiwa amekasirika, akaamuru mwako wa moto wa tanuru uongezwe (mara saba) kuliko kawaida yake. Lakini watu watatu hawakuogopa, walikuwa na imani thabiti kwa Mungu, walikuwa tayari kufa kuliko kumtenda Mungu dhambi. Kutoka 20:5 “Usivisujudiewala kuvitumikia;kwa kuwa mimi,Bwana,Mungu wako,ni Mungu mwenye wivu ,nawapatiliza wenye maovu ya baba zao hata kizazazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao”. Mungu wa Shadraki, Meshaki na Abedinego, ni Mungu wetu pia ni yeye msaada wetu wakati wa matatizo. Tujipe moyo, yupo kwa ajili yetu sisi ambao ni kondoo wa malisho yake. Sisi ni kazi ya mikono yake. Alituchagua alituita, alitukomboa, alitusafisha, ili tuwe watumishi wa  Mungu peke yake. 

 

Yeye ni mfinyanzi na sisi ni vyombo vyake. Tunajua ya kwamba, siku moja mbinguni tutafanana naye kwani sura yake iko ndani yetu. Kwa kuwa sisi ni mali yake, ni lazima tufanye mapenzi yake. Sisi sio wa dunia hii, bali wa mbinguni. Tumeitwa naye ili tuwe vyombo vya kumtumikia katika maisha yetu yote. Basi na tuende katika utakatifu bila kulaumiwa kwani sisi ni wasafiri. 

 

Hapa sio kwetu, kwetu ni mbinguni, tupo safarini kuelekea nchi mpya. Paulo aliandika maneno ya kutia moyo kwa Waefeso “mkavae utu mpya,ulioumbwa kwa namna ya Mungu katika haki na utakatifu wa kweli. »(Efeso 4:24). Basi uvueni uongo,mkaseme kweli kila mtu na jirani yake ;kwa maana tu viungo kila mmoja kiungo cha mwenzake. »  Waefeso 4:25,  na   Waefeso 5:8 hanasema hivi ; « Kwa maana zamani mlikuwa giza ,bali sasa mmekuwa nuru katika Bwana ;enendeni kama watoto wa nuru ». 

 

Msafiri lazima endelee mbele illi aweze kufika kwake. Angalisho! Yawezekana, umezungukwa na anasa na mambo mengine yanayoweza kukuvutia na kukufanya usahau uendako, usisimame, endelea na safari yako. Usiangalie kulia wala kushoto, lakini timiza lengo la kufika uendako. Lengo lako siyo kujichanganya na wazaliwa wa ulimwengu huu, ili usiige tabia na mienendo yao. Usijisahau kwani shetani naye ana nia ya kukurudisha nyuma ili uifuate njia yake. 

 

Siku moja jioni katika maono, nilimuona mtu  katikati ya njia, kando yake kuliwa na kundi la watu waliokaa kwa mzunguko kando ya njia. Walikuwa wanacheza na kunywa, walikuwa wakifanya starehe za kila aina. Mtu huo  akatoka njiani na kwenda kando ya njia ili kuangalia wanachofanya au kuangalia michezo yao. Mtu huo  alisimama kando ya kundi lile la watu na kuanza kuwaangalia. Sauti ilinijia kama mtu anayesema hivi:( mwanangu Bill Graham na watumishi wengi wameandika vitabu lakini pia wengi wao hawapo tena sasa enenda ukaandike kitabu kiitwacho « jinsi ya kuendelea katika njia ya wokovu. » utalinganisha na huyu mtu  aliyeacha njia, kuliko kuendelea na safari yake, anatoka na kwenda kuangalia watu wanaocheza). Asubuhi yake nikajiuliza, hivi mimi naweza kuandika kitabu? Sijafundishwa uandishi, sijafundishwa theolojia, ….. nikawa na maswali mengi. Nilimwamini Mungu aliyeniambia niandike, na nikaanza kuandika. Lengo la kitabu hiki kidogo, ni kutaka kuwatia moyo ili muendelee kukaa ndani ya Mungu na kuendelea mpaka mwisho. Wengi walianza safari lakini wakaishia katikati ya njia. Maneno haya yatawasaidia kwani ni Mungu ndiye mwalimu. Sura kadhaa nilizifunuliwa na Mungu mwenyewe. Nimeuona mkono wa Mungu wakati wa kuandika kitabu hiki. 

 

Neno la Mungu katika Luka 6:40 linasema “Mwanafunzi hampiti mwalimu wake, lakini kila mwanafunzi akishahitimu huwa kama mwalimu wake”. Bwana alinifundisha mambo mengi. Na kile alichonipa ndio hiki tunachoshiriki pamoja. 

 

Siyo kwamba ninajua mbinu za kutoanguka katika mitego, hapana. Kile nachoweza kusema ni kwamba; uwe na imani na Bwana wako. Daudi alisema katika Zaburi 23:1 “Bwana ndiye mchungaji wangu, sitapungukiwa na kitu. Mstari wa 4 sitaogopa mabaya, kwa maana wewe Bwana utaniongoza, utanipigania, utanitetea, hicho ndicho kinachonitia moyo”. Kama tutayainua macho yetu kwa Yesu, atatulinda na kutufikisha mwisho wa safari yetu. Tunapitia nyakati tofauti, ngumu kwani tunapitia magonjwa, vita, umasikini, n.k ……… ila tuna ushindi kwa sababu Bwana yupo pamoja nasi katika safari, jipe moyo! Kitambo kidogo tutakuwa pamoja na mpendwa wetu Yesu. Hatutaumizwa tena, wala kulia tena, bali tutakuwa katika furaha ya milele, Amen. 

 

Mambo ya kukatisha tamaa yametuzunguka, lakini angalia mbele, fuata maagizo ya Bwana wako, rudia kusoma amri zake na sheria zake. Omba bila kukoma na Bwana atakutia nguvu ili uendelee kushinda mbinu za shetani. Mungu wa Meshaki, Shedraki na Abedinego ni Mungu wako, atakuepusha na yote. 

 

Endapo utasahau maagizo unaweza ukasahau njia na kuanza kufuata njia nyingine. Tumfuate kiongozi wetu Yesu. Katika Zaburi 80:2 “Mbele ya Efraimu, Benjamini na Manase uziamshe  nguvu yako, uje utuokoe”! Bwana anawalinda watu wake kama kondoo. Ni lazima kondoo aijue fimbo ya mchungaji wake. Mchungaji wetu alidhihirisha upendo wake kwetu pale msalabani, alitukanwa, alichomwa mkuki, lakini alikubali yote kwa ajili yetu sote. Alikuwa na kusudi la kutuokoa. Jina lake litukuzwe. 

 

Mtunzi wa Zaburi alisema (Zab 16:5 – 8) “Wewe ee Mwenyezi Mungu ndiwe riziki yangu kuu, majaliwa yangu yamo mikononi mwako …………….. namweka Mwenyezi Mungu mbele yangu daima yuko pamoja nami, wala sitatikisika. Ni Daudi aliyesema hayo. Alitambua kuwa naye pia ni kondoo wa Bwana. Ni yeye aliyekuwa Bwana wa maisha yake. Ndiyo, Bwana anajali maisha yetu, anajali mipango yetu. Ni kweli Bwana ni ufunguo wetu na yupo karibu na sisi siku zote. Apewe sifa. 

 

BIDII 

 

Katika mchezo wa kandanda kama katika michezo mingine zinasikika sauti tofauti za kelele; mfano kele za kukata tamaa kushindwa au za furaha endapo mmoja kati ya wachezaji ataingia katika chumba kisichokuwa chake, kelele zitasikika kila mahali, kwa watazamaji. Mwamuzi wa mchezo anatoa onyo kwa mtu asiyetii kanuni na kufanya makosa mara kwa mara. Anamsifu mchezaji bora anayeshinda. Wachezaji Wanakuwa na lengo moja tu la kupata ushindi. Kabla ya hapo  wanafanya mazoezi muhimu na kumsikiliza kiongozi wao . 

 

Tuchukue mfano wa mbio za mita 100. mkiwa watu 6 kila mmoja na njia yake. Endapo wakati wa kukimbia uliingia katika njia ya mwenzako, hata kama umefika wa kwanza utaondolewa kwani hukufuata kanuni ya kutoingia kwenye njia ya mwenzako. Ni lazima ufuate maelekezo. Daudi alisema: “Nimeyahifadhi maneno yako moyoni mwangu ili nisikutende dhambi”. Utakuwa mbali na dhambi kwani neno la Mungu ni kioo kinachoonyesha uhusiano wetu na Mungu. Wewe ulianza kumfuata Bwana, usikate tamaa. 

 

Wakimbiaji wote wanaorodheshwa katika orodha ya washiriki. Wamepitia mazoezi mbalimbali ili wajinyakulie ushindi. Wana wa Mungu, wasafiri, wanapaswa kufanya mazoezi ya kiroho ili waweze kusimama wakati wa matatizo. Mpiga mbio anatakiwa kupata  lishe itakayo mwezesha kuwa mwepesi nakuwa na nguvu ili asiyumbe . 

 Katika njia iendayo mbinguni, hakuna watakaofika bila kualikwa, kila mmoja na njia yake na pia anajua kule anakoelekea, kiu na njaa vyaweza kukukosesha nguvu, lakini endelea kukimbia kwani muda uliobaki mbele yako ni mchache. Tunakaribia kufika. 

 Jipe moyo msafiri, jitie nguvu, mpendwa wetu anakaribia kuja kutuchukua. Usiangalie kulia au kushoto, endelea na safari yako ya kuelekea msalabani. Roho Mtakatifu atakusaidia, jitie nguvu. Manabii wapo kwa kitambo
tu,  bali mtegemee Bwana anayeweza kukushika mkono wako kwa kuwa wewe ni kondoo wa malisho yake. Anakuona, analijua jina lako nawe unamjua. Mfuate naye atakuongoza daima. 

 

Mungu anajua walio wake na kila alitajaye jina lake ajitenge na uovu                (2 Tim. 2: 19) kwa kuwa anatufuata popote, basi na tujilinde ili tusiwe na lawama mbele zake. Tuendelee kuwa waaminifu. Paulo alimwandikia Timoteo juu ya kuvipiga vita vya imani vizuri. Mara zote, tofauti kuenda sawa na mapenzi ya Mungu, kuwa na imani, upendo, uvumilivu, utu wema, macho ya muamuzi yako juu yako na atafurahi siku ataona umejipatia taji ya ushindi. Masikio yako yatasikia kelele nyingi, lakini usizisikilize wala kugeuka nyuma angalia mbele. Kiongozi wako anakusubiri mikono wazi akikutia moyo na kusema hongera, hongera! Walionunuliwa kwa damu ya Yesu na kuitunza mioyo yao, watakusanyika katika utukufu wa Mungu pindi baragumu itakapopigwa. Ni furaha iliyoje!!! Atatufariji na tutakuwa na furaha milele hata milele. Haleluya! 

 

Hivyo basi, wapendwa endeleeni kuwa imara katika imani ndani ya Yesu Kristo. Na kuzama ndani ya imani ili kukamilisha kazi ya Mungu, 

(1 Kor. 15:58) Mkijua ya kwamba kazi yenu sio bure. Tuombeane sisi kwa sisi, tutiane moyo. Paulo aliandika kwa Wakorinto “……… kwani mtatusaidia kwa maombi ………. Ndipo Mungu atajibu kupitia maombi yenu. Na wengi watamtukuza kwa ajili yetu”. 

 

 

 

 (2 Kor. 1:11). Ni kweli maombi ni nguvu inayomsukuma Mungu kutenda, ila anajibu maombi ya yule atakayetii kanuni zake kwani yeye alisema, “Shikeni hukumu mkatende haki,kwa maana wokovu wangu u karibu kuja na Haki yangu kufunuliwa.’’ Isaya 56:1. 

 

Shikaneni mikono, ombeaneni na Mungu atafanya. Vumilieni matukano, na mapigano haijalishi yatatoka wapi, endeleeni katika njia ya Yesu Kristo. Endeleeni kulisoma neno la Mungu ili ujue kile Mungu anachokitaka kwako. Isaya 56:2 “Heri afanyaye haya na mwanadamu ayashikaye sana ;azishikaye sabato asizivunje,auzuiaye mkono  usifanye uovu wao wote.’’ Methali 3:31 “Kwa kuwa Bwana anawachukia wamchukiaye, bali anawapenda wampendaye”. 

 

 

Tuzingatie neno hili, ya kwamba tunapiga mbio, na bado hatujafika. Sasa, kumbukeni kwamba kiongozi wenu anachunguza kila mlifanyalo na hatua za miguu yetu anazichunguza ili apate kujua kama unafaa kupata medani ya ushindi au la. Anachunguza pia mawazo yetu, mipango yetu na bila kusahau matumizi ya muda wa kutumika kwa ajili yake. Ayubu alitambua kwamba yupo anayechunguza njia zake na akasema, “Waitia miguu yangu katika mkatale,na kuyajua mapito yangu yote ;wajiandikia alama kuzizunguka nyayo za miguu yangu. » Ayubu 13:27 . ni uchunguzi wa hali ya juu!!! Mungu huchunguza kila tunalofanya kila siku, ni Mungu wa ajabu na mwenye nguvu. 

 

Usipokuwa mwangalifu, waweza kusema: nitaiba kitu fulani kwani hakuna atakayeniona, unasahau kwamba macho yake yapo kila mahali. Mungu ni Mungu, sio mwanadamu, yeye huchunguza hata maneno yatokayo vinywani mwetu, anaona yote tunayowaza. Yeye alituachia Roho Mtakatifu, ili tuweze kuzima mishale ya yule adui shetani. Tuenende katika nuru. 

 

Biblia inasema katika 2Timotheo 1:7 “Kwa maana Mungu hatukupa Roho ya woga;bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi. »  Mungu apewe sifa kwani kupitia Roho wake mwenye nguvu tunapata kumshinda shetani. Roho wa Mungu anatuwezesha kusema kwa mamlaka na kujiamini kwani Biblia katika Mathayo 10:20   “Kwa kuwa si ninyi mtakaosema, bali ni Roho wa Baba yenu asemaye ndani yenu”. Wakati wa majaribu tusipunguze bidii, bali tuendelee kupambana ili tujipatie taji iliyo andaliwa kwa washindi. 

 

Shetani anaweza kukudanganya, oh, sio kweli kwamba Yesu alifufuka katika wafu! Mwambie rudi nyuma yangu shetani, ninajua ya kuwa Yesu alikufa na baada ya siku tatu alifufuka tena kwa ushindi. Shetani anaweza tena kukuambia,  Kwa nini unajifanya kushuhudia watu, huku maandiko huyajui? Wewe mjibu ya kuwa, Yesu anayeishi ndani yangu anayo mistari mingi ya kuwafundisha watu ambao hawamjui. Anaweza tena kukwambia kwa nini ufundishe wakati hujasomea teolojia? Mjibu kuwa Roho Mtakatifu ndiye mwalimu mzuri wa teolojia. 

 

Paulo aliandikia wa Waefeso watiane moyo mkisezana kwa zaburi na tenzi na nyimbo za rohoni,huku mkiimba na kumshangilia Bwana mioyoni mwenu(.waefeso5:19) .  tena Paulo anasema kwamba tuvae silaha zote za Mungu tukijua kwamba hatuwezi kumshinda shetani bila kuwa na nguvu au kuwa na silaha, na silaha hizo tunazipata katika ushirika wetu na Mungu. Shetani anafanya kila mbinu za kuturudisha nyuma, kwani anajuwa muda wetu wa kuvalishwa taji umekaribia. 

 

Tuenende katika kweli siku zote, na tutangaza habari njema  kwa ulimwengu wote,tuwe na imani pia.Tuangalie kwa nini  Paulo aliweka utofauti katika silaha hizo.Ni kwa sababu adui yetu si mwanadamu bali ni roho chafu,ni nguvumbaya katika ulimwengu wa giza. 

 

1.    Ili upigane na Roho, ni lazima upigane katika Roho, hatuna tunachoweza kutumia zaidi ya maombi, ukweli, imani, usawa, kiasi katika kutenda mema, nk … tunayepambana naye sio mtu ili tumpige mapanga, visu. Yeye ni roho chafu. 

2.    Tunatumia silaha hizo ili tuweze kushindana na vita mbalimbali za shetani 

3.    Ili tuweze kusimama imara baada ya mapambano. 

 

Silaha alizoandika Paulo, ni za muhimu sana katika nyakati hizi. Tunaona mtu wa vita anapoingia vitani, anakuwa na mavazi maalum kama vile viatu, soksi, mkanda, kisu, kofia, bila kusahau silaha nyingine. Mungu apewe sifa kwa kutupatia silaha za vita ya kiroho. Kila Mkristo ni lazima aseme kweli, siyo uongo, kwani shetani ndiyo baba wa uongo. Ukweli unatoka kwa Mungu kwani alisema mwenyewe ndani ya biblia ya kwamba yeye ni kweli. Yesu Kristo ni njia kweli na uzima. (Kazi ya mkanda ni kufunga sketi au suruali) ili nguo isiweze kuanguka chini na kuacha ukiwa uchi. 

 

Mkanda unamaanisha kweli. Askari ni lazima awe na panga au mkuki ambao unamaanisha neno la Mungu. 

 

Neno la Mungu ni upanga mkali katika vita: Yesu alimshinda shetani kwa neno. Yesu alisema, imeandikwa ……… neno la Mungu lisitoke ndani yako, na ndani ya kinywa chako! Mtamshinda shetani kwa neno la Mungu. Neno la Mungu ni silaha muhimu katika vita. Neno la Mungu ni kioo kinachoonyesha uhalisi wetu (jasiri au dhaifu, Mkristo au la). Askari anavaa kofia ili kuzuia kichwa. Kofia inamaanisha wokovu tunaotakiwa kuwa nao popote. Tunajua ya kwamba Mungu aliweka utajiri mkubwa ndani ya vichwa vyetu. Ukipigwa panga kichwani unakufa papo hapo, bila kuwa na wokovu wewe ni kitu bure. Mungu alitufufua kutoka kwa wafu kupitia wokovu. Tulikuwa wafu katika dhambi na Yesu akaturudishia uzima kupitia damu yake pale Golgota. 

 

Tunalazimika kupokea wokovu tuliopewa na Yesu kwa neema. Wokovu ni silaha kubwa katika mapambano na shetani. Kama hauna wokovu, auhesabiki katika kundi la askari hai kama biblia inavyosema, unafanana na maiti au mfu, maana yake, mtu aliyekufa kiroho, hawezi kupigana vita ya shetani. Mungu atusaidie kuwa hai kiroho ili tuwe washindi. 

 

Tuangalie silaha nyingine ni vazi la kujikinga kifuani, linamaanisha uadilifu. Ukiwa mkweli siku zote utatembea katika uadilifu. Mungu anapenda watuwaadilifu wanaofanya mapenzi yake. Pita katika njia ambayo Bwana aliitengeneza kwa ajili yetu. Ukifanya kinyume na mapenzi ya Mungu, Mungu atakushambulia  pia wewe hutashinda vita vya kiroho .Lakini ukifuta maagizo ya Mungu ,Mungu atakulinda na kukutetea, atakufichambali na shauri la siri la watendamabaya, mbali na ghasia ya watu wafanyao maovu.(Zab 64:2 ). Mungu anakutana na mtu mwadilifu anafanya mapenzi yake kwa furaha. Mungu akisema fanya hiki au kile, usikatae, fanya, tena kwa furaha, atakuja kukutana na wewe. Mtapigana pamoja naye tena kwa nguvu zote. Mungu asifiwe, aendelee kuwa muadilifu, ni silaha inayotegemezwa na mkono wa Mungu, na utamshinda shetani. 

 

Hakuna wasi wasi kwa mtu anayefanya mapenzi ya Mungu kwa furaha, kwani ana uhakika na anachokifanya na Mungu anambariki. 

 

Tuseme juu ya silaha nyingine muhimu ambayo ni ngao, inayomaanisha imani, iwe daima kama ngao mikononi mwenu, iwawezeshe kuizima mishale ya moto ya yule mwovu. Waefeso 6:16 “Shetani anafanya kila mbinu ili kuipindua imani yenu, kwa hiyo bila imani hauwezi kumshinda, kwa kuwa alimjaribu Yesu mwana wa Mungu. Na wewe anaweza kukujaribu tena, anaweza kutumia maneno mazuri mfano “Wewe ni mzuri, na kupenda nk ….. ili kukuangusha. Tena anaweza kutumia maneno yanayofana na ukweli ili kukuchanganya katika kile unachoamini. Katika bustani ya Eden, alimwambia Eva: hivi ni kweli Mungu aliwaambia “Msile tunda lolote ndani ya bustani?” (Mwanzo 3:1). Huyu nyoka mjanja kuliko wanyama wengine, alijua wazi kwamba Mungu aliwakataza wasile tunda la mti wa kati ya bustani unaoonyesha mema na mabaya. 

 

Mungu hakusema wasile matunda ya miti yote. Mungu alikataza miti miwili tu! Na akatoa adhabu juu ya mtu atakayekula. Shetani alitaka Eva aamini ya kwamba Mungu ni muongo. Mwanzo 3:4 “Nyoka akajibu” hamtakufa, Mungu alisema hivyo kwa sababu anajua kwamba mkila tunda la mti huo mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya. Hivyo ndivyo shetani anavyoweza kuja kukuambia ili akuchanganye kiimani. 

 

Ni kweli ya kwamba shetani anajua siri za Mungu? Siyo kweli, Bwana aliwaambia siku mtakayokula mtakufa. Hiyo ndiyo adhabuyenyewe. Sasa sheteni alitaka kumaanisha kwamba anawafunga macho waone kile Mungu alicho waficha. Mungu atusaidie sana. Shetani anatuwinda kwakila njia na yale maagizo tuliyopewa na Mungu. Lakini endelea kuwa mwaminifu. Shetani akija kukwambia hivi au vile, mwambie ya kwamba hatujifunzi kutoka kwake, bali tunajifunza kwa Mungu, Roho Mtakatifu na neno lake anaweza pia kukudanganya na kusema ukaibe milioni moja katika pesa za kimarekani, utakuwa tajiri, utajenga majumba, utanunua magari ya kifahari, nk ……… ndiyo unaweza kuwa tajiri, lakini unaweza pia ukafa kabla ya kufurahia utajiri wako. Kwa nini asikuambie kwamba ukiiba utafungwa maisha! Oh ni furaha iliyoje kuendelea kuwa mwaminifu kwa Mungu na maagizo yake, Mungu hasemi uongo. Kuwa na imani uweze kuzima mishale ya shetani. Shetani alimwambia Eva siku mtakapokula mtakuwa kama Mungu, siyo kweli. Mungu ni mmoja na anajitosheleza. Hakuna anayefanana naye, ni muumbaji wetu na sisi ni kazi ya mikono yake, Apewe sifa. 

 

Sasa tunaamini ya kwamba tunamfuata yeye aliyeshinda shetani. Kwa sababu hiyo tunazo nguvu za kumshinda adui. Askari wa Mungu pia anatakiwa kuwa na amani popote kama viatu vyake. Tuwe na amani na watu wote. 

Sura hii ni muhimu kwa msafiri anayeendelea mbele japo wakati wa shida. Katika Waraka wa kwanza wa Mtume Petro anawatia moyo Wakristo waliokuwa wametawanyika katika mikoa mitano ya kaskazini na kusini mwa Asia. Maanzilishi wa Kanisa walikuwa wakiabudia Wakristo au waliotawanyika ni Paulo na wenzake. Wapagani walikuwa wakiwatesa Wakristo kwa mateso mengi, niyo maana, Petro anawatia moyo na kuwakabidhi kwa mtu wa Mungu waliyeteseka naye pamoja. Petro aliwatia moyo waendelee kuishi maisha ya utakatifu, pia kuwa waangalifu katika ushirika na Kristo. Na pia akawaambia “Wakati ule hamkuwa taifa la Mungu, lakini sasa ninyi ni taifa lake kwa neema. Tena akawatia moyo ili wadhihirishe uaminifua wao kwa Mungu hata wakati wa mateso. Aliwafundisha juu ya uhusiano kati ya mtu na Bwana wake, heshima kwa wanandoa kuishi kwa hekima mbele ya wasioamini, nk …… 1Petro 2:11 “Wapenzi wangu, nawasihi kama wapitaji na wasafiri ziepukeni tamaa za mwili zipiganazo na Roho”. 1 Petro 4:19; “Basi wao wateswao kwa mapenzi ya Mungu na wamwekee amana roho zao, katika kutenda mema kama kwa  Muumba  mwaminifu”. 

 

Mtume Petro alitoa maagizo kwa niaba ya wazee wa kanisa, kwa vijana na kwa Wakristo wote waendelee kuwa imara wakati wa mateso, kwa kutegemea ahadi za Mungu. 

Kama wasomaji wa barua za Petro walitakiwa kudumu katika imani pamoja na matatizo waliyokuwa nayo, ilikuwa hasa kwa ajili ya ushuhuda wao mbele ya wasiomjua Bwana. Ilibidi maisha yao, tabia zao yatangaze kazi ya Mungu. Biblia inasema ………. “Mlichaguliwa ili muitangaze kazi nzuri ya yule aliyewaita kupitia  vikwazo mpaka utukufu ili kuanza kazi na kumtukuza Mungu siku atakapokuja”. Tumsifu Mungu na kujitenga na tamaa zilizotuzunguka wakati wa ujinga. 

 

Tunaambiwa tuonyesha utii wetu kwa Bwana, tukatae kila aina ya ukali, uongo, unafiki, uvivu, utani, uzalimu, tumkaribishe Mungu ili aweze kutufanya kuwa mawe yafaayo katika kuujenga mwili wake. Mungu anatupitisha kwenye majaribu ili tuweze kuwa imara katika imani. Tunafahamu kwamba dhahabu inakuwa halisi mpaka inapopitishwa kwenye moto; vivyo hivyo imani yetu ambayo ni zaidi ya dhahabu, lazima ipitishwe kwenye majaribu, ili iwe thabiti. Hapo mtapokea sifa na utukufu na heshima siku ile Yesu Kristo atakapofunuliwa. 1 Petro 1:7. 

Watakaovumilia mpaka mwisho, ndio watakaopewa thawabu, kwa hiyo tuwe wavumilivu katika shida, tufurahiye hata kama yanaweza kuwa mazito na ya kuhuzunisha kwa ni ya muda kidogo tu. Tunajua baada ya yote, tutazungukiwa na utajiri wa Mungu. Petro aliandika “Ni baraka zisizooza, kuharibika, au kufifia. (1 Petro 1:4 – 5) 

 

 

 

THAWABU YA USHINDI 

 

“Lakini mwisho wa mambo yote umekaribia ;basi, iweni na akili,mkeshe katika sala.’’(1 Petro 4:7). Tunajua ya kwamba kila kitu kina mwanzo na mwisho wake. Mhubiri alisema, kila jambo lina wakati wake, muda wa kupanda na wakati wa kuvuna, wakati wa kuzaliwa na wakati wa kufa, kama kuna mwanzo wajambo ni lazima kutakuwa na mwisho wa jambo. Yesu alikwenda mbinguni, na atarudi kutuchukua.Tutaishi naye milele,tumeshaanza safari,na muda si mrefu tutamaliza safari. Saa ya mwisho imekaribia kama mtume Petro alivyosema ‘’Mwisho wa kila jambo umekaribia’’ Neno hilo ‘’Mambo yote’’ linamaana gani ? Yawezekana uchungu,vilio,matatizo,inawezekana kujifurahisha, utajiri, vicheko, heshima, nk……… mwisho wa hayo yote umekaribia. Mwisho ni wakati muhimu unaosubiriwa na watu wote. Inafanana na mtu anayefanya safari na sasa amefikia ukomo wa safari yake. Kila tunachokiona kitafikia mwisho wake. 

 

Mwisho unakaribia, hatujui siku ngapi zimesalia mbele yetu. Lakini tunahakikishiwa na Roho wa Mungu ya kuwa muda uliobaki ni mchache, bado kidogo maisha yetu yatafikia mwisho wake. Kwa sababu hiyo, Petro anashauri kuenda katika utakatifu na uamusho wa maombi, Mungu atusaidie ili tuwe na kiu ya maombi, tunajua yakwamba Mungu anaongea na watu wake kupitia maombi, pia katika maombi tunatakaswa pia kwenye maombi Mungu anatufunulia yaliyofishwa. Roho wa Mungu anachunguza mipango ya Mungu na kutufunulia. Mtu wa Mungu anaishi pamoja na Mungu,Mtu wa Mungu anatumika pamoja na Mungu na anamtumkia Mungu.Tuwe na roho ya uamsusho wa maombi kwa sababu mambo yote yataenda kufikia mwisho na Yesu atakuja mawinguni. Kama mwisho unakuja ni kweli na uzima mwingine utaanza, uzima wa watu wa Mungu na watu wake  wale waliompokea kuwa mwokozi wa maisha yao. Kwa wengine ni maisha/uzima wa wao pamoja na shetani waliyemtumikia. Wataishi na shetani kule jehanamu. 

 

Biblia inasema; hatujajua vile tutakavyokuwa mbinguni, ila tunaamini ya kuwa tutafanana na Yesu. Kwa sasa (Wakristo) ambao ni wana wa Mungu, wametawanyika kote duniani, lakini siku inakuja ambapo wote tutakusanyika karibu na Yesu. Yeye atakuwa nuru yetu. Katika Ufunuo 7:9 Yohana aliona umati wa watu wa kila taifa, lugha zote kila kabila hakuna matengano, wote tutavaa sawa (kanzu nyeupe na matawi mikononi) tutamtukuza Mungu kwa lugha moja. Kinachotutofautisha sasa ni (mfano; mila, desturi, mikoa, nchi, nk …….). tutakuwa sote mabibi harusi wa Kristo, naye Bwana harusi. Ndiyo maana wapendwa wangu tunapaswa kuombeana na kutiana moyo katika Bwana. Imeandikwa (Waebrania 12:14) “Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, ila ulio uatakatifu ambao hapana mtu atakayemuona Bwana asipokuwa nao”. Na Yakobo aliandika; “Ndugu zangu, msinung’unikiane ninyi kwa ninyi msije mkachukumiwa na Mungu, mwamuzi amesimama mbele ya milango” (Yakobo 5:9). Muwe na amani na watu wote muombee waliowaudhi, muwapende jirani zenu muwafanyie mema kwa uwezo wenu kwa sababu mwamuzi yuko mlangoni, anakaribia kuingia. 

 

Kuishi maisha matakatifu maana yake ni kulinda mioyo yetu na dhambi kwani wenye dhambi hawatamuona Bwana, watakwenda jehanamu kwa shetani. Wakristo watabaki wakiishi kama watu wa familia moja, wawe kitu kimoja kiroho na kimwili. Kusaidiana kama walivyofanya Wakristo wa kwanza. (Mdo. 4:32) Na jamii ya watu  walioamini walikuwa na moyo mmoja na roho moja ;wala hapana mmoja aliyesema yakuwakitu chochote alichonacho ni mali yake mwenyewe ;bali walikuwa  na vitu vyote  shirika. 

 

Wakristo wa kwanza waligawana vitu vyao kwa furaha. Walitoa mali zao kwa wengine sawa na mahitaji yao. Tunajua pia kuwa upendo hustiri wingi wa dhambi. “Upendo unazidi yote, na utumaini yote. Unapompenda mtu kwa moyo wako wote, ina maana unaweza kugawana naye kile ulicho nacho na kumtosheleza. Pendaneni, kati yenu kusiwe na matengano. Madhehebu yasitutenganishe kwa kusema mimi ni wa dhehebu fulani siwezi kuomba na wa dhehebu jingine. Hapana, sisi sote ni wake Kristo. Tumekombolewa sote kwa damu ya dhamana ya Yesu atakayerudi kutuchukua sote. Huko Mbinguni hakutakuwa na madhehebu, kabila huko mbinguni. Tutaishi na kurithi mbingu moja sote pamoja. Wapendwa katika Bwana muda umekaribia na Bwana harusi anakuja  hima kutuchukua. Tuwe na uamusho wa maombi. Maisha ya baadaye yamefichwa. Lakini biblia inatufunulia wazi katika ufunuo wa Yohana. 

 

Tunaweza kujiuliza maswali mengi, tutakwenda wapi baada ya kifo? Itakuwaje? Tutakula nini? Kwa neon moja ni kwamba tutakuwaje baada ya kifo? Ni kweli kuna maisha baada ya kifo biblia inasema; Yohana alifunuliwa akaona vitabu viko kwenye  mikono ya malaika wakiwa na vitabu ndani yake yameandikwa majina ya waliookoka, na kingine kimeandikwa matendo ya watu wote wanayoyafanya hapa duniani. Tunaimani kwamba kua mbingu pale Yesu alipokwenda baada ya kufufuka. Na wakristo watakaa naye huko baada ya kifo. (Ufunuo 21:8) “Lakini watu waoga, wasioamini, wapotovu, wauaji, wazinzi, waabuduo sanamu na waongo wote sehemu yao ni katika  lile ziwa liwakalo moto kiberiti, hii ndio mauti ya  pili”. 

 

Tumetoka kuona sehemu mbili (mbingu kwa ajili ya watakatifu, na ziwa la moto kwa wenye dhambi). Wafu watafufuliwa ili kuhukumiwa na Mungu mwenyewe. Watahukumiwa sawa na matendo yao na kazi zao. Yohana aliona wafu wakubwa kwa wadogo wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu  vikafunguliwa ; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa  katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao.(Ufunuo 20:12 – 15). Kupitia Ufunuo wa Yohana, tunaona kwamba inatupasa kutenda mema, kwa sababu kuna malaika anaandika matendo yetu ukimsaidia masikini malaika anaandika ndani ya kitabu cha matendo.Tunaweza tukafanya kazi nyingi lakini tuangalie kwamba je majina yetu yameandikwa kwenye kitabu cha uzima, Maana jina lako kama halipo kwenye kitabu cha uzima utatupwa kwenye ziwa la moto (jehanamu). Lakini hao ni wakina nani watakaotupwa jehanamu; ni wale waliokataa kumpokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yao; 

 

Yohana aliona tena (Ufunuo 20:11) “Kisha nikaona kiti cha Enzi kikubwa cheupe nay eye aketiye juu yake; ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso wake na mahali pao hapakuonekana. (Ufunuo 21:1). Kisha nikaona  mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza  na nchi ya kwanza zimekwisha kupita, wala hapana bahari tena. 

 

Yohana aliona mbingu na dunia ya zamani vikitoweka, lakini aliona mbingu na dunia mpya. (Ufunuo 21:2) Kisha nikaona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya,ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu,umewekwa tayari kama bibi-arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe.  Mstari 3. Ufunuo 21 “Kisha nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema , Tazama , maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake, Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao. Tunakuwa na furaha hapatakuwa na vilio, manunguniko, taabu, magonjwa wala kifo tutafutwa machozi. Bwana apewe sifa. 

 

Kuna siku ambayo tutaishi katika raha ya milele. Tunaona dunia na mbingu ya kwanza vitapita, ila tutaishi katika mbingu mpya, Yerusalemu mpya anakokaa Mungu na watakatifu wake. Biblia inasema kuwa Yerusalemu mpya ilikwishaandaliwa kama vile bibi harusi anavyojipendezesha ili kukutana na bwana harusi. Inatuonyesha wazi kuwa mji huo ni mzuri, Yohana aliona mji unaong’aa kama mawe ya thamani angavu kama kioo. Mstari wa 18”. Mstari (wa 16). Mji wenyewe ulikuwa wa mraba, upana na urefu wake sawasawa na mapana yake. Akaupima mji kwa ule mwanzi; ulikuwa kama maili elfu na mia tano; marefu yake na mapana yake na kwenda juu kwake ni sawasawa. Soma  Ufunuo wa Yohana 21;17 ‘’Akaupima ukuta wake, ukapataa dhiraa mia na arobaini na nne, kwa kipimo cha kibinadamu,maana yake cha malaika. 

 

Ufunuo 21:22 23; Nami sikuona hekalu ndani yake; kwa maana  Bwana Mungu Mwenyezi  na Mwana Kondoo, ndio hekalu lake. Na mji ule hauhitaji jua wala mwezi  kuungaza , kwa maana utukufu  wa Mungu huutia nuru,na taa yake ni Mwana-Kondoo. Milango ya mji huo itakuwa wazi hakutakuwa na usiku Mstari wa 26; nao wataleta utukufu  na heshima  ya mataifa  ndani yake. Oh mji huo ni mzuri! Mji huo utakuwa makao yetu na pamoja na Bwana wetu. Wateule wa Mungu tutunze utakatifu ndani yetu kwa Bwana Yesu anakuja kutuchukua. Ametuma malaika wake kumuonyesha mtume Yohana  kwamba; Mbinguni hakitaingia kamwe  chochote kilicho kinyonge, wala yeye afanyaye  machukizo na uongo, bali  wale walioandikwa  katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo. 

 

Yesu alisema “Tazama naja upesi, na kila ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo”.(Ufunuo 22:12). Na Yesu alisema, Heri yao wale wanaoosha mavazi yao, wapate kuwa na haki ya kula tunda la mti wa uzima, na haki ya kuingia mjini kwa kupitia milango yake. 

 

Ndugu na dada, Mungu atafuta machozi yetu na atatupa taji ya thamani ya ushindi (tutaishi naye milele, Amen). Ufunuo 21:7. Ufunuo 22:1 – 2 ; Kisha akanionyesha mto wa maji ya uzima, wenye kung ‘aa kama bilauri, ukitoka katika kiti cha enzi cha Mungu na cha Mwana Kondoo, katikati ya njia kuu yake. Na upande huu na upandee huu  wa ule mto, ulikuwapo mti wa uzima, uzaao matunda ,aina kumi na mbili, wenye kutoa matunda yake kila mwezi na majani ya mti huo ni ya kuwaponya mataifa. 

 

 

Siku moja tutalipwa ujira wa kazi ya Mungu tunayoifanya. Yohana aliona kila mtu atakavyosimama mbele ya kiti cha Enzi cha Mungu kusubiri hukumu. Biblia inasema ya kwamba tutahukumiwa kutokana na matendo yatakayokuwa yameandikwa ndani ya kitabu cha hukumu. Na Yesu atatuvika taji kutokana na kazi nzuri tutakayofanya. 

 

Jipe moyo ndugu yangu, na dada yangu, endelea kufanya kazi ya Mungu kwa bidii, ukijua ya kuwa siku inakuja ambayo tutalipwa. Tumika wakati wote iwe wakati wa jua au wa mvua, bila kuogopa au kujali watu wanasema nini juu yako, bali elekeza macho yako juu ili uweze kutimiza lengo katika kazi ya Mungu. Angalisho! Lazima uwe na uhakika kwamba jina lako limeandikwa katika kitabu cha uzima kwani wote ambao majina yao yatakuwa nje ya kitabu hicho watatupwa katika ziwa la moto. (Ufunuo 20:15)    

 

 

 

 

 

SURA YA V 

 

WEWE NI NANI? 

 

Unaweza kueleza mambo mengi yanayokuhusu mtu flani. Biblia  inatuonyesha kuna watu wengi wanaouliza Mungu ‘’mimi ni nani?” tuangalie mfano wa Musa, wakati Mungu alipomchagua kuliongoza Taifa la Israel, Mungu akasema katika Kutoka 3:7 – 9. “Kisha Mungu akamwambia “Nimeyaona mateso ya watu wangu ya watu wangu walioko Misri nami nimekisia kilio chao kwa sababu ya wasimamizi wao maana nayajua maumivu yao. Mstari wa 10, Haya basi nitakutuma sasa kwa Farao ili upate kuwatoa watu wangu, watu hao wa Israel, kutika Misri. 

Mungu alimpa Musa amri hii ‘’Nenda kwa Farao’’. Musa aliona ni vigumu sana kwake kwenda mbele ya Farao akasema ‘’mimi’’ siwezi kwenda kumuona Farao na kuwatoa Wana wa Israel Misri!”  tunaweza tukajiuliza kwa nini Musa alisema “mimi”. 

 

Alijiona dhaifu, mpole na mtu asiyeweza kwenda kwa Farao, kwani alikuwa mtu hatari na wa kuogopwa sana. Mungu akamtia nguvu na akamuahidi kwenda pamoja naye. Kutoka 3:12. Mungu akasema ‘’Nitakuwa pamoja nawe”. Yawezekana na wewe ukawa kama Musa. Mungu akikutuma kazi yake na kukwambia yuko pamoja nawe, wewe nenda bila hofu, anajua uwezo na udhaifu wako. Wewe sema ‘’Ndio Bwana’’ utakapokubali utaona miujiza ya Mungu. Musa alisema, mimi? Kwa Farao, Mungu akasema, nenda na uwatoe waisrael Misri, na uwapeleke katika nchi nzuri. Mungu anajua mapito yetu na yuko tayari kutuokoa. Unaweza kujiuliza, kwa nini Musa alijiona dhaifu, lakini kumbuka kuwa Mungu anachunguza watu wake na  yupo tayari kutuokoa kwenye tatizo lolote, anajua watumishi wake na anawaita ili wafanye kazi yake. 

Unaweza ukaona kwamba wewe ni dhaifu lakini Bwana Yesu yeye anajua utajiri uliomo ndani yetu. 

 

Mungu aliyetuumba kwa mfano wake, ndiye anajua namna gani tunaweza kuwa msaada katika kazi yake takatifu. Swali lina kuja! “wewe ni nani? Musa naye alimuuliza Mungu: “Bwana wewe ni nani? Kwa hiyo tunaelewa ya kwamba Musa alitambua kwamba ni Mungu anayesema naye. Lakini alitaka kujua uwezo wake na nguvu zake kwa kuwa aliahidi kuwa pamoja naye katika mpango mzima wa kuwakomboa waisrael kutoka Misri. Mungu alimjibu, “Mimi niko ambaye niko”. Mimi ni Mungu (Kutoka 3:14) “Mungu wetu asifiwe! Alijitambulisha kwa Musa alijitambulisha kwako pia, atajitambulisha na kwa wengine. 

 

Bwana yuko hai,tena ni wa milele, Haleluya! Yesu kristo ni yeye yule, jana na hata milele. (Waebrania 13:8) Upendo wake hauna mipaka wala haubadiriki nguvu zake, uwezo wake haubadiriki, ukuu wake ni wa milele  yeye ni wa milele, Yeye ni niko. Huyo huyo ndiye atakaye pamoja nasi katika utumishi. Nawe unaweza kusema “mimi?” mbona sijui kusema, sina ufahamu wa neno la Mungu? Mimi? Wa familia flani? Mimi, mimi,nk, unaweza kutaja mapungufu mengi ya kujikatisha tamaa, lakini Bwana anakwambia “Fanya” au “Nenda” au “Sema” Maana Mungu ndiye anayejua moyo wako ndiye aliyekutuma na ndiye atakayekusaidia, ukitegemea nguvu na uwezo wake utafanikiwa. Mungu alijua udhaifu wa Musa, na alijua pia ugumu wa moyo wa Farao na tabia zake mbaya, lakini akamtuma Musa, mdhaifu kwa mtu mbaya Farao. Kwani yeye ni Mungu anayejidhihirisha katika kila jambo. 

 

Bila mkono wa Mungu, Musa asingefanikiwa. Na wewe kama Mungu alivyokuita umtumikie ni hakika atakuiwa pamoja na wewe, Mungu anatumika pamoja na watumishi wake. Mtunzi wa Zaburi alisema, pamoja na Bwana tutatende makuu. Bwana alimuonyesha Musa jinsi atakavyofanya  pia alimuonyesha mwisho wa kazi hiyo.  Kutoka 3:21” Nami nitawapa  watu hao kufadhiliwa  mbele ya Wamisri; hata itakuwa  hapo mtakapokwenda zenu hamtakwenda kitupu. 

 

Katika mstari wa 21, Mungu anaonyesha jinsi gani Musa na Waisrael watakavyopata ushindi, sio tu kutoka Misri? bali kutokana na utajiri wao. Maneno hayo yalimtia Musa nguvu na kuanza kusahau mapungufu yake. Na sasa alifikia hatua ya kuziona nguvu za Mungu na sio udhaifu tena. 

 

Mpendwa mtumishi wa Mungu aliye hai! Hamuwezi kufika mbali kwa kuangalia udhaifu wenu, lakini siku mtakapokubali wito wa Mungu, Nguvu za Mungu zitakuwa pamoja nanyi na mtaona miujiza ikitendeka. Ni kwa uweza wa Mungu tu , tunapofanikiwa kufanya kitu cha maana. Kwenye kazi ya Mungu tunachota nguvu ndani ya Yesu, kwa neno lingine ni Mungu mwenyewe na uweza wake unafanya kazi kupitia sisi. Kwa hiyo siwezi kujivuna eti nimefanya hiki au kile , kwa sababu sio mimi niliyekifanya bali ni Bwana Yesu ndiye aliyekifanya, Hivyo ni Bwana Yesu anapaswa kushukuliwa. Tukiangalia mbali sana tunaweza kuona kwamba mtumishi wa  Mungu anatakiwa kuwa na  uhusiano mzuri kati yake na  Mungu. Bila uhusiano na Mungu, kazi ya Mungu itafanyika kimwili, kwani unaongozwa sasa na mapenzi yako na siyo Roho wa Mungu. Ni jambo jema kuwa na ushirika na Roho wa Mungu katika maombi. 

 

Mtu wa Mungu ni lazima ajitenge mbali na dhambi. Tambua ya kwamba kabla ya kuwa mtumishi  katika Kanisa au huduma yeyote, unatakiwa kuwa mtumishi wa Mungu kwanza, Tambua yakuwa wote wanaofanya huduma ya Mungu sio wote watumishi wa Mungu, wengine ni watumishi wa shetani wanaopjiingiza kwenye huduma hizo. Ni Mungu mnayemtumikia atakayekuwezesha katika kazi yake kwa hiyo kama huna ushuhuda mzuri mbele za Mungu haifai kuwadanganya washirika wako, kwa sababu kumbuka kabisa Mungu hayupo pamoja nawe katika huduma yako. Mungu aliyekuumba anakuona kokote ulipo, anajua mawazo yako, anajua mahitaji yako, anakuona kila mahali. Huyo Mungu ni mkombozi wetu, ndiye aliyetiokoa na dhambi zetu zote, anataka  tukubali wito wake popote atakapotutuma, Na usiseme kama Musa alivyosema, Sema ndiyo Bwana nakubali atakutumia kuokoa wale wote walioko gizani(ambao hawajampokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yao). Mtaona kuwa ni heshima kubwa sana kumtumikia Bwana. 

 

Nakumbuka Mungu aliponiambia niandike kitabu hiki, nilisema ……………….. oh Bwana! Mimi! Ambaye sijaisoma Biblia? Ambaye sina hiki na kile. Maswali yote hayo yalikuwa yananionyesha vile nilivyokuwa na mapungufu katika kuandika kitabu. Lakini Mungu alinihakikishia ya kuwa atakuwa pamoja nami, ndipo nikaanza kuandika, sasa nimemwona Mungu, na nimeamini ya kwamba ni yeye anayefanya kazi yake. 

 

Sasa namtumikia Mungu, apewe sifa kwani anafanya kazi kubwa ya kunifunulia maandiko, na mimi naandika. Swali linakujia, wewe ni nani? Unaweza kujitambua? Yawezekana ndiyo, au hapana. Biblia inasema, moyo wa mtu ni mdanganyifu, bali Mungu ndiye pekee ajuaye viumbe wake. Unaweza kujiona huwezi, kumbe unaweza, tena unaweza kujiita umeokoka, kumbe hujaokoka. 

 

Mungu akiuliza: Françoise ni nani? Sitaweza kujibu kwa sababu naulizwa na Mungu ambaye ananifahamu zaidi ya vile ninavyojifahamu. Lakini kama wewe ungeniuliza swali hilo, ningekujibu ya kuwa; mimi ni mwanamke, mtumishi wa Mungu katika (Umoja wa Wanawake wa Kikristo Burundi) mama, watoto, nk ……. Pia ingeniwia vigumu kusema uzuri na ubaya wangu. Lakini kama ningemuuliza Bwana, mimi ni nani? Angeniambia kila kitu kuhusu mimi. Kutoka 4:10 “Lakini Mungu akamwambia Musa, iwe Bwana wangu, mimi sina ufasaha wa kuongea tangu zamani; hata baada ya kusema na wewe, ulimi wangu ni mzito. 

Musa aliKuwa anadhihirisha wazi kwamba, ana matatizo ya kutoongea vizuri au hawezi kujielezea vizuri mbele za watu. Bwana akasema katika mstari wa 12 “Mimi nitakIongoza kinywa chako, na kukufundisha namna ya kusema”. 

 

Mungu anayo majibu ya matatizo yetu. Musa hakuamini kwamba Mungu anaweza akamsaidia  kuongea ndiyo maana akamwita Haruni anayeweza kusema ili waambatane naye. Mungu akamkasirikia Musa ambaye alikuwa mgumu kuamini. Tukijumlisha haya yote, tunaona kwamba Musa pia alikuwa mwoga, asiyependa  kwenda peke yake. Lakini Mungu alijuwa kwamba Haruni anaweza, ila hakumpa kazi hiyo. 

 

Kwa sababu Musa alisisitiza, Basi, Mungu akasema, ni yeye atakuwa akisema mahala pake. (Kutoka 2:16). Kupitia sura hii, tunaona Musa anamkabidhi Haruni wito wake hata siku za leo, watumishi wengi wanakabidhi huduma zao kwa marafiki ……… wanasahau ya kwamba, Mungu asipotumika pamoja nao, kazi yao ni bure na haitafika mbali. Siyo uwezo wa kusema “ndiyo” kunafanya kazi ya Mungu, siyo kwa sababu huyo alisoma Biblia ndiyo maana anaweza kuifanya kazi ya Mungu. 

 

Lakini wakimuomba Mungu, anaweza kuwakubali kama alivyomkubali Haruni (Kutoka 1:15). 

 

Pamoja na ujuzi wa Haruni wa kujua kusema, lakini asingeweza kufanya mambo makubwa bila Mungu kuingilia kati. Mungu atusaidie kupata ufahamu wa kazi yake. 

 

Siku moja, mchungaji mmoja aliniambia: “Tumemuwekea mtu mmoja mikono awe mtumishi kwani Kanisa sasa limekuwa na watu wengi”. Nikamuuliza, “Mlifanyaje?” akajibu “Tulichagua watu nane wenye ushuhuda au tabia njema na kuwaombea ili wawe viongozi. 

 

Ni kama Musa alivyomuita Haruni, kwani alimwona anafaa. Ndivyo ilivyo kwetu pia, tunaangalia Oh! Petro alisomea Biblia uingereza anaweza kuwa mchungaji wa Kanisa langu. Oh Suzana ni mwanamke muombaji, anaweza kutusaidia katika haya, nk …… wengi kati ya waamini wanao wito wa kumtumikia Mungu. Basi kaeni karibu nao, watieni moyo, waombeeni, na kwa wakati wa Bwana, wataweza kuwa watumishi. Sielewi kwa nini Mungu amenifunulia jambo hili, anataka kukusaidia, wewe mtumishi wa Mungu,  ila nina swali juu yako. Je wewe ni Musa? Au wewe ni Haruni? Vyovyote ulivyo, uko kazini mwa Mungu. Muombe Mungu atumike pamoja nawe, na akuongoze katika kazi yake. Mwamini na kumtegemea yeye na utaona miujiza. 

 

Turudie katika somo letu. Mungu akikuuliza wewe ni nani? Nilisema ya kwamba ni kutaka kujua kama unajijua au la. Muache Mungu aseme juu yako kwani anakujua. Mungu alijifunua kwangu na kujionyesha vile nilivyo. Kabla ya hayo nilijiona Mkristo safi, kwani nilimuona Mungu akitenda miujiza kupitia mimi. Hivyo sikuwa najiona kuwa na kasoro mbele za Mungu, nilijiepusha na mambo mengi. Watu wengi hawajui madhaifu yao. 

 

Unaweza kuwatukana watoto au wafanyakazi wako wa ndani wakifanya makosa, au kugombana na wengine, haijalishi mnagombania nini. Wewe ni nani? Unanielewa vizuri? Mimi nilijijua ni nani baada ya kuwa na uzoefu wa mambo mengi yanayohusu  maisha yangu. Nilikua Mkristo mchangamfu, mwenye furaha, mkarimu nk ……. Lakini sikujua ya kwamba nilikuwa na hasira, mkali! Mungu asifiwe kwani alinifungua na kuniweka huru. 

 

Wewe ni nani? Je unaelewajinsi  ulivyo? Wewe ni mtu mwaminifu? Wewe ni mwenye hasira? Mzinzi? Unaweza kujielewa kiasi, lakini Mungu anayetaka kukufungua anaweza kukuonyesha ulivyo ili akuponye. Yesu aliwaambia Wafarisayo (kizazi cha nyoka). Wanafiki, unaweza kujiita Mkristo safi, lakini je mwenendo wako unamuwakilisha Kristo? Mara nyingi wanaojiita tumeokoka, wanamuaibisha Kristo. Ndani ya Mkristo kuna tabia za kimwili? Niligundua ya kwamba, baadhi ya tabia zimefichika. Tunamuomba Mungu atufunulie wazi ili tufunguliwe. 

 

Kwa mfano, katika barua ya Paulo kwa Timoteo (Tim 2:24) …. “Mtumishi wa Bwana asigombane. Anapaswa kuwa mpole kwa watu wote, mwalimu mwema na mvumilivu”. Sasa wewe ni nani? Mungu ataka kukukomboa ili akutume, kwa kuwafundisha wengine walio gizani. Je uko tayari? Mungu anatumika na wote, uwe mwanamke au mwanaume. Anatumika na wote wenye mioyo iliyopondeka. Unaweza kuwa mdogo kama Daudi, au mzee kama Abrahamu, mwanamke kama Debora, Abigauli, nk ……….. anaweza kutumika hata na wale ambao hawakusoma, wenye vyeo, matajiri na masikini. Mungu anajidhihirisha katika kila hali. 

 

 

Tuangalie mfano wa Nuhu, alikuwa na watoto watatu Shemu, Hamu na Jafeti. Alikuwa mwadilifu na mchaji wa Mungu bali wengine walikuwa watenda dhambi. Mungu akaamua kuwaangamiza. Akaamua Nuhu ajenge safina. Mwanzo 6:9 – 22. 

 

Kwa kuwa aliamriwa kuwaingiza wanyama pia, ina maana ilibidi awe na majani ya kuwalisha kwa muda wa siku 40. na kwa ajili ya watu, pia alitakiwa chakula  cha kutosha. Ingekuwa kazi ngumu na ya kuchoshwa (Mwanzo 7:5) wewe ni nani? Je unamtii Bwana wako? Au ni mtu wa masababu sababu kwa Mungu? Unataka umtume mwingine nafasi yako? ungependa Mungu akuletee (Haruni) ili mtumike pamoja? Yawezekana unasema kwamba huwezi kuiacha familia yako kwa ajili yake. 

 

Unataka nini ili uitikie wito? Unataka nyumba? Mali? Magari? Ndiyo, Mungu anaweza kukupatia, lakini sio tabia nzuri mbele ya macho ya Mungu. Mungu anasema: “Nitakuwa pamoja nawe popote utakapokwenda”. Mwamini Mungu. 

 

Unaweza kujiuliza kwa nini Mungu alikuchagua kama ulivyo? Yeye aliyekuchagua  anajua sababu ya kukuchagua ukiwa mchafu. Mimi nilikubali. Nenda na utasema kila Mungu atakachokuweka ndani ya moyo wako. Ni heshima iliyoje kutumika na Mungu mwenye nguvu. Usijitetee sana, ila omba akutakase ili ukubalike. Lengo la Mungu ni kuwafungua watu wake ili tuirithi nchi inayotiririka asali na maziwa. 

 

Tuangalie mfano wa Abrahamu, alipata watoto wengi ……….. “Wazawa wake watatoka kwa Isaka, Abrahamu alikuwa na watoto wengi, bali mpango wa Mungu ulitimia kupitia Isaka. Tujue pia kwamba Mungu alimwambia Rebeka ambaye alikuwa na watoto wawili (Yakobo na Esau) “Warumi 9:13) nilimpenda Yakobo, na kumkataa Esau. Mungu ni mwaminifu katika mpango wake Alimwambia Rebeka maneno haya kabla ya watoto hao kuzaliwa. Je tunaweza kusema Mungu anaupendeleo? Hapana. 

 

Wito wa Mungu, hautegemei mapenzi ya mtu, kazi yake, ila inategemea na lengo ambalo Mungu anataka kulitimiza (Warumi 9:17) 

 

Mungu anapenda jina lake litukuzwe popote ulimwenguni kupitia kwako. Mungu anapenda kukutumia pamoja na udhaifu wako. Sasa usiogope, aliye pamoja nawe ni mkuu na katika jina la Yesu Kristo, mtatenda makuu. Utajitambua kupitia neno la Mungu na kwa ufunuo wa Roho Mtakatifu. Naamini sasa umejitambua. 

 

 

 

 

 

MAOMBI 

 

Maombi ni nini? Ni kuwasiliana na Mungu. tunajua ya kwamba kuna aina mbalimbali za maombi mfano: (maombi binafsi au ya jumuiya), maombi ya kufunga, maombi katika lugha ngeni, nk ……….. sifahamu zaidi, ila najua maombi ni kuzungumza na Mungu. 

 

Mara nyingi, napenda kuomba, na baada ya maombi, naweza kupata majibu ya mahitaji yangu katika Biblia, pia wakati namsifu na kumwabudu Mungu. siku moja, niliota nikaona mtu akinifunika kichwa kwa kitambaa. Nikakataa ila nilikuwa nikiona waamini wapya wakifunika vichwa vyao kwa vitambaa. 

 

Sikuipenda hiyo tabia kwani nilijua haimo ndani ya Biblia. Nilikuwa najua ya kwamba Paulo aliwaandikia Wakorinto 11:1 – 6. “Nilijiuliza, kwa nini mabinti ambao hawajaolewa wanapenda kujifunika vichwa, mstari wa tatu: lakini napenda mjue pia kwamba, Kristo ni kichwa cha kila mwanamume, na mwanaume ni kichwa cha mkewe, na Mungu ni kichwa cha Kristo”. Kama mwanamke anaomba bila kufunika kichwa, anakosa heshima kwa mumewe. 

 

Kama Biblia inavyosema katika Wakorinto wa kwanza 11:4 – 14 ………… basi kila mwanaume anayesali au kutangaza ujumbe wa Mungu huku amefunika kichwa chake, hiyo anamdharau Kristo ……….. endelea kusoma mstari wa 13 na 14. 

 

Ndugu msomaji, sijui vile unavyoamini juu ya vazi lako. Lakini Paulo anasema ya kwamba ni vizuri kuwa mwanamke kuwa na nywele ndefu. Ila ni aibu kwa mwanaume kuwa na nywele ndefu. Mwanamke alipewa shela pekee na Mungu ambayo anatakiwa kuwa nayo waziwazi bila kuificha tena kwa furaha, kwa kuwa imetoka kwenye ghala la Mungu, na hiyo shela ni nywele. Mstari wa 15 “Lakini kwa mwanamke kuwa na nwele ni heshima kwake. Nywele zake ndefu amepewa ili zimfunike”. Napenda kuwaambia dada zangu katika Kristo ya kwamba, usifiche utukufu ambao Mungu alikupatia. 

 

Kitu kingine ni hiki, sio Mungu anayetukuzwa ninapotunza nwele zangu, bali ni mume wangu, hata nikivaa nguo nzuri nikapendeza, ni mume wangu atakayesifiwa na watu. Oh! Angalia mke wa Juvenali alivyopendeza. ! Kutokana na somo hilo, mimi sipendi tabia hiyo ya kuvaa kilemba kichwani. 

 

Nilipoona mtu ananifunika kichwa, nilikataa japo aliendelea kunifunika kichwa. Akaniambia siku utakapoanza kuvaa kitambaa kichwani, nitafurahi . Nilipotoka usingizini, nilimuuliza Mungu, unataka nini kwangu? Mimi, nivae kilemba kichwani? Nikasema haiwezekani. Niliendelea kutafakari ile ndoto, basi nikaanza kuvaa kilemba. Sikujali watu watasema nini juu yangu nilivaa kwa muda wa siku 10. 

 

Asubuhi moja, nikamuuliza Mungu kwa nini kwa muda wa siku 10 nimevaa kilemba huku ndani ya nafsi yangu siamini juu ya vazi hilo, na wala siamini ya kwamba kila anayevaa kilemba kichwani ni mtakatifu, bali Mkristo safi anajulikana kwa matendo yake na mwenendo wake. Siyo hali ya nje inayomkamilisha mtu. Nikaingia ndani ya chumba changu cha kazi(ofisini), na kuanza kuomba kimoyomoyo kwani sikutaka mtu yeyote asikie, bali nilichukua kalamu na Biblia na karatasi yangu ili niandike kile Mungu atakachonijibu. Ndipo Mungu akajibu na kusema, kilemba ulichoona siyo vazi la kimwili kama unavyodhani. Baada ya Mungu kunielewesha juu ya ndoto yangu, nikamuuliza tena, je naweza kuvaa sasa hiki kilemba? Akajibu; “Mpe kaizari yaliyo yake, na Mungu yaliyo yake” (Mathayo 22:19 –21). 

 

Baadayenikauliza juu  ya kile kilemba, aliniambia nisome 1 Samweli 17:39 …….…….  “Siwezi kwenda vitani nikiwa nimevaa mavazi haya, kwani mimi sijazoea”. Kwa hiyo akayavua. Kupitia sura hii Mungu akaniambia ya kwamba, alitaka kunifundisha mambo mengijuu ya kilemba, lakini kwanza niwaambie watu ya kwamba, Mungu hapatikani ndani ya kilemba, bali  kwa mtu aliyepondeka moyo na kuwa safi. 

 

Kupitia ndoto hiyo, Mungu alinipa kazi ya kwenda kuwaambia watu wabadirishe mienendo yao kwani hayupo ndani ya viatu vizuri au nguo nzuri, nk …… yuko ndani ya moyo safi. Ndani ya Kanisa letu, wengi waliamini kwamba kuvaa vilemba ndiyo utakatifu lakini namshukuru sana Mungu kwani kupitia ushuhuda huo wengi walibadilika. Mungu alinipatia tena kitabu cha Ezekiel 13:17 – 23, mstari wa 17 “…….. wageukieni wanawake wa taifa lako ambao wanatabiri mambo ambayo wameyawaza wao wenyewe. Tamka unabii dhidi yao na kuwaambia kuwa Bwana Mwenyezi Mungu asema hivi, “Ole wenu wanawake mnaoosha tepe za hirizi za kuvaa mikononi mwa kila mtu na kutengeneza shela zenye hirizi za kila kimo ili kuyawinda maishaya watu wangu. Mnadhani mtasalimisha maisha yenu wenyewe? Mstari wa 21 …….. Nitazinyanyua shela zenu na kuwaokoa watu wangu mikononi mwenu; nao hawatakuwa tena mawindo mikononi mwenu …..”. ndugu msomaji, ninakushuhudia juu ya kile ambacho Bwana alisema na mimi. 

 

Na wewe wasaidie wengine ambao hawajapata ufahamu juu ya vazi hilo. Utapata ujira wa kazi yako. Baadhi ya Wakristo wanashindwa kuomba bila kuweka kitambaa kichwani. Je kitambaa ndiyo ufunguo wa maombi? Mpaka wengine wanakuwa watumwa wa vitambaa. Wakati mwingine Mungu anatupatia mifano mingi kupitia ndoto, omba tafsiri kwa Mungu. Lakini pia kuwa mwangalifu na ndoto, hakikisha ya kwamba imetoka kwa Mungu, penda kusoma neno, kwa sababu Biblia ndiyo taa katika njia zetu. Omba sana, ili uweze kupindua mipango ya shetani ya kukuangusha. Kichwa cha somo letu kinahusu maombi. Nasisitiza kwamba, majibu ya maombi yetu yako katika maombi, kusikia sauti ya Mungu, n.k ……. Pia anaweza kujibu saa hiyi hiyo au baadaye kama apendavyo. 

 

Majibu mengine ya maombi yaweza kuchelewa, endelea kumtukuza Mungu na ukuu wake, ……… tuangalie mfano wa Daniel na wenzake wakati walipotafsiri ndoto ya mfalme Nebukadeneza, Mungu alijibu haraka kwa sababu angekawia Daniel na wenzake wangeuwawa kabla ya jibu lake kufunuliwa.Kuna Maombi mengine yanahitaji majibu ya haraka kwa mfano: maombi ya kuomba Mungu akupe mtaji wa pesa kwa ajili ya mradi wako. Mungu anaweza kujibu mapema au kukawia, itategemea na uzito wa hitaji lako. 

 

Endelea kuomba siku zote, lakini usisahau kumshukuru kwa kile ambacho amekwisha kukutendea. Pia mfanye kuwa rafiki yako wa karibu na kumuomba ushauri, yupo kwa ajili yako. 

 

Nilipokuwa nasoma darasa la 9 nilimuomba Mungu anifunulie mambo ya kujifunza ili niweze kufaulu katika mitihani. Na niliomba  “Bwana nionyeshe masomo ya kujifunza ili niweze kufaulu mitihani kwani wewe ndiye ujuaye yote Asante kwani utafanya”. Usiku wa siku hiyo Mungu alinionyesha katika ndoto ubao mweusi ukiwa umeandikwa ukurasa na kichwa cha mtihani huo wa hesabu. Asubuhi na mapema nikawaambia wenzangu juu ya ukurasa tutakaofanyia mazoezi. Tuliandika hesabu hizo na kuzitumika, baadaye tukapelekwa katika ukumbi wa kufanyia mitihani. Tukashangaa kuona mtihani tuliopewa ulikuwa ni juu ya hesabu zile zilze tulizofanyia mazoezi asubuhi! Mungu wa ajabu kwani wote tuliweza kufaulu. Hiyo ndiyo faida ya kupenda maombi; usione maombi kuwa kama mzigo, bali yafanye kuwa sehemu ya maisha yako.  Kupitia maombi utaweza kujua makusudi ya Mungu juu ya Taifa lako au familia yako. Wahubiri wakubwa au wa kimataifa kama Billy Gram, Yougnicho na wengine watenda miujiza, sio kupitia umaharufu wao, bali ni watu waombaji sana, wamefanya maombi kuwa kama pumzi zao. Ukitaka kuwa kama wao, jenga tabia ya maombi, na utakatifu. 

 

Kuwa na tabia ya maombi, kwanza kunakufanya ujitambue na kujirekebisha, kwani maombi ya mwenye dhambi hayana kibali machoni pa Mungu. kwa hiyo mara zote utapenda kuishi maisha ya kumpendeza Mungu. na utakapoona umeteleza kidogo, utamuita Roho Mtakatifu akusaidie. Tabia ya maombi pia itakupeleka kupenda kusoma Biblia. Mara zote Mungu anapenda kuwatumia watu wa maombi kufikisha ujumbe wake kwa watu wake. Tabia ya maombi itakufanya kuwa mtu aliyepondeka moyo. Mungu alipomchagua Daudi, hakujali kuwa alikuwa mdogo, bali aliangalia unyoofu wake. Tunaona kwamba baadaye Daudi alimtenda Mungu dhambi, lakini Roho Mtakatifu alimfunulia dhambi yake. Aina maana kwamba tutatenda dhambi kwanza ili tulipe gharama, hapana, siku zote tamani kuwa na woga wa Mungu na kuongozwa na Roho Mtakatifu ili usimtendee Mungu dhambi. Mungu awabariki, Amen.      

 

   

 

SURA YA VI 

 

WATU WA FAMILIA YANGU 

 

Wagalatia 3:26 “Kwanjia ya imani, nyinyi nyote mmekuwa watoto wa Mungu kwa kuungana na Kristo”. Yohana naye anaongeza katika 1 Yohana 3:1 – 2; oneni, basi jinsi Baba alivyotupenda mno hata tunaitwa watoto wa Mungu! na kweli ndivyo tulivyo ……………. Wapenzi wangu, sisi ni watoto wa Mungu sasa lakini bado haijaonekana wazi jinsi tutakavyokuwa. Lakini tunajua kwamba, wakati Kristo atakapotokea, tutafanana naye ……….. 

 

Tunamshukuru Mungu kwa kumtoa mwanaye wa pekee kufa msalabani  kwa ajili ya dhambi zetu. Tulikuwa tumekufa katika dhambi. Biblia inasema ingawa tulikuwa tumekufa kwa sababu ya dhambi, alitufanya hai pamoja na Kristo. (Waefeso 2:4 – 5). Mungu kwa huruma zake kwetu, alifanya tendo hili la kutufia ili kutupatia tumaini la millele. 

 

Ndugu msomaji, Mungu alipojitoa, alitoa uhai wake  ili nasisi tue  hai katika yeye. Uhai wake unapoingia ndani ya mtu unaleta mabadiliko hata kama mtu ni mbaya kiasi cha kuwa adui wa Mungu. lakini uhai wake (damu) inapopenya ndani ya mtu huyo anabadirika kabisa. 

 

Baada ya kumpokea Yesu, nilipata ndugu na dada katika Bwana. Haijalishi dhehebu au matakwa ya madhehebu yao. Mfano, mkatoliki anayesimama kuhubiri huku amevaa hereni na kuweka dawa nywele zake, au ni muanglikana ambaye amevaa kanzu ndefu na kitambaa kichwani, au ni mpentekoste, nk …….. 

 

Upande wangu mimi sikujiwekea mipaka, niliwaona wote ni sawa kwani tumeunganishwa na Kristo.Kilicho tupatanisha na wengine ni “Damu ya Yesu “. 

 

 

Watu wa familia yangu,nazungumzia familia yangu ya Mbinguni. 

Hapa duniani ,tuna familia tofauti.Familia yangu ya Mbinguni,niwale wote waliyempokea Bwana Yesu kama mwokozi wa maisha yao.Yaani,wameingizwa ndani ya utawala wa Mungu,kupitia kuoshwa dhambi zao na Damu ya Yesu. 

Watu hao wako duniani kote.Familia yangu ni pana mno.Na sasa wewe kama hujaingia bado,unasubiliwa kwa hamu kubwa.Saa hii ni muhimu kwako,kukubali na kuingia.Familia hii,ni nzuri sana,sijawahi kuona.Leo katujuane wote,lakini,muda si mlefu,palapanda ya Mungu ikilia,tutakusanyika wote,na kuingizwa kwenye makao yetu ya milele,kama alivyo tuahidi Bwana wetu Yesu.(Yohana14:1-3)”Msifadhaike mioyoni mwenu;mnamwamini Mungu,niamini na mimi.Nyumbani mwa baba yangu mna makao mengi;kama sivyo ningaliwambia;maana naenda kuwaandalia mahali.Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali,nitakuja tena niwakaribishe kwangu,ili nilipo mimi nanyi muwepo.” 

Kaka yanyu,dada yangu,kaza mwendo ujipe moyo,karibu tutafika kwetu.Kumbuka ,hapa duniani tupo kwa muda,lakini tusisahau jukumu letu kuu,ni kujaza watu wengi ndani ya familia yetu.Tuna biashara nzuri,yenye utajili mwingi sana,tumufanyie kazi Bwana aliye tuleta hapa duniani.Tujaze ufalme wa Mbinguni. 

Kwa nini naitwa mtoto wa Mungu? Ni kwa sababu nimezaliwa na Mungu.(1Yohana5:18)”Twajua ya kuwa kila mtu aliyezaliwa na Mungu hujilinda,wala yule mwovu hamgusi.”Aliyezaliwa na Mungu ni mwenyeji wa nyumba ya Mungu pia.( Efeso2:19)”Basi tangu sasa ninyi si wageni wala wapitaji,bali ninyi ni wenyeji pamoja na watakatifu,watu wa nyumbani mwake Mungu.” Tuna Roho moja na Baba yetu wa Mbinguni sisi ni Roho moja  na Yesu.(1 kor 6:17)”Lakini yeye aliyeungwa na Bwana ni Roho moja naye.”Mili yetu ni hekalu ya Roho aliye ndani yetu.Sisi sasa ni mali ya Bwana.(1kor 6:19-20)”Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la RohoMtakatifu aliye ndani yenu,mliyepewa na Mungu?Wala ninyi si mali yenu wenyewe;maana mlinunuliwa kwa thamani.Sasa basi,mtukuzeni Mungu katika miili yenu.” 

 

 

Namshukuru sana Mungu kwa kunifungua macho ya kiroho! Kwani wote waliompokea Yesu kama mwokozi wao, nawapenda kwani ni ndugu zangu, wana wa familia moja, Baba mmoja, Roho mmoja, wana wa Mungu. wakati wa Agano jipya kulikuwa na makundi mawili tofauti, Wayahudi na Wapagani; Wayahudi waliwaona wapagani kama mbwa, walijenga ukuta kati yao ili Myahudi safi asiweze kula pamoja na Mpagani au asiweze hata kuingia ndani mwake hata kuwe na matatizo. 

 

Yesu alikufa msalabani kwa ajili ya Wayahudi na Wapagani, na siku ya Pentekoste aliwamwagia wote Roho Mtakatifu. Hapo ushirika kati ya ndugu ukaumbika upya na watu wakafurahia umoja huo. Ndipo habari njema za msamaha na maisha mapya zikaenea pote Yerusalemu na Yudea. 

 

Mtume Paulo aliandika kwa Waefeso 2:13 – 16 “Lakini sasa kwa kuungana na kristo Yesu, ninyi ambao hapo awali mlikuwa mbali, mumekaribishwa kwa njia ya damu ya Kristo ……….. kwa mwili wake, Kristo aliuangamiza uadui wao; kwa msalaba wake aliziunganisha jamii hizo kuwa  moja na kuzipatanisha na Mungu”. 

 

Baada ya Yesu kufa msalabani na kuvunja mipaka iliyokuwa kati ya ndugu, sasa wote ni kitu kimoja, hakuna Myahudi tena. Hakuna sababu ya kuendelea kujenga ukuta kati yetu, tunapofanya hivyo tunamaanisha kwamba damu ya Yesu haikutupatanisha au haina maana yoyote. 

 

Katika upendo wa Mungu, namchukulia kila mmoja aliyempokea Yesu kama ndugu yangu. Waebrania 2:11,12) “yeye anawatakasa watu dhambi zao naye pamoja na wale waliotakaswa, wote wanaye Baba mmoja. Ndiyo maana Yesu aoni aibu kuwaita hao ndugu zake, kama asemavyo “Ewe Mungu, nitawasimulia ndugu zangu matendo yako. Nitakusifu katika kusanyiko lako. Warumi 8:29 maana hao aliwachagua tangu mwanzo; ndio aliowateua wapate kufanana na mwanaye ili mwana awe wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi. 

 

Nakuombea wewe ndugu ambaye hujaamua kupokea msamaha wa bure kutoka kwa Kristo Yesu. Na kama umeamua kumpokea Yesu, sema maneno haya kutoka kwa Roho wa Mungu: “Karibu Yesu ndani ya moyo wangu”. Ukimkubali utaona maajabu katika maisha yako, pia utapewa jina jipya: mwana wa Mungu, ndugu wa Yesu, mrithi wa ufalme wa Mungu. 

 

Tuombe: Mungu Mwenyezi, wewe uliyemtoa mwanao pekee kufa kwa ajili ya dhambi zetu, nakuomba unisamehe dhambi zangu, zifute kwa damu ya mwanao Yesu Kristo. Natambua kuwa mimi ni mwenye dhambi na ninakukaribisha uingie ndani yangu. Fanya makao ndani ya maisha yangu, nataka niwe mwanao, mmoja wa watoto wako. Ahsante Mungu kwa kunisamehe. Katika Kristo Yesu nimeomba haya, Ameni! Oh! Asante ndugu yangu kwa kuuklubali upendo wa Mungu. upendo unaotuongoza na kutuokoa, kutuponya! Baada ya kumpokea Yesu na kadiri utakavyoendelea katika wokovu, ndivyo utakavyoendelea kukua na kumjua yule uliyempokea. Pia utaelewa mengi kuhusu yeye. Hutakuwa mgeni tena, bali mmoja wa warithi wa ufalme wa Mungu. 

 

Wakristo wengi bado wameweka mipaka kati ya ndugu kwa kusema, oh! Yule siyo wa dhehebu letu, na yule hajaokoka kwani bado anavaa hereni masikioni, na yule ndugu hajaokoka kwani ana ndevu nyingi. Tunaweza kujenga mipaka mingi juu ya wengine. lakini tunapoyajumlisha yote hayo tunatambua kuwa siyo vinavyomfanya mtu awe kamili. 

 

Kitu muhimu ni kumuona mtoto wa Mungu kama ndugu yako. Siwezi kumuacha mtu ambaye Baba yangu anamwita mwanaye. Tuwakubali wengine kama ndugu zetu wana wa baba mmoja katika familia moja 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

UMOJA WA NDUGU 

 

Kupenda kuwa kitu kimoja kumeelezewa vizuri katika Yohana 17:20 – 23 ……… nawaombea ili wote wawe kitu kimoja. Baba! Wawe ndani yetu kama vile wewe ulivyo ndani yangu nami ndani yako ……… mimi nimewapa utukufu ule ule ulionipa mimi, ili wawe kitu kimoja kama nasi tulivyo mmoja. Hayo ndiyo maombi ya Kristo aliyoomba mara tatu ili Wakristo au wamwaminio wote wawe kitu kimoja kabla ya kusulubiwa.Umoja una nguvu. 

 

Baada ya muda mfupi Yesu alielekea msalabani ili kutimiza alichosema kupitia kifo. Waefeso 2:13 – 16, Wagalatia 3:28 “Hivyo hakuna tena tofauti kati ya Myahudi na Mgiriki, mtumwa na mtu huru, mwanamume na mwanamke. Nyote ni kitu kimoja kwa kuungana na Kristo Yesu. Tena “sisi ambao ni wengi tunaunda mwili mmoja katika Kristo”. Mungu anapenda tuwe na umoja katika Roho. Sisi ni kitu kimoja kupitia msalaba wa Yesu Kristo 

Tabia ya watu wa familia ya mbinguni,ni 

 

Kuwa na umoja,pamoja na upendo. 

Watu wanaopendana ,upendo wao unaonekana katika umoja(wanasaidiana,wanomba pamoja,n.k).Lakini,ukitaka kujuwa kwamba Fulani nafulani hawapendani,utakuta,hawana umoja wowote 

Tuwe na umoja,tushirikiane kwenye kazi ya Baba yetu, tuombeane.Tumuombe Mungu abadirishe tabia zetu,atupe Roho ya ushirikiano.Kila mtu amuone mwenzake kuwa ni bora,tutamani kufanya kazi kwa kulitukuza Jina la Yesu,na watu wa mataifa wajifunze kuishi kwa upendo,na umoja.Neno la Mungu linasema, tukipendana Mungu hukaa ndani yetu.(1Yohana 4:12,16)”Hakuna mtu aliye muona Mungu wakati wowote.Tukipendana,Mungu hukaa ndani yetu,na pendo lake limekamilika ndani yetu.Na sisi tumelifahamu pendo alilo nalo Mungu kwetu sisi,na kuliamini.Mungu ni upendo,naye akaaye katika pendo,Mungu hukaa ndani yake” 

.Upendo wetu na Baba udumu.Tunampenda Mungu kwa kushika amri zake,na kutii neno lake(Yohana 14:21,23)”Yeye aliye na amri zangu,na kuzishika,yeye ndiye anipendaye;naye anipendaye atapendwa na Baba yangu;nami nitampenda na kujidhihirisha kwake.Mtu akinipenda,atalishika neno langu;na Baba yangu atampenda;nasi tutakuja kwake,na kufanya makao kwake.”Uhai wa Mungu ndani yetu ,unaonekana ndani ya tabia ya upendo.Tukitengana,Mungu hayupo pamoja nasi,bali ibilisi ameshika usukani.Jichunguze ndugu yangu,umrudiye Mungu naye atakusaidia. 

 

 

“TUONDOE MIPAKA 

 

Kwa imani sisi sote tuliompokea Yesu ni kitu kimoja, lakini wengi wetu hatuna umoja huo bali tunaonyesha kutengana : 

 

Umetengeneza mipaka gani kati ya ndugu yako? Je unajumuika na wenzako, au mpaka awe wa kanisa lako,au wa lugha yako ? Vunja mipaka ya ukabila, dhehebu, rangi, taifa n.k. ……. 

 

Katika Waefeso 2:13 – 16 Mungu alionyesha maana ya kitu kimoja kwa kuwaunganisha wenzangu, weusi, kijani au mzee nk ……… kuwa kitu kimoja pale alipomtoa mwanaye ili awafie wote. 

 

Mungu hajasema usiitwe wa kabila au taifa au rangi Fulani, bali anachotaka ni kwamba tuondoe tofauti zetu kwa wengine kwa kuwa yeye ni mpatanishi, na alikwisha kutuvua mipaka kutuleta pamoja kupitia damu ya mwanaye wa pekee. 

 

Pia anataka kwa umoja huo, wengine watamani kumjua yeye. Tukisoma Mdo 15:1 “Basi watu wengine walifika Antiokia kutoka Yudea wakaanza kuwafundisha wale ndugu wakisema, “Kama  hamtataihiriwa  kufuatana na mapokeo kama alivyoamuru Musa hamtoweza kuokolewa “Watu hao walimaanisha kuokoka ni kutii sheria za Musa. Ujumbe huo kutoka kwa watu wa Yudea kwenda Antiokia hau kuwa mzuri walitaka kuweka mpaka kati ya mtu aliyetahiriwa na asiyetahiriwa. Watu hao walifikiri kuokoka ni kuwa Myahudi: lakini walipokaa pamoja na kujadili juu ya mipaka kati yao wamwachiye Mungu achunguzaye mioyo aamuwe. (Mdo 15:8 – 9), “Naye Mungu anayejua mioyo ya watu, alithibitisha kwamba amewakubali kwa kuwapa nao Roho Mtakatifu kama alivyotupa sisi”. 

 

Je unawakubali Wakristo wengine ambao wanatofauti na wewe? Husemi kwamba siwezi kushiriki na wewe kwani unaabudu Kanisa tofauti na la kwangu? Au kama unasali tofauti na dhehebu langu hujaokoka. Au bado unaamini kuokoka ni kutahiriwa? Au unamshuhudia mwingine kuacha dhehebu lake na kuja Kanisani kwako? Je unaamini kwamba Kanisa lako ndilo lina misingi sahihi ya Kikristo? 

 

Mungu akufunulie zaidi. Mungu, kwa kudhihirisha kuwa amewakubali alijaza Roho Mtakatifu. (Mdo 15:8) kwa kuwa tunaamini kuwa tunaokolewa kwa neema, basi tuamini pia kuwa Mungu anaangalia utu wa ndani. Kwa nini kuweka mipaka kwa mtu aliyeamini neno la Mungu na kwa kuwa mwana na ndugu wa Kristo Yesu (Mdo 15:9). Je wewe ni wa muhimu zaidi ya Mungu aliyeonyesha upendo wake kwao? …….” Kwani umjaribu Mungu kwa kuwabebesha Wakristo wengine mizigo? (Mdo 15:10). 

 

Rafiki katika Bwana, mungu atusamehe! Na atupe mtazamo mpya. Sisi sote ni wasafiri, tunaelekea kwa Baba yetu mmoja, basi natushikane mikono, ili kwa pamoja tuweze kumshambulia adui yetu, tuombeane, tuivue mipaka tuliyojiweka kati ya Wakristo wa makanisa mengine. Tuwapende hata wale ambao bado wako nje ya kundi letu. Mungu anawakubali kama walivyo, pamoja na tabia zao na mila na desturi zao. Tujivue mipaka ili tuweze kumuona Mungu.Mipaka inazuia watu wasipendane,wasishirikiane.Mipaka kati ya watoto wa Baba mmoja haifai. 

Tunapashwa kuweka mipaka katiyetu na shetani ili tusishirikiane kwenye kazi zake.lakini ,katika familiya yangu natakiwa kujenga marafiki wengi,ikiwezekana wote.Maana,tukiungana ,tunamshambulia adui yetu kwa nguvu zote. 

 

Attention!,Angalia usije ukapokea imani potofu kwa kuwakubalia wenye imani nyingine eti nao ni wana wa Mungu,eti ni watoto wa  familia yako.Angalia pia,usiwabaguwe watu wa familia yako,eti kwa sababu hawaabudu kwenye dhehebu yako,au ukitazama mavazi,jinsi ya kujipamba n.k.Sisi,watu wa dunia hii,mambo ya Mungu tunayajua kiasi,lakini tunamshukuru Mungu kupitia Roho wa Mungu aliye ndani yetu,tunafunuliwa kidogo kidogo.Kwa maana hiyo,kama unaona mtu wa familia yako ana mwenendo siyo mzuri,unamuonya kwa upendo.Tuna kazi ya kujenga watu wenye tabia nzuri ya kimungu kupitia mafundisho.Kwa maana hiyo,tusibaguwe wapendwa wenzetu,bali tuwafundishe,na tuwaeleweshe,kama Roho wa Mungu alivyo tufundisha na sisi,au kama neno la Mungu lilivyo tufundisha,ili na wenzetu wabadirike mwenendo. 

Tunapashwa kutiana moyo,na kusaidiana kama watoto wa Baba moja.Sisi,tukumbuke kwamba ni wasafili.Tusisinzie,bali tuamke,tujiweke tayali kwa unyakuo.Kila mtu atahukumiwa kulingana na matendo aliyoyatenda hapa duniani.Tutahukumiwa kulingana na Amri kuu.(Marko12:30-31)”Nawe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote,na kwa Roho yako yote,na kwa akili zako zote,na kwa nguvu zako zote.Na ya pili ndiyo hii,Mpende jirani yako kama nafsi yako.Hakuna amri nyingine iliyo kuu kuliko hizi.”Tukifika,Yesu atasema,nilikuwa nanjaa,nilikuwa na kiu,nilikuwa naumwa,nilikuwa kifungoni hamkuja kuniona.Tujuwe,tukiwafanyiya wenye mahitaji,tunamfanyia Yesu Mwana wa Mungu.(Matayo25:31-46). 

Tufanyie wote mema,sanasana,watu wanyumba yetu aufamilia yetu.Amen. 

 

 

SURA VII 

 

MAHUSIANO YAHUSUYO MWENENDO WA MKRISTO 

 

Katika safari yetu ya kwenda Mbinguni, tunakutana na vikwazo vingi na kati ya vizuizi hivyo vipo vingine ambavyo ni mitego inayoweza kuturudisha nyuma au kuchanganya sauti au matakwa ya Mungu na ya mwanadamu. Matatizo hayo pia yanatupelekea kujulikana kwa msimamo wetu kiroho. Tunajua ya kwamba %kristo halisi ni yule anayetambua kuwa kunywa pombe, kuvuta sigara, kwenda katika muziki, kuvaa suruali (kwa binti au mama) nk ……… ni dhambi. 

 

Siku moja nilishangaa kumuona mchungaji (hakuwa wa Kanisani kwangu) alikuwa akinywa pombe katika ukumbi mmoja wa starehe. Nikaanza kuchambua Kanisa lake na kusema hawajampokea Roho Mtakatifu, na pia siyo wasomaji wa neno. Mungu anisamehe. Siku nyingine nilimuona ndugu aliyeokoka akimsalimu dada mwingine aliyeokoka kwa busu. Niliumia sana na nikawaweka katika kundi la wapagani, ilikuwa vigumu kwangu kuwakubali watu waliokuwa na tabia tofauti na za kwangu. Hatua kwa hatua Mungu aliniponya, nikaondokana na tabia hiyo. Na kwa mapenzi yake nami nawafundisha wengine. 

 

(Marko 7:5 – 8) jioni moja, Wafarisayo walishangaa kuwaona wanafunzi wa Yesu wakila bila ya kunawa mikono, na wakamuuliza kwa nini wanakula kwa mikono najiisi? Yesu akawajibu waziwazi “……… ninyi mnaiacha amri ya Mungu na kushika maagizo ya watu” tena akasema. “kama mimi nilivyowapenda, nanyi pia mpendane”  akasema hiyo ni amri mpya. 

 

Tutakapowatenga wengine kwa ajili ya matakwa ya mtu na kuacha kutii amri tuliyoachiwa na Mungu ya kwamba tupendane, hatutakuwa na tofauti na Mafarisayo. 

 

Tuchukulie ya kwamba moyo wa Mkristo haukujengwa na uzoefu tulionao. Tusome Marko 7:18, 21 maana, kutoka ndani, moyoni mwa mtu, hutoka mawazo mabaya, uasherati, wizi uuaji. Kutokana na sura na mistari hiyo, hatuna kazi ya kuhukumu mwingine kwa kumuangalia hali yake ya nje. Na wala hatuna haki ya kutunga sheria juu ya mtu. “Mstari wa 19. kwa maana hakimwingii moyoni, ……” mstari wa 20. kitu kinachotoka ndani ya mtu ndicho kinachomtia najisi. 

 

Jambo la pili, tunakuta katika kitabu cha (Wakolosai 2:21 – 23) “Msishike , Msionje , msiguse (mambo hayo yote huharibika wakati wa kutumiwa);hali mkifuata maagizo ya wanadamu? Mambo hayo yanaonekana kwamba yana hekima,katika namna ya ibada mliyojitungia wenyewe,na katika kunyenyekea,na katika kuutawala mwili kwa ukali;lakini hayafai kitu kwa kuzizuia tama za mwili.” 

Tumeona kwamba yote hayo ni maagizo ya kibinadamu juu ya vitu viharibikavyo.Sheria ya mwanadamu haina nguvu ya kuizuia tamaa ya dhambi.Bado,watu wanaenderea kutenda dhambi.Damu ya Yesu tu ndiyo yenye nguvu,kuzuia kiu ya pombe,kukomesha uharibifu wote ndani ya mtu. 

 

Tunaweza kusema kuwa kutunga sheria nyingi nyingi juu ya vitu mbalimbali, juu ya kuukalia wokovu. Tutakapoanza kuweka matabaja juu ya watu wanaokula au kugusa vile ambavyo tunaviona kuwa dhambi, basi tutawapoteza tunapashwa   kuwapenda kama walivyo. Tuwaongoze kwa upendo na sio kwa sheria zinazowahukumu.Paulo,anawaambia wa kolosayi kwamba,msiguse,msionje,msishike,vinaonekana kwamba ni vitu vyenye hekima.Anasema tena kwamba sheria hiyo,inatawala mwili kwa ukali.Anasema tena kwamba vinaonyesha unyenyekevu.Paulo,anawasifia sana jinsi gain walivyojitahidi kuzuia watu ili wajilinde wasiharibikiwe na pombe,maan ni mbaya,inaleta madhara mengi.Lakini pomoja na hayo ,anonyesha kwamba sheria hizo hazifai kuzuia tamaa.Maana izo ni sheria watu waliyejitungia tu.Anasema “katika ibada mliyojitungia wenyewe.” 

 

Ndiyo, kuna ukweli wa malengo. 

  

 

Yawezekana tukawa na lengo moja katika kutumika, bali kwa kuwa tumeumbwa tofauti na kila mtu na vile anavyoelewa maandiko. Hivyo kila mmoja atatumia ujuzi wake kibinadamu au hata kiakili ili aweze kutimiza malengo ya kazi yake. Sasa basi, tusimame juu ya msingi tuliopokea pale tulipompata Kristo, akafanyika kuwa mwalimu na kiongozi wetu. Tuishi sawasawa na neno lake na siyo ya kwenda kwa akili au mapokeo ya kidunia. (Yohana 16:13)”Lakini yeye atakapokuja,huyo Roho wa kweli,atawaongoza awatie kwenye kweli yote;kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe,lakini yote atakayoyasikia atayanena,na mambo yajayo atawapasha habali yake.” 

 

 

Ushuhuda 

Siku mmoja,mme wangu alinipa hitaji niliombee.Alikuwa hajaokoka,lakini alikuwa anakwenda kanisani.Aliniambia eti nimuulize Mungu kwamba kunywa Pombe ni dhambi.Nilimuuliza,je nimekosa cha kuombea hata nimusumbuwe Mungu namna hiyo? Akasisitiza,wewe Omba tu.Nikaomba kama kidogo tu “Mungu,mmewangu aliuli eti kunywa pombe ni dhambi?” Siku hiyo jioni nikaota tuko pamoja na wakristo wengi kutoka madhehebu mengi.Nikaona niko pamoja na wale wenye shuguli nikaona jinsi wanavyo changanya maji kwa kuwaandaliya vinywaji,mkutano muzima.Sasa nikaona wanawapelekea kinywaji kimoja kutoka kwenye unga wa mtama.Nikaona wengi kutoka kanisani kwangu (pentekosti)wakakataa kupokea kwasababu kwetu kutumia kinywaji hicho ni dhambi.Nikaona Mchungaji moja tunaye mpenda sana nay eye yuko pale.Washirika wake wakamuperekea malalamiko kwamba watu wamewaletea pombe,wanawaletea majaribu.wakaenderea kusema eti hawa watu hawajaokoka hwamujui Mungu.Nikaona wana pokea maji kwenye kilahuli.Huyo Mchungaji akawajibu,kwa ukali na kuwakemea akasema,nyinyi mnasema mumeokoka lakini hamujui maandiko!Kitu chochote kiingiapo tumboni hakiwezi kumunajisi mtu kwa sababu kitatoka nakuingia chooni.Lakini kinacho najisi mtu ni kile kitokacho moyoni mwake.Akaenderea kuwekemea na kuwaonyesha kwamba wao ndio hawajaokoka kwa sababu moyoni mwao bado kuna kiburi,na kuhukumu wengine.Kisha nikawaona wanainamisha vichwa vyao kwa aibu.Ndipo nikazinduka kwenye ndoto hizo. 

Nilipata shida kumperekea mume wangu jibu hilo.Maana niliona,nikimwambia hayo ,mojakwamoja ataendera na ulevi wake.Lakini niliomba Mungu sana alafu nikamwambia.Nilipomwambia alishukuru sana akaendera napombe,nami akataka kuniingiza kwenye pombe lakini mimi nikakataa. Akaniuliza kwanini nisitumii ,nikasema,mimi ndani ya Yesu nina uhuru katika vyote.Lakini ninatumia vile tu ambavyo vinanisaidia maishani mwangu.Hatakama nina uhuru kwa vyote,vile njuwa vinaweza kuniharibu sivitumii,kwa usalama wangu.Nikamwambia,najuwa pilipili ninzuri kwa wale wanayeitumia,lakini mimi nayichukia maana inaniumiza. 

Namshukuru sana Mungu jinsigani ni wa ajabu.Mume wangu aliokoka akaachana na pombe maana anashuhudia mwenyewe kwamba haiwezi kunajisi mtu lakini inaweza kuharibu ushuhuda wa mtu.Nashukuru sana makanisa yetu ya Kipentekoste ametuzoeza vizuri,kutotumiya vinywaji vilivyochachuka.Lakini pia wangetwambia kwamba si dhambi mtu akaacha kwa hiali yake. Shetani ni mjinga sana ni mpotofu,kila saa anawahubilia watu waache ukweli wa Mungu na kuzingatia maagizo ya wanadamu. Na sasa ndivyo anavyofanya kwenye makanisa mengi.Watu wameacha pombe kabisa,hawatumii,wanajitesa sana huku wakijuwa eti wameokoka lakini,bado hawajaokoka maana mpaka leo,ni wizi hawamtolei Mungu fungu la kumi,bado ni wazinzi ,fitina, chuki,ukorofi,mawazo mabaya ,majivuno na mengine mengi….(Marko 7:21-22).Watu wengi,wamejitahidi kutetea neon la Mungu,lakini mimi na wewe hatuwezi kulitetea,Roho mtakatifu tu ndiye anayeweza,maana analielewa vizuri.Tuombe Mungu na tupende kujisomea maandiko.Yesu mwenyewe aliwauliza wanafunzi wake akawambia hata ninyi hamna akili?Hamfahamu ya kwamba kila kitu kilicho nje ya mtu,kikimwingia,hakiwezi kumtia unajisi;kwasababu hakimwingii moyoni, ila tumboni tu;kasha chatoka kwenda chooni?Kwakusema hivi alivitakasa vyakula vyote.(Marko 7:17-19).Hapa wanafunzi nao walishangaa kuona Yesu mwenyewe anasema hayo.Ni sawasawa na wewe unavyo nishangaa kwa kusoma hayo.Unatamani mtu mwingine asije akavisoma.Lakini kama Yesu mwenyewe amevifungua wazi kwa mafarisayo kwanza,akiwaonya makosa wanaofanya kwa kuacha maagizo ya Mungu na kuzingatia sheria wanojitungia wenyewe,Yesu hata uwe nani,hawezi kushirikiana nawe kama unageuza amri ya Baba yake,yaani Mungu.Wanafunzi wake,tunasoma jinsi wali muuliza wakiwa faragha.”Hata alipoingia nyumbani na kuuacha mkutano,wanafunzi wakamuuliza habari za ule mfano.”Mstari wa17.Mfano huo alikuwa ameusema ni mfano gain? Yesu,mafarisayo wamewashtaki wanafunzi wake eti wanakula bila kunawa mikono,na kitendo hicho wanahisia kwamba ni unajisi huo.Ndipo Yesu sasa akawambia kwamba unajisi siyo kitu kiingiapo tumboni bali nikitu kitokacho moyoni nicho kinacho munajisi mtu.Ukisoma Marko 7 yote utaona na mengine walikuwa wameyageuza waka acha amri ya Mungu wakafuata maagizo ya wanadamu.Mstari wa 10na11 unaonyesha jinsi walivyogeuza ile amri isemayo kuhusu kuheshimu wazazi.Yesu alikuwa anawaonya,ili wazingatiye amri ya Mungu.Turudi kwenye ile ndoto,huyo Mchungaji niliye muona si mwingine nafikili ni malaika wa Mungu alitumwa ili kutukumbusha maandiko.Hao washirika wake walisema na kiburi nakuonyesha kwamba hao wengine ni wapogani kabisa.Aliwakemea na kuwaonyesha kwamba amri ya Bwana inatuagiza kupendana,siyo kuchukiana kwa sababu hazina msingi.Tumruhusu Roho wa Mungu atufunurie na mengine ili tutende sawaswa na mapenzi ya Mungu.Tuihubili neno,tusigeuze.Bibliainasema (Mithali20:1)”,Mvinyo hudhihaki,kileo huleta ugomvi;na akosaye kwa vitu hivyo hana hekima”.Je kwa nini ujiletee ugomvi,na hapo ukijuwa kwamba ugomvi una munajisi mtu maana huu unatoka moyoni?Mpendwa nakushauri,pamoja na kuwa vyakula vyote vimetakaswa,jihadhali sana shetani asije akakudanganya,eti mbona wengine wanatumia lakini niwazima?Je,unaweza ukaona watu wanaogerea kwenye bahali,tena wanatoka kwenye maji salama,lakini isiwe sababu yakukupeleka wewe huko kwenye maji maana huko ni kwenye hatali kubwa.Wewe kama hujui kuogerea mara mmoja utazama, pia utakufa.! 

Pia, 

 

 Ni dhambi kubwa kulewa mvinyo,maana neno la Mungu linatuagiza kujazwa Roho mtakatifu. 

 

Katika huduma tunaweza kutofautiana katika katiba, ila kwa kuwa tunaunganishwa katika upendo wa Kristo, Roho Mtakatifu atatusaidia kuchukua mizigo au udhaifu wetu. Mdo 18:26 

 

Tumeona mfano mzuri katika sura hiyo, tumejifunza kuwakubali wengine wakiwa wachanga, basi sisi tuliokomaa kiroho tuwasaidie kufikia pale tulipo,na sisi pia tutamani kusonga mbere maan hatujafika bado. Tunaona vile Prisila na Akila walivyomchukua kwao Apolo, ambaye alikuwa akifundisha maandiko bila ya kuwa na ufahamu wa maandiko. Lakini Prisila na Akila walimfundisha, tena kwa upendo, kwani walimchukua kwao. 

 

Tunatakiwa kuiga mfano huo, iwapo mmoja kati yeti atatereza kidogo, basi na tumwite pembeni na kumsaidia ili awe mtumishi mzuri, kama alivyokuwa Apolo baada ya kufundishwa kando. 

 

Kiu yangu kubwa ni kutaka kuona kila mtu akifika hatua ya kumkubali mwingine kama alivyo, na kuweza kuwasaidia wengine wakue na kukomaa kiroho. 

 

Ndani ya Kanisa, kuna watu wa aina mbili. Walioamini na wasioamini. Na wote wanaruhusiwa kulisikia neno la Mungu. sasa wale ambao hawajabadilishwa nao wana mambo yao. Endapo tutawatenga kwa kuangalia yale wafanyayo, bado hatutakuwa tumewaonyesha upendo wa Kristo. Na tunaweza pia kuwapoteza. Mathayo 13:24 – 30, 36 – 43). Mungu mwenyewe atatenganisha magogo na ngano siku ya mwisho. 

 

Kwa kuwa tunatofautiana, basi kila mmoja ana aina Fulani ya maisha anayopenda kuishi. Kwa mfano: mmoja anaamini kula vitu vyote ni dhambi, na mwingine anaamini kula mboga za majani tu ndio sahihi, mwingine anaaamini kwamba siku zote ni sawa, na mwingine anaweza kusema hapana siku moja tu ndiyo ya muhimu. Watu wote hawa ni wa Mungu hatuna haki ya kumuhukumu yeyote kati yao, tuwaache kama walivyo na kuwakubali kama walivyo. Tufuate vile Biblia inavyosema. (Warumi 14:1 – 2) 

 

Kuwakubali wengine hata wenye imani dhaifu kunapelekea au kunaumba hali ya kutomkwaza ndugu yako (Warumi 14:1). Mkaribishe kwenu mtu aliye dhaifu wa imani lakini msibishane naye juu ya mawazo yake binafsi. Mstari wa 14:14,  “Katika kuungana na Bwana Yesu, nina hakika kwamba hakuna kitu chochote kilicho najisi kwa asili yake: lakini mtu akidhani kwamba kitu Fulani ni najisi, basi kwake huwa najisi.” 

 

 

 

Msafiri mwenzangu, penda sana kulisoma neno la Mungu, ili uweze kukua na kujua kutofautisha maagizo ya Mungu na mapokeo ya katiba ya madhehebu yetu ambayo yanaongozwa na watu. Tukijua ya kwamba Mungu anahukumu kutokana na amri zake na siyo katiba na sheria za watu. Pia tusisahau kwamba sote tunajenga mwili wa Kristo japo Mungu alitupatia vipaji tofauti. 

 

Hivyo, tuungane pamoja katika Bwana, tupendane, tusaidiane kwa pamoja tumshambulie adui yetu, na siyo kushambuliana sisi kwa sisi. Kile unachoamini kuwa ni sawa machoni pako, basi fanya kwa ajili ya Bwana. (Warumi 14:22 – 23). Usiharibu kazi ya Mungu au usiwe sababu ya anguko la mwingine kwa kile unachoamini juu ya vyakula nk ……….. 

 

Ndugu msomaji wito mkuu kwetu sisi ambao ni watoto wa Baba mmoja wa kuishi kwa amani, na bila kumkwaza mwingine. Ukijua ya kwamba Mkristo safi, ni yule anayefanya kitu kwa faida ya mwingine, na siyo ya kwake binafsi: Warumi 14:21, 1 Kor 10:23 – 24, 1 Kor 10: 32 – 33. 

Mungu atusaidie na atusamehe kwa yale tuliyowatendea ndugu zetu, kwa kuwakandamiza,kuwahukumu, na kwa kutoonyesha upendo wa Mungu kwa ndugu zetu. Mungu atusaidie kuanza upya katika kuchukuliana mizigo. Pia atusaidie kuendelea mbele. 

 

Mungu atubariki, Amen 

SURA VIII 

 

SHUHUDA 

 

Ushuhuda wa kwanza: “Muujiza kati ya nyingine” 

 

Ndugu msomaji, ninazo shuhuda nyingi, na kati ya hizo nimechagua shuhuda chache muhimu zitakazokusaidia. 

 

Kama ulivyokwisha kusoma katika kurasa zilizopita ya kwamba, nilimpokea Yesu nikiwa na miaka 7. Na mpaka sasa nina miaka 35 bado naendelea na Bwana, pia nimeuona ukuu wake. Mungu aliyenitumia tangu nikiwa mdogo, ndiye huyu anayenitumia mpaka sasa kwani yeye habadiliki. Na anaweza akakutumia hata wewe, kwa kuwa yeye hajali umri, umbo, nk ….. vyovyote ulivyo Mungu anaweza akakutumia, lakini uwe tayari. Nakumbuka katika umri huo mdogo niliweza kufundisha watoto wa umri wangu habari za Yesu, na Mungu aliponisaidia kutoka masomo ya chini na kuanza masomo ya juu, bado niliwaleta wengine kwa Yesu. 

 

Mwaka 1985,nilikuwa nasoma mwaka wa 9, Mungu alitenda muujiza kwangu. Nilikuwa katika ndoto, nikaona kundi kubwa la watu wakiimba  kwa furaha, kati yao akatokea mtu mmoja akaja pale tulipokuwa mimi na rafiki yangu( Noadie Manirabona), akasema kwamba sisi pia tunaalikwa kuungana na kundi lile la waimbaji ili tumwimbie Bwana, lakini twende kwanza kuwaaga wazazi wetu Ili wajuwe tumeenda wapi.Rafiki yangu ambaye alikuwa akiishi karibu ya sehemu hiyo , alikimbia na kwenda kuwaambia wazazi wake, na baada ya muda mfupi alirudi na kuniambia kwamba ameruhusiwa aende kujiunga na kundi lile ,ndipo aliniambia ;” natanguria mimi na wewe utanikuta pale “nami nikaenda haraka sana kuwauriza wazazi wangu nami waniruhusu niende nikawambia jinsi yule mtu ametwambia yote,lakini nilitoka kwenye ndoto hiyo bila kujua kwamba nimeruhusiwa au bado.  Ndipo nikaanza kumuuliza Mungu maana ya ile ndoto. mungu akaniambia, watu ulioona wakiimba kwa furaha, siyo wa duniani tena, bali ni watu waliokufa wakiwa wamemjua Bwana. 

 

Jambo la pili, kwanini mtu huyo alituomba twende kwanza kuomba ruhusa kwa wazazi wetu.? Jibu lake ni kwamba: Roho Mtakatifu ametufahamisha kwamba tumepewa mwaliko wa kwenda kuungana na watakatifu wa Bwana wako huko mbinguni.kazi yawo nikumsifu Mungu kila wakati. Nikauliza swali ya tatu ; kwanini rafiki yangu(Noadia Manirabona) aliniambia kwamba ametanguria nami nitamukuta kule? Ndipo Bwana akanifunguriya ufahamu kwamba binti huyo arisha fariki mwaka 1 uliyo pita  . lakini ,zingatiya lile alipo sema kwamba nawewe muda simrefu utamukuta hukohuko. 

 

Baada ya ufafanuzi huo, nilikosa raha kabisa, muda wote nilikuwa nikitetemeka, nilijua kwamba muda si mrefu nitakuwa maiti na ndipo nilipopata andiko la Petro wa Pili, 1:14 “Najua kwamba karibu nitaweka kando mwili huu wenye kufa kama Bwana alivyoniambia wazi wazi. » 

 

Nilimuomba Mungu mambo matatu: 

 

1.    Nilimuomba Mungu nikasema, basi nikifa, nataka nizikwe karibu na nyumbani kwetu ili wazazi wangu wasipate taabu ya kutembea mwendo mrefu. 

2.    Mungu anitakase nife nikiwa mtakatifu. 

3.    Na kwa kuwa nimepata mwaliko huo tayari, nilipenda kwanza kuaga rafiki zangu wajue kwamba naenda Mbinguni. 

 

Zingatia: Ndoto hiyo niliipata mwaka 1984, mwezi wa nane .Mwezi wa tisa tulianza mwaka wa shure ili tumalize  muhula wa kwanza  mwezi wa kumi na mbili.,huku nikiwa bado na siri hiyo ndani yangu. Pamoja na kuwa niliwapenda sana washirika wenzangu wa kikundi cha maombi lakini sikuwaambia chochote kuhusu ndoto yangu hiyo. Lakini kabla ya kwenda likizo ya muhula wa kwanza, nilipata tena ndoto nyingine, niliona mwili wangu ukigawanyika vipande vipande , mara hii sasa nikamuadithia dada moja rafiki yangu, ambaye alishangaa na kunitamkia waziwazi kwamba ndoto hiyo inasema kwamba  nataka kufa. Ndani ya moyo wangu nilijua kwamba sasa ni wakati wa Bwana kutimiza kile alichonionyesha . Sasa nikaanza kuwaaga rafiki zangu, niliwatakia mapumziko mema na sikukuu njema ya Noel na mwaka mpya. Lakini niliwaambia kwamba yawezekana hawataniona tena, japo waliniuliza maswali mengi, ila sikuwa na wajibu zaidi ya kuwapa andiko la Petro wa pili 1:14.Tumeenda likizo kila mwanafunzi kwao.Nilipofika nyumbani,mapumziko yangu yalijaa mawazo. Siwezi kuelezea vile nilivyokuwa nikijisikia katika likizo hiyo, nilijua nitakufa lakini sikujua lini, na vipi. Usiku wa kuamkia siku ya kurudi shule, nilipata ndoto iliyokuwa na mambo muhimu matatu: 

 

1.    Nilisika sauti ikinikataza kwenda pamoja na wengine shuleni siku ya kufungua shule. 

2.    Niliona mwili wangu ukiwa umewekwa chini, na umegawanyika vipande vipande, watu walikuwa wakilia sana,na kuweka vumbi kwenye mwili huwo.nikasikia sauti ikisema tukio hio itatokea jumatatu talehe 7/1/1985. 

3.    Jumapili utapata wageni wawili msichana na mvulana, utapenda uwaambie vile unavyojisikia, lakini utawaogopa watu watakaokuwa pamoja nao. 

 Nilitii   sauti ya Bwana,  kesho yake ilikuwa jumamosi sikuenda pamja na wengine shuleni(nilikuwa boding), Jumapili yaani kesho yake nilielekea Kanisani, huko nikakutana narafiki yangu mwingine jina lake  (Niyongabo Emmanuel). Nilimueleza huyo ndugu juu ya ndoto zangu, ndipo akaanza kuniombea ili Mungu aniongezee siku kama alivyofanya kwa Hezekia  ili niweze kumtumikia.(2Wafalme 20:5-6)”…Rudi,ukamwambie Hezekia, mkuu wa watu wangu,Bwana ,Mungu wa Daudi baba yako asema hivi ,Nimeyasikia maombi yako ,na kuyaona machozi yako ;tazama ,nitakuponya ;siku ya tatu utapanda nyumbani kwa Bwana.Tena, nitazidisha siku zako,kiasi cha miaka kumi na mitano,nami nitakuokoa wewe na mji huu….” Baada ya kumaliza maombi hayo, nilimsindikiza huyo ndugu, ndipo niliporudi nyumbani na nikafunga geti maana ilikuwa mida ya saa moja usiku.Nilimaliza kufunga geti tu gafla nikaona wageni wengine wanagonga ni lipo fungua nikawaona watu wawili  (mwanaume jina lake Salvatori Sindayigaya na msichana aitwaye Jeanne Ndikumana) walikuwa wakija kutuona. Nikapiga kelele ya shangwe,oh! Bwana unanipenda! 

 

Niliwapokea wageni hao kwa shangwe na tukaomba pamoja, na pia tukatiana moyo na maneno mengi usiku huo ilikuwa tarehe 6 /1/1985 nikakumbuka kuwaambia juu ya ndoto zangu,(nilikua nakumbuka kwamba kesho yake nitaaga dunia kwa ajali,lakini tuliomba na rafiki Emmanuel Niyongabo,sijui kwamba Bwana amekubali kuniongezea siku kama alivyofanya kwa Hezekia au la.) 

 

  Baadaye  nikajiuliza kwa nini Mungu alinionyesha wageni wawili na ikatokea? Kwanini aliniambia nisiambatane na wenzangu siku ya kufungua shule? Sikupata jibu, bali nilikuwa nikiangalia saa yangu ya mkononi mara kwa mara ili kusubiri muda wangu .   Ndipo nikajiuliza hivi mbona yale yote Bwana aliniambia ametimia ;[kutokuenda shuleni pamoja na wengine, kuona wageni musichana na muvurana] ndipo nikawaza sana juu ya tarehe 7/1/1985 nikasema bila shaka kesho nitakufa kama vile Mungu alisema. 

 

Nikajiuliza je awa watu wamekuja kulala kwetu nisipo waambia wanaweza wakakasirika kwa nini sijawaambia.nikataka kuwaambia lakini nikaogopa kaka yangu alikuwa pamoja na si.pia alikuepo binamu yangu .Niliogopa kusema hayo wakati hao watu wako huko nilijua kwamba watalia sana na wazazi wangu watajua yote.kwa hio nikaogopa. Nikarudia ile ndoto inayo sema ;utakuwa na wageni utataka kuwaambiya hali yako lakini utaogopa watu watakuwa pamoja na wageni hao.  Nimerazimika kuwaambia ili wajuwe kesho yake kuna nini. Tulikesha kwa maombi mpaka asubuhi.nilijiandaa kwenda sasa shule nikapanda gari nikiimba na sauti kubwa ili waabilia wote wasikie injili kwa sababu niliogopa kwamba wameweza kufa bila kusikiya injili na kutubu .nimewahubiria kwa uwezo wangu wote.nimemuuliza mama mmoja ,je umeokoka?utafanyaje hiyi gari ikifanya ajali?akasema Mungu haweze kufanya hivyo na mtoto huyu mgomgoni. nilianza kumshuhudia yule mama habari za Yesu na kumuuliza kama yuko tayari kumpokea Yesu 

 

Baada ya kusafiri kwa kilomita chache, nilisika sauti ikiniambia: “Angalia mahali mlipo! Ni hapa ndipo ajali ingeweza kutokea, lakini kwa sababu ya maombi yako, nimewaponya. Baada ya dakika chache lile gari lilipinduka, sikuelewa ilikuwaje, ila nilisikia watu wakisema: “Bila maombi ya binti huyu mdogo tungekufa sote” na yule mama aliyebeba mtoto naye alisema; “Mimi binti huyu aliniambia kuwa tutapata ajali nikabisha,wote wakanishangaa. lakini namshukuru Mungu kwani hakuna aliyekufa wala kuumia kati yetu. 

 

Ndugu msomaji, Mungu ni mtenda miujiza. Kile alichowafanya watu enzi za kale , hata leo anafanya. Kifupi ni kwamba nilifika shule ambapo nilikuta wenzangu walinipokea kwa furaha, na wengi wao waliniuliza maswali mengi. Wengine waliniuliza maswali yaliyomaanisha kuwa mimi ni Nabii wa uongo, wengine wakaniuliza nimefufuka lini. Maswali yote hayo sikuyajibu haraka, nilikasirika na kujiuliza kwa nini niko hai, ndipo nikamwambia Mungu anipe jibu la kuwapatia wenzangu ili muujiza alionitendea usiwe jambo la dhihaka na utani. Mungu akaniuliza, “siyo wewe uliyeomba nikuongezee siku?nikasema ni mimi nimeomba hilo . Tena ukaomba uzikwe karibu na nyumbani kwenu ili wazazi wako wasipate kutembea mwendo mrefu? Nimejibu ni mimi nimeomba hilo.ndiyo maana nimekukatalia usiende shure pamoja na wengine.ili iyo ajari iwepo wakati yuko karibu na nyumbani yako sawa na ulivyoniomba. Nikaendelea kumuuliza “Ulimiongeza Ezekieli miaka 15, je mimi umeniongezea miaka mingapi? Je, ikiwa kama myaka 100 sitochoka kukufuata(kuenderea na wokovu) halafu iwe hasara kwangu kuliko ungenichukua  nilipokwa tayari?. 

 

Jibu   ;  nilikuwa kwenye chumba cha maombi(wakati na muuliza Mungu maswali yangu ya uchungu) na ndani ya chumba hicho harikuwepo kabati ya vitabo vya wa padri(shule hio ilikuwa ni shule ya wa katholiki,na chumba hicho walikuwa wanakitumia kwa maombi) . katika maombiyangu hayo nilisikia sauti ikiniambia: “nenda kafungue kabati na utapata jibu lako katika moja ya kitabu utakachokikuta humo.” Nilikuwa na mashaka na sauti hiyo kwani hapo chumbani palikuwa na vitabu vingi. Kwa hiyo sikuweza kuitii sauti hiyo. Lakini iliendelea kusisitiza. Basi niliomba Mungu,nikasema,kama hii sauti imetoka kwako,nakuomba unisamehe kwa kutoitii.Nikanyanyuka nakuerekea ile kabati ya vitabu nikaanza kupekuwa vitabu.Nikaona kitabu kimoja cha nyimbo sauti ikasema jibu lako lipo ndani ya kitabu hicho,nikakipekuwa nikakuta barua iliyoandikwa yafuatayo:”Ma fille,ce que je voulais que tu saches ce que tu n’as plus a`t’inquie’ter.Personne ne peut profiter de toi ,te faire du mal ou te maltraiter a`moins que se soit ma volonte’.Ta vie est dans les creux de ma main,tu peux me faire comfiance en toute chose.En continuent a` me remercier tu verras comment je mais parfaitement chaque details de ta vie Amen.” Hii ni lugha ya kifaransa,tafsiri yake ni hii: 

 

“Binti yangu nilichotaka ufahamu ni kwamba,hakuna cha kuogopa tena.Hakuna mtu atakae kutishia au kukufanyia ubaya wowote isipo kuwa kwa mapenzi yangu tu.Uhai wako uko mikononi mwangu,unaweza kuweka matumaini yako kwangu kwa kila jambo. Ukienderea kunishukuru,utaona jinsi gani nitaenderea kukufanyia mema maisha yako yote Amen.” 

 

Barua hiyo nzuri ilikuwa ni jibu kwa maswli yangu yote,na mahitaji yangu yote ya badaye.Nilikuwa na hofia kwamba nitarudi nyuma,amenijibu,maisha yangu yote yako mikononi mwake.Nilikuwa na sikitika jinsi wanafunzi walikua wananisema,alinijibu,hakuna mwanadamu atakae ni tishia au kunifanyia ubaya wowote isipa kuwa kwa mapenzi yake tu.Tena,ameniandikia akisema,”Binti yangu.”Mpendwa msomaji wa kitabu hiki ,barua hii,niliyandika moyoni na siwezi kuyisahau.Alicho nifanyia Mungu ni kikubwa mno.Amenirudishia uhai ili nimtumikie.Na leo hii,nakuhubiria kwamba Yesu ukimuomba atakujibu.Kama unaumwa anaweza kukuponya,kama una maswali ,anaweza kukujibu,mwamini tu.Barua hii,imenipa tumaini wa maisha yangu.Najivunia kuwa ndani ya Yesu naye ni kweli amesimamia ahadi yake ya kunifanyia mema siku zote.Jina la Bwana libalikiwe. 

 

Ni kweli Mungu alinirudishia uhai wangu tangu (7/1/1985 Mpaka leo  2008) ni miaka 23 iliyopita. 

 

Mpendwa msomaji, Mungu anasikia na anajibu maombi. Endelea kuniombea ili nitimize makusudi ya Mungu. (Amosi 3:7) “Hakika, Bwana  Mungu hatafanya neon lolote,  bila kuwafunulia watumishi wake manabii siri  yake”. 

 

USHUHUDA WA PILI  

 

Baada ya miaka 10 kupita, niliendelea kusoma elimu ya juu katika masomo ya ufundi. Cha kushangaza ni kwamba nilikuwa nikiumwa mara kwa mara. Nilipomuuliza Mungu kwa nini nimekuwa mdhaifu kiasi kile alinijibu ya kuwa, ulisema nikuongezee siku ili unitumikie ili unitumikie na si vinginevyo”. Lakini nikamwambia Mungu hata hapa chuoni bado nakutangaza? Akaendelea kusisistiza anapenda nimtumikie. Siku nyingine nilifika darasani nikaanza kutetemeka kama mugonjwa wa maleria nikapelekwa kwenye kituo cha Afya, ambapo daktari alipomaliza kunipima alisema kuwa sina maleria  .Kwa sababu anaona na umwa lakini hajaona ni ugonjwa gani ,aka niandikiya cheti kinacho niruhusu kupumzika kama siku 10 nikiwa nyumbani .Nilienderea kumuuliza Mungu, kwa nini naumwa ila ugonjwa haujulikani? Alinijibu vile vile kwamba nimtumikie. Ndipo akanipatia ujumbe wa mtu mmoja aliyekuwa akiishi sehemu iitwayo Ngozi(Burundi). Nilikuwa bado sijawahi kufika uko, pia sikuwa namfahamu mtu aliyekuwa akinituma kwake. Ndipo katika maono, akanionyesha alama na jina la huyo mtu. Kwa kuwa kilikuwa kipindi cha mapumziko, nilipanda gari la kwenda Ngozi, japo sikupajua, lakini mkono wa Mungu ulikuwa juu yangu ukiniongoza. Na nilipofika nilipokelewa na watu wa Mungu kwa furaha. Nilikaa mahali hapo kwa muda wa wiki moja nikihubiri injili.Nilihubili pia  katika Kanisa la Kipentekoste, pia nikahubiri katika kambi ya Askari wa Ngozi. Na Mungu alinitumia kwa jinsi ya ajabu. Hiyo ilikuwa safari yangu ya kwanza ya injili. Namshukuru Mungu kwani niliweza kufikisha ujumbe kwa ndugu yule. Lakini bado sauti iliendelea kusema ndani yangu kwamba “Nilikuongezea siku ili unitumikie mimi peke yangu”. Ila sasa sikujua kitu gani nifanye katika shamba la Mungu. 

 

Siku nyingine nilipata ndoto kwamba nimepooza, usiku ulipokuchwa, nilijikuta nikiwa nimepooza viungo vyangu vyote. Sikuweza kufanya lolote. Ndugu zangu Emmanuel BUcumi na Elyphaz NIYONGABO pale Nyakabiga hawakuelewa ugonjwa ulikuwa umenipata na nini cha kufanya. 

 

Walimuita dada yangu aliyekuwa akifanya kazi BRB. Pia walimuita rafiki yetu (Safari Reuben). Waliponiona hali yangu, mara moja walichukua gari na kunipeleka kituo kimoja cha Afya “Prince Louis Rwagasore”. Daktari aliyenipokea alinifanyia mazoezi ya viungo lakini alitaka kunilaza lakini nafasi ilikuwa imejaa. Nikapelekwa katika kituo kingine cha Askari cha Kamenge. Hakuna aliyeelewa nilikuwa naumwa nini, kwani pamoja na kupooza, bado nilikuwa nikiongea vizuri, kucheka, na sikuwa naumwa popote. Basi wakanishauri nisirudi chuoni. Sawasawa na sauti ya Mungu aliponitaka nisirudi shule, basi ugonjwa huo ulidumu kwa siku tatu tu. Ndipo nilipoendelea na kazi ya Mungu nikiwa nyumbani Nikisubili mwaka wa shule uishe ili nihamishiwe shule kwani familia yangu wamedhani kwamba labda nikihamishwa pengine naweza nikaenderea na masomo bila shida.(lakini mimi nilijua ni Mungu anataka ni mtumikie tu). 

 

Zamani nilijiona kwamba siwezi, lakini sasa ninaweza yote katika yeye anitiaye nguvu, ninachofanya ni kutii kila anachosema. 

 

 

USHUHUDA WA TATU 

 

Mwaka 1996 nilikuwa na miaka miwili katika ndoa, ilikuwa tarehe 29 mwezi wa kwanza,mwaka huwo wa 1996. Mungu alinionyesha katika maono, mtu mmoja aliyekuwa akifuata njia ya wokovu na alipofikia nusu ya safari yake, aliwaona watu, kundi kubwa lililokuwa linaimba nyimbo za dunia , kucheza na kunywa pombe , mtu   huyo alitoka katika njia yake na kuelekea kando ya njia walipokuwa watu wale. 

Alipofika karibu  ya pale,alisimama nakuanza  kuzungusha viuno vyake taratibu kama anayecheza muziki. Ndipo nikasikia sauti ikisema: “watumishi wengi ,wameandika vitabu kama wakina  Billy Graham  na wengine wengi lakini  wengi wao  wameisha fariki .Sasa ni zamu yako ya kuandika kitabu kiitwacho “Jinsi ya kuendelea katika njia ya Wokovu” akaniambia ni shike sana mufano wahuwo mtu ni musaidie asonge mbele , aache kutamania mambo ya dunia ,ashinde vishawishi.Ndipo   nilipoanza kuandika, japo mwanzoni niliogopa. Lakini asante Yesu kwani sasa unacho mkononi mwako ukisomacho. 

 

Mungu aliniongoza, na Roho wake akawa mwalimu wangu, kwani sijasomea biblia ila ninayaweza yote katika yeye anitiaye nguvu. 

 

 

 

 

USHUHUDA WA NNE 

 

Mungu aliniita  nimutumikie    

 

Tazama kwa bidii ilivyokuwa: 

 

Nilikuwa nafundisha watoto wa shule ya msingi Stella Matutina (Bujumbura-Burundi); nilipenda sana taaluma ya kutumika pamoja na watoto, nilikuwa na wafanyakazi wenzangu Wakristo na watoto wangu wawili Igor na Billy wanafunzi katika shule hiyo. 

 

Jioni ya tarehe 28/1/2000, niliona mtu aliyefanana na mchungaji wangu akaniomba nimsindikize kesho yake ili kumuona mchungaji mwingine aliyetoka mkoa mwingine. Kwa kuona jinsi kulivyokuwa mbali, nilijiuliza, “Nimeshaahidiana na mume wangu kwenda mahali sasa nitamwambia nini huyu mchungaji anayetaka nimsindikize? Haraka nilimuambia mchungaji kuwa nataka niongee na mume wangu kwanza. Akaanza kuongea kwa hasira; “Kwani anaweza kukuzuia?” nikajibu, anaweza kukubali au kukataa. Ghafla akafungua Biblia na kuniamuru nisome Ezekiel 2:3, 4 ila katika kusoma andiko hilo, aliendelea kuongea akiwa nyuma ya mgongo wangu maneno haya;“nani aliyempa mtu mdomo? Nani awezaye kufanya mtu kuwa bubu au kiziwi, au kipofu, sio mimi Bwana?” nani anayeweka uhai na mauti? Nani mwenye uwezo na mamlaka kwako, sio mimi Bwana….!      Nilitetemeka kwa hofu ya hayo maswali. 

 

Niligundua kumbe si mchungaji aliyekuwa akiongea nami bali ni Bwana aliyeongea nami. Baada ya kuongea alitoweka, rafiki yangu alinikuta nikitetemeke na nikamueleza jinsi Bwana alivyoongea nami na nikamwambia  Bwana ameisha niambia nimutumikiye  , ila sikukubali, utafikiri si kwangu alikokuwa akiongea, ila sasa…. siwezi kumkwepa….!  ! Nikazinduka usingizini asubuhi nikafungua Biblia ili kusoma lile andiko nililoota. Kichwa cha somo “Wito wa Ezekiel .” Aya ya kwanza na ya pili inatuonyesha jinsi gani Mungu anavyoita watu, na jinsi gani anavyomsikia mtu anapoongea. Aya ya 3 “Wewe mwanadamu …” aya ya nne “Watu hao ni wafidhuli …………….”. kwa aya hizi, nilielewa kuwa Bwana ameniita ili kumtumikia, na kwamba hakuna mtu aliye na uwezo juu ya maisha yangu. Asubuhi yake nilimsimulia mume wangu, naye akasema hiyo ni sauti halisi ya Mungu. 

 

Baada ya siku chache tarehe 7/1/2000, sauti iliniambia “Anza sasa kuomba ruhusa ya kuacha kazi”.Asubuhi nikamueleza mume wangu kuhusu hilo ,na swala hii likawa ngumu kwake kukubali nami nikajiuliza maswali mengi ; niache kazi niende wapi? Kufanya kazi gani ? Na watoto wangu Igor na Billy  ambao bado wako chekechea itakuwaje? Na pia si rahisi kukuachisha kazi kama hawana mwingine wa kushika nafasi yako pia ilikuwa katikati ya mwaka wa shure.Inabidi nisubiri angalau wakati wa rikizo.Iyo sauti ya bwana ikanirudia “anza sasa.”Mungu alinisaidia kupitia mume wangu .Nikapata  ruhusa baada ya siku tatu tu.Nimekaa nyumbani myezi  4 , na maombi yangu alikuwa kumshukuru Mungu kwani nilitenda alioniagiza. Lakini  roho yangu ikajiuliza kazi gani Mungu anataka ni mufanyie kama ni kuhubiri injili mbona nilikuwa nayifanya! Lakini nikajipa moyo  kwa sababu nimefuata maagizo ya Mungu. Wakristo wengi baada ya kujua kwamba siko kazini tena wakaniuliza kazi gani natarajia kufanya ,wengine wakanifuata nyumbani waone nafanya nini,na mengine mengi …. Jibu langu lilikuwa:”nasubiri mapenzi ya Mungu”. 

 

Jioni moja ,Mungu akanionyesha katika maono  yafuatayo;tulikuwa ndani ya ukumbi ambawo halipuepo wanawake wengi tukisubiri muhubiri .Baada ya kukaribishwa  tukiwa sisi wote tume kaa,nikagunduwa kwamba mwalimu wetu hayupo  nikajuwa kwamba ni mimi natakiwa kusimama na kuendereza shuguri.Ndipo nikasimama nikawaimbisha huku moyoni napanga kitu gani kinafuata;kwa sababu nilikua sijui ratiba ya siku hiyo au mwalimu wakwanza aliishia wapi.Moyoni nikasema hakuna shida nitaweza kwasababu haya mambo ya injili siyo mageni kwangu! Kwa hiyo nikasimama kwa ujasiri nikahubiri. 

 

Nilipo maliza nikaona mtu ananiletea karatasi imeandikwa  mambo mengi  akaniambia nisaini na niweke muhuri ,nikafanya. Akanipa vitendeakazi vyote ,na muhuri kwa ajili yaku saini.Nikazinduka kwenye ndoto hiyo. Asubuhi nikajiuliza Bwana wangu ndoto hii inamaanisha nini? Awo wanawake ni wawapi? Mimi nita saini kama nani? Wako wapi awo watu?jibu sina lakini Mungu ndiye anayajuwa yote.!Uwo muda wa myezi 4 nilikuwa nikingoja utimilifu wa hayo maono.Ndipo nikamhusisha mchungaji wangu ili ayo maono naye ayajue.”Naye akaniambia:”kabisa niwito halisi wa Mungu ,yeye mwenyewe anajua atakavyo kutumia,wewe endelea kuomba. lakini akasikitika kwa sababu nimeacha kazi bila kujua nitafanya nini. Lakini alipo sikia kwamba mume wangu alikubali akaona hana jinsi yakufanya. 

 

Akaniambia nipige magoti aniombee ili mapenzi ya Mungu atimizwe. 

  kulikuwa kikundi Fulani cha akina mama ambapo nami nilikuwa mwanachama muanzilishi. Mwenyekiti wake alipomaliza muda wake pamoja na kamati nzima na ndipo nikachaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Chama hicho. Nilitumika na chama hicho na Bwana akaonekana. Ndipo nilipogundua maono yale. Ndugu mtumishi wa Mungu mtegemee yeye aliyekuita, hubiri injili, (2 Timotheo 1:8)”basi usionee haya ushuhuda wa Bwana  wetu ,wala usionee haya mimi mufungwa wakebali uvumilie mabaya pamoja nami kwa ajili ya injili,kwa kadili ya nguvu ya Mungu;ambaye alituokoa akatuita kwa mwito mtakatifu,si kwa kadiri ya matendo yetu sisi,bali kwa kadiri ya makusudi yake yeye na neema yake.Neema hiyo tulipewa katika kristo yesu tangu milele..”   2 Timotheo 2:15),”Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu,mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumuya kwa halali  neno la kweli.       (2 Timotheo 1:14)”Ilinde ile amana nzuri kwa Roho mtakatifu akaye ndani mwetu .” 

       

 Shamba la Mungu ni kubwa, halina mipaka ………. Zaburi 24:1 “Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya Bwana,dunia na wote wakaaondani yake.” 

 

Jipe moyo mtumishi wa Bwana, Mungu yuko kazini hata sasa, atakulinda, ongozwa na Roho Mtakatifu. Matatizo na shida zipo, ila tunamtumaini Bwana. Daudi anasema katika Zaburi 23:1 “Bwana ndiye mchungaji wangu sitapungukiwa na kitu…..” 

 

Msomaji mpendwa shuhuda zote nilizokueleza na miujiza yote niliyokuambia , ni Bwana ndiye alinitendea…!  utukufu na uweza ni kwa Yesu Kristo. Paulo anasema katika Warumi 15:18 “Maana sitathubutu kutaja neno asilolitenda kristo kwa kazi yangu ,mataifa wapate kutii, kwa neno au kwa tendo,kwa nguvu za ishara na maajabu,katika nguvu za roho mtakatifu……”, 

 

Kwa kudhihirisha kuwa Kristo ndiye aliyekamilisha kazi ndani yake. Paulo asingeweza chochote ila Bwana. Nami pia namshukuru Mungu anayetenda haya yote ndani yangu. (2 Wakorinto 3:5 – 6 ) “Si kwamba twatosha sisi wenywe tukifikiri neno lo lote kwamba ni letu wenyewe ,bali utoshelevu wetu watoka kwa Mungu . Naye ndiye aliyetutoshereza kuwa wahudumu wa agano jipya ….” Paulo anadhihirisha kwamba hatuwezi kufanya chochote, isipokuwa yote yatokayo kwa Mungu. Kwa hiyo hatustahili kujiinua kwa ajiili ya utumishi, Mungu mwenyewe atakuinua. Utukufu kwa Mungu pekee  AMEN. 

 

 

 

 

 

 

 

 

MTUMISHI MWEMA WA MUNGU 

 

Mtumishi wa Mungu ni yule aliyeitwa na Mungu ili kumtumikia, huwezi kutegemea upate mshahara ikiwa huna aliye kuajiri. Anayeajiri ni Mungu mwenyewe. Naongea na wewe mtumishi wa Mungu aliye hai. Ni heshima ya pekee kuchaguliwa miongoni mwa watumishi. Kuna watumishi wengi kutoka kila kona ya dunia; hao wana utumishi wa kila aina na uliogawanyika. Wengine wamepewa kuhubiri injili, wengine kusaidia wagonjwa, wengine kutembelea wafungwa ………. Wengine kama Roho Mtakatifu anavyowatuma. Katika hayo yote tukumbuke kuwa ni Mungu ndiye tunayemtumikia na ndiye atakayetulipa. Wengine wameitwa kuchunga kanisa, wengine mitume, wengine wainjilisti na manabii …. Efeso 4:11. 

 

Hapo tunaona kuwa Mungu ni Mungu atoaye huduma tofauti kama atakavyo. Mtumishi wa Mungu usife moyo kwa ajili ya matatizo na vikwazo unavyokutana navyo katika huduma. Mungu ndiye aliyekuita, atakusaidia alikuahidi kuwa na wewe ni kweli hatakuacha. Shetani aweza kujiinua hapa na pale, usiogope, Bwana hawezi kubadilika atalinda kazi yake. Unaweza kuona kuwa umelemewa na huduma, nakupa changamoto kaka na dada, tegemea nguvu ya Mungu aliyekuchagua, mwamini utaona miujiza. Pamoja na Yesu tunatenda maajabu. Aliye ndani yetu ni mkuu kuliko aliye ndani ya ulimwengu huu. Biblia inasema “Mtu akimtumikia Baba atamuheshimu” ni bora kuheshimiwa na Bwana, ni raha kumtumikia Mungu. Mungu aliahidi kuwa atajifunua katika hali zote. Angalia baadhi ya ahadi kwa yule anayekubali wito wa Mungu. 

 

1.    Kuwa mikononi mwa Mungu ili kulindwa. 

2.    Mungu atakuwa mbele yako nawe utafuata nyayo zake. Mungu atatengeneza njia (Isaya 45:3) 

3.    Mungu atakubariki (atakufichulia hazina yake ili ujuwe umeitwa kwa jina lake (Isaya 45:3) 

4.    utapata jina la heshima (kuwa mtumishi wa Mungu ni heshima kubwa) Isaya 45: 

 

Kaka na dada Mungu alitupenda , alitupa kazi ya heshima. Tunapaswa kuenenda katika heshima ya utumishi kama Bwana alivyotugawia. Sio kwamba tumebeba jina tu, bali maisha yetu yote yadhihirishe kuwa tu watumishi wa Bwana. Tuwe waaminifu kwa Mungu, naomba Mungu asamehe watumishi wote wasio waaminifu kwake. Mungu alipokuita alijua kula kwako na kuvaa kwako. Wengi hutaka wajue vyanzo vya mapato ya wachungaji. Wanasahau kwamba Mungu aliahidi kumpa mtumishi wake thamani iliyofichwa. Mungu anatuheshimu. Sifa kwa Mungu, Mungu hutulinda popote, hata shetani anapotuwinda. 

 

Siku hizi shetani hujifananisha na malaika wa nuru. Sauti yaweza kukuambia “Tazama unahitaji pesa ili kukuza Kanisa lako, ili kulisha familia yako, ili ununue gari, viwanja  n.k ..” sasa utafanyaje?twende tufungue Kanisa lingine pale ambapo “X” mfanyabiashara atakuwa mchungaji “Y” atakuwa muinjilisti, na “Z” atakuwa mwalimu ……….. hivyo tutapata mafungu ya kumi na sadaka kutoka kwa wafanya biashara na matajiri waliomo ndani ya Kanisa. Tutaunda kwaya ambayo fulani atakuwa kiongozi, tutatumia vyombo vya muziki na tutaruhusu watu kucheza, nakadhalika ……….” Katika hayo yote wazo muhimu ni jinsi gani kupata pesa ili kufanikisha haya ……. Wazo hilo linakusukuma uanzishe Kanisa na kuweka watu ili wakufanikishie hili na lile. Kuanzisha Kanisa ni ufunuo wa Mungu peke yake, na siyo mikakati ya mtu. Tujiulize ni nani tunayemtumikia . shetani mara kwa mara hutuambia neno “maskini” na pia “huwezi” ila Mungu anatuambia kuwa tu matajiri na tunaweza kwani nguvu yake imo ndani yetu, sifa kwa Mungu. 

 

Biblia inasema “Nimeweza yote katika yeye anitiaye nguvu” shetani pia anaweza kuweka ndani yetu Roho ya ombaomba. Mtumishi wa Mungu hastahili kuombaomba badala yake anapaswa kusaidia  wengine, na kugawia maskini. La sivyo tuombe Mungu afungue milango. Unapaswa kuhubiri kwa neno na kwa matendo. Kazi ya Mungu isiwe biashara (uchuuzi). Tumepewa bure tutoe bure. Tunapaswa kufundisha waumini kutoa na kutajirisha nyumba ya Bwana na Mungu aliahidi kumbariki yeye atoaye sadaka (kwa hiyari) na fungu la kumi. Moyo unaotoa kwa Bwana uwe wa furaha (mkunjufu). Siri na ufunguo wa baraka ni utoaji. Msomaji wangu kama ilivyoandikwa katika Matayo 19:29, mtumishi mwema wa Mungu anajua kuwa Bwana yu pamoja naye. Anajua kuwa amejitoa masaa , siku, miezi miaka … kwa ajili ya Bwana. Mungu ameahidi kukulipa. Hakuna awezaye kulipa uchovu, muda na shida tunazopata kwa ajili ya Bwana, ni Mungu tu awezaye kulipa. 

 

Mungu atabariki kazi za mikono yetu na kutupatia mahitaji yetu. Tuwe na tumaini kwake na kumtazama yeye. Atatunza watoto wetu na familia zetu. Tutambue kuwa tunafanya kwa ajili ya Bwana, Kanisa ni la Bwana, tunapowekea mtu mikono tuwe na hakikisho kuwa Bwana anatenda. Mungu anapenda watu wake na anawalinda  na ndiyo maana Mungu anaweka karama katika Kanisa ili: 

 

1.    Kuandaa watu wa Mungu kutimiza maagizo ya ukristo. 

2.    Kuendeleza mwili wa Kristo katika imani. Hayo yote yanatuleta pamoja katika umoja wa imani kwa mwana wa Mungu. Pamoja na umoja wa imani na ufahamu huu wa mwana wa Mungu tukiwa wakomavu hatuwezi kuwa tena watoto wachanga ………… (Waefeso 4:12 – 15) 

 

Msomaji mpendwa Mungu anataka tuwe wakomavu kiroho kwani siku hizi shetani hupindua maandiko, watu wamekuwa kama watoto, wanapindua maandiko na kuleta mafundisho ya kugawanya makanisa. (mfano, Fulani si wa kanisa letu, wala hajaokoka, Fulani anashiriki na madhehebu yasiyokuwa ya kwetu jitengeni naye ……….) tuwe wakomavu na tutofautishe mafundisho bila msingi. Hakuna anayeweza kukabidhi madaraka kwa mtoto mdogo. Lazima tujue kutofautisha mema na mabaya. Tutumike kwa umoja wa roho, sio katika migawanyiko na wivu, kwani  hiyo ni roho inayotoka kwa ibilisi ili kuligawa Kanisa la Mungu na hata taifa na makabila. Ila Mungu anaweza kutupa mawazo mwanzo mpya na umoja tena, sifa kwa Mungu. Tusimame kwenye zama zetu. Mungu atusaidie kupata ufahamu wa kiroho, tuwe na umoja tusikumbwe na mafundisho ya uongo. 

 

HITIMISHO 

 

Wapensi katika Bwana, je inawezekana kuandika neno moja muhimu kurasa zote na kutoa hitimisho muhimu kwa kila mmoja wetu? Yesu aliyafanya katika mahojiano yake na Nikodemu. “Yohana 3:16”. Mungu anataka watu wote waokolewe alidhihirisha upendo wake kwa kumtoa mwanaye wa Pekee ili afe msalabani ili kila atakaemwamini asipotee. Hili neno “kila aaminiye “ linatuonyesha tena kuwa na wito kwa wokovu unamhusisha mtu mwenyewe kibinafsi ila chini ya masharti mawili “wanaopotea” na “wawe na uzima wa milele”. 

Ili kuokoka inabidi kumuamini Yesu mwana pekee wa Mungu aliyetumwa ulimwenguni aliinuliwa msalabani kama nyoka wa shaba jangwani. Yohana 3:14 – 15. imani ni uhakika katika ahadi za Mungu. kuuangalia msalaba kunatuosha dhambi zetu. 

 

1 Petro 2:24 …………….. sehemu ya mwanadamu na Mungu ni tofauti bila mipaka, ni Mungu ndiye aliyeanza kutupenda, ndiye anayetutakasa kwa maisha ya milele. Ila kati ya upendo wa Mungu kwa wanadamu na karama ya uzima wa milele, imeungamanishwa kwa binadamu wao kwa wao kama kuiunganisha “imani”. Mungu anatuzaa upya. “Kila aaminiye” katika mwana wake hili “kila” ni wewe na mimi tunaoamini sadaka ya neema ambayo Mungu alitutolea. Ukiwa na dhamiri kuwa una dhambi na upotevu, geuza macho yako umtazame yeye aliyeangikwa mtini na upeleke dhambi zako kwake. Sasa Mungu atafuta zote na kukupa uzima wa milele. Lengo la maandiko haya ni kwa ajili ya kutusaidia ili tuwe katika njia sahihi iliyonyooka. 

 

Tuelekeze malengo yetu: ya kutawala na mpenzi wetu Yesu Kristo kule mbinguni. Mtu asiwadanganye, inatupasa kuendelea na njia ile tulioianza na kufuatilia licha ya matatizo, mpaka tutakapopata ushindi. Tujipe moyo mkuu kwa maombi, tumtazame tu Yesu na kwa kusoma neno na kuziangalia ahadi zake. Tumpinge shetani anayetudanganya usiku na mchana, tuwe na imani kwa Bwana, na muda si mrefu tutaona mji wetu tunaotamani.Mungu awabariki Amen 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

FRANÇOISE HABONAYO 

 

 

 

Françoise HABONAYO, alizaliwa mwaka 1967 katika Manispaa na Mkoa wa BURURI, Kusini mwa BURUNDI, AFRIKA YA KATI 

 

 

 

Alimpokea Bwana Yesu kama Mwokozi pekee, akiwa na umri wa wiaka 7, akabatizwa katika maji mengi mwaka 1975, na kubatizwa katika Roho Mtakatifu, kabisa terehe 8 Machi, 1979. 

 

Uhusiano wake na Bwana Yesu ulidhihirika tangu akiwa mtoto mdogo hadi leo. Kokote alikosomea na kutumika aliacha ushuhuda mzuri kwa ajili ya Bwana. Anapata raha mno kutangaza habari njema za Yesu Kristo. Anataaluma ya ualimu, aliyoanza tangu 1990 mpaka 2000, wakati Mungu alipomuita  kumtumikia kwa muda wote .Alianzia huduma ya Mungu  katika  Shirika inayoitwa “UNION CHRETINNE DE FEMME AU BURUNDI” “U. C. F. B.” kwa kifupi (Umoja wa Wanawake wa Kikristo wa Burundi) ambapo ametumika kwa muda wa miaka miwili akiwa Mwenyekiti na mwakilishi wa  U. C. F. B. 

 

Katika usiku wa tarehe 29 Januari 1996 Mungu alimpa mama Françoise HABONAYO maono ya kuandika kitabu kinachoitwa “Jinsi ya Kuendelea Katika Njia ya wokovu,” na ni Mungu mwenyewe aliyefunua mchoro wa jalada la kitabu hiki. Kundi la watu wanaocheza,na kufurahia raha za dunia;  chini ya njia katika majani, na mmoja kwenye  njia ya Ukristo, kuliko kuendelea; anaacha njia yake ili kufurahia yanayofanywa na wengine, kwa kugairi njia yake ya Wokovu. 

 

Baada ya mapigano marefu , mwisho kiko mikononi mwako “Labda kitabu hiki kitakuweka mbali na dhambi, au dhambi zitakuweka mbali na kitabu hiki”. 

Laisser un commentaire