Titre:Upatanisho.
Kimeandikwa naMwalimu
Francoise Habonayo.
Mwaka 2010,Sweden.
SHUKRANI.
Shukrani zangu kwa Bwana Yesu,alie niagiza kufanya kazi hii na kunifanikisha.Pia shukrani nyingi kwa watu wote waliyejitowa ili kazi hii imalizike.Natoa shukrani nyingi kwa watu wa familia yangu ,kwa msada wao wa pekee.wote Mungu awabariki,mtapokea ujira wenu,na Bwana Yesu kwa kazi mlioifanya..
Yaliyomo :
Kuhusu mwandishi
Shukrani
Utangulizi.
Sura 1.
Kujitambua.
Wewe u Mungu uonae.
Hasira.
Ushuda.
Sura ya 2.
Madhara ya dhambi.
Shuhuda.
Je magonjwa yote ni tunda la dhambi?
Sura ya3.
Uponyaji.
Shuhuda.
Kwa nini tusamehe ?
Maombi.
Mwisho.
Kuhusu Mwandishi.
Halelua,namshukuru Mungu aliye mtumia Francoise Habonayo, kwandika kitabu hiki.Mwandishi huu,ni mzaliwa wa Burundi Afrika,kwa sasa anaishi Sweden (Europe).Mama huyo ana watoto na mume.Alianza kutumika akiwa bado mdogo,akishirikiana na watoto wenye umri kama wa kwake maana aliokoka akiwa na miaka 7 ya kuzaliwa.Yeye kwa sasa ana umri zaidi ya miaka 40 ya kuzaliwa.Utumishi wake ,ni mwalimu wa neno la Mungu.Tangu mwaka wa 1996,Bwana alimwagiza kutoa vitabu.Kwa sasa,kazi hii ya uwaandishi inaendelea.Hiki ni kitabu chake cha 4.Alisema,yeye ni chombo tu,maana kila asemalo ndani ya vitabu vyake ni ufunuo kutoka Mbinguni.
Jinsi nilivyo pata kitabu hiki.
Ushuhuda,
Siku mmoja,nilikuwa kule Afrika,nchi ya Tanzania,Bwana alinionyesha msalaba ,lakini ulikuwa umekatika(kama unavyoona kwenye kava yake), ni kasikia sauti inaniambia kwamba watu wanatakiwa kupatana na Mungu haraka iwezekanavyo.Nikasoma karibu na msalaba huyo maandishi haya;
“..naye alitupa huduma ya upatanisho ,yaani,Mungu alikuwa ndani ya Kristo,akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake,asiwahesabie makosa yao;naye alitia ndani yetu neno la upatanisho.”
Nilipo amka kutoka kwenje maono hayo,nimetafuta kwenye biblia maandiko hayo nikayapata hapa, 2Kor 5:18-19.
Basi ndugu,mimi si mwandishi,bali ni mjumbe tu kwa ajili ya Kristo,kana kwamba Mungu anasihi kwa vinywa vyetu;twawaomba ninyi kwa ajili ya Kristo mpatanishwe na Mungu.
Mungu awabariki wote ,amen.
Utangulizi
Kitabu hiki kidogo :UPATANISHO,ni ufunuo kutoka kwa Mungu.Naomba usome kwa makini usikie sauti ya Bwana kuhusu maisha yako mwenyewe.
Watu wengi tumefarakana na Mungu kwa matendo yetu maovu.Mahusiano yetu na Bwana amekatika, na madhara mengi ya metupata.
Tunaangamia kwa magonjwa, kwa maumivu ya namna mbalimbali, kufukuzwa kazi, kuonewa,n.k.
Pamoja na shuhuda mbalimbali na ufunuo wa roho wa Bwana,naamini kwa msaada wa kitabu hiki,kitakusaidia kujitambuwa vizuri,ukishajitambuwa,utapata msaada wa upatanisho uliyopo katika damu ya Bwana Yesu.Kupitia ufunuo utakao upata ndani ya karatasi hizi,utapata huduma nzuri ya kupatana na Mungu wako,utarejea afya yako,mali zako na amani yako pia.
Neno la Mungu linaonyesha vizuri Kum 28:29, “Utakwenda kwa kupapasapapasa mchana,
kama apapasavyo kipofu gizani,wala hufanikiwi katika njia zako;nawe utaonewa siku zote na kutekwa nyara,wala hapatakuwa na mtu wa kukuokoa”.
mst 22 unasema; “Bwana atakupiga kwa kifua kikuu,na kwa homa,na kwa kuwashwa na kwa hali ya moto,na kwa upanga,na kwa ukaufu,na kwa koga,navyo vitakufukuza hata uangamie”.
Ndugu msomaji,hali hii tunaiona kila siku.Tunaumwa,homa isiokoma,mawasho,vita,mambo haya yapo,lakini maranyingi tunasema ni shetani amefanya hayo.Lakini tunaona kwamba ni Bwana anaeyafanya kwa wale wote wanaemchukiza kwa dhambi zao.(Kwa mfano,kutokwenda kanisani kumwabudu,kuamini wachawi,kuroga,uuaji,uzinzi,kuamini miungu mingine,,ulevi,n.k).
Bwana usiposikia maagizo yake na kumtii,ni kweli utapigwa vibaya. Kum 28:58
“Kama hutaki kutunza kufanya maneno ya torati hii yalioandikwa katika kitabu hiki ,upate kulicha jina hili la fahali na utisho,BWANA MUNGU WAKO;ndipo atakapofanya Bwana mapigo yako awe ya ajabu,na mapigo ya uzao wako,mapigo makubwa kwa kweli,ya kudumu sana,na magonjwa mazito ya kudumu sana.”
Bwana ni mwenye rehema nyingi sana.Tukimrudia anatupokea vizuri.Na laana zote tulizopata kwa kukemgeuka maagizo yake, tukitubu na moyo wote,tutarudishiwa baraka zetu zote.
Neno lake linasema.Kum 28:8-9
“Bwana ataiamuru baraka ije juu yako katika ghala zako,na mambo yote utakayotia mkono wako;naye atakubalikia katika nchi akupao Bwana,Mungu wako.Bwana atakuweka uwe taifa takatifu kwake,kama alivyokuapia;utakaposhika maagizo ya Bwana,Mungu wako na kutembea katika njia zake.”
mst 13 “Bwana atakufanya kuwa kichwa ,wala si mkia;nawe utakuwa juu tu,wala huwi chini,msipokengeuka katika maneno niwaamuruyo leo kwa lo lote,kwenda mkono wa kuume wala wa kushoto ,kwa kuifuata miungu mingine na kuitumikia.”
Kitabu hiki kitakuonyesha jinsi, maneno haya ya Mungu,anatendeka katika maisha yetu ya kila siku. Bwana ametupiga mara nyingi kwa magonjwa, kwa njaa na mapigo mazito sana.Hayo yote ni kwa sababu tumekengeuka neno lake.Tumemtenda dhambi.Tunakula matunda ya kazi zetu. Wewe na mimi tuliepatanishwa na Bwana ,tumepewa huduma hii ya upatanisho. Kitabu hiki kitakuletea mwanga wa upatanisho,ili ukiisha patana tena na Bwana ,uingie shambani uhudumie wengine.
Ashukuliwe Mungu wetu aliyetupa huduma ya upatanisho (2kor.5 :18) .Haleluia ! Kabla ya kutupa huduma hii, tulipatanishwa kwanza na Mungu kupitia kifo cha Yesu ,zaidi
sana baada ya kupatanishwa tutaokolewa katika uzima wake. (Rum.5 :10).
Mungu awabaliki wasomaji wote!.Amen.
Sura ya 1.
Kujitambua.
Neno hili linahitaji ufafanuzi wa Roho wa Mungu zaidi.Watu wengi,ni rahisi sana kutambua rafiki zao ,kama wamezoeana sana,au wamekaa mda mrefu pamoja.Lakini,ni vigumu sana kujitambua,wewe mwenyewe.
Mara nyingi ,ndani ya familia,mume anaweza akamjua vizuri mke wake.Yeye anaweza kutaja vizuri tatizo au tabia mbaya anayeiona mara kwa mara kwa mke wake.Vivyo hivyo na mke ,anajua vizuri tabia mbaya anayeiona mara kwa mara kwa mume wake.Mfano:
“Tatizo lako hata tukikwambia husikii!”
Au, mwingine unasikia akisema:
“Wewe shida yako hujui kukubali kosa, ndiyo shida yako wewe!”
Hayo yote, yanatuonyesha jinsi gani mwanadamu ni vigumu kujitambua.Lakini Bwana anatujua vema
sana kila mmoja wetu.
Wapo wengine Biblia inatuambia walikuwa hawajijui kabisa. Mfano ni Musa, maana tunasoma, wakati Bwana alipomtokea katikati ya moto, yeye alisogea ili aangaliye lakini sauti ya Bwana ikamkataza kusogea maana alitakiwa avue kwanza viatu kabla ya kusogea. Tunayasoma ( Kutoka 3:4-5) ,
“Bwana alipoona yakuwa amegeuka ili atazame,Mungu akamwita kutoka katikati ya kile kijiti ,akasema Musa! Musa! Akasema mimi hapa. Naye akasema , Usikalibie hapa;vua viatu vyako miguuni mwako;maana mahali hapo unaposimama ni nchi takatifu.”
Musa alikua hajui kwamba anavyo viatu anatakiwa kuvua ili amsogelee Mungu.Alipoambiwa alifanya kisha akasogea na Mungu akaongea nae.Watu wengi hatujijui kabisa ; tunahitaji msaada wa Mungu . Yapo maovu mengi tunatembea nayo, tena tunampenda sana Mungu tena tunamtumikia lakini yapo maovu mengi ya kuvua,tumuombe Bwana atufunulie ili tupatane na Mungu wetu kabla ya hukumu ya mwisho.
Mara nyingi Mungu anatujulisha jinsi tulivyo kupitia njia zake.Zakaria kwa kutoamini maneno ya unabii kupitia kinywa cha malaika,alitiwa ulemavu wa ulimi,akawa hawezi tena kusema, lakini kwa mda tu.Biblia inamtaja kama mtu mwaminifu aliye na kibali mbele za Mungu.Lakini hata yeye alikuwa hajui kwamba si mwepesi wa kuamini unabii,mpaka alipoona maajabu amemfikia akaamini sasa.Bwana anazo njia nyingi kutueleza maovu au mapungufu yetu yote.
Hata Miliam dada yake na Musa,alikuwa hajui kwamba manung’uniko ni kosa kubwa mbele za Mungu,mpaka alipotiwa ukoma mwilini mwake ndipo akaamini kwamba amekosea akaomba rehema akapona baada ya mda(siku 7).
Hata mimi,maranyingi Mungu ananionyesha makosa yangu kupitia mapigo mwilini mwangu.Nikimulilia Mungu na kumuuliza ninini hii,ananiambia kosa langu,nikitubu na kunyenyekea napona hapohapo.
Ushuhuda.
Mtoto wetu mmoja,aliumwa kidonda kwenye muguu wake.Tumeweka dawa nyingi lakini kikabaki palepale.Tukaomba sana,hata maombi hajasaidia.Tukaamua kuacha ,kwa sababu tulikuwa hatuoni njia nyingine ya uponyaji wake.Kidonda kilipofikisha miezi kama 4,nikajiuliza hiii ni nini Bwana Mungu?,Tumefanya kosa gani mbele zako? Ndipo Mungu akatukumbusha kosa tulilofanya(mimi na mume wangu zamani,kanisani kwetu wakati nilikuwa na mimba ya mtoto huyo).Kumbuka mtoto huyo alikuwa na miaka 12,lakini kosa tulilofanyia kanisani ilikuwa zamani sana,tulikuwa hatujaitubia kumbe ilikuwa imebaki nakusimama mbele zetu.Tulishangaa kweli,tukamshukuru Mungu kwa neema yake na huruma zake kwetu.Tulinyenyekea na kuomba msamaha ,kesho yake nikaenda kuangalia kidonda cha mvulana huyo nikakuta kimekauka.Bwana apewe sifa milele.
Zaburi 86:15 “Lakini wewe, Bwana u Mungu wa rehema na neema , mvumilivu, mwingi wa fadhili na kweli.”
Mungu wetu ni mvumilivu sana, tena ni mkweli.Amejaa rehema na neema nyingi, hakuna wa kufanana naye.kama siye Bwana anae tuonyesha makosa yetu ,si rahisi kukumbuka kosa ya miaka 12 iliyopita!
Yeremia 44:9-11,
“Je mumeusahau uovu wa baba zenu ,na uovu wa wafalme wa yuda,na uovu wa wake zao,na uovu wenu wenyewe,na uovu wa wake zenu,walioutenda katika nchi ya yuda ,na katika njia kuu za Yerusalemu? Hawaja nyenyekea hata leo,wala hawakuogopa,wala hawakuenda katika sheria zangu,wala katika amri zangu ,nilizoweka mbele yenu,na mbele ya baba zenu.Basi kwa sababu hiyo Bwana wa majeshi,Mungu wa Israeli,asema hivi,Tazama nitaelekeza uso wangu juu yao,ili niwaletee mabaya,hata kukatilia mbali yuda yote.”
Ndugu msomaji, usifikiri Bwana anasahau, hapana,dhambi yote uliyoifanya kama hujaitubiya bado iko pale pale.Muombe Bwana ayifunue kabla ya hukumu,na Mungu akubariki.
Njia za Bwana si mapigo tu, anaweza akakuonyesha kosa lako kupitia njozi za usiku.
Ushuhuda.
Usiku mmoja Mwaka huu wa 2009,mwezi huu wa 9,Bwana alinionyesha tuko tunasafili kwenda mbinguni.Nikaona baadhi ya wasafili hawako tayali kuingia kwenye chombo cha usafili,maana walikuwa wameacha masanduku yao sehemu nyingine.Nikawauliza ,je mbona hamjaleta masanduku yenu,mnataka kutuchelewesha,mnafikili gari ikija,mtasema eti tusubili,hapana mtaachwa.!!
Nikawaona wanarudi haraka kuchukuwa vitu vyao.Walikuwa wawili, mmoja alikuwa amevaa vizuri, mwingine alikuwa uchi.
Nilipo amka asubuhi nikauliza Bwana maana ya ndoto hiyo, akaniambia kwamba huyo aliye uchi, ni kusema yeye ni mkristo mzuri, lakini haja mfanyia Bwana huduma yeyote.
Wapo wengi kama huyo, hawajui kwamba sisi wote waliyemwamini Bwana tuna kazi tuliyepewa ili tuifanye; kumtumikia Bwana wetu, kuleta wengine waje kwake.
Nikauliza huyo mwingine naye ni nini? Bwana akasema kwamba wakati alikuwa mwanafunzi university,amekuwa na rafiki yake wa kike.Walikuwa wanaishi
kama mke na mme.(walikuwa hawajafunga ndowa lakini),bwana huyo,alipo maliza shule,alimdanganya dada huyo kwamba atarudi baada ya wiki mbili,kumbe huko ndipo kumuacha mojakwamoja) kumbuka kosa hilo alilifanya,imepita miaka miingi(kama 15),kwa sasa bwana huyo ameoa,ana mke na watoto wakubwa,pia ni mtumishi wa Mungu.Lakini dhambi hiyo ya kumdanganya dada huyo bado ilikuwa palepale.
Bwana huyo alipo sikia ujumbe huyo,alikili nakutubu mbele za Bwana Yesu,alinyenyekea ,akaomba rehema kwa Mungu,pia akamtafuta huyo dada akaomba msamaha kwamba alimdanganya ,pia akamjulisha kwamba sasa ameoa ,akataja jina la mke wake ,akamueleza kwamba anawatoto pia.Naamini kwamba dada huyo,alipo ona hajarudi amehuzunika sana,akaumia ,na huzuni hiyo inaweza ikawa imemharibu sana.Lakini alipo mwambia wazi kwamba ameoa ,akomba msamaha kwa dhambi zote walikuwa wanafanya ,dhambi ya uzinzi,na uongo,n.k..
Hapa imeleta picha nyingine ya ushuhuda,na mawazo ya kumsubili amefutika kabisa.
Kweli Mungu ni mwenye rehema nyingi.Kama siyo Mungu ninani angekumbuka mambo ya zamani sana
kama hayo? Nani angejua kwamba dhambi hiyo ingemfanya asiingie Mbinguni? Kumbuka hata
kama ni Mtumishi wa Mungu lakini dhambi hiyo ilikua bado juu yake. Ashukururiwe Bwana kwa neema yake ya ajaabu, na uvumilivu wake!!!
Tuendelee na somo letu la kujitambuwa.kama nilivyotangulia kusema , bila ufunuo wa roho wa Mungu si rahisi mtu kujijua jinsi alivyo.
Unaweza usijue kwamba wewe ni mbinafsi, au wewe ni mchoyo.Ili ujigundue,anaweza Bwana akakuweka kwenye mazingira ambapo unahitajika kujitoa kwa ajili ya wengine.Unajikuta wewe si mwepesi kufanya jambo hilo,badala yake unataka wengine wakufanyie hata
kama wewe hunauhitaji huo.
Ushuhuda.
Siku mmoja kule Afrika,tumefanya sherehe kanisani,tukaambiwa,kila mtu atafute zawadi ampe mwingine.Wengi wameleta wakawazawadia watu kanisani.Lakini wengine walikuwa wanakaa tu wakisubili wengine wawaletee.Hapo niliweza kuona kwamba wengi walikuwa hawana utayali wa kujitowa kwa wengine bali walikuwa wanahitaji waletewe.
Neno la Mungu linasema,
“Nafsi ya mtu mkarimu itawandishwa;anyweshaye atanyweshwa mwenyewe.Awanyimaye watu nafaka,watu watamlaani;..”Mithali 11:25-26.
Unaweza usijue kwamba wewe ni mtu wa tabia ya kujikweza(kujiweka juu),unajikuta katika maongezi yako unataja vitu vikubwa tu,kila mtu unamtajia ,hata kama hajakuuliza,ilimradi tu asikie kwamba wewe si wa kawaida.Neno la Mungu linatukataza kujikweza.Linatwambia tunyeyekee ili wakati wa Bwana ukifika tutapandishwa tu.Hata kwenye karamu ,tunashauliwa tusijiweke mbele wasije wakatuweka nyuma ikawa aibu kwetu,bali tujiweke nyuma ili mwenye kutualika akiona tunastahiri kukaa mbele atatuita nakututoa huko nyuma na kutukalisha mbele.Hapo itakuwa fahari kwetu.
Iko tabia mbaya tena yenye uhalibifu sana;tabia ya kutoomba msamaha.Neno “NISAMEHE”linakuwa nzito sana.Kama wewe ni mwepesi kwa jambo hilo,kweli wewe ni mheri.Wengi sana wanaweza kutoa haraka msamaha,bila shida.Mtu akikujia unamsamehe,pia hata kama hajakujia unamsamehe.Ila,wewe kuanguka mbele ya mtu na kuomba msamaha nijambo ambalo halipo,au haliwezekani kabisa. Bwana atuwezeshe kuvaa unyenyekevu hata mbele za wengine si mbele za Bwana tu.
Ushuhuda.
Siku mmoja Bwana alinionyesha kwenye ndoto ya usiku dada mmoja alikuwa rafiki yangu sana.Nimeona ananijia akanipiga sana akanilukia shingoni kama anataka kuniua.Nimeshindana naye,lakini nikajikuta simuwezi.Nilipotaka kumujibu kwa ngumi na mateke akaongeza spidi ya kuniangamiza nikajikuta sina njia nyingine ya kujikomboa kwa uharibifu huyo .Nilipo sema nisamehe,nisamehe,!!!,mara akaniacha,akaondoka.Nikagundua kwamba neno “NISAMEHE”ni siraha yenye ushindi.Hata kama unaonewa,wakikushambulia,usibishane kwa maneno au kujieleza,sema tu nisamehe utaachiliwa. Kuomba msamaha ni neno zuri inaonyesha unyenyekevu,na mabishano ni kuonyesha kiburi.
Neno la Mungu linasema,
“kiburi huleta mashindano tu;…”Mithali 13:10 .
Mungu atusaidie.
Tabia ya kutoshaulika;hii ni mbaya sana .Mtu anajiamini sana hata kama si ndani ya kweli yeye hata umshauri hakubali.Tabia hii inachelewesha muujiza.Maana kama unahitaji kufanya kitu bila ushauli wa wengine unaweza ukadumbukia kwenye shimo ambao kutoka huko vitakugharimu sana.Ni vema kujiamini lakini pia kubali kwamba wengine wanaweza kuwa na ujuzi kuliko wewe.Sasa uwasikilize na uwakubali.
Mithali 13:10
“Kiburi huleta mashindano tu ;bali hekima hukaa nao wanaoshauriana.”
Kushauriana ni vizuri ,maana ndani yake kuna hekima.
Biblia inatupa mfano wa Musa jinsi alikuwa na kazi nyingi sana.Alikuwa anachoka mno,akaja mzee wa siku nyingi akampa ushauri.Alivyowukubali akafanikiwa,kazi ikaenda vizuri zaidi bila uchovu wowote.
(Kutoka18:19) “Sikiza sasa neno langu,nitakupa shauri,na Mungu na awe pamoja nawe;….”
mst21, “zaidi ya hayo utajipatia katika watu hawa walio na uwezo,wenye kumcha Mungu,watu wa kweli,wenye kuchukia mapato ya udhalimu;ukawaweka juu yao,….”
(Mst20), “Nawe utawafundisha zile amri na sheria,nawe utawaonyesha njia inawapasa kuiendea,na kazi ambao inawapasa kuifanya.”
Mst22 “Nao wawaamue watu hawa siku zote;kisha kila neno lililo kubwa watakuletea wewe,lakini kila neno dogo wataliamua wenyewe;basi kwako wewe mwenyewe utapata nafasi zaidi,nao watauchukua huo mzigo pamoja nawe.”
Mst24 “Basi Musa akasikiza neno la mkwewe,akayafanya yote aliyokuwa amemwambia.”
Hapo tumeona mfano mzuri wa mtu aliyokubali ushauri,akafanikiwa kwa kazi yake.
Pia Biblia inatwambiya kwamba;
“ akubaliye kurudiwa huwa katika njia ya uzima;Bali yeye aachaye maonyo hukosa”.Mithali 10:17.
Ipo tabia nyingine mbovu ya;kutojiamini,unajiweka mstali wa nyuma katika kila kitu.Hii ni ulemavu wa nafsi kudumaa,ina tokana na watu kukuvunja moyo,kukuonyesha ukali,na kukufanya ukose ujasili.
Lakini inakupasa kujikomboa katika damu ya Yesu,na kuomba sana ili hali hii iondoke,maana wewe ni mtu muhimu sana katika ufalme wa Mungu,tena iko mali nyingi ndani mwako na wengine wanaihitaji ili iwasaidie.Shetani anakuweka uwe mstali wa nyuma ,wakati wewe una hekima ya ki Mungu ndani mwako,shetani huyo,anakufanya uamini wengine wakati wao walikuwa wanatakiwa kuiga kwako na kuongozwa na shauri lako.
Ushuhuda.
Mama mmoja mtumishi wa Mungu wa siku nyingi,Bwana alimuonyesha yuko darasani anasoma pamoja na watoto wengine,akaona yupo dada mmoja anaonekana kama mwalimu wao,alikuwa anamshambulia darasani,baadaye akaja kumuuliza kwamba amekasirika,maana aliogopa mama huyo asije akamsemea vikawa vibaya kwake, kwa maana mama huyo kumbe alikuwa mwalimu wa darasa hilo na dada huyo alikuwa ni mwalimu mtarajiwa (alikuwa anafanya stage,alikuwa si mwalimu bali stagiaire) akauliza maana ya ndoto hiyo .Mungu alimfunulia kwamba yeye hatakiwi kujiweka nyuma kama mwanafunzi,bali ashike majukumu yake ya kufundisha huku akiwasaidia hao watumishi watarajiwa ili wajue jinsi kazi ya Bwana inavyo fanywa,asije akaingia kwenye mtego wa shetani wa kuharibu kazi ya Bwana kwa kunyamanza wakati wa kuinuka na kutoa maelekezo mazuri.
Biblia inasema,
“liko baa nililoliona chini ya jua,nalo ni kosa litokalo kwake yeye atawalaye,ya kuwa upumbavu huwekwa mahali pa juu sana ,nao wakwasi hukaa mahali pa chini .Mimi nimeona watumwa wamepanda farasi nao wakuu wakienda kwa miguu juu ya nchi kama watumwa.”Muhubiri 10:5-7.
Baada ya maono hayo, mtumishi aliomba rehema kwa Bwana maana alikuwa ameacha nafasi yake ya utumishi na kujiweka mstari wa nyuma kama mwanafunzi.Ndipo sasa akaanza kushambuliwa visivyo stahili. Roho ya kujishusha na kutojiamini ishindwe kwa jina la Yesu, nguvu na uweza kutoka kwa Bwana vitufunike ,na ujasiri wa Roho wa Bwana utuatamie tuyitende kazi ya Mungu ,na Bwana atutie nguvu.!!!
Kutojitambuwa kumesababisha madhara mengi sana.Hasira inatawala;hata kitu kidogo kinakukasirisha,huna uvumilivu,ukiona haki imekosekana ,hapo hapo hasira inawaka,
Mhubili 7:9 “usifanye haraka kukasirika rohoni mwako ,maana hasira hukaa kifuani mwa wapumbavu.”
unaachilia,unajifunza kuwa kwenye nafasi ya yule aliyotenda hayo,utajikuta ,labda amesahau,au amekuwa na kazi nyingi,au amepata wageni au ujumbe hujamfikia. Badala ya kukasirika,muulize polepole akueleze kwa nini ametenda hivyo.Jifunze kuwa mpole,na mtulivu ,tufuate nyao za Bwana wetu Yesu,maana,
“ yeye hakutenda dhambi wala hila haikuonekana kinywani mwake.Yeye alipotukanwa hakurudisha matukano,alipoteswa hakuogofya,bali alijikabidhi kwake yeye ahukumuye kwa haki.”1Pet 2:22-23.
Ipo tabia nyingine ya kujikuta una usemi siyo mzuri.
kilakitu unakiona kigumu hata kitu rahisi unasema hukiwezi.Vile vile,katika maongezi yako unajikuta wewe mtazamo wako ni kusema “hiki sicho,siyo hivo,wewe huwezi,usifanye,wewe umekosea,n.k….”Maneno haya,anaonyesha mtu wa kukatisha tamaa.Ukiwa rafiki wa mtu kama huyo,hutasonga mbele,utadumaa,au utashindwa kabisa na kuacha malengo yako.Muombe Bwana akubadilishe maana anaweza. Tabia hiyo,inakukwamisha wewe nafsini mwako,maana tunajua kwamba ulimi unaumba.Ukikili kwamba utashindwa,ni kweli utashindwa.Yapo maneno ni mazito kumwambia mtu.Ku mwambia, “wewe umekosea” jambo hili,linaonyesha ,kuhukumu,kulaumu,kumuweka chini kabisa hata akose cha kujibu.Hata kama ni kweli amekosea,ungetafuta maneno mepesi ya kumuonyesha vile angetakiwa kufanya lakini hajafanikiwa kuvifanya,labda siku nyingine atavifanya.Kumwambia mtu “wewe huwezi”,jambo hili linakatisha tamaa,pia linakushusha chini.Kuliko kusema hivo,hata kama ni kweli hawezi ,bora umwambiye ;ili ufanikiwe ,tafuta vifaa hivi na vile utafanikiwa.Au pita kwenye njia hii utafika.Mueleze njia ya kufanikiwa ,msaidie kwa maneno yako umtie moyo ili aendelee,afikie malengo yake,na Bwana akusaidie.Tumuombe Bwana atusamehe ,tumekosesha watu raha bila kujua, tumewahuzunisha na kuwakatisha tamaa, Bwana atubadilishe, atuwezeshe tuwe msaada kwa wengine wote wanae tusikia ,tusiwe tena vikwazo kwao,na kwetu pia,maana neno la Bwana linasema
“Mtu atashiba mema kwa matunda ya kinywa chake,..”Mithali 12:14.
Ukali pia ni tabia inayoendana na hasira,lakini hiyi ni tofauti na hasira.Ukali ni kufoka au kusema na sauti ya tishio.Watu watakuogopa,hata iwe habari njema watashindwa kukufikishia.Biblia inasema kwamba aliye mkali hujisumbua mwilini mwake.
Mithali 11:17.
“Mwenye rehema huitendea mema nafsi yake,Aliye mkali hujisumbua mwili wake.”
mtu mkali wanamuogopa,wanakuwa kama wafungwa mbele zake.,hawana amani kwa sababu ya tabia hiyo.Kama hujitambui utapona je?Hata daktali ili akutibu, anakuuliza una shida gani?,unaumia wapi? Kutoka lini? Na wewe unajieleza vizuri.Tunahitaji kutambua matatizo yetu ili tupone.Tuombe sana Mungu afungue ufahamu wetu ili kila mtu ajitambue. Tukijitambua,tutajua kuomba maombi yenye matunda.Ni sawa na kupiga kitu kwa kulenga sawasawa.Na Bwana awe pamoja nasi.
Yesaya alijitambua kwamba yeye ni mwenye midomo michafu,ndipo malaika akagusa midomo yake na mkaa akawa safi. Wewe ukoje? Mwambiye Bwana shida yako atakusaidia.Yeye ni mwenye rehema na neema nyingi sana,hatafungia nje sauti yako,wala hatapuuza maombi yako.Tangu zamani,wote waliyemkimbilia wamekuwa salama.
Zaburi 86:15,
“lakini wewe, Bwana,u Mungu wa rehema na neema ,Mvumilivu,mwingi wa fadhili na kweli.”
Mwambie Bwana akubadilishe,akuponye na tabia zako mbovu maana zinakuua wewe,zinakuletea magonjwa zingine zinaumiza jirani yako,watu wa nyumbani mwako,n.k,…
Tumuombe Bwana atujulishe jinsi tulivyo na atuponye maana yeye ni mwenye rehema nyingi,hakuna jambo asiloliweza.
Zaburi 86:16
“Unielekee na kunifadhili mimi; mpe mtumishi wako nguvu zako,umwokoe mwana wa mjakazi wako.”
-Wewe u Mungu uonaye.
Mtu mwenye macho humfichi kitu.Lakini kipofu hata umuonyeshe haoni.Watu tunasema tunaona lakini hatuoni.Dunia hii imetupofusha na watu waliotuzunguka na vingine vingi. Lakini Mungu alie mbinguni anaona wanadamu wote. Anaona nyuma na ndani ya mtu. Mimi jina langu ni”HABONAYO” maana yake ni ;Mungu ndie aonaye .
Katika kitabu cha, Mwanzo 16:13.Tunasoma neno hili;
“wewe u Mungu uonaye”
Mungu alimtuma malaika wake kwa mjakazi wa Ibrahimu, jina lake Hajiri.
Hajiri alipata mimba kwa Ibrahimu.Wakati huo akaanza kuvunja heshima kwa Sara bibi yake.Naye Sara akaanza kumtesa ndipo Hajiri akakimbia na mtoto tumboni.
Malaika wa Bwana akamuuliza;
Mwanzo 16: 8-9
“Hajiri ,wewe mjakazi wa Sarai,unatoka wapi,na unakwenda wapi?Akanena; nakimbia mimi kutoka mbele ya bibi yangu Sarai.
Malaika wa Bwana akamwambia,rudi kwa bibi yako,ukanyenyekee chini ya mikono yake”
Hajiri alikua hajui anaelekea wapi.Tena hajasema kwanini aliteswa na bibi yake.lakini Mungu alimwambia “jina lake, na kazi aliompa ” Tazama neno hili; “Hajiri, wewe mjakazi wa Sarai…”
Kwa sababu Mungu alitambuwa kwa nini alimkimbia bibi yake alimwambia ujumbe huu;“ Rudi kwa bibi yako”.Ujumbe wa pili ilikuwa ushauli, kwa sababu ya kiburi na kukosa heshima.
“Nyenyekea chini ya mkono wake”.
Mungu anakuona hata na wewe. Anaona unaishije, unateseka vipi na unafanya nini.Watu wengi wanasema ni watu wa Mungu lakini ni kujidanganya tu.Wanakua kwenye vikundi wanaomba, wana imba lakini hawajui kwamba Mungu anaona hata ndani kwenye mawazo yetu.Unaweza ukajiuliza kwa nini Mungu aliuliza Hajili eti anakwenda wapi?Unafikili Mungu alikuwa hajui? Alikuwa anajua ,lakini alikuwa anataka kuona kwamba Hajili anajitambua kwamba ni yeye mwenye makosa au la.
( Isaya 29:13)
“Watu hawa hunikaribia na kuniheshimu kwa vinywa vyao,bali mioyo yao imefarakana nami,na kicho chao walicho nacho ni maagizo ya wanadamu waliyofundishwa.”
Mungu hadanganywi kwa sababu anaona kote.Ukimkaribia mkaribie na moyo wako wote msafi.Na ukumbuke kuzingatia maagizo yote ya Mungu ili umwabudu kwa roho na kweli.
(1Sam 16:7)
“…Bwana haangalii kama binadamu aangaliavyo maana binadamu huangalia uso wa nje bali Mungu huutazama moyo”.
Tuisafishe mioyo yetu,tumkaribie Bwana tukiwa wa safi,huku tukijua kwamba mda si mrefu Bwana Yesu atarudi, nasi tutakwenda naye mbinguni. Mungu anajua watu wake.Anaona kila wakati ,hatuna haja ya kuogopa shida tulizo nazo,cha msingi tuchunge mioyo yetu kwa sababu shida nyingi tulizo nazo ni matokeo ya dhambi tulioifanya.
Kumbuka Hajiri aliteseka na kukimbia kwa sababu ya kiburi chake kwa Sara.
Yupo mama mwingine kwenye Biblia,jina lake Miriam,yeye alishikwa na ugonjwa wa ukoma kwa sababu amenung’unikia Musa mtumishi wa Bwana(Hesabu 12:10-15).
Manung’uniko ya Miriam,alisababisha shida nyingi sana.
Watu wake walilia,waliomba sana,walihuzunika,pia waliahilisha safari waliokuwa nayo wiki nzima yaani (siku saba zote).
Watu wake ,walitubu kwa ajili ya kosa lake ili Mungu amurehemu.Wamefanya huduma ya upatanisho kati ya mama huyo na Mungu wake.Miliam alifanya kosa kubwa sana mbele za Bwana.
Mara nyingi manung’uniko anafanyika kwa siri sana. Unaweza usijue kwamba furani anakunung’unikia,lakini Bwana anaye ona kote anatambuwa vyote vinavyo fanywa na wanadamu,haswa watu wa Mungu.
Miliam ni mtumishi aliye fanya kazi kubwa pamoja na kaka zake; Musa na Haruni,lakini dhambi ilipo ingia moyoni mwake,Bwana aliona vema amhubilie mwenyewe kwa njia zake,ili afundishike , ili naye aweze kufundisha wengine.
Kumtia ukoma mwilini mwake ilikuwa ni adhabu nzito sana kwake,ya kumfanye awe mnyenyekevu na azidi kumheshimu Mungu na kumuogopa.Kweli Mungu ndiye aonaye!!!tena ndiye mwenye uweza!!!!
Biblia,inatuambia mtu mwingine , Jina lake ni Zakaria ,tunasoma habali yake katika ( Luka 1:1-20). Yeye na mkewe walikuwa wazee sana walikuwa hawana mtoto, mke wake alikuwa tasa. Yeye, pamoja na uchungu wake wa tatizo la kuwa tasa,aliendelea kumpenda Mungu na kumtumikia kwa uaminifu.
Biblia inasema ;
“wote wawili walikuwa wenye haki mbele za Mungu,wakiendelea katika amri zote za Bwana na maagizo yake bila lawama.”Luka1:6.
Ndipo sasa alipokuwa akitumika hekaluni mwa Bwana,
malaika akamtokea akamwambia kwamba anamletea habali njema,
kwamba dua lao limesikika,kwamba mke wake Elzabeth,atamzalia mtoto wa kiume,akamwambia jinsi mtoto huyo atakavyokuwa na kazi nzuri atakayefanya ya kurejeza wa Israeli kwa Mungu wao,,na kugeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto,pia na kuwatilia waasi akili za wenye haki ,na kumwekea Bwana tayari watu waliotengenezwa.(mst 16 na 17)
Pamoja na kumueleza hayo yote, Zakaria ,bado ,hajaamini alishikilia kwamba ni wazee,kupata mtoto ni jambo kwake aliona limesha pitwa na wakati.
Zakaria alimwambia malaika hivi: “Nitajuaje neno hilo,maana mimi ni mzee,na mke wangu ni mkongwe wa siku nyingi.”Luka1:18.
Malaika akaendelea akajieleza kwamba ametumwa na Mungu kumpasha habali hizo njema.(mst19)
Hapa tunaona ,mtumishi wa Mungu,mwenye sifa nzuri mbele za Bwana,akishindwa kuamini ujumbe wa Mungu.
Kumbe sasa shida yao ya mda mrefu imewaharibia maisha yao ya kiroho.
Bwana ndiye anaye ona !!!
Bwana aliona kwamba shida yao ya kutokuwa na mtoto ni ndogo kuliko kufa kiroho.Bwana ni mwenye upendo mwingi sana,aliponya roho yake kwanza ,na alipo fufuriwa imani yake ,akapokea sasa mtoto.
Unaonaje angempa mtoto kwanza bila kumfundisha?? Bila shaka ,kama roho yake haijakarabatiwa angeendelea na manung’uniko baadaye(kwa nini kupata mtoto wakati sina mda wa kumlea?,au angesema ona sasa watu wanaanza kutucheka na kushangaa! N.k..),au hangefurahia ipasavyo muujiza.
Bwana anatambua yote. Unaweza ukawa na sifa nzuri mbele za watu ,maana wao ndio wanaotoa ushuhuda kwetu. Wanatuona tukimwimbia Bwana,tukihubili,tukiombea wagonjwa ,n.k. Wanatupa sifa nzuri sana.Lakini Bwana anaye ona ,anajua wewe una ugonjwa gani. Bwana anajua ashugulikie nini ndani mwako ili upate mafanikio ya kudumu.
Zakaria,Bwana amemtia kuwa bubu kwa mda.
Jambo hilo naamini limemfanya awe mnyenyekevu mbele za Bwana ,na kumuomba rehema kwa kutokuamini kwake,na Bwana alimsikia. Watumishi wengi si rahisi kuwaonya,lakini Bwana anazo njia za kumbadilisha mtu.Dhambi iliyofichika nani awezaye kuiona?
Bwana peke ndiye aonae.
Tumuombe Bwana alete uhai ndani ya nafsi zetu.
Tuombeane wapendwa ili tuwe hai rohoni.Watu wengi wanatumika lakini hawana uzima wa Mungu ndani mwao.
Inawezekana,uchungu wa shida yako imekuwa nyingi hata huoni tumaini lingine.Bwana akuokoe ,akuinue,na akufufue na akupe nguvu mpya.Zakaria na mkewe wamepona nafsini mwao,baadaye wakaona muujiza. Bwana amewaona ! .Neno la Bwana linasema,
“Nimekufundisha katika njia ya hekima ,nimekuongoza katika mapito ya unyofu,uendapo,hatuwa zako hazitadhiikika,wala upigapo mbio,hutajikwaa.”Mithali 4:11-12.
Mpendwa unayesoma habari hii,Bwana ndiye anayeona kote.Tena anatambua na mawazo yetu yote,pia na nia zetu kati ka kila jambo tulifanyalo.Sasa basi ,tuwe wazi mbele zake,tusiwe wanafiki,bali tuwe wasema kweli.Naamini Bwana ameshakufundisha mara nyingi,kama alivyonifundisha na mimi pamoja na wengine wengi.Mimi na wewe tushirikiane katika maombi ili tusaidie na wengine .Dhambi zote tunazifanya kwa siri.Lakini Bwana anazitambua zote.Kwa nini mpendwa usitubu na kukili udhaifu wako ili akusaidie upate amani ya kweli katika Kristo Yesu? Yeye anakuhitaji ili akusaidie,anaona jinsi dhambi zimekulemea sana,anataka akupe uhai wake,je uko tayali kumpokea ili akusaidie?Kama jibu lako ni ndiyo namhitaji Yesu ili abadilishe maisha yangu, omba pamoja nami ukifungua moyo wako kabisa mbele za Bwana na sauti kubwa.
Sema,
Ee Bwana naja mbele zako sasa,nakili mbele zako kwamba mimi ni mwenye dhambi,nimetumikia shetani mda mrefu sijapata amani,sasa Bwana naja kwako,nakugeukia wewe Yesu mwana wa Mungu,nakuomba ukaoshe dhambi zangu zote nilizo zifanya nikiwa najuwa, nazingine nilizozifanya bila kujua.Bwana ukazifute zote ndani ya damu yako, ukanioshe niwe safi kabisa.Namuacha shetani nakugeukia wewe, niwe wako siku zote za maisha yangu.Futa jina langu katika kitabu cha hukumu na kuliandika katika kitabu cha uzima.Asante Bwana kwa kuniokoa.Tangu sasa ni wako,nitakufuata na kukutumikia.Na baada ya siku zangu hapa duniani ,tutaishi pamoja na wewe mbinguni.Kwa jina lako Yesu Kristo naomba hayo Amen.
Bwana Yesu nakushukuru kwa wokovu wako.Asante Yesu kwa kunikubali kuwa mtoto wako.Unishike na nguvu zako ee Bwana nisirudi nyuma bali nisonge mbele hadi mwisho wa safari yangu.Asante Yesu,wokovu wangu na ngome yangu,kimbilio la maisha yangu!!!.
Kama wewe hutaki kumpokea Yesu kama mwokozi wa maisha yako,na wewe nakuomba useme maneno haya,ukiwa umefungua moyo wako,sema;
Bwana Yesu nimesikia habari zako kwamba unaona kote,sasa nami Bwana najua kwamba umenijua na kunitambua kwamba mimi ni mwenye dhambi.Ni kweli mimi nimwenyedhambi nahata sasa najisikia siko tayari kukupokea moyoni mwangu.Nakuomba Bwana Yesu,unisaidie nisife kabla sijakupokea kama mwokozi wa maisha yangu.Pia nakuomba uendelee kunifundisha ndani ya kurasa zinazofuata ili nifundishike.Bwana unifahamishe neno lako nikujue wewe na nisimalize kitabu hiki kabla hujagusa moyo wangu.Naomba hayo katika jina lako Yesu.Amen.
-Hasira.
Napenda tuzungumze juu ya tabia moja mbaya sana ,imejificha mno.Tabia hii,imeua watu wengi sana,imesababisha matengano kati ya ndugu na ndugu,tutaiangalia kwa upana.
Hasira imeandikwa kwenye Biblia. Inaonyesha kwamba inaleta dhambi.Inaweza pia ikasababisha magonjwa.Hasira inaweza pia ikatoka kwa Mungu kama umemkosea kama wana wa Israeli walivyo muasi na kufuata miungu mingine.
(Kumb 31:16)
“Bwana akamwambia Musa,angalia wewe utalala na baba zako;na watu hawa wataondoka ,wataifuata kwa ukahaba miungu ya kigeni ya nchi waiendeayo kuwa kati yao, nao wataniacha mimi na kulivunja agano langu ,nililofanya nao.”
Kwa kuacha agano la Mungu, neno la Mungu ndilo linalotuonyesha kwamba (ni dhambi). Hasira ya Mungu iliwaka yuu yao.
( Kumb 31:17)
“Ndipo hasira yangu itakapo waka juu yao siku hiyo, nami nitawaacha, nitawaficha uso wangu, nao wataliwa, tena watajiliwa na mambo maovu mengi na mashaka…”
Kama mmekasirika msitende dhambi.Jua lisizame wewe ukiwa na hasira hata kama una haki ya kweli kama Yesu, wakati wale waliodharau hekalu la Mungu mpaka wakafanyia humo biashara .Yesu alikasirika. Hasira ile ilikuwa takatifu, (Mat 21:12-13) na,(Yohana 2:14-16.)
Hasira ya mwanadamu ni mbaya sana ina madhara makubwa inaleta magonjwa mengi sana kama vile;
-Mapigo ya moyo
-shida ya kupumua,
- presha
-vidonda vya tumbo
- kuchanganyikiwa
Hasira inakuja eidha wamekukosea eidha haki yako haijatekelezwa.Hasira inakuja wakati umeshindwa ku samehe.
Hasira inakuja hivi: unakaa ukitafakari kwa nini wametenda hivi au hivi usiku kucha unawaza; kwa nini ?hupati jibu siku mbili au tatu, moyo wako unaanza kuwa na uzito sana, unapumua kwa kuvuta sana.Wengine wanashikwa na kitu kama jiwe shingoni, wengine wanasikia maumivu kwenye kichwa (unachanganyikiwa).
Wengine tumbo linaanza kuvimba.
Biblia inasema
Mithali 30:33
“Kwa maana kupiga maziwa huleta siagi na kupiga pua hutokeza damu; kadhalika kuchochea hasira hutokeza ugonvi.”
Tuombe Mungu atuondolee hasira,
“tuwe na roho ya upole na utulivu iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu .Maana hivyo ndivyo walivyokuwa wakijipamba wanawake watakatifu wa zamani, waliomtumaini Mungu, na kuwa tii waume zao”.(1Pet 3:4-5)
Kwa hiyo hasira ni kama pepo wa shetani. Inakuvamia na kukutayarishia mambo machafu sana.
Ukiwa umekosewa na mtu, muone, mtengeneze pia umsamehe.
Hasira ni hali ya kukasirika .Ukimkasirikia mtu ni kusema hakuna tena upendo kwake, pia moja kwa moja shetani anaingiza mafundisho yake.Kama ulikuwa na heshima kwake unaanza kumdharau, kumsema vibaya na mengine mengi.
Hasira inakugeuza kuwa kichaa au inakuletea sumu kwenye ufahamu, ukiona mtu anakupandikizia hasira ndani yako usipokee.Usikubali bali ukatae kwa nguvu zako zote maana lengo la ibilisi ni kukutega wewe unaetendewa.
Paulo naye anawandikia waefeso eti wawe na hasira lakini wasitende dhambi.Jua lisichwe na uchungu wenu bado haujawatoka,wala wasimpe ibilisi nafasi.Efeso 4:26-27,31&zab4:4.
Ushauri wa Paulo mstari wa 32 unasema;
“Wa saidiane,wa hurumiane,wa sameheane.”
Ushuhuda.
Ndugu mpendwa, namshukuru Mungu ameniponya na hasira.Mimi, nimemuona Bwana akinishindia hasira, lakini nakuhakikishia kwamba kabla sijateswa nalipotea.
(Zaburi 119:67) inasema
“Kabla sijateswa mimi nalipotea, lakini sasa nimelitii neno lako”.
(Zaburi 119:75)
”Najua ya kuwa hukumu zako ni za haki, Ee Bwana,na kwa uaminifu umenitesa”.
Namshukuru Mungu amenifunulia dhambi iliekuwa inanitesa muda mrefu.Kusema kweli nilikuwa sijui kwamba nina hasira.Siku moja mfanyakazi wangu wa ndani amenijibu vibaya nikaumia kiasi cha kuumwa.Mapigo ya moyo akaanza,nikimuona tu au nikisikia sauti yake,moyo ulikua unapiga sana ,nikaanza kupumua kwa kuvuta.Nilipo tulia nikatafuta muda tukaongea nikapona magonjwa hayo mpaka leo.Ndipo nikagundua kwamba magonjwa mengi anatokana na hasira.
Siku nyingine nimejikuta kumbe mimi nilikuwa natenda dhambi bila kujuwa.Nikiona unafanya kitu sio kizuri nilikua mwepesi kuku hukumu. Hapo nilikuwa sijajua kwamba natenda dhambi maana hukumu ni ya Mungu peke yake.Neno la Mungu linasema kwamba
“….yeye ahukumuye kila mtu bila upendeleo…”(1Petro 1:17)
Neno la Bwana linasema katika kitabu cha
(Warumi 11:33)
“Jinsi zilivyo kuu utajiri na hekima na maarifa ya Mungu! Hukumu zake hazichunguziki wala njia zake hazitafutikani.”
Namshukuru Mungu nilikuwa nimepotea Bwana akanitesa kwa mapigo yake ili nijifunze kwake na kurekebika.Kwa uaminifu wake amenitesa, na hukumu zake ni za haki.
Ameniondolea lawama na dharau, ameniondolea hasira na jeuri nalitukuza jina la Bwana .Nami namuomba Bwana
“asiliondoe neno la kweli kinywani mwangu kamwe, maana nimezingojea hukumu zake”(Zaburi 119:43).
Kuna dhambi nyingine mbaya inaitwa “chuki”.Ili ujuwe kwamba unayo,unajikuta kwa ajili ya neno, Fulani ameliongea,ukaona halipendezi machoni pako.Unajikuta yule mtu aliolisema humpendi tena, maana amekuhuzunisha.Unajitahidi kumukubali moyoni mwako lakini unajikuta ukimuona tu,amani inatoweka bila sababu.Dawa si nyingine,ni kumuombea ili ile roho inayotenda kazi ndani yake ya kukukosesha amani imtoke.Ukiyikemea itaondoka nawe utakuwa na amani naye.Kumbe kila mtu ni mzuri lakini mara nyingi roho ya uharibifu inatumika kupitia watu.Kwa hiyo usimtukane mtu ukimuita shetani na kumuombea afe au akimbie mbali na wewe hapana, lakini angamiza ile roho inayopata nafasi kupitia yeye.
Usisahau kwamba adui yetu ni ibilisi,naye anatuwinda kupitia njia nyingi.
Ukipambana na roho itaondoka na wewe utaokoka kwenye mitego ya ibilisi.
(Zaburi 124:7-8)
“Nafsi yetu imeokoka kama ndege katika mtego wa wawindaji, mtego umevunjika, nasi tumeokoka.Msaada wetu u katika jina la Bwana,aliezifanya mbingu na nchi.”Haleluya .
Sura ya 2:
Matokeo ya dhambi.
Dhambi ni mbegu inayoleta mazao mengi
Mfano
Wizi unaleta mauti(Jambazi anaweza akapigwa risasi akafa)
Uongo(unaweza kushuhudia uongo kule mahakamani ukapelekwa gerezani)
Ni mifano mingi tu lakini nataka tuangalie tunda la dhambi linaloitwa Magonjwa.Yaani,nikusema unatenda dhambi matokeo yake unapatwa na magonjwa.
Magonjwa mara nyingi tunadhani ni kazi ya shetani kwa upande mmoja inawezekana lakini upande mwingine ni matokeo au tunda la dhambi. Si kila dhambi inaleta magonjwa hapana dhambi zingine zinaweza zikaleta raha kwa muda huo huo au zikaleta furaha kwa mda mfupi ndio maana mwandishi wa Zaburi 73 :3-6 amesema;
« Maana naliwaonea wivu wenye kujivuna nilipo iona hali ya amani ya wasio haki.Maana hawana maumivu katika kufa kwao,na mwili wao una nguvu.Katika taabu hawamo wala hawapati mapigo pamoja na wanadamu.Hivyo kiburi kimekuwa mkufu shingoni mwao.Jeuri huwavika kama nguo ».
mst wa 17-18 « Hata nilipoingia patakatifu pako na kuutafakali mwisho wao,hakika wewe huwaweka penye utelezi,huwaangusha mpaka palipoharibika. »
Mst wa 27-28 unasema « Maana wajitengao nawe watapotea ;umewaangamiza wote waliokuacha wewe.Nami kumkaribia Mungu ni kwema kwangu ;Nimefanya kimbilio kwa Bwana Mungu.niyahubiri matendo yako yote. » Haleluya !
Mtunga zaburi yeye aliwanaonea wivu wabaya wakistawi sana lakini aliambiwa kwamba mwisho wao ni mbaya.Sasa tumeweza kuona kwamba unaweza kutenda dhambi ukwa salama ukaendelea kustawi,mpaka mwisho utakapo hukumiwa na kutupwa motoni.
Hapa tunaangalia jinsi magonjwa yanaweza kuwa mshahara wa dhambi na mara nyingi bila huruma na rehema za Mungu unaweza ukafa wakazika kabisa lakini mara nyingi ukiomba msamaha na kutubu unapona kabisa, jina la Bwana libarikiwe.
Ushuhuda (1)
Siku mmoja dada mmoja alishuhudia kwamba,aliumwa macho,akatibiwa muda mrefu,macho yakaendelea kumuumiza akakata tamaa,maana aliomba sana lakini hakupona,aliweka dawa lakini hakupona aliuliza Mungu afanye nini tena?Bwana akamfunulia kosa alilolifanya likamsababishia apigwe namna hiyo akatubu na kuomba rehema kwa Bwana akapona hapo hapo.
Zab119:77
”Rehema zako zinijie nipate kuishi,maana sheria yako ni furaha yangu.”
Mstari huu unasema kwamba rehema za Mungu zikikujia utapata kuishi.
Ushuhuda (2)
Mpendwa mwingine alishuhudia kwamba alihuzunishwa na mchungaji wake siku moja,huyo mpendwa akajenga chuki moyoni mwake kwa huyo mtumishi wa Mungu,ndipo Bwana akampiga na ugonjwa,wa kuteguka kiuno.(Alikuwa ananyanyua boxes nzito akitaka kufanya usafi) Akalala siku tatu na maumivu makali mwilini mwake alipouliza kwa nini hayo alimpata Mungu akamjulisha kosa alilolifanya akaomba Bwana amrehemu akapona baada ya siku 3.
“Neno la Mungu linasema usimnenee mabaya mkuu wa watu wako”(Mdo 23:5)
Kutoka 22:28“usimtukane Mungu wala usimlaani mkuu wa watu wako”.
Mtume Paulo alikuwa anajieleza mbele za watu hivi ;mimi kwa dhamiri safi nimeishi mbele za Mungu hata leo hii (Mdo 23:1)Ndipo sasa mtu jina lake Anania akaamuru Paulo apigwe kwenye kinywa chake ndipo sasa
Paulo akasema
“Mungu atakupiga wewe ukuta uliopakwa chokaa wewe umeketi kunihukumu sawasawa na sheria nawe unaamuru nipigwe kinyume cha sheria (Mdo 23:3)”
Paulo alikuwa anasema kweli huyu kuhani Anania amempiga kinyume cha sheria.Pia ni kama ukuta uliopakwa chokaa,tena ni kweli Bwana atampiga nayeye kwa sababu amefanya vibaya kwa mtumishi wa Mungu Paulo.Sasa haya maneno ya Paulo yameonekana kuwa matusi kwa sababu yamenenwa juu ya mkuu.
Ndipo sasa Paulo akajieleza ya kwamba alikuwa hajuwi ya kwamba Anania alikuwa kuhani mkuu.Maana yake angejua kuwa ni kuhani mkuu asingesema hivyo.Maana neno la Bwana linasema tusiwalaani wakuu.
Huyo mpendwa alikuwa anajua kwamba aliyefanya kosa ni huyo mchungaji wake aliyemhuzunisha.Lakini Mungu hakuangalia mtumishi huyo bali aliangalia jinsi huyo mpendwa alivyojiweka vibaya na kutokuendelea na heshima na upendo kama mwanzoni.
Mkuu ni mkuu.Baba ni baba na mtoto ni mtoto.Mkuu akikuonea usijali,mpende tu mengine Bwana mwenyewe atashughulika nayo.
Zab119:92.
”Kama sheria yako isingekuwa furaha yangu, hapo ningalipotea katika taabu zangu.”
Tuna taabu nyingi duniani lakini ,tusipo shika sheria ya Mungu ,tutapotea na kufa katika taabu zetu.
-Je ni kweli magonjwa yote ni tunda la dhambi?
Hapa tunasema hapana magonjwa mengine ni vifaa vya Mungu anavyotumia kwa kutulea kiroho au kutuelimsha juu ya unyenyekevu au kuzuia majivuno.
Tunaona mfano wa Paulo alivyokuwa anaumwa sana.Yeye si kwamba amefanya dhambi lakini yeye amepata neema kubwa sana ya kuona maono ya Mungu ndipo Bwana akampa mwiba mwilini mwake.
Paulo aliomba sana Mungu ili apate uponyaji. Neno la Mungu linasema, (kwa ajili ya kitu hicho nilimsihi Bwana mara tatu kwamba kinitoke.Naye akaniambia neema yangu yakutosha maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu),
Paulo alielewa kusudi la Mungu kwake na mwiba huo.
(Na makusudi nisipate kujivuna kupita kiasi, kwa wingi wa mafunuo hayo nilipewa mwiba mwilini ili anipige nisije nikajivuna kupita kiasi)
(2kor 12:7).
Magonjwa ya Paulo, yalikuwa yanamlinda ili asijivune kupita kiasi maana aliona ufunuo mkubwa sana.
Amesema kwamba alinyakuliwa mpaka peponi akasikia maneno yasiotamkika , ambayo haijuzu mwanadamu ayanene.(2ko 12:4).
Paulo ameona maono makuu, mpaka nayeye kama mwanadamu anajisifu sana.Lakini anasema anajizuia ili mtu asimhesabie zaidi ya hayo ayaonayo kwake au ayasikiayo kwake. (mstari wa 6)
Mtu akisema jinsi Bwana anavyomtumia sana watu wanaweza wakakufananisha na Malaika au Mungu mwenyewe. changamoto ni kwamba tuwe tunajizuia kueleza yote au tutumie hekima alioitumia.
Paulo aliposema ;
(namjua mtu mmoja katika kristo sasa yapata miaka kumi na mine kwamba sasa alikuwa katika mwili sijui, kwamba alikuwa nje ya mwili sijui Mungu ajua .Mtu huyo alinyakuliwa juu mpaka mbingu ya tatu) (2Kor 12:2).
Magonjwa ya Paulo Bwana aliyatumia kama kifaa cha kumlea,ili Paulo azidi kuwa mnyenyekevu mbele za Mungu.Kama Mungu ana makusudi na ugonjwa wako hata waombe,hata wakutibu hutapona maana Bwana kusudi lake ndilo kubwa kuliko uponyaji.Tusisite kuomba uponyaji wala tusijilaumu kama jibu lake ni la.Tujue ya kwamba tukiomba Bwana Yeye anatusikia kwa kuwa sisi ni watu wake,mali zake.
vifaa vya Bwana si magonjwa tu , kuna vingine kama ,njaa,kukosa kazi,kuhalibikiwa(kama ulikuwa una vitu vingi ukamuacha Mungu,Bwana anaweza akaviondoa ukabaki huna chochote ili upate muda wa kumtafuta Bwana na kumtumikia vizuri).
Ushuhuda(1)
Mwinjilisti mmoja aliomba Bwana amfanikishe kimaisha lakini mpaka leo, ni mtu wa Mungu lakini hali yake ni ile ile.Alipomuuliza Mungu,Bwana akajibu kwamba ni kusudi lake ili awe hivyo,maana akifanikiwa hatakuwa na nguvu za Mungu kama mwanzo.
Ushuhuda (2)
Mpendwa mmoja alishuhudia kanisani kwamba alipata kazi ya ulinzi,wezi wakaja wakaiba naye akapelekwa gerezani.Alikuwa mkristo lakini alisema kwamba alikuwa wa mwisho kuingia kanisani na alikuwa wa kwanza kutoka,maana yake kama ibada ilianza saa tatu asubuhi yeye anaingia saa tano ili atoke kabla ibada haijaisha.Tangu alipotoka gerezani anashuhudia kwamba anakuja kanisani mapema,anasubiri ibada iishe tena akipata nafasi anahudhuria vipindi vya katikati ya wiki.
Bwana ni mwema tena anajua udhaifu wetu.
Ushuhuda(3)
Namjua kwenye Biblia mfalme Nebukadreza alikuwa mtu mkubwa sana.Alikuwa na roho ya kujivuna sana,pia alikuwa hamjui Mungu,kuwa ni Mungu mkuu wa kuogopwa na kutisha.Alikuwa hajawahi kuona uweza na mamlaka ya Mungu.Alikuwa anajua kwamba yeye tu ndiye mfalme,juu yake hakuna mwingine.Neno la Mungu linasema kwamba,Bwana alimshusha chini akakaa porini pamoja na wanyama,muda wa miaka 7.Kiburi kikaisha ,akatambua uweza wa Mungu na nguvu zake.Ndipo akasema hivi!
“Hata mwisho wa siku hizo,mimi Nebukadreza nikainua macho yangu kuelekea mbingu,fahamu zangu zi kanirudia,nikamhimidi yeye aliye juu,nikamsifu na kumheshimu yeye aishiye milele;Kwa maana mamlaka yake ni ya milele,na ufalme wake hudumu kizazi hata kizazi;Na watu wote wanaokaa duniani wamehesabiwa kuwa si kitu,naye hufanya apendavyo katika jeshi la mbinguni na katika hao wanaokaa duniani wala hapana awezaye kuuzuia mkono wake wala kumuuliza unafanya nini wewe.(Dan 4:34-35)
Mfalme Nebukadreza Bwana alimpiga pigo kubwa ili aelewe uweza na nguvu zake Mungu.Pia,ametumia miaka mingi sana kumuelimisha.
Anasema,
“hata mwisho wa siku hizo,mimi Nebukadreza nikainua macho yangu kuelekea mbingu.”
Nebukadreza ujanja wake wote ulikuwa umekwisha,
kiburi chake kikakoma ,
sauti ya maneno ya majivuno ikageuka kuwa (sauti ya mnyama),
mwili wake ulikuwa umenona ukawa kama wa mnyama
nywele zake zikawa kama manyoya ya tai,
kucha zake kama za ndege .
Alikuwa mtu wa watu akafukuzwa na wanadamu,
alikula chakula cha kifahari,(akapelekwa kula majani kama ng’ombe) (Dan 4:33)
Alipoinua macho yake juu kwa mwenye nguvu (Mungu),ndipo akatambua ukuu na uweza wake,akamhimidi akimsifu na kumheshimu,maana amegundua kwamba kumbe Mungu ni wa kunyenyekewa milele.Anatawala mbinguni na duniani.Ni mwenye mamlaka ni mfalme wa wafalme.
Anasema tena,wale waendao kwa kutakabari kuwadhuru(Dan 4:37).
Ushuhuda huu unaonyesha jinsi Mungu anatumia matatizo kumhubiria mtu au kumuonyesha jinsi ya kumpenda Mungu.
Mateso ni kifaa kingine cha Mungu. Mwandishi wa Zaburi amesema
“Kabla sijateswa mimi nalipotea,lakini sasa nimelitii neno lako(zab 119:67)”
”Najua ya kuwa hukumu zako ni za haki,Ee Bwana na kwa uaminifu umenitesa.(zab119:75)”
katika sura hii tunaona kwamba dhambi ni mbegu na ina matunda mengi kama (magonjwa,shida,njaa,kuondolewa cheo,dharau,kuteswa na kadhalika).Pia hivyo vyote vinaweza vikawa vifaa vya Mungu ili uokolewe au uelimishwe kiroho.
Kila jambo analokutendea ni jema tena ni ya kweli na ya haki.Kuna mateso mengine anatoka kwa shetani kama yale ya Yobu.Tusikose kuombeana sisi kwa sisi ili kusudi la Mungu lipate kutimizwa ndani ya Maisha yetu.
Sura 3 : Uponyaji.
Ndungu mpendwa napenda kuongelea neno “uponyaji” ukisikia Fulani amepona,maana yake alikuwa anaumwa.
Uponyaji ni kazi itokayo kwa Mungu kupitia njia ya maombi au njia ya matibabu.Lakini vyote ni uweza wa Mungu pekee.
Tumesha ona kwamba uponyaji unahitajika pale palipo magonjwa pia tumeona magonjwa mengine ni tunda la dhambi
Sasa basi ili tupate uponyaji ni dawa moja tu.
“kutubu na kuomba rehema kwa Mungu”.
Tunasoma neno la Bwana lina sema
“Ungameni dhambi zenu na kuombeana mpate kupona. (Yakobo 5:16)”
Tumeshaona shuhuda za watu waliopigwa magonjwa kwa ajili ya dhambi.Walipo mlilia Mungu na kutubu, wakapona hapohapo.
Sasa kumbe, kwa wengine kuhusu magonjwa yao, wanahitaji kutubu ili wapate kupona.
Pia tuelewe kwamba uponyaji unaweza ukaupata kupitia kwa watu wengine wenye karama za uponyaji kama ilivyokuwa 1korintho 12:9
Hapa tunaona ni karama ”za” kuponya na si karama ”ya” kuponya. Maana yake hii karama inatumika kwa njia nyingi au kwa sababu kuna magonjwa mbalimbali.
Basi sasa tumeona kwamba kwa wengine uponyaji unapatikana kwa kutubu dhambi walioifanya. Kwa mfano Miriamu alipopatwa na ukoma kwa kunun’gunikia mtumishi wa Mungu Musa. Walimuombea msamaha kwa Mungu akapona baada ya siku saba.
Wengine waliombewa wakakosa uponyaji wa magonjwa yao,lakini wakapata uponyaji wa roho zao.Mfano ni Paulo,aliendelea kuumwa na kuambiwa kwamba neema ya Mungu inamtosha.
Ndipo akasema “basi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi ili uweza wa Kristo ukae juu yangu.Kwa hiyo napendezwa naudhaifu,na ufidhuli,na misiba,na adha,na shida,kwa ajili ya Kristo, maana nilipo dhaifu ndipo nilipo na nguvu”.(2korintho 12:9-10)
Karama za kuponya zilizo onekana kwa njia tofauti kupitia mitume.
Wengine wamepata uponyaji kupitia mikono ya mitume kwa kuwekewa mikono kama neno linalosema.
“Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio;kwa jina langu watatoa pepo,watasema kwa lugha mpya;watashika nyoka hata wakinywa vitu vya kufisha havitawadhuru kabisa;wataweka mikono yao juu ya wagonjwa nao watapata afya(Mk 16:17-18).
Hii njia ya kuwaombea wagonjwa kwa kuwa wekea mikono,inatumika sana hata na siku hizi za leo.
(Mdo28:8-9) “Ikawa babaake Publio alikuwa hawezi homa na kuhara damu.Paulo akaingia kwake,akaomba,akaweka mikono yake juu yake,na kumpoza.Yalipo kwisha kutendeka hayo wengine waliokuwa na magonjwa katika kisiwa wakaja wakapozwa.”
Kwa Jina la Yesu mpaka leo kupitia mikono ya watumishi ,wagonjwa wanapona,haleluia.! Wewe uliyeteseka na uonevu wa shetani,kimbilia watumishi wa Mungu watakuombea kwa jina laYesu utapona.
Biblia inatuambia njia nyingine yakobo aliyesema katika waraka wake alisema hivi
“Mtu wa kwenu amekuwa hawezi?Na awaite wazee wa kanisa wamuombee,na kumpaka mafuta kwa jina la Bwana(Yak 5:14).”
Wengine waliokuwa wanapata uponyaji kupitia nguo na leso ya watumishi wa Mungu.
Paulo alikuwa anatumika sana kupita kawaida hata wagonjwa waliletewa nguo na leso kutoka kwenye mwili wake magonjwa yao yakaondoka na pepo wachafu wakawatoka.(Mdo 19:11-12).
Pia tunasoma jinsi gani Namani alipata uponyaji wa ukoma wake,yeye hakuombewa bali aliagizwa zoezi moja (Kujichovya ndani ya mto yordani mara saba.) alipolifanya akapona.Pia Tunasoma kwamba Yesu alimponya kipofu kwa kumuwekea udongo machoni pake.
Ushuhuda
Mpendwa mmoja anashuhudia kwamba anajua jinsi gani uponyaji wa ugonjwa wa ukimwi unavyosumbua sana dunia nzima unapatikana.Anashuhudia kwamba alifanya uovu mwingi mbele za Mungu.Wakati wa kutubu aliweka wazi mambo yote aliyofanya sirini akayaweka nuruni ndipo na ugonjwa huo ukatoweka mpaka leo.Anasema ukitubu kweli kweli bila kuficha chochote unapata uponyaji.Maana shetani anapata nguvu ,wakati wewe unapoonyesha kwamba si mwenye dhambi.Mara unalalamika eti mwenzako ndiye kakuletea,na kuchukiana bure.Nakuhakikishia kwamba ,ugonjwa wa ukimwi unapona!.Fungua moyo wako,ukubali kosa ulilolifanya,useme imekuaje,uwe tayari kueleza kila kitu,ugonjwa huo utajikuta umeshapona kabisa.Mpendwa huo anashuhudia uponyaji wake,kupiia zoezi hilo la kuwa wazi kwa mwenzake na kumuomba msamaha.
Ushuhuda
Mama mmoja anshuhudia kwamba mfanyakazi wake wa nyumbani alimtukana na kumfokea hadharani,mamahuo aliumia sana moyoni.Akawa anshindwa kuelewa kwa nini uyo amefanya hivyo.Aliwaza sana,baada ya siku tatu,akaanza kupumua kwa shida.Baada ya hapo akasikia sauti ya huyo dada,moyo wake ukapiga sana.Akaenda hospitalini daktali akamuuliza ni nini kilichomuhuzunisha akajibu“sitaki hata kuyarudia yalionikuta”daktali akamuuliza ni mume wako aliyekuumiza?Akajibu hapana ni mfanyakazi wangu.Daktali akamwambia kama ni hivyo kwa nini uteseke si umfukuze?Akajibu kumfukuza siwezi maana nataka aendelee kuishi nami maana watoto wangu wamemzoea.Hata hivyo anafanya kazi vizuri,alichonifanyia sii kawaida yake.Basi daktali akampa dawa akameza,baadaye mapigo ya moyo yaliendelea akimuona,au akisikia sauti yake au akiwaza yale aliyomfanyia.Siku moja akaamua akae naye wazungumze kuhusu jambo hilo.Bwana akampa ujasiri huyo mama,wakatengeneza wakaombana msamaha,amani,nakuelewana vikarudi.Mama huyo anashuhudia tangu siku hiyo kipindi hicho alipata uponyaji wake amen.
- Msamaha ,dawa ya uponyaji.
Magonjwa mengine yamesababishwa na “uchungu”kwa mfano umefiwa na wazazi wako wote na ndugu zako wote.Iwe ni katika vita au wamekufa kwa ugonjwa,unajikuta unawaza sana, usiku hulali,unafikiria maisha yako yatakuwaje.
Ili upate uponyaji ni kuachilia moyo wako.Unaujengea msimamo mwingine kama hivi :“ni kweli wazazi wangu wamefariki wote na ndugu zangu wote,lakini bado mimi nipo ni neema ya Mungu,amenipenda sana Mungu amenilinda mpaka leo, atanitunza na kunisaidia kuishi kama wengine”.Ukiona majirani zako usianze kuwaza wale uliowapoteza,bali mshukuru Mungu kwa sababu majirani zako bado wapo,na mnaweza kusalimiana,na kushirikiana kwa mambo mengine.Ukiachilia moyoni mwako nakutokufikiria mambo aletayo uchungu,utajikuta umepona kabisa .
ugonjwa wa pumu,vidondavya tumbo, mara nyingi unatokana na “hofu”au “hasira”.Hizi mbegu zote ni “mbovu”
Ushuhuda
Mtoto wangu jina lake Derrick,wakati alipokuwa darasa la pili alisumbuliwa na pumu. Tulimpeleka hospitalini daktari akatuuliza; “ndani ya familia yenu kuna mtu anaumwa hivi”Tukamjibu hapana.Akasema,huyu mtoto uliza shuleni kama hana shida, halafu muwape tahadhari wasiwe wanamfokea kwa sababu ana hofu.Tukapeleka ujumbe shuleni kwamba mtoto ana shida kutokana na hofu.Kweli walitusaidia alikuwa ana matatizo na mwalimu wake wa hesabu,aliniambia kwamba mwalimu huyo ni mkali sana anamuogopa.
Mpendwa Mungu akusaidie kuacha hofu . “(Luka 6:37)Achilia waliokuumiza msihukumu nanyi hamtahukumiwa,achilia,nanyi mtaachiliwa.Ukiachia na kusamehe wale wote waliekuumiza moyoni mwako,roho yako itakuwa salama na magonjwa yote atapona kabisa.
-Kwa nini tunapaswa kusamehe?
_ili tupate uponyaji wa magonjwa yetu.
_ili Bwana asikie maombi yetu na atusamehe na sisi makosa yetu.(Mat 6:15)
_ili Bwana apokee sadaka zetu na zaka zetu(Mat 5:23-24)
_ili Bwana akuongezee siku zako za kuishi
(mithali 10:27)kumcha Bwana huongeza siku za mtu,bali miaka ya wasio haki itapunguzwa.
_ili tuweze kuwa salama tukiwa na roho safi(Efeso 4:31) “uchungu wote na ghadhabu na hasira na kelele na matukano yaondoke kwenu pamoja na kila ubaya”.
_tusiposamehe hatutaingia mbinguni(ufuuo 21:27)
“na ndani yake hakitaingia chochote kinyonge wala yeye afanyae machukizo na uongo,bali wale walioandikwa katika kitabu cha uzima cha mwana kondoo”
Ndugu yangu unayesoma kitabu hiki,kusamehe elewa kwamba ni kwa faida yako.Usipotoa uchafu ndani ya chumba chako(moyo wako)uchafu huo,utasababisha moyo wako kukosa amani.Pamoja na hayo,utapata magonjwa mwilini mwako kama nilivyokuonyesha,kama magonjwa ya moyo,vidonda vyo tumbo,kuchanganyikiwa n.k….
Vile vile hutakuwa na maendeleo ya kiroho,pia unahatarisha maisha yako.Kwa sababu usipoachilia utakufa na magonjwa hayo.
Basi sasa utasameheaje mtu kama hakuombi msamaha?
Inawezekana hajui kwamba amekukosea,basi nenda kwake mzungumze kuhusu jambo hilo.Baada ya hapo ataelewa kuwa amekukosea au sivyo,.(Mat 18:15)nenda ukamuone ukiona hakuombi msamaha badala yake anaendelea kukuumiza,basi muache,,lakini moyoni mwako umuachilie kwa kuwa hajui alitendalo.
Luk 23:34 “Yesu akasema Baba, wasamehe,hawajui watendalo. Wakagawa mavazi yake wakipiga kura.”
Ukipata bahati yule aliyekukosea akaja kukuomba msamaha,msamehe kutoka moyoni.
(Luk17:4) “na kama akikukosa mara saba katika siku moja,na kurudi kwako mara saba akisema natubu,msamehe”.
Hata kama ni wewe umemkosea,unatakiwa kumuendea nakumuomba msamaha.
Biblia inasema “makwazo hayana budi kuja lakini ole wake mtu ambaye yaja kwa sababu yake”.(Lk 17:1).
Ndugu yangu usiwe sababu ya makwazo!Bwana atusaidie kabisa.Tunatakiwa kusamehe kila kosa na kila wakati,tukiwasamehe waliotukosea tutakuwa tumewaponya.
Tumrudie Mungu, tupate uponyaji, wa magonjwa anayotusumbua tupate pia uponyaji wa nafsi zetu .
“Heri aliyesamehewa dhambi zake na kusitiriwa makosa yake”(Zab 32:1).
Wengine tumeona kwamba wanasumbuliwa na mkono wa Mungu mwenyewe.
“kwa maana mchana na usiku mkono wako umenilemea.Jasho langu likakauka hata nikawa kama nchi kavu wakati wa kaskazi”(Zab 32:4).
Ukijua kwamba ugonjwa wako ni mkono wa Mungu sio wa shetani basi mrudie Mungu kwa kutubu ili akurehemu.
“Nalikujulisha dhambi yangu wala sikuuficha upotovu.Nalisema nitayakiri maasi yangu kwa Bwana,nawe ukanisamehe upotovu wa dhambi yangu.Kwa hiyo mtu mtauwa akuombe wakati unapopatikana,hakika maji makuu yafurikayo,hayatamfikia yeye”(zab 32:5-6).
Ukimjulisha Bwana shida inayokusumbua ukimwonyesha hasira yako na chuki yako,mueleze hofu yako,uovu wako wote Bwana atakulinda na maji akufurikapo hayatakufikia.Kwa sababu mapigo ya waovu hayatakufikia
“naye mtu mwovu ana mapigo mengi,bali amtumainiye Bwana fadhili zitamzunguka.Amen.(Zab32:10)”
Ndugu unayesoma kitabu hiki,umegunduwa mwenyewe kwamba,magonjwa mengi anatokana na hali ya moyo wako.Uchafu wa moyo wako ndio uliyekuhalibu;chuki ya mwenzako,hasira kwa watoto wako,hofu ya maisha,uchungu mwingi,yote haya ndiyo aliyekuharibu.Na wewe bila kujuwa umepoteza hera nyingi ukitafuta uponyaji lakini bado hujapona.Na shetani anakuhubiria kwamba (ugonjwa huu hauna tiba,utakufa tu).
Nisikilize,eh rafiki yangu nikueleze,magonjwa yote anapona,Yesu ni dawa kwako wewe umwaminie.Mwendee Bwana yesu kwa imani,umfungulie moyo wako,akuondolee lile takataka lote la dhambi,akuoshe nawe uwe safi,basi hapo shetani atakosa chakushikilia ,na magonjwa yote atatoweka kabisa kwa Jina la Yesu.
Watu wengi wametafuta uponyaji waliombewa, lakini hawajapona kwa nini?Kwa sababu wengi walimwendea huku wakitaka uponyaji tu sio kwamba wametubu dhambi zao,Hawajachaguwa kumpa Yesu maisha yao atawale.Tafuta kusamehewa dhambi na kuoshwa kwa damu ya Yesu na magonjwa yote ataondoka.
Mithali 16:6 “Kwa rehema na kweli uovu husafishwa ;kwa kumcha Bwana watu hujiepusha na maovu.”
Moyo wako ukiwa safi, ni kusema,hakuna hasira tena,hakuna chuki,ugomvi n.k…..,
“Njia za mtu zikimpendeza Bwana hata adui zake huwapatanisha naye.”Mithali 16:7.
Ukimwamini Yesu,utasamehewa dhambi zote,tena utapata amani ,tena atakupatanisha na adui zako ,njia zako zikimpendeza Mungu.
Biblia inasema kwamba
“ Njia kuu ya mwenye haki ni kujitenga na uovu,na yeye ashikaye njia yake huihifadhi nafsi yake”.Mithali16:17.
Tafuta kupatana na washitaki wako,amani ni dawa tosha.Neno la Mungu linasema
“Yeye apandaye uovu atavuna msiba,na fimbo ya gadhabu yake itakoma.”Mithali 22:8.
BwanaYesu akusamehe na akuponye magonjwa yako yote. Bwana ni mwenye nguvu,hakuna jambo linalo mshinda.Mwingize moyoni mwako ,mpe maisha yako atawale,yeye ni uzima,na wewe atakupa furaha yake .
”Bwana atageuza matanga yako kuwa machezo;atakuvua gunia na kukuvika furaha.Zaburi 30:11.”
Bwana akubariki sana.
Umesoma kwamba magonjwa mengi ni pigo kutoka kwa Bwana ili mkosaji apate kunyenyekea na kuomba rehema kwa Bwana. Si kila magonjwa anayetoka kwa Bwana ,maana tunajua kwamba mengine ni uonevu wa shetani tu .lakini kama ni uonevu wa shetani ,tukikemea kwa jina la Yesu mgonjwa atapona.Ila kama ni pigo kutoka kwa Bwana hata uombe hutapona bali dawa yake ni kunyenyekea na kuomba rehema kwa dhambi zako na utapata uponyaji wako.Napenda kukukumbusha pia kwamba hapa ,tunaomba Bwana atujulishe ni kitu gani kimesababisha pigo hilo.Hapa ndipo tunaona kazi ya nabii akitumwa na Bwana kukufahamisha,au akitumia njozi za usiku,au kutumia neno lake.n.k….Ukiomba Bwana atakujulisha maana yeye hana upendeleo.Pia ni mapenzi yake upate kupona,uwe na raha na amani maishani mwako.
Tuombe.
Baba yetu uliye mbinguni,mwumba wa mbingu na nchi na vyote viijazavyo,utukufu na heshima ni vyako milele ,amen.
Baba,katika jina la mwanao Yesu Kristo,naja mbele zako,nikimsogeza baba huyu , kaka huyu,mtumishi huyu, mbele zako ,Bwana wa huruma nyingi ,na kusii ,ukamurehemu Ee Bwana,ukamuangaliye kwenye shida yake,Bwana wa majeshi ukamkomboe,mvute Ee Bwana mwenye nguvu,ukamsamehe makosa yake yote.Amekusahau,akaegamia na kuweka tumaini lake kwa mali zake ,kwa waganga wa kienyeji,kwa sanamu ,Bwana damu yako Ee Yesu ikamuoshe na kumtakasa,umsamehe kwa uovu wake wote ,umkubali Ee Bwana,ukamponye na magonjwa yake yote,umweke huru,ukamtoe kwenye mateso yake yote.Asante Bwana kwa huruma zako na rehema zako na upendo wako.Naomba nikiamimi katika jina lipitalo majina yote Yesu Kristo,amen.
Baba yetu na Mungu wetu,naja mbele zako nikimleta mama huyuna dada huhu,na mtoto huyu,Bwana mwenye huruma ukamhurumie,ukamfahamishe chanzo cha shida yake ,Bwana na kuomba mpe roho ya unyenyekevu mbele zako ,roho wako mtakatifu akamuatamie,mjulishe kosa lake ukampe kutubu na kukuamini wewe muweza wa yote.Bwana ukafute dhambi zake zote,ukamtakase kwa damu yako ya thamani,Bwana ukamweke huru mbali na maumivu yake yote.Bwana mkubali na kusii,ukampatanishe tena nawe .Asante Bwana kwa upendo wako,na rehema zako kwa mama huyu na dada huyu.Nashukuru Bwana,nikiamini,katika jina lako Ee Yesu mwana wa Mungu.Amen!!
Ndugu msomaji,Bwana akubariki
kwa kutubu dhambi zako na kuamini damu yake,bila shaka utapata amani na raha yake ukisha shikamana naye!!
Yeremia 3:12-14,
“Enenda ukatangaze maneno haya kuelekeya upande wa askazini,ukaseme,Rudi,Ee Israeli mwenye kuasi,asema Bwana;sitakutazama kwa hasira;maana mimi ni mwenye rehema,asema Bwana,sitashika hasira hata milele.Ungama uovu wako tu;ya kwamba umemuasi Bwana,Mungu wako,na njia zako ,zimekuwa nyingi kuwaendea wageni chini ya kila mti ,wenye majani mabichi ,wala hamkuitii sauti yangu ,asema Bwana.Rudini enyi watoto wenye kuasi,asema Bwana ;maana mimi ni mume wenu ;…”
Bwana wetu Yesu,aliye tupatanisha na Mungu kwa damu yake ya thamani,akubariki .Amen.
Mwisho.
Kitabu hiki cha upatanisho,kinatufundisha kwamba Mungu hana upendeleo.Ukiacha maagizo yake utashika vile vile adhabu yake.Uwe umeokoka au hujaokoka,uwe mkubwa au mdogo,mweusi ua mweupe n.k….Wengi wamefarakana na Mungu,lakini walipogundua uovu wao wakatubu wamepata rehema na uponyaji ya taabu zao.Shuhuda mbalimbali zimekuonyesha namna ya uponyaji.Kitabu hiki ni msaada kwa maisha yako na kwa mwenzako pia.Uwe tayari kuwasaidia wengine ili na wao wapate kuwekwa huru.Naamini kwamba shida yako na taabu yako ya mda mrefu,leo hii itakoma.Maana amenijulisha Bwana kwamba kitabu hiki ni dawa kwa magonjwa yote.Bwana akubariki ndugu msomaji wa kitabu hiki.
Mithali13:15.
“Ufahamu mwema huleta upendeleo;bali njia ya haini huparuza.”
Je, na wewe umepata ufahamu mwema?Basi, upendeleo wa Bwana umekuzukia.Machozi yako Bwana ameyaona!
Kujitambuwa kwako ndiyo mafanikio yako.
Upatanisho wako na Mungu wako ndio ufufuo wako!
Msamaha na kuachilia ndiyo mfereji uletao uponyaji.
Upatano wako na ndugu yako,ndio amani yako.
Mimi na wewe tumepewa huduma hii ya Upatanisho ili watu wamrudie Mungu na kuwa na maisha mazuri ,marefu.Mungu akubariki ndugu,tuombeane na tujitie moyo ,tuiendeleze kazi ya Bwana.Amen.
——————————————————————————————–
Titre : UFUNUO WA FAMILIYA.
Yaliyomo :
Utangulizi ;
Sura ya1.
Mungu,mwanzilishi wa ndoa.
Msaidizi wa kufanana naye.
Uumbwaji wa mwanamke wa kwanza.
Umuhimu wake.
Mwili mmoja.
Sura ya2
Dhambi huvunja ndoa.
Uzinzi
Ushuhuda
Utafanyaje ili ndoa yako ipone?
Watoto watarudishwa lini?
Sura ya3
Jinsi ya kurejeshwa kwa watoto kwao.
Jinsi ya kukabidhiwa watoto.
Ushuhuda
Muhimu kuzingatia.
Utangulizi.
Je unaelewa mambo ya Rohoni?
unapenda kuyajua?
Napenda kukujulisha mambo makuu ya Mungu nilivyofunuliwa kuhusu familia zetu za hapa duniani.
Maswali mengi yapo.Unaweza ukajiuliza kwa nini mme na mke hawaishi kwa raha na upendo, wakati walioana wakiwa wanapendana?
Unaweza kuelewa kwa nini watoto wana tabia tofauti, wengine wanapenda baba kuliko mama,wengine hawapendi watoto wao?Au wazazi wanaonyesha ubaguzi katika watoto wao.Kuna mambo mengi anaweza akaonekana,na mengine ya ajabu hayaonekani kwa macho ya mwilini.Naomba unisikilize kwa makini nikikufunulia mambo haya.
Kuhusu mwandishi.
Kitabu hiki ni ujumbe kwa watu wa Mungu,uliyefunuliwa ili wajue chanzo cha shida nyingi ziliopo ndani ya familia mbalimbali.Mwalimu ,Francoise Habonayo ni mwanamke kutoka nchi ya Burundi,ni mtumishi wa Mungu tangu utoto wake,alimpokea Yesu akiwa na umri wa miaka 7,alitumika sana siku za ujana wake,mpaka leo hii anamiaka zaidi ya 40,ana mme na watoto,pia wote nyumbani ni watumishi wa Mungu. Mama huyo,anaendelea kumtukuza Bwana kwa njia ya kuhubili kanisani kama mwalimu, na kufundisha kwa njia ya kwandika vitabu vya injili.Mama huyo amepata ufunuo kuhusu familia za hapa duniani,amefundisha sana semina za ndoa,ameandika na vitabu vingine kuhusu maisha ya ndoa.(kitabu”Fundisha watu wangu”, pamoja na kingine kwenye lugha ya kirundi:”Mtimwaribwabimenye”?).
Kitabu hiki ,kitakusaidia kujua chanzo cha watoto wako kuwa na tabia tofauti,kitakusaidia pia kurejea amani na upendo ndani ya familia yako.Pia,kitakufundisha namna ya kuomba ili mali zako zilizo ibwa na shetani zikurudie.Naamini kitabu hiki kitabadirisha maisha yako ya ndoa ,ukizingatia maagizo au masharti ya Mungu kuhusu ndoa.Naomba Mungu ufunuo huu,ukuletee mwanga ili upate ufufuo wa familia yako,na pia uweze kupeleka ujumbe kwa wengine ili nao wapone.Mungu akubariki sana.
Sura ya 1.
Mungu ndiye mwanzilishi wa ndoa.
Kwanza kabisa swala la ndoa ni jambo jema la kukubalika mbinguni.Mungu aliumba mtu wa kwanza duniani anaitwa Adamu.Mwamzo2:7.”Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi,akampulizia puani pumzi ya uhai;mtu akawa nafsi hai.”
”Bwana Mungu akapanda bustani upande wa mashariki ya Edeni akamweka ndani yake mtu huyo aliyemfanya.”Mwa2:8
”Bwana akachipukiza katika ardhi kila mti unaotamanika kwa macho na kufaa kwa kuliwa.”Mwa2:9.
”Ukatoka mto katika Edeni wa kuitilia bustani maji,na kutokea hapo mto huo ukagawanyika kuwa vichwa 4.”Mwa2:10.
Mungu mwenyewe aliumba mtu,akapanda mwenyewe miti kwenye bustani,akaweka mwenyewe maji ya kumwagilia.Lakini,Adamu kazi yake ilikuwa kutunza na kuendeleza kazi Mungu aliye anzisha tu.Kwa kuendeleza bustani,Mungu alikuwa ameweka mbegu ndani ya miti ile ili Adamu asihangaike kutafuta mbegu.
Mwa1:29.”Mungu akasema tazama nimewapa kila mche utoae mbegu,ulio juu ya uso wa nchi yote pia,na kila mti,ambao matunda yake yana mbegu;vitakuwa ndivyo chakula chenu…”
Biblia inatueleza kwamba Adamu aliumbwa ili atumike ndani ya bustani hiyo ya Edeni,ailime na kuitunza.Mwa2:15.
Pia atawale juu ya wanyama,maana na wao waliumbwa kutoka katika ardhi.
Mwa2:19.”Bwana Mungu akafanyiza kutoka katika ardhi kila mnyama wa msituni na kila ndege wa angani,akamletea Adamu ili aone atawaitaje;kila kiumbe hai,jina alilokiita Adamu likawa ndilo jina lake.”
Mungu alimpa kazi kubwa naye akaifanya.
Mwa2:20.”
”Adamu akawapa majina yao kila myama wa kufugwa na ndege wa angani,na kila mnyama wa mwituni;…”
Ndugu msomaji wa kitabu hiki, Mungu mwenyewe ndiye aliyeona kwamba Adamu ana uhitaji wa msaidizi.
Ndani ya wanyama wale woote,Adamu hakuona aliyekuwa angeweza kumsaidia ,maana vyote vilikuwa vimewekwa chini ya utawala wake.Hangeweza kupata msaada katika vitu visivyo na uwezo.Kulikuwa hakuna kiumbe chenye mfano wake.
Mwa2:20 ”….lakini hakuonekana wa kumsaidia Adamu aliyefanana naye.”
Msaidizi wa kufanana naye.
Adamu,mtu wa Mungu,kiumbe chenye mfano wa Mungu,(pumzi yake imetoka kwa Mungu),na umbo la mfano wa Mungu,(maana Biblia inasema hivi;
Mwa1:26.”Mungu akasema,na tumfanye mtu kwa mfano wetu,kwa sura yetu…”),anahitaji msaidizi.
Kazi zilikuwa nyingi,hana wa kuongea nae,upweke mwingi,n.k..Atoke wapi msaidizi wa Adamu jamani?Mwenye uweza kama wake,maana kama unataka mtu agusaidie ni lazma awe na uwezakama wako ili muendeleze wote kazi vizuri.Siku hizi kazi ikigushinda vipo vifaa vya kukusaidia.Mfano,ukitaka kufua nguo,si lazima utumie mikono yako tu,zipo mashine zinaweza gufua badala yako.Kulima,zipo mashine n.k.Naamini,maendeleo ya leo ni mazuri kuliko ya mwanzo.Hata hivo,Adamu alikuwa hajaona,msaidizi wa …..Kufanana na ye……
Atoke wapi wa kumsaidia wenye sifa ya ….kufanana na ye….?
Mungu anajishughulisha na shida zetu.
Uumbwaji wa mwanamke wa kwanza duniani.
Mwanamke yeye hakuumbwa kwa udongo wa ardhi,yeye aliumbwa kutoka kwenye mfupa wa mwanadamu,kisha akaufanya mwanamke.
Mwa2:21-22.”
”Bwana Mungu akamletea Adamu usingizi mzito,naye akalala;kisha akatwaa ubavu wake mmoja,akafunika nyama mahali pake.Na ule ubavu alioutwaa katika Adamu Bwana Mungu akaufanya mwanamke,akamleta kwa Adamu.”
Haleluia! Bwana mwenyewe alimtafutia msaidizi ,mwenye sifa za kufanana naye.! Mungu ndiye mwanzilishi wa ndoa.
Mungu mwumba wetu ,amemletea Adamu mke.
Mungu daima ndiye mhusika mkuu kwenye swala la ndoa.Maana ndiye anajua ni yupi wa kufanana na wewe.Wasaidizi wanaweza wakapatikana,lakini wenye sifa ya kufanana,Mungu pekee ndiye anajua.
Mithali31:10.
”Mke mwema ,ni nani awezaye kumwona?Maana kima chake chapita kima cha marijani.”
Adamu alipo amka na kumuona huyo mke,alisema katika kitabu cha
Mwa2:23.
”sasa huyu,ni mfupa katika mifupa yangu,na nyama katika nyama yangu,basi ataitwa mwanamke,kwa maana ametwaliwa katika mwanamume.”Paulo naye aliandika hivi;
1Kor11-12:”Maana mwanaume hakutoka katika mwanamke,bali mwanamke katika mwanamume.Wala mwanamume hakuumbwa kwa ajili ya mwanamke ,bali mwanamke kwa ajili ya mwanamume.”
Malaika wa Mungu wanapendezwa sana wanawake wakivaa kichwani dalili ya kumilikiwa.1Kor11:10 .
”Kwa hiyo,imempasa mwanamke awe na dalili ya kumilikiwa kichwani kwa ajili ya malaika.”
1Kor11:11-12.
”Walakini,si mwanamke pasipo mwanamume,wala mwanamumue pasipo mwanamke ,katika Bwana.”Katika Bwana wote ni sawa;
1Kor11:12 .
”Maana kama mwanamke alitoka katika mwanamume,vile vile mwanaume amezaliwa na mwanamke.;na vitu vyote asili yake hutoka kwa Mungu.”
Na vitu vyote (watu,wanyama,miti,maji,mawe,n.k..),vitu tulivyo navyo,maumbile,rangi,n.k asili yake hutoka kwa Mungu.
Adamu hakuumbwa kwa ajili ya mwanamuke,lakini mwanamke aliumbwa kwa ajili ya mume,lakini,Adamu alihitaji msaidizi.Sasa kumbe,wanawake wapo kwa hitaji la wanaume.Katika uumbaji,mwanamke alionekana wa mwisho.Yeye,si kusema kwamba alikuwa amesahaulika,cha msingi ni kwamba na yeye ameumbwa na Mungu,akapewa pumzi yenye uhai wa Mungu,wakaumbwa wote kwenye mfano wa Mungu.
Mwa1:27.
”Mungu akaumba mtu kwa mfano wake,kwa mfano wa Mungu ,alimwumba mwanaume na mwanamke,aliwaumba.”
Uwepo wa mwanamke ulionyesha umuhimu wake wa pekee.
Umuhimu wa mwanamke.
-Anahitajika katika kazi maalumu ka kuendeleza uzao duniani.Kama vile Bwana Mungu alikuwa amewaza kazi ya bustani ya Edeni,kwa kuandaa mbegu ,vile vile Bwana Mungu alikuwa ameandaa mbegu za kuendeleza uzao duniani.Na wanadamu ,mbegu zimewekwa ndani ya miili yao.Kama vile machumgwa mbegu zimo ndani ya tunda la machungwa.
Biblia imetwambia kwamba hakuna mume bila mke,wala mke bila mume maana mume anazaliwa na mwanamke.
Kazi ya Eva(mke wa Adamu),ilio mfanya awe lazima mke,ni uzao.Maana uzao unapatikana kati ya mke na mume.
Mungu alipomaliza kuumba mke na mume,aliwabarikia,
Mwa1:28.”Mungu akawabarikia ,Mungu akawaambia,zaeni mkaongezeke,mkaijaze nchi;mkatawale samaki wa baharini na ndege wa angani na kila kiumbe kiendacho juu ya nchi.”
Kazi ya pili,ni kufanya kazi ya kutawala juu ya viumbe vingine.
Kazi hii ilionekana ni kubwa kwa Adamu mpaka akahitaji msaidizi.Utawala haujapewa Adamu peke yake,maana neno laBwana linasema hivi,
”Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu,wakatawale…,Mwa1:26”
Haijasema akatawale,lakini imesema wakatawale.
Kazi ya tatu;kutunza bustani na kuilima wakisaidiana na Adamu.
Si wawili tena bali mwili mmoja.
Ijapokuwa wanadamu wa kwanza wametoka kwenye mwili mmoja,maana Eva ametoka kwenye ubavu wa Adamu,tumevisoma Mwa2:21.
Adamu alipoletewa mkewe,alifurahi sana,akaridhika naye.Alitamka maneno matamu sana,alisema…sasa huyu ni mfupa katika mifupa yangu na nyama katika nyama yangu.Mwa2:23.
Ndoa ilianzishwa na Mungu mwenyewe kure kwenye bustani ya Edeni.Mungu ndiye afanyaye mke na mume kuwa mwili mmoja.Si wawili tena,bali mwili mmoja.Ijapo kuwa watu hata kama wameoana ummoja huu wa kuwa mwili mmoja,hauonekani kwa sababu shetani naye anamafundisho yake ,ndiyo maana unakuta kwa wale wanaemcha Mungu wanajitahidi kuzingatia hiyo sheria ya kimungu kwamba mke na mme wakioana wanageuka kuwa mwili mmoja,lakini kwa wale wasiyefuata sheria ya Bwana kwao shetani anawambia kwamba si kuwa mwili mmoja bali ni kukaa pamoja lakini wakijitahidi kuheshimiana.
Ndugu msomaji wa kitabu hiki,ndoa ni kazi ya Mungu.Tuzingatie sana sheria yake,tusiwe kama mataifa wasiemchamungu wanavyofanya.Mume ni kichwa cha familia,na mke ni msaidizi wake.Msaidizi inamaanisha kusaidiana kwa pamoja.Ndani ya upendo na heshima zote.Si mmume atawale mke au mke atawale mmume,lakini kwa pamoja wanatawala juu ya mali zao,juu ya mashamba na juu ya mifugo yao.
Mwa1:28”Mungu akawabarikia ,Mungu akawaambia zaeni mkaongezeke,mkaijaze nchi,na kuitiisha;mkatawale samaki wa baharini,na ndege wa angani,na kila kiumbe chenye uhai kiendapo juu ya nchi.”
Kwa ushirikiano ;wanazaa,wanatawala,wanasaidiana kufanya maagizo ya Bwana.
Mume +mke=mwili mmoja.
Adamu(mme)+Adamu(mke)=Adamu.
Mwa5:2.”Mwanamume na mwanamke aliwaumba,akawabariki akawaita jina lao Adamu,siku ile walipoumbwa.”
Adamu mume baada ya kuangushwa na nyoka,alimbadilishia jina na kumpa mke wake jina la Hawa
Mwa 3:20.”Adamu akamwita mkewe jina la Hawa;kwa kuwa yeye ndiye aliye mama wa wote walio hai”Dhambi inaanza kuleta mgawanyiko,tena utukufu waliyekuwa nao ukaisha kwa sasa Mungu anawatafutia mavazi ya ngozi yakuwafunika.
Mwa3:21.”Bwana Mungu akawafanyia Adamu na mkewe mavazi ya ngozi akawavika.”Lakini tangu mwanzo walikuwa uchi bila shida yote.
Mwa2:25.”Nao walikuwa uchi wote wawili,Adamu na mkewe,wala hawakuona haya.”
Dhambi yao ilisababisha Mungu kuwafukuza katika bustani ile walipokuwa wakiishi.
Mwa3:24.”Basi akamfukuza huyo mtu,akaweka makerubi,upande wa mashariki wa bustani ya Edeni,na upanga wa moto uliyegeuka huko na huko kuilinda njia ya mti wa uzima.”
Dhambi ililetea ardhi laana ndiyo maana ardhi haitoi mazao ya kuridhisha.Watu wanakula kwa jasho lao nyingi, miti ya laana imemea ardhini (michongoma na miiba) ,
hii ndio adhabu ya AdamuMwa3:17-19.
Nyoka naye imelaaniwa kuliko wanyama wote.Atatembea kwa kuburuza tumbo,tena chakula chake ni mavumbi.Tena kumewekwa uadui kati yake na mwanamke na uzao wake wote.Nyoka atapondwa kichwani naye ataponda kisiginoni.Mwa3:14-15.
Mwanamke naye,Bwana akamwambia kwamba atazaa kwa uchumgu
Pia atakuwa na tamaa kwa mume wake,vile vile mume wake atamtawala.Mwa3:16.
Tumeshaona kwamba tangu mwanzo kabisa Mungu alikuwa ametuwekea kila kitu ili tuishi kwa raha yote.Lakini kwa sababu ya dhambi mwanadamu amepewa adhabu kulingana na kosa lake la kutomtii Mungu na kushika maagizo yake.
Swali .Je laana hizi bado zipo,hata kama tumeokoka?Ndiyo kwa sababu ni hukumu ilietolewa na Mungu mpaka mtu apfe.Angalia neno hili Mwa3:19.”kwa jasho lako utakula mpaka utakapoirudia ardhi,ambao katika hiyo umetwaliwa ;kwa maana u mavumbi wewe,nawe mavumbini utarudi.”
Mtu anakula kwa jasho mpaka apfe.Nyota inaenda kwa kuburuza tumbo mpaka mwisho wake.Wanawake nao mpaka leo wanatawaliwa na waume zao ,tena wanazaa kwa uchungu. Lakini nimeona mabadiliko
Kwa wale walieokoka.Wakati wa kuzaa wanauchungu lakini kidogo sana.Anaweza akawa na uchungu dakika 10 tu,lakini yule asimjua Bwana akateseka kwa siku 5 au zaidi.Vile vile nyumba za wale wanaemcha Mungu wanajitahidi kwa msaada wa Bwana kuzingatia sheria ya kuheshimiana na kupendana .Mume aliyeokoka na mke alieokoka wanakuwa mwili mmoja ,wanaweka wazi mambo yao yote,hakuna mme kutawala juu ya mke wake.Ndani ya Kristo yote anakuwa mapya.Mwanamke ni utukufu wa mwanaume.1Kor11:7.
Mfano mzuri wa familia ya kimungu.
Kumbuka daima kwamba Mungu alikuwa pamoja na familia ya kwanza ,aliyeiweka mwenyewe.
Amewapa kila kitu ili waishi kwa raha na amani.Bustani nzuri yenye matunda ya kila aina,mto wa kumwagilia ile bustani hata na chakula cha mifugo Bwana Mungu amikiweka.Mwanadamu ni ku furahia kazi ya Bwana.
Kama Mungu alipokuwa na familia ya kwanza ndipo na leo yupo pamoja na familia ya leo hii.Mtumishi wa Mungu Ayubu alitufunulia hayo.Anakumbuka kipindi shauri la Mungu lilipokuwa ndani ya familia yake.Ayu29:4-5
”Kama nilivyokuwa katika siku zangu za kukomaa,hapo siri ya Mungu ilipokuwa hemani mwangu.Wakati Mwenyezi alipokuwa akali pamoja nami,nao watoto wangu walipokuwa wakinizunguka…”
Siri ya Mungu imo hemani mwa familia ya watakatifu.
Pia baraka tele zimo pamoja na watakatifu wake.
Ayu29:6
”Wakati hatua zangu zilipokuwa zikioshwa kwa siagi,nalo jabali lilipomiminia mito ya mafuta!”.
Uwepo wa Bwana ukidhihirika ndani ya familia yako , tabia zako wote wakuonapo watazishuhudia.
Ayu 29:11,
” Sikio liliponisikia ,ndipo likanibarikia;na jicho liliponiona likanishuhudia.”
Watu watakuheshimu,pia watakubariki,maana utakuwa mtenda mema kwa maskini na yatima .
Ayu29:13.
”Baraka yake yeye aliyekuwa karibu na kupotea ilinijia;nikaufanya moyo wa mjane kuimba kwa furaha.”
pia utakuwa msaada mkubwa kwa wenye mahitaji,Ayu29:16.
”Nalikuwa baba kwa mhitaji,na daawa ya mtu nisiyemjua niliichunguza.”
Utukufu wa Bwana utakuwa daima ndani ya familia takatifu.Pia utakuwa msaidizi wa ndoa nyingi maana ziko gizani.Hekima ya kimungu itakuwa pamoja nanyi,si kwa sababu ndoa yako niya siku nyingi,hapana lakini,ni kwasababu,roho wa Bwana yumo ndani mwenu.
Ayu32:8-9.”Lakini imo roho ndani ya mwanadamu,na pumzi za mwenyezi huwapa akili.Sio wakuu walio wenye akili,wala sio wazee watambuao hukumu.”
Tabia ya familia inatakiwa kuwa mfano wa kuigwa katikati ya mataifa.
1Pet3:8.
”Neno la mwisho ni hili,mwe na nia moja,wenye kuhurumiana,wenye kupendana kama ndugu,wasikitivu,wanyenyekevu,watu wasiyelipa baya kwa baya,au laumu kwa laumu,bali wenye kubariki kwa sababu hayo ndiyo mliyoitiwa ili mrithi baraka.”
Wanawake,tuwe na mapambo asiyoharibika;ya upole na utulivu,kama walivyojipamba wanawake watakatifu wa zamani,waliomtumaini Mungu na kuwatii waume zao( 1Pet3:4-5).Mapambo ya mwanamke najua nimengi, nami ni mwanamke mwenzenu,lakini yanaharibika.Yasiyoharibika ni mapambo ya rohoni.Kutii waume zetu…!Bwana atusaidie na aendelee kutuwezesha.Najua kutii kwa mwanamke si rahisi sana,ni kama kujikana.Tumeombwa hivyo,kwa sababu ndani ya tabia zetu havipo.Bali tunataka sisi watu wanyenyekee kwetu.Bwana atusaidie.
Waume,nanyi,kaeni na wake zenu kwa akili;na kumpa mke heshima,kama chombo kisicho na nguvu;na kama warithi pamoja wa neema ya uzima,kusudi kuomba kwenu kusizuiliwe.
Kama chombo kisicho na nguvu.Na vilinganisha na glasi ya kunywea maji.Unakuwa makini nacho,maana ukiangalia vibaya utakivunja.Glasi ni nzuri tena ya thamani sana,ni chombo kisicho na nguvu.
Pia mke ni mrithi pamoja na wewe mwanaume wa neema ya uzima.Maana na yeye amepewa neema ya kuumbwa kama mume naye alipata neema hiyo yakuumbwa .wote wamepata neema ya uzima.
Waume kaeni sasa kwa akili na wake zenu!Ni vyombo vionekanavyo kuwa havina nguvu lakini vyahitajiwa sana.Angalia jinsi alitafutwa msaidizi wa Adamu akakosekana mpaka Mungu akalazimika kumuumba.
”Wala mwanamume hakuumbwa kwa ajili ya mwanamke bali mwanamke kwa ajili ya mwanamume.(1Kor11:9)”Alipewa neema ya uzima.kama kiungo kisicho na nguvu lakini cha hitajiwa sana.Sasa
Kila mtu atafute faida ya mwenzake.
1Kor 10:24.”Mtu asitafute faida yake mwenyewe bali ya mwenzake.”
Sura2.
Dhambi,sababisho ya ndoa kuvunjika.
Ndoa inahitaji mshikamano,ummoja kati ya mume na mke.
Watoto ni zawadi atoayo Bwana mwenyewe.
Si katika uwezo wa mke au wa mume bali ni uwezo wa Bwana.Mkikosa watoto,msilaumiane,bali mufarijiane.Najua ni vigumu sana,lakini pamoja na hayo,Bwana ni yule yule,pamoja na jalibu kuna mlango wa kutokea. Ndani ya maisha ya ndoa tunatarajia upendo,amani na furaha.Na hivyo vyote vinapatikana kwa Bwana pekee.Kutokuwa na mtoto ni jaribu,lakini kama wewe una hilo,wengine wanajaribu zingine.
1Kor10:13.
”Jaribu halikuwapata ninyi,isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu;ila Mungu ni mwaminifu;ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo,lakini pamoja na lile jaribu,atafanya na mlango wa kutokea,ili mweze kustahimili.”
Dhambi ya uzinzi ni sumu ya ndoa.
Tangu zamani Mungu alikuwa akihuzunika sana watu wakifanya uasherati.Hasira ya Bwana inawaka juu ya waabuduo sanamu.
1Kor 10:8.
”Wala msifanye uasherati kama wengine wao walivyofanya ,wakaanguka siku moja watu ishirini na tatu elfu.”Angalia jinsi gani hasira ya Bwana inawaka juu ya waovu.! Muwe na hofu ya Mungu maishani mwenu,isije ikawapata hasira ya Bwana.
Ayu31:3.
”Je!siyo msiba kwa wasio haki,na hasara kwao watendao uovu?”
Ayubu yeye anasema kwamba amefanya agano na macho yake,kwamba hataangalia mschana,maana anajua akijiachilia kwa ngono,atapata hasara na msiba kutoka kwa Mungu.Anaendelea kusema kwamba hata kama akiangalia,moyo wake huwezi kuandama macho yake,tena hatatowa mali yoyote kwa uzinzi.
Ayu31:4-5.
”Je yeye hazioni njia zangu,na kuzihesabu hatuwa zangu zote?Kwamba nimetembea katika ubatili,na mguu wangu umeukimbilia udanganyifu.”mst7 ”kwamba hatua yangu imekengeuka na kuiacha njia,na moyo wangu kuyaandama macho yangu,tena kwamba kipaku cho chote kimeshikamana na mikono yangu”mst9 .”Kama moyo wangu ulishawishwa kwa mwanamke,nami nimeotea mlangoni kwa jirani yangu..”Yobu anasema kwama,kama amefanya uovu wa namna hiyo,anafaa kuadhibiwa vibaya.
Dhambi la uzinzi ni moto uteketezao hata uharibifu,Ayu31:12
Je kama Ayubu alifanya agano na macho yake,tena moyo wake huwezi kuandama macho yake,wewe umefanya agano gani na mwili wako?
Kilicho mfanya afanye agano na nafsi yake si kingine,anahofu ya Mungu maana amesema ;
”Kwani sehemu ya Mungu itokayo juu ingekuwa nini,na urithi wa Mwenyezi utokayo juu?Je siyo msiba kwa wasio haki na hasara kwao watendao uovu?Ayu31:2-3.
Anasema tena,
”Kwani msiba utokao kwa Mungu ulikuwa na kitisho kwangu,na kwa sababu ya ukuu wake sikuweza kufanya neno.”Ayubu 31:23.
Hofu ya Mungu itakulinda na wewe.
Dhambi inasababisha agano la Mungu kuvunjika.
-Agano la Mungu halitekelezwi kwa hiyo mambo yote yanavurugika.
Kumbuka hapo juu tumesoma jinsi Adamu na Hawa walipofukuzwa katika bustani yao ya Edeni.
Hebu turudie kueleza jinsi gani ndoa inaweza kuvunjika(kitabu fundisha watu wangu)
Ndoa ni wawili tu.Mme na mke wake. Ukiingiza upendo wa ndoa kwa mtu mwingine tayari umeshavunja ndoa ya kwanza.Hatakama mtaendelea kuishi kama mme na mke, ndoa yenu ni bandia au feki,maana ulimwengu wa roho unatambua ndoa nyingine.
Kwa mfano
Mme mke
Juvenal + Francoise=Juvencoise(ndoa halali,mwili mmoja).
Juvencoise ;wanaishi kwa upendo na amani na watoto wao,wanaishi kwa raha kwa sababu ndoa hii ni ya kimungu.Roho wa Mungu yupo hemani mwao .
Juvenal akijitoa akaambatana na mke mwingine au Francoise akijitoa akaambatana na mme mwingine, tayari ndoa ya kwanza(Juvencoise) imevunjika.Imeundwa nyingine katika ulimwengu wa roho.
Kwa mfano ;-Juvenal+Rose.=Juverose, ndoa feki, bandia lakini mwili mmoja.
(1korinto 6:16) “Au hamjui yakuwa yeye aliye ungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana asema wale wawili watakuwa mwili mmoja.”
Pamoja na kuonekana mbele za watu kwamba ndoa ya (Juvencoise) ipo, ulimwengu wa roho au mbele za Mungu, haipo, badala yake ziko mbili tofauti. ( hiyo ya kwanza iliovunjika, na hiyo ya pili bandia.)
(Isaya11:3-4 ) amesema Mungu hata hukumu kwa kuyafuata ayaonayo kwa macho yake,wala hata onya kwa kuyafuata ayasikiayo kwa masikio yake,bali kwa haki………..
Mungu, anahukumu kwa haki.Usiseme amenisingizia au amenionea na watu wengi wanahukumu mtu kwa kusikia hata kama ni uongo na wengi wanaficha mambo yao ili asionekane na wewe ukiwaona utasema ile ndoa ni safi kweli.Wanapendana sana! Kumbe si kweli ndoa yenyewe haipo.Mungu atusaidie! Yeye ni mwenye haki, tena ni mwaminifu.
(Isaya 11:5)”na haki itakua mishipi ya viungo vyake, na uaminifu mshipi wa kujifungia”
Tumeonyesha dhambi ya uzinzi tena mara nyingi ndio inasababisha ndoa kuvunjika.
Kuzini.
Kuzini kunafanyika kwa njia 3(Kama tulivyo onyesha kwenye kitabu (Ntimwaribwabimenye)pia kwenye kitabu (Fundisha watu wangu)
1 Kuchafua mashuka
2 kuweka kilemo au kilaka kwenye mashuka.
3 kuchafua chupi na kuichana
1.Mashuka anatandikwa kwenye kitanda.kuyachafua maana yake “Kumpapasa papasa kwenye mwili wake,na kumbusu ,ukiwa umejificha mtu asikuone na huko unajua si mume wako au si mke wako.”Hii ni dhambi kubwa mbele za Mungu.Kitendo hiki kwa wengine kinaambatana na vizawadi vidogo vidogo,chakula hotelini,maneno mengi yenye kuamsha tamaa ya uzinzi.Vitu kama hivi ni machukizo mbele za Mungu.(Dhambi hii inaitwa uzinzi kwa njia ya kuchafua mashuka.)
2.kutia kilemo au kiraka kwenye mashuka ; ni kuweka mtu moyoni wakati wa ushirikiano wa(mme na mke)kwa tendo la ndoa.Huku ukifurahia huyo mtu uliyemuweka kama vile unafanya ushirikiano naye hata kama yuko mbali na wewe.Tendo hili ni chukizo mbele za Mungu.Hii pia ni uzinzi kupitia njia hii ya kutia kiraka.
3.kuzini na mwingine wa nje ya ndoa yako.(Kufanya tendo la ndoa na mtu mwingine wa nje ya ndoa yako.Ni dhambi kubwa sana ,inaitwa kuchana na kuchafua chupi.)
Uzinzi huu wa kwanza,unaweza kuuita tamaa,maana hapa hatuoni kwamba wamefanya tendo la ndoa,lakini wamezini.Sawa sawa na neno la Mungu pale Yesu aliposema kwamba ukimuangalia mwanamke na kumtamani moyoni umesha zini.
(Mathayo 5:27-28) “Mmesikia kwamba imenenwa usizini;lakini mimi nawaambia,kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.”
Elewa sana kwamba hapa,unaweza wewe ukamtamani moyoni mwako,ukamwendea,ukamuomba awe rafiki yako au mpenzi wako.Anaweza yeye asikubaliane na wewe.Ukimshika kwa nguvu tunasema umembaka.Ila akikukubalia kupendana nawewe,ndio maana mnatafuta siku ,mnapanga ,mnaonana,mnaongea mnakula huku mukijifurahisha kwa kuamsha tamaa ya uzinzi(munabusiana na maongezi yenu ya uchafu tupu.) Hapo ni jambo lingine nje ya kubakwa.Ni makubaliano kamili kati ya watu wawili.Vili vile hali hii ni mbaya sana ina ambatana na mazawadi anayethibitisha upendo wenu.Kwa lugha ya ufunuo tumefunuliwa kwamba hii ni ndoa katika ulimwengu wa roho.(tumefafanua zaidi katika kitabu “Fundisha watu wangu” uk. Wa 29.
Ushuhuda.
Dada mmoja amekutana na mwanamke akauulizwa;Hebu niambie,ni wewe nimesikia unatembea na mume wangu?Dada huyo alishtuka akasema si kweli hatujawahi kutembea na mume wako.Akaendelea kusema; kama nimefanya hivo,nifike nyumbani Mungu aniue nife!Huku anaanza kudondosha machozi.Mama huyo akamwambia ,Mungu hataki ufe ,ila anataka uishi ukamtumikie.Akaendelea akamuuliza,niambie sasa umefanya nini?Akajibu,alikuwa anakuja kazini kwangu kunifuata huko,siku zingine ananipigia simu,alikuwa ananitafuta yeye siyo mimi.!Huyo mama anaendelea,kwa nini hukuniambia kwamba anakusumbua?Ulikuwa unapenda hein!!! Sasa niyeye alikuwa anakuingiza kwenye gari yake? Anakupeleka kukununulia chakula unakubali?Mbona ulikuwa ukiwa na shida unampigia?Amekununulia nguo na mapochi na wewe unafurahia!!Yeye ni nani kwako? Ni mume wako au ni mchumba wako? Nakwambia hivi yule ni mume wangu,sasa pesa zote ulizotumia kutoka mikononi mwake,nenda ukahesabu vizuri zote unirudishie,Unasikia? Akatingisha kichwa akakubali kurudisha vyote.Mama huyo akamuuliza tena ,mbona umempigia nilipoitikia mimi ukakata simu,ulikuwa umejua kwamba ni mimi? Akajibu ndiyo.Kumbe dada huyo alikuwa anatembea na mume huyo siku nyingi sana.Tena dada huyo alijifanya rafiki wa huyo mama,huku akijua kwamba ameiba mume wake.Angalia ,mume huyo na dada huyo hawajawahi kufanya tendo la ndoa au mapenzi,lakini Mungu amewahesabiya kwamba ni wazinzi kwa sababu ya tamaa. Mume huyo,baada ya kuonywa na Mungu alitubu,akamuomba mke wake msamaha,naye akamsamehe.Akamuomba na yule dada amsamehe lakini dada hakufurahia maana alikasirika kuona uhusiano huu umevunjika.Huyo mke alipo mwendea huyo dada,alimhimiza kutubu na kuacha njia za makona kona ya kihuni,maana huyo dada alikuwa muimbaji kanisani,alimjibu kwamba amesha tubu na kumrudia Mungu.Mama huyo akamwambia umetubu wapi mbona hujaja kuniomba msamaha na ni mimi umeniibia mume? Wewe hujajua namna ya kutubu dhambi ya uzinzi?Akainama chini na mama huyo akamuacha.
Kuhusu ushuhuda huu,zingatiya kwamba hawajawahi kufanya mapenzi lakini wamehukumiwa kufanya dhambi ya uzinzi.Hii ni dhambi kubwa sana mbele za Mungu.Kwa mtazamo mwingine ni kusema mume huyu alikuwa na wake wawili mbele za Mungu.Lakini wenyewe hawajui. Wanona ni urafiki wa kawaida maana ,wanaongea tu,wanafurahia pamoja ,wanasaidiana n,k…..lakini na wao walikuwa wanaona kwamba tabia hiyo si takatifu,ndio maana walikuwa wanajificha mke huyo asi waone .Wamefanya hivyo zaidi ya mwaka mzima na walikuwa tayari kuendelea .Bwana atusamehe.!!Mungu alipoona uovu huyo unaendelea akaingilia kati akamtandika huyo mume na mkono wake,ndipo akaomba rehema kwa Mungu na kutubu.Jina la Bwana libalikiwe.!Mpendwa msomaji wa kitabu hiki,angalia vizuri mwenendo wako na wewe.Usiwe kama wapendwa hawa.Ukiendelea huku na wewe Bwana amekwisha kuonya kupitia kitabu hiki,ole wako! Bwana hatakuachia nawewe,anakusubiri utubu,urekebishe mwenendo wako.Mbona unajifariji?je hujui kwamba Mungu anaona,anajua,pia anatambua.Umfiche nini sasa?Yale mazawadi yako unaetoa kwa siri,yale maongezi kwenye simu unayemwambia,yale mawazo ya moyo wako,vyote vimerekodiwa na Bwana.Nakushauri,usipuuze ujumbe huu,maana Bwana anakupenda hataki uangamie.Mungu hana upendeleo,kama alivyompiga baba huyo,ndivyo na dada huyo alivyo pigwa.Maana wote walikuwa wakosaji mbele za Mungu. Ashukuliwe Mungu alivyowapiga wakatubu na kurekebika.Aliye iba mali za watu,amesamehewa ,lakini analipa deni la watu.Hebu ona,aliambiwa ahesabu yote aliyepata ,….Na wewe ukihesabu utaweza? Hata ukikadilia ndani ya mwaka ni hera nyingi sana,utazitoa wapi? Mungu anajua.Dada huyo alikubali kulipa ,tena alikadilia akasema zinaweza zikafika kiwango hiki.Lakini hakuweza kulipa hata angalau kidogo kidogo kwakuwa maisha alikuwa magumu sana hata mshahara wake ulikuwa haumtosherezi mahitaji yake,tena ilikuwa ndiyo sababu alikuwa anamuomba hera baba huyo.Mungu ni mwenye haki sana.Alipoona kwamba dada huyu halipi angalau kidogo,alimlipia yeye kwa njia zake.Kama alikuwa analipwa kwa mfano 150.000sh kwa mwezi,akawa alitakiwa kulipa matumizi ya mwaka moja,túseme kwa mfano alitakiwa kulipa 3.000.000sh.Mungu alitumia boss wake kazini akamfukuza kazini.Akikaa na kuhangaika na kazi lakini Mungu alikuwa anajua kwamba alikuwa analipa deni la Bwana mpaka amalize. Dada huyo alimwambia mama huyo eti amefukuzwa kazini sasa hana jinsi ya kulipa ,lakini mama huyo akamfunlia kwamba si yeye aliyeibiwa mali bali ni Mungu mwenyewe,ndiyo maana Mungu ndiye alihusika kumpiga hivyo kwa kukosa kazi.Lakini deni likiisha lipwa anarudishwa kazini. Ndugu, ulikuwa hujui kwamba Mungu anatisha? Yeye anachunguza kila kitu.Angalia jinsi Mungu hajamhurumia dada huyo mwenye kipato kidogo, hata akafukuzwa kazi.
Watu wengi wanapenda vitu,pesa,n.k.Kwa nini kutamani mpaka umkosee Mungu. Fanya kazi kwa mikono yako, utapata mahitaji yako.
Mapato mengi ya waschana(si wote lakini) ni mapato ya ukahaba.Wanawake wengi mapato yao,ametoka kwenye njia za uasherati.Ndugu ,usipende mapato ya uovu maana Mungu anachungulia kutoka juu,na anaona kila kitu.
Biblia inasema, “Ole wake yeye aipatiae nyumba yake mapato mabaya,ili apate kukiweka kioto chake juu,apate kujiepusha na mkono wa uovu.”Habakuki 2:9
,Mst wa 11,unasema, “Kwa maana jiwe litapiga kelele katika ukuta ,nayo boriti katika miti italijibu.”
Kwa maana nyingine,wewe unayejifurahisha kwenye mali si za haki,unajijengea bara na majonzi mengi.Maana Bwana atayaweka wazi yote,ole wako usipo acha na kuenenda katika njia sahihi na za haki.
Kulipa si hiali ni lazima.
Shuhuda .
Mtumishi wa Mungu mmoja(mwanaume),alishuhudia kwamba alikuwa anapendana na mwanafunzi (wa kike).Binti huyo alikuwa annaishi kwenye familia ya mtumishi huyo.Siku mmoja shetani akaingia kwenye moyo ya mtumishi huyo,akaanza kumtamani.Kwa sababu kulikuwa na watoto wengine ndani ya familia hiyo,ilikuwa ngumu kwa mtumishi huyo kuwa na mda na binti huyo peke yake.Shetani akampa mbinu ya kufanya,alikuwa anawachukuwa watoto wote kwenye stalehe,anawanunulia soda,chakula,n.k.Siku nyingine,anamwita peke yake ili amuonyeshe daftali amsaidie kufanya homwork.Akifika huko,wanaanza maongezi machafu,kubusiana,n.k.huku wengine wanafikili anamsaidia masoma.Amefanya hivo mdamrefu kama miaka zaidi ya 2.Siku mmoja mtumishi huyo Bwana akamuonekania akatubu zambi hiyo ya kutamani mwanafunzi huyo,akatubu kwa Mungu,Kwa mschana,na kwa mke wake.Siku mmoja,mwanafunzi huyo akaja nyumbani na hera 29.500sh,akamkabidhi mama wa nyumba hiyo,akasema ameyakokota njiani.Wakaomba Mungu ili wajuwe ni nini haswa,Mungu akawaambia kwamba Bwana anawarudishia mali yao Shetani alio iba kupitia ushirikiano wa mtumishi huyo na mwanafunzi huyo.Walishangaa sana kujua kwamba Mungu anachunguza hata nia zetu.Angalia,alikuwa anachukuwa pamoja na watoto wengine.Akimnunulia kitu wote anawapa.Kumbe Mungu alikuwa anaweka kando matumuzi ya mwanafunzi huyo.Maana alikuwa anahesabika kama mke wake kwa sababu ya makubaliano ya mapenzi hata kama hawajafanya tendo la ndoa(tumeonyesha kwamba kuku ni kuzini kwa njia ya kuchafuwa shuka.).Lakini yale mabusu,yale maneno ya kuamsha mapenzi,zile soda,vyote vilikuwa vina rekodiwa mbinguni.Ndiyo maana walipo tubu vizuri na mali zilizotumika zikarudishwa.Jina la Bwana libalikiwe.Hata mume wako asijue au mke wako,yuko Mungu ajuae.Nia ya moyo inajulikana mbele za Mungu.
Ufahamu wa Bwana hauna mfano ,na kazi yake haizuiliki.
Tumeshoana kwa upana dhambi ya uzinzi kwa njia ya kuchafua mashuka. Kupitia uovu huu huwezi kupata mtoto isipokuwa kupitia hii njia ya tatu (kuzini au kufanya mapenzi na mtu wa nje).
Uzinzi kwa njia ya “kutia kilaka au kilemo kwenye shuka”,
Mkipata watoto ni kusema kwamba wamezaliwa kwa damu na nyama na wazazi wao halisi,lakini ukweli ni kwamba,kama rohoni alikuwa anazini na mwingine,huyu mtoto, atakuwa na roho nyingine( maana amezaliwa chini ya kivuli cha uzinzi cha mama mwingine au baba mwingine.). Kama vile Yesu alikuwa amezaliwa na roho wa Mungu (au chini ya kivuli cha Mungu mwenyewe)lakini alizaliwa kupitia Mariamu.Yesu amezaliwa na Roho mtakatifu,na hawa watoto watakuwa wemezaliwa na roho ya shetani au ya uzinzi na kuzaliwa na(wazazi wake).
Mungu angekufunulia ungejuwa: kumbe huyu mtoto amezaliwa na mme huyu lakini mama yake sio mimi ni mwingine. Hiki ndicho kilicho sababisho ya watoto wengi kuwa na tabia tofauti.Au unajikuta hakupendi kama mama yake, anampenda baba tu. Kunauwezekano mkubwa,kama watoto hawajaokoka, wanaishi chini ya roho ya uzinzi, watoto si wao bali ni wa baba mwingine au mama mwingine lakini kwa mtazamo wa macho ya kimwili tunaona ni watoto wa familia Fulani kumbe si kweli.Bwana atusamehe na atusaidie.
Na uzinzi huu wa 3, unaonekana hata kwa macho ya kimwili. Utatambua kwamba Baba fulani,amezini na binti fulani wamezaa mtoto fulani. Huu mtoto akiletwa nyumbani mama mwenye ndoa, atamlea lakini kila mtu ataelewa kwamba si wake bali ni wa mmewe.Au mtoto anaweza akawa amezaliwa na baba mwingine na mama huyu akaolewa akiwa na mtoto huyo. Kila mtu ataelewa kwamba huyu mtoto ni wa mama si wa baba mwenye ndoa.
Tumesha onyesha kwamba Mungu ndiye mwanzilishi wa ndoa.Na wenye ndoa ni mume na mke.Biblia imetuonyesha kwamba wanageuka kuwa mwili mmoja si wawili tena.Lakini mmoja wao akijitoa na kupendana na watu wengine na kuzini nao,anakuwa mwili mmoja nao.Maana yake,ndoa yao yakwanza imevunjika hata kama kwa macho ya kimwili muko pamoja.Lakini Mungu anatambuwa kwamba ndoa haipo tena.Kinacho kuonyesha ,unakuta hakuna upendo nyumbani kama wa zamani,kila siku ugomvi,hakuna kuelewana,dharau n.k.Kwa kuogopa kuchekwa na watu ,mnavumilia mkabaki pamoja lakini ukweli ni kwamba uhai wa ndoa haupo.
Je utafanyaje ili ndoa iliyovunjika ipone?
- Kutubu kwa Mungu.
Kwa sababu umevunja Amri ya Mungu.’’usizini” Kutoka20:14 ,
pia viungo vyetu na mwili wetu si vya kahaba bali ni vya Mungu.
(1kor 6:15) “Je!Hamjui ya kuwa miili yenu ni viungo vya Kristo?Basi,nivitwae viungo vya kristo na kuvifanya viungo vya kahaba?”
-Kutubu kwa mke au kwa mme wako.
Kwa sababu umevunja amri ya ndoa.”mwili si wako bali ni wa mme wako.Mwili wa mme si wake bali wa mke wake.(1cor7:4)
-Usisahau kumwambia huyo kahaba
kwamba hutarudia kufanya hayo maovu naye. Unamshuhudia kwamba ulikuwa humpendi bali unampenda mme wako,au mke wako.Onyesha mbele yake kwamba unachukia ulichokifanya.Ikiwezekana vile vitu uliyempa,fanya mbinu zote uvirudishe ili aone kwamba uhusiano naye wote umekwisha.Kwa sababu umemuomba msamaha mwenzako,mwambie kwamba mlikuwa mnapendana na Fulani,ili huyo kahaba aone kwamba hutarudia kwake.Na mwenzako aone kwamba ni kweli hutarudia, kuambatana na kahaba huyo. Tamka maneno ya kumwomba msamaha mke wako mbele ya kahaba huyo.Hiki kitendo kina nguvu 2.Kwanza, kinavunja upendo wako na kahaba huyo, pia kinaimarisha upendo na mke wako.
Ni nguvu zijengazo ndoa iliyevunjika.Kwa sababu ulikuwa umetoa upendo wako kwa kutamka kwamba unampenda huyo kahaba,lakini sasa unatamka mbele yake kwamba humpendi unapenda mke wako.Ulimwengu wa roho unatambua sana mapatano au agano la maneno.Pia maneno unayunganisha na imani kwamba ni kweli hutarudia.Lakini kama humaanishi moyoni mwako ,vile vile shetani anatambua kwamba hujaacha huyo kahaba.Lakini ukimaanisha,pamoja na kutamka ,kitu kipia kinaumbika.Ndoa iliyevunjika inajengwa upia.Na mke huu anafurahi kuona kahaba huyo anafedheheka mbele yake.
Ndoa iliyojengwa kwa kuzini itavunjika,na ndoa halali itarejeshwa ukitubu vizuri.
Kumbuka tumesema kwamba ukifanya uzinzi kupitia njia ya (kuweka kiraka kwenye shuka,maana yake,kuweka au kuwaza mwingine mukiwa kwenye tendo la ndoa),unaweza ukapata watoto,na hao watakuwa si wako lakini hata kama niwewe umewazaa,watakuwa watoto wenye utawala mwingine .Sasa basi,ukitubu vizuri kwa kumrudia Mungu na kurudia mume wako au mke wako ,tumeshaona kwamba ndoa inajengwa upya.Ndoa harari inapatikana kwa msaada wa Bwana.Sasa swali,
Je,ndoa ikirejeshwa na watoto watabaki huko,chini ya kivuli cha uzinzi?
Watoto waliyo zaliwa kwa kuzini(kutia kiraka mashuka).Wao kimwili wako katika familia za wazazi wao.Ila roho zao ziko kwenye wazazi wengine au wako chini ya utawala wa wazazi wasiye onekana.Ana weza akawa na baba yake lakini mama yake (ni roho ya mama mwingine).Mtoto yuko chini ya utawala wa mama asiyejulikana.
Ndoa ikirejeshwa na watoto,wata rudishwa kwenye familia zao.
Ni kusema ,ile roho ya mama asiyeonekana ,itatoka,ataletwa kwa utawala wa mama yake mzazi,atageuzwa tabia,akili na atapewa upendo wa mama yake.Atarudishwa kutoka kwenye mikono ya roho wa uzinzi na kuwekwa huru,ndani ya wazazi wake.
(Zaburi 126:4) “Ee Bwana, uwarejeze watu wetu waliofungwa, kama vijito vya kusini”.
(Walawi 25:41) “Ndipo atakapo toka kwako aende zake, yeye na wanawe pamoja naye,naye atairejea jamaa yake mwenyewe,tena atairejea milki ya baba zake.”
Bwana ni mwenye nguvu na mwenye uwezo wa kurejesha watu pamoja na milki zao.Atawatoa kule waliko fungiwa na kuwapeleka nyumbani mwao.
(Hosea 11:10-11.) “…Kwa maana atanguruma,nao watoto watakuja kutoka magharibi wakitetemeka.watakuja wakitetemeka kama shomoro,toka Misri,na kama hua,toka nchi ya Ashuru;nami nitawakalisha katika nyumba zao,asema Bwana.”
Watarudishwa lini?
Muda wa kurudishwa,unatokana na kufunguliwa kwa baba au mama. unaweza ukaokoka ukabadilika kabisa,ukatenda matendo ya watakatifu lakini,shetani akakusumbua na yale mambo yako ya zamani.Tamaa ikarudia mara kwa mara,na wewe ukawa unapambana nayo,unaweza ukafunguliwa kwa tamaa ya uzinzi baada ya miaka mingi.Namjua mtu aliyeokoka namaanisha kutubu na kumpokea Yesu maishani mwake, tarehe 21/7/2004.Alisamehewa dhambi zake zote lakini alifunguliwa tarehe 15/3/2007.Inawezekana hujui mambo ya kufunguliwa,hapa namaanisha (delivrance).Zipo pepo kutoka kwa shetani zinaingia mtu na kumtumikisha vibaya.Pepo hizo ni zile chanzo chake Kiko kwenye internet (kwenye pronographie au ma filamu ya ngono n.k).Wengi hata kama wameokoka kama hawajafanyiwa maombezi wamebaki wakisumbuliwa na pepo hizo.Tofautisha kuokoka na kufunguliwa.Kuokoka ni moyo umempokea Bwana na dhambi kusamehewa.Lakini kufunguliwa ni kupona ugonwa fulani.Mara nyingi dhambi ya uzinzi inatokana na pepo ya uzinzi.Lakini sio kilasiku zambi hiyo inatokana na pepo hiyo,hapana inaweza ikatokana na tamaa yako mwenyewe.Kwa mfano,pepo inakubadilisha hakili zako,mfano unaweza ukazini na mtoto wako au na mdogo wako au na baba yako?Hiyo si tamaa ya kawaida bali ni pepo.Tamaa ya kawaida inakuja ukiwa na akili timamu.Mtu umemuona mzuri,au umeshawishika kwa njia fulani.Hii, kama wewe ni mkristo lakini umerudi nyuma ,husomi tena biblia au huendi tena kanisani au moyoni mwako mda wa mambo ya Mungu ni mchache,hapo unaweza kushambuliwa na tamaa yako mwenyewe.Vile vile kama umeokoka lakini hujaombewa zile pepo zikaondoka fahamu kwamba ukiregea kidogo zinakusumbua tena.Na vifananisha na mtu mgonjwa wa ukimwi au ugonjwa mwingine.Hata kama umeokoka unasamehewa dhambi lakini sio kusema kwamba na ugonjwa unapona.Lakini unaweza kuombewa ugonjwa ukapona.
Tuendelee sasa na yule mtu aliyeokoka talehe 21/7/2004,hata kama ameokoka na kusamehewa dhambi zake,pepo hiyo ya uzinzi imemsumbua tena siku nyingi hata Bwana alipo mfungua tarehe 15/3/2007.Ile roho ilimtoka na mashambulizi yote aliyekuwa akiambatana na roho hiyo.Tangu siku hiyo alipofunguliwa,ndipo na watoto wake walianza kurudishwa kwanzia yule mtoto wa kwanza wa kuzaliwa.
Elewa kwamba hizo roho ndizo zilizohusika kwa kuzaliwa kwa mtoto huyo,tumesema kwamba wanazaliwa chini ya kivuli cha roho ya uzinzi.Sasa pepo hiyo ikitoweka ndipo na watoto watarejea kwao kwa sababu hakuna kifungo tena wako huru katika ulimwengu wa roho. Wanarejea kwao tangia mtoto wa kwanza kuzaliwa.
Jinsi watoto wanavyorejeshwa kwao.
Watoto wenyewe hawana shida yeyote, kama nirivyosema maana wanaona wanaishi na wazazi wao, lakini katika ulimwengu wa roho, hawaishi hapo, sikiliza ushuda huu.
Ushuhuda.
Baba mmoja kutoka kule Afrika alishudia akasema;
mimi ni baba wa watoto wengi, nina mke mmoja na sisi wote tumeokoka.Nimefunga ndoa ya kikristo,lakini nilikuwa sijaokoka.Nilikuwa mwenye dini tu.watoto wote niliwazaa kabla sijaokoka kasolo mmoja wa mwisho.Nilipo kubali kuacha dhambi na kumpokea Yesu, niliendelea kuishi maisha ya wokovu na kufurahia sana wokovu.Lakini kuna roho nyingine bado zilikuwa zinanisumbua baada ya kuokoka,lakini baada ya miaka 3,nilifunguliwa, zikanitoka nikawa huru, jina la Bwana libarikiwe.
tarehe 21/7/2004 nilitubu na kujutia dhambi na kumpokea Yesu kama Bwana na mwokozi wa maisha yangu, nilikombolewa tarehe 15/ 3/2007.Hapo ndipo nilipata kibali kwa Mungu kuwa mme wa mke wangu na baba wa watoto wangu,kumbuka kupewa kibali na Mungu ni tofauti na kupewa kitu chenyewe.Unaweza kupata kibali cha kuchumbia mtu,lakini siyo kusema kwamba kibali hicho kimekupa mke hapo hapo.Namshukuru Mungu,nilipo kombolewa, nimepewa kibali kwa familia yangu.Nilikuwa na mke na watoto wengi lakini kwa sababu nilikuwa bado sijaokoka,na ndoa yangu ilikuwa kwenye giza tupu.Lakini kwenye macho ya mwilini havionekani.Unaona tu baba, mama na watoto wanaishi kama wengine,wanavaa,wanajenga nyumba,wana raha N.K.
Lakini ulimwengu wa roho,wanatambua kwamba,baba huyu,anapenda wanawake wengine,kwa hiyo ana ndoa nyingi,na watoto aliozaa si wa kwake maana ni mazao ya roho chafu iliyo muongoza wakati wa lile tendo..Kwa neno lingine ,ni mazao ya roho ya uzinzi,watoto wake wote si wake bali ni watoto wa uzinzi au waiozaliwa kwa tendo la uzinzi kupitia kutia shuka kilaka (walipatikana wakati ulipokuwa na mwenzako lakini ukawa unamutumia kama chombo tu huku ukiwaza mwingine).Basi mambo hayo yote,anaonyesha jinsi gani watoto hawana wazazi,baba huyu hana mke,na mke hana mme.Basi,kama alivyosema kwamba alipofunguliwa,alipewa kibali cha kuwa na familia,kibali hicho amekipata tarehe 15 / 3/2007alipo funguliwa zile pepo zikamtoka.Kibali hicho kinafananishwa na sisi tuliyempokea Yesu.Tunatarajia kwenda kufunga ndoa na Bwana Yesu na kuishi naye milele.Lakini tunayo iyo ahadi tunasubili siku ilioamriwa na Mungu mwenyewe.Hapa baba huyu anashuhudia kwamba amepewa kibali kuwa baba wa familia .Anasubili lini atawakabidhiwa.
Jinsi ya kukabidhiwa watoto wako.
Siku mmoja mke wake,alionyeshwa wapo kitandani na mme wake wakilala usingizini.Gafla wakaona mama mmoja analeta kitoto kichanga kama cha miezi 4,anakiacha katikati yao kisha akaondoka. Mama huyo akampenda sana huyo mtoto na kumhurumia sana.Akasema kesho nitamnunulia pampers,maziwa na nguo nyingi,walipoamka huyo mama akamsimulia mmeo kwamba amemuona mama mmoja amewaletea mtoto mchanga kama wa miezi 4,siku hiyo sasa,mtoto wao wa kwanza alikuwa na sikukuu ya kuzaliwa kwake( birthday),ndipo huyu mama akamnunulia vitu vingi sana wakafurahia birthday hiyo walipouliza maana ya ndoto hiyo waliambiwa kwamba alikuwa kwenye kifungo cha mama mwingine (aliyemzaa kwa roho ya uzinzi)nasiku hiyo amerejeshwa nyumbani kwake.Kumbuka,amemleta akiwa mchanga,tena mweusi lakini hali halisi alikuwa ametimiza miaka 12 tena ni mweupe.Nikusema amechukuliwa akiwa mdogo sana,amekaa miaka mingi kwenye vifungo amerejeshwa kwa mama na baba yake.Ndoa halali,famiia halali iliyokombolewa na Bwana mwenyewe.Hiyo sikukuu yake ilikuwa na maana kubwa kwenye ulimwengu wa roho ,siku ya kutoka kifungoni na kurejeshwa kwa wazazi wake
(Hosea 11:10-11)”maana atanguruma nao watoto watakuja kutoka magharibi wakitetemeka,watakua wakitetemeka kama shombo toka Misri na kama hua mimi nitawakalisha katika nyumba zao,asema Bwana.”
Birthday iliofuata ni ya mtoto wao wa mwisho,yeye alizaliwa katika nuru,maana baba huyo alikuwa amesha okoka.Hakuna kurudishwa maana yeye yupo ndani ya familia.
Aliyefuata kurudishwa ni mtoto wao wa 3,maana huyu ndie birthday iliyofuata.Na huyo,wameonyeshwa analetwa kwenye nyumba yao,akiwa na wafanyakazi 2 wa kumhudumia.Mmoja anashughulika na chakula chake na mwingine anashughulika na usafi wake na nguo zake.Kesho yake akaja mama mwingine kuchunguza kwamba mtoto amehudumiwa vizuri kisha akaondoka . Asubuhi mama akamwambia mmeo kwamba ameletewa mtoto wao wa 3 lakini amekuja na watu wakumhudumia,wakaomba Mungu kuuliza maana ya ndoto hiyo.
Mungu akawajibu kwamba ,mtoto amerejeshwa kwao,hao watu ndio walikuwa wanamhudumia sasa,amerudishwa kwa wazazi wake.Mfanyie sherehe kubwa nzuri maana malaika mbinguni wana shangilia,mtoto huyu amerudishwa kwao.Huyu yeye amerudishwa akiwa mkubwa kidogo kama vile mtoto wa darasa la pili,lakini hali halisi ni mtoto wa darasa la 4, Wakauliza kwa nini amekuja na wafanyakazi na mama yule akaja kukaguwa kwamba amehudumiwa vizuri?Bwana akawambia kwamba;ni kwa sababu siku hiyo ya birthday yake ilikuwa ni siku ya Alhamisi wakasema watamfanyia sherehe siku ya Jumamosi. na siku hio ilikuwa haijafika isipokuwa tarehe yake ya kuzaliwa ilikuwa imepita .Sasa Mungu amewaagiza malaika waendelee kumuhudumia mpaka mtakapo mpokea kwa sherehe na furaha na shangwe.Ndipo wakamfanyia sherehe kubwa ya furaha nyingi.
Baadaye mama akapokelewa kama mke wa baba huyo,akakabidhiwa mamlaka ndani ya nyumba.Baada ya hapo watoto waliendelea kurudishwa siku ya kuzaliwa kwao.Na mme huu akakabidhiwa mkeo siku ya kuzaliwa kwake,mama huyu alionyeshwa , anambeba mtoto mikononi alipoangalia vizuri huyo mototo akageuka kuwa kibaba kilefu mikononi mwa mama huyo.Ndipo akanza kukemea akisema toka shetani katika jina la Yesu! Ndipo kile kibaba kikakimbilia baharini kisha akazinduka kwenye ndoto hiyo. Alikuwa anakumbatia mme siyo mwenyewe ilikuwa ni pepo iliye vaa sura ya mume wake.Ilipotoweka ndipo mwenyewe akarejea mke wake na watoto wake siku ya kuzaliwa kwake. Haleluia.Walishangilia kwa furaha na kufanya sherehe nzuri.Mama huyo alikuwa chini ya utawala wa roho ya mme lakini si mume wake.Siku hiyo,utawala wa zamani ulianguka,naye akakabidhiwa mme kutoka kwa Bwana mwenyewe.Kwa hiyo mambo ya kale yamepita,yote yamekuwa mapya.Ndoa mpya na watoto halali.
Jina la Bwana libarikiwe.
Kumbe siku ya kuzaliwa ina maana kubwa mbele za Mungu.Ndio siku Mungu aliyopangia mwanadamu cha kufanya hapa duniani.
Hebu tuangalie mfano wa familia hii ili tuelewe vizuri.
| Birthday(tarehe ya kuzaliwa)
|
Kurejeshwa
Kwanzia mtoto wa kwanza
|
| Marc Tarehe 10/1/1962
|
Thime Tarehe 30/6/2007
|
| Suzana Tarehe 4/10/1967
|
Dany Tarehe 13/7/2007
|
| Thime Tarehe 30/6/1995
|
Josias Tarehe 20/9/2007
|
| Benny Tarehe 2/10/1996
|
Benny Tarehe 2/10/2007
|
| Josias Tarehe 20/9/1998
|
Suzana Tarehe 4/10/2007
|
| Nathan Tarehe 24/2/2001
Joseph Tarehe 21/4/2004
|
Marc Tarehe 10/1/2008
Nathan Tarehe 24/2/2008
|
| Dany Tarehe 13/7/2005
|
Joseph Tarehe 21/4/2008
|
Mume jina lake Marc alizaliwa tarehe 10/01/1964,na mke wake Suzana alizaliwa tarehe 4/10/1965.Wamezaa watoto 6.
Mtoto wao wa kwanza anaitwa Thime,alizaliwa tarehe30/6/1995.
Mtoto wa pili kuzaliwa anaitwa Benjamin,alizaliwa tarehe2/10/1996.
Mtoto wao wa tatu kuzaliwa anitwa Josias,alizaliwa tarehe 20/9/1998.
Mtoto wao wan ne kuzaliwa anaitwa Natan,alizaliwa tarehe24/2/2001.
Mtoto wao wa tano kuzaliwa anaitwa Joseph,alizaliwa tarehe 21/4/2004.
Mtoto wao wa mwisho kuzaliwa anaitwa Dany,alizaliwa tarehe 13/7/2007.
Kumbuka alishuhudia kwamba alikuwa mwenye dini tu.Alifanyia ndoa kanisani,watumishi wakaibariki.Lakini ameshuhudia alikuwa anatembea na wake wengi.Maana yake hata kama mbele ya watu alikuwa na mke mmoja,mbele za Mungu alikuwa na wake wengi.Kumbe sasa ndoa ilikuwa haipo ,hajawahi kuwa na mke bali alikuwa na wake.Kumbe sasa na huyo aliyekuwa anahesabika kama mke wa ndoa alikuwa si wake.Yeye niseme aliingizwa tu kwenye kundi ya makahaba wengine.Lakini kwa sababu mke huyu alikuwa hajui kwamba mumue wake hajaokoka,maana yeye alikuwa ameokoka huku akijua kwamba na mwenzake ameokoka,kumbe si kweli.Ulimwengu wa roho unatambuwa kwamba mama huyo hajawahi kuwa na ndoa harari mbele za Mungu ,bali alikuwa na ndoa harari mbele za watu na mbele ya selikari.Lakini mbele za Mungu alikuwa hana mume,wala mume alikuwa hana muke(alikuwa na wake),wala walikuwa hawana watoto.Ameshuhudia kwamba ndoa yake ilikuwa kwenye giza tupu,au niseme ilikuwa haipo kabisa .Alipo tubu na kumrudia Mungu akasamehewa,nuru ikaangazia maisha yake.Akawa mkriso muzuri anae hofu ya Mungu moyoni mwake.Hapa hajarudia wale wake wa pembeni maana ameshaokoka.Lakini zile pepo zimemufuata na kumshambulia naye akaendelea kuomba mpaka zikamtoka,akafunguliwa. Ndipo amesema akapata kibali kuwa na mke na watoto.Sasa,siku ya kuzaliwa kwake ndipo alipata mke,na mke wake siku ya kuzaliwa ndipo alipata mume halisi. Watoto nao wamerejea familia hiyo kwanzia tarehe ya kuzaliwa kwa mototo mkubwa.
Kumbuka tena ameokoka nakumrudia Mungu tarehe 21/7/2004.Hapa hajakabithiwa wala kuwa nakibali kuwa baba au mume wa mkewe.Lakini ameokoka,bali ndoa bado iko kivulini mwa pepo la uzinzi.Alipo kombolewa,akafunguliwa tarehe 15/3/2007,ndipo aliahidiwa.Maana yake ameshapata kibali anasubili lini wafike.
Angalia siri ya Mungu,kwanzia tarehe hiyo ya kufunguliwa,kama ni kuangalia tarehe za kuzaliwa zinazofuata,ni tarehe 21/4/2005,alipozaliwa mtotoJoseph.Si mume huyo wala mama huyo walierudishwa ,Lakini ,alianza kurudishwa,mzaliwa wa kwanza ,jina lake Thime.Angalia kwenye kichapo hapo juu.Wengine wamefuata kurudishwa kulingana na jinsi tarehe zinazofuatana.
Ndugu msomaji umeelewa mambo hayo?Naamini maswali mengi unayo,kama wengine waliponiuliza,haya mambo umeyatoa wapi?Bwana ndiye alinifunulia hayo,tena akaniagiza niwaandikie watu wa Mungu waelewe kwamba dhambi ya uzinzi ni mbaya sana .Inavunja ndoa,inasambaratisha watoto,lakini ashukuliwe Mungu aliyetufunulia jinsi wanavyorejeshwa.Kila mtu akarudishiwa nafasi yake.
Muhimu Kuzingatia
Kurejeshwa kwa familia
Kinacho fungia watoto nje ya familia zao ni uovu wa wazazi wao.wazazi wakirejeshwa na wao watareshwa.Hesabu za Mungu ni njema.Mzaliwa wa kwanza ana maana kubwa mbele za Mungu. Biblia inaagiza kwamba tunatakiwa kutoa sadaka kwa ajili ya mzaliwa wa kwanza.
Kutoka 22:29 imeandikwa hivi: “Usikawie kuleta malimbuko ya matunda yako na ya vinywaji vyako.Mzaliwa wa kwanza katika wanao waume utanipa mimi.”
Ndio maana Mungu akaomba Ibrahim atoe mwanae kuwa sadaka kwa Bwana naye akawa mwaminifu kumtoa mpaka Mungu akashuhudia uaminifu wake,akamhurumiya badala yake akamuonyesha kondoo akayitoa badala ya mwanae. Hata leo tunatakiwa kutoa sadaka kwa Bwana kwa ajili ya mzaliwa wa 1.
Zingatia kuwafurahisha kwenye sikukuu zao za kuzaliwa maana unajuwa vizuri wanachopenda.
Hakikisha pia unamfanyia siku hio ,usiseme nitamfanyia siku nyingine,maana siku hiyo atarudishwa harafu atakosa wakumpokea.
Pia hakikisha unampatia vitu vyake siyo vya kuazima sehemu ,kwa mfano,mama huyo alishuhudia kwamba mototo wake wa nne,alikuwa anapenda sana midori ya gari au pikipiki,ndipo akaenda kwa jirani yake akakuta watoto wake wana midori mingi mizuri akasema ,nitampelekea mdori huu wa pikipiki kwenye sherehe yake tena atafurahi ,atawuchezea kisha hamu ikiisha nitawarudishia.Ndipo akamletea zawadi hiyo,mtoto akafurahi sana.Baada ya mwezi akamrudishia huyo jirani yake.Alipo lala usiku huo,Bwana akamuonyesha kwamba mtoto huyo amelala kifuani kwa mama mwingine,akaona anamkemea huyo mama amuachie,huyo mama akaondoka akamuacha na mtoto akakimbia,alituma watoto wengine kumuita lakini hakurudi,ndipo akaamua mwenyewe kwenda kumuita akaendelea kukimbia mbali nae kwenye milima,akatumia mamlaka ya jina la Yesu kwa ukali,mtoto akamrudia.Ndipo akauliza Mungu maana ya ndoto hiyo akaambiwa kwamba siku yake ya kuzaliwa mtoto amefunguliwa lakini amepokelewa na zawadi sio zake.Alipo zirudisha ,baada ya mwezi ,ndipo akafunuliwa kwamba kumbe mtoto amefunguliwa lakini hajarejeshwa kwao ,bado anatangatanga ,mama huyo alifanya haraka kumununulia midori mingine ya kwake mtoto akafurahi sana akarejea nyumbani kwake.Jina la Bwana libarikiwe!
Kumbe mpendwa kinacho sababisha kurejea ni Zawadi zako.Sio vitu vya wengine.Zawadi nzuri ya kukufurahisha.Tunamshukuru Mungu kwa mafunuo yake ya ajabu ya kurejesha ndoa zetu na familia zetu Amen.
Hivi basi,tunaona kwamba,familia zinarejeshwa kutokana na kufunguliwa kwa wazazi kwanza,cha pili kwanzia mzaliwa wa kwanza cha tatu ,kwenye tarehe yake ya kuzaliwa.,cha nne,zawadi nzuri ya kufurahisha,ya kwake.
Tuombe Mungu tufunuliwe zaidi mambo haya ili tujue siri zimo ndani yetu na kwa watoto wetu kupitia siku za kuzaliwa .Mungu awabariki.
Nataka usichanganyikiwe nakuanza kuwaza sana juu ya ndoa yako na watoto wako,mambo haya yapo kwenye ndoa za gizani.(kama wewe hujaokoka,bado unaenderea na kujifurahisha na mambo kama hayo,anza kujirekebisha na kumrudia Mungu,na mengine atafuata kama nilivyo kujulisha hapo juu).Lakini kama wewe umeokoka,na mwenzako ameokoka,maisha yenu yako nuruni mambo haya hayawahusu,kwani nyiye mnahofu ya Mungu ndani mwenu,hakuna uzinzi ,mnaishi kwa kuheshimiana,nyie ndoa yenu na familia yote iko kwenye nuru.Muendelee kupendana na kumtumikia Bwana kwa pamoja.Na Mungu yupo ndani mwenu.
Mungu,mwanzilishi wa ndoa,anajua kwa kukupatia mume au muke huyo,alikuwa anatarajia nii kwenu.Adamu na Hawa Bwana amewabariki,akawambia,zaeni mkaongezeke,mkatawale juu ya nchi,nk…Na nyie ndugu Bwana amewabariki,mumezaa,mumeongezeka,mna mali nyingi,sasa basi,mmtumikie Bwana,hubili injili watu wamrudie Bwana wao,maana siku hizi,ndoa nyingi ziko kwenye giza tupu.Lakini Mungu,bado anaokoa,anasamehe tena anarejesha vilivyopotelea kwa shetani,vinarudishwa kwa jina la Yesu.
Niseme nini ndugu,inawezekana ukawa kama baba huyo tuliyejifunza kwa ushuhuda wake.Yeye alikuwa mwenye dini tu.Alikuwa amebatizwa kama wewe na mimi,alikuwa anaimba nakumtolea Bwana sadaka kama mimi na wewe tunavyofanya,na mambo mengi aonekanayo ni mema.Lakini,pamoja na hayo,alikuwa mzinzi,na dhambi nyingine nyingi ,kama uongo,unyanganyi,chuki,hasira n.k….Siku moja neon la Bwana likamjia akaamua kuacha dhambi na kuokoka.
Leo hii tunafurahia ushuhuda wake.
Sasa wewe nawe uko kama yeye?
Au wewe hata kuingia kanisani huingie?
Au wewe umeokoka kabisa mambo kama hayo huyajui.?
Kama ni hivo,hongera ndugu yangu!Songa mbele na Bwana aendelee kukupigania na kukushindia mpaka umalize safari yako ya hapa dunuiani.
Kama wewe hujaokoka,nakushauli ukubali Yesu mwana wa Mungu aingiye maishani mwako atawale.!
kisha muombe afute maovu yako yote ndani ya damu ya Yesu,akusamehe.Afute jina lako kwenye kitabu cha hukumu ,aliandike kwenye kitabu cha uzima.Pia umuombe msamaha mwenzako,nauachane kabisa na wale waliyekuwa wahabara wako.
Mungu akubaliki na akusaidie.
Ndugu,maisha yako,ni uamuzi wako.Ukitaka unaendelea na uovu wako,ukitaka vile vile unaamuwa kubadilika.
Nimekushauri ,kama unataka kubadilika,hebu sema ukimaanisha sala hii;
Bwana Yesu naja mbele zako.Mimi ni mwenye dhambi nyingi nawe wajuwa.Bwana nakuombaunisamehe uovu wangu wote.Futa dhambi zangu zote ndani ya damu yako ee Yesu.Futa jina langu katika kitabu cha hukumu nauliandike ndani ya kitabu cha uzima.Tangu sasa nimeamua kukufuata na kukutumikia.Asante Bwana kunikubali kama mototo wako,kwa jina lako eeYesu naomba nikikuamini .amen.
Hongera ndugu kuokoka.!Nafurahi sana kwa uamuzi wako, hata mbinguni malaika wanashangilia!Uu ndio mwanzo wa maisha yako na Kristo.Utafurahi sana maishani mwako,raha ya kweli na amani ya kweli vinakukumbatia milele.!!!!.
Ubariliwe na Bwana.
—————————————————————————————
Titre; Hata mto ufurike, yeye hatetemeki…
Yariyomo:
Sura 1: Mtumishi wa Mungu.
Nyumba ya Bwana
Wanyama; watumishi wa Mungu
Hasira; chanzo cha dhambi nyingi.
Ushuhuda
Maombi
Sura 2.Huduma ya nabii
Nabii Elia
Utii
Usiogope
Ukarimu.
Sura 3.Utoaji.
Ushuhuda.
Onyo.
Sharti za kutoa.
Sura 4 :Ushuhuda ; kuhusu kanisa.
Ushuhuda :Safari ndefu
Ushauri kuhusu safari.
Ushuhuda :Mwaliko wa harusi.
Dibaji.
Ndugu mpendwa,naamini ,umeshasoma vitabu vingi,lakini hiki,hakika kitakuvusha kwenye daraja na kukupereka kwenye ngazi nyingine.Kama Mungu amependezwa kitabu hiki kikufikie,ni kwa sababu ya kazi maalum anayetaka ifanyike kwako,kama ilivyofanyika kwangu nakwa wengine waliyepata habali za kitabu hiki.kama vitabu vingine vilivyokusaidia ukafika hapo ulipo,iko tumaini pia ya katabu haka kadogo kwamba katakuletea utamu wa pekee.Mimi sina ujuzi mkubwa wa neno la Mungu,ila,nakuletea habali kama nilivyofunuliwa na Mungu.Ndiyo maana,sura nyingi nimeandika kwamba ni Ushuhuda.Au pia ningeweza kuandika Ufunuo.Kitabu hiki kinazungumziya kuhusu watumishi mwenye ,huduma mbalimbali,sana sana unabii na utoaji kanisani.Pia kinazungumzia kuhusu safari yetu ya kuelekea Yerusalem mpya kwamba imekaribia,pia katabu haka kanaleta mwanga kuhusu kadi ya mwaliko wa harusi ya mwana kondoo kwamba zimesha sambazwa tayari tangu 1992 nilipo letewa na malaika ili niwape mataifa mbalimbali,sana sana kitabu hiki kinatuhimiza kuwa tayari ,mda kidogo palapanda italia na wenye mwaliko watakalibishwa kuingiya Yerusalem mpya.Haleluia !
« Heri,heri, heri,…. Walioalikwa, walioalikwa, walioalikwa,… karamu ya mwana kondoo !!!!! »
Sura ya 1.
Mtumishi wa Mungu
Mtumishi yeyote anaitwa mtumishi kwa sababu; anatumika.Anaweza akawa ameajiliwa na mtu mwingine na hapo anaitwa mtumishi wa mtu huyo.Kama ameajiliwa na Bwana anaitwa mtumishi wa Bwana.Kama ameajiliwa na Shetani anaitwa mtumishi wa Shetani.Tena unakuwa na mahali unapofanyia kazi hizo.Unaweza ukatumika sokoni(ukiuza vitu.)Unaweza kutumika ofisini (ukifanya kazi za ofisi)au shuleni (ukiwa mwalimu unafundisha).
Au unatumika kanisani (ukiwa mtumishi wa Mungu kanisani),au ukawa unaabudu sanamu (ukiwa chini ya mti au juu ya milima )ukimtumukia Shetani.
Sasa tuangalie mtumishi wa Bwana anayefanyia kazi yake kanisani nyumbani mwa Bwana.Kanisani ni jengo la kawaida lakini heshima yake ni kwa sababu ni nyumba ya Bwana.Napenda ndugu wapendwa tukumbushane kwamba nyumba ya Bwana ni mahali patakatifu hata kama imejengwa na mikono ya wanadamu.Madhabahuni ni mahali patakatifu zaidi.Tunatakiwa kuheshimu nyumba ya Bwana,tusiruhusu watoto kugeuza kuwa mahali pa kuchezea.Mungu ni mwenye wivu ,tuwe makini sana tulinde vizuri nyumba ya Baba yetu. Vile vile tuwe makini sana na maneno tunaye tamka kanisani.Wengi wanatoa ahadi na wasizitimize wakati wameahidia nyumbani mwa Bwana.Bwana anachunguza kila kitu maana yeye hasahau wala haachii.Ole wako mpendwa usieheshimu nyumba ya Bwana na kuiona kama kawaida tu!
Haya nayokuambia ni Bwana amenifundisha,singeweza kushuhudia jinsi ilivyokua lakini fahamu kwamba nyumba ya Baba ni nyumba takatifu inastahili heshima yake na Mungu awabariki.
Ushuhuda.
Siku mmoja ,tulikuwa kanisani ,nikatoa zawadi ya simu kwa mama mmoja hapo kanisani.Simu hiyo ilikuwa zawadi niliopewa na mme wangu.Tena ilikuwa ya gharama.Lakini,hata nilipoitoa kwa mama huyo,nilikuwa namaanisha kwamba nitampa nyingine niliyekuwa nayo nyumbani,tena mpya kabisa.Sasa watu wakafurahi wakashangaa jinsi nilivyoweza kuzawadia wengine simu hiyo.Pia mme wangu alikuwepo akashangaa jinsi gani naweza kugawa simu aliyeninunulia tena kwa gharama.Nikamwambia kwamba nitampa nyingine nilieiacha nyumbani.Akasema huwezi kufanya hivo wakati wote wameona kwamba umempa hiyo hiyo.Nikakataa kuitoa maana nendelea kusema kwamba moyoni nilikuwa namaanisha nyingine.Nikamwendea yule mama nikamueleza kwamba sitampa hii,lakini nitamletee nyingine ipo nyumbani.Hata hivo akafurahi.Lakini tangu hapo roho wa Bwana akasema moyoni mwangu kwamba natakiwa kutoa simu hiyohiyo maana ndiyo nilipotoa mbere ya watu tena kanisani,nyumbani mwa Bwana.Sauti hiyo nikaipuuza,nikatoa hiyo nyingine yenye bei ndogo.Siku chache zilipopita,nikaenda kanisani kwenye maombi,nikaisahau nyumbani.Nikatuma kijana wangu aende akaichukue kisha aniletee kanisani.Akaenda akaileta,lakini alipo fika njiani,akakutana na majambazi walikuwa wamevaa nguo za polisi,wakamsachi ,wakachukuwa ile simu na kwenda zao.Kijana wangu alikuja kanisani na kunieleza yaliyomkuta huku akitetemeka sana.Nikamwambia hamnashida,tutapata nyingine.Nilihuzunika,nikaomba rehema kwa Bwana maana nimetenda dhambi kutosikia sauti ya roho wa Bwana iliponiambia nitoe simu hiyohiyo.Bwana atuhurumie wapendwa.Tusitende kinyume na roho zetu.Kama unatenda hiki,vile vile roho yako iwe inasema hivohivo.Kama roho yako haipendi basi usitende.
Nyumba ya Bwana ni takatifu,na roho wa Bwana yupo hapo,yeye ni shahidi wa kweli.Bwana alituma watu wanichukulie simu ili nikumbuke kutubu.Wasingeyiiba singekumbuka kuomba msamaha wa dhambi ya uongo niliyefanyia kanisani(kutoa kisicho).
Kwa nini tunajenga nyumba ya Bwana?
2Nya2:4-6.
Mstari hii inasema kwamba ni ili kumwabudu ,kumtolea sadaka n.k.Tena hili ilikuwa agizo kwa wa israeli wote.Pia Nyumba ya Bwana ni nyumba ya sala. Marko 11:17.
”Akafundisha akasema ,je!Haikuandikwa ,Nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa mataifa yote?Bali ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyang’anyi.”
Nyumba ya Bwana ni hema pa kukutania watu wa Mungu,na kutiana moyo,kufarijiana kufanya huduma za rohoni.Si pango la waovu,bali ni hema la watakatifu wanapokutania kumusifu Bwana Mungu.
Singeweza kumaliza kipengele hiki bila kukukumbusha kwamba hatutakiwi kuingia nyumbani Mwa Bwana na mikono mitupu.Tumletee sadaka zenye kumridhisha Mungu wetu.
Filip4:18.
”Lakini ninavyo vitu vyote na kuzidi tena nimejaa tele;nimepokea kwa mkono wa Epafrodito vitu vile vilivyotoka kwenu,harufu ya manukato,sadaka yenye kibali,impendezao Mungu.”
Kumbe tukijitoa kwa watumishi wa Bwana tunamtolea Mungu sadaka impendezayo.Na Mungu ukimtumikia nayeye atakurudishia,maana yeye hari deni la mtu yeyote.Sadaka yake kwako ni baraka zake kwako.Bwana akikufanikisha kwa kukubaliki ,ni kusema amekupa sadaka yake.Hata wanyama na ndege anawakumbuka akawapa sadaka.Ulikuwa hujui? Soma
Ezek39:17-20.”Na wewe mwanadamu ,Bwana Mungu asema hivi;sema na ndege wa kila namna,na kila mnyama wa kondeni,jikusanyeni,mje,jikusanyeni pande zote muijilie sadaka yangu,niifanyao kwa ajili yenu,naam,sadaka kubwa juu ya milima ya israel,mpate kula nyama na kunywa damu.”
mst 19. ”Nanyi mtakula mafuta na kushiba,mtakunywa damu na kulewa,na sadaka yangu nilioyifanya kwa ajili yenu.”
mst20.
”Nanyi mtashibishwa mezani pangu Kwa farasi na magari ya vita,na mashujaa na watu wote wa vita,asema Bwana Mungu.”
Bwana Mungu anaye wapa sadaka ndege na wanyama wakashiba,atashindwa na wewe kukufurahisha ndugu yangu?
Zaburi 134:1-2.
”Tazama ,enyi watumishi wa Bwana ,Mhimidini Bwana,nyote pia.Ninyi mnaosimama usiku katika nyumba ya Bwana.Painulieni patakatifu mikono yenu,na kumhimidi Bwana.”
Zab135:1-6.
Haleluya.
Lisifuni jina la Bwana ,enyi watumishi wa Bwana,sifuni.Ninyi msimamapo nyumbani mwa Bwana,Nyua mwa nyumba ya Mungu wetu.Msifuni Bwana kwa kuwa Bwana ni mwema,liimbieni jina lake kwa maana lapendeza.Maana najua mimi ya kuwa Bwana ni mkuu ,na Bwana wetu yu juu ya miungu yote.Bwana amefanya kila lililompendeza,katika mbingu na katika nchi,katika bahari na katika vilindi vyote Amen.
Watu wa Mungu tunamjengea Bwana nyumba ya kuabudia na wale wa abudu sanamu vile vile wanajengea satani.
2Fal 19:37.”Ikawa alipokuwa akiabudu nyumbani mwa Nisroti,mungu wake…..”
Sasa basi ,Mungu wetu wa mbinguni anataka nyumba yake iheshimike.
Cha pili,wamwabuduo tumwabudu katika roho na katika kweli.Tumwabudu na mioyo iliyo safi ndiyo manukato yenye kupendeza machoni pake.1Nyak 16:29.
”Mpeni Bwana utukufu wa jina lake;leteni sadaka,mje mbele zake;Mwabuduni Bwana kwa uzuri wa utukufu.”
Watu wa Mungu tunatakiwa kujiweka sawa tuingiapo nyumbani mwa Bwana,tukivaa nguo zenye heshima (nguo za kujisitili miili yetu).
1Tes4:4
”Kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake katika utakatifu na heshima.”
Nyumbani mwa Bwana, wapo viumbe visivyo onekana kwa macho,malaika wa Bwana wanakaa pamaja nasi kanisani,pia roho wa Bwana anakuwepo,bila kusahau Mungu mwenyewe anayehotubia kanisa(wakristo),kupitia kinywa na umbo la mtumishi wake. Malaika hao,wanazunguka na kuangalia watu wote jinsi walivyo vaa.
Ushuhuda.
Siku moja,nilionyeshwa kwenye ndoto za usiku ,tuko kanisani nikaona nimeva nguo fupi na shati isiyo na mikono.Nikaona mtu anayechunguza kila mkristo jinsi alivyo vaa.Nilipoona anasogelea kiti changu nikaona naanza kushusha sketi yangu na kufunika mikono yangu navidole.Alipo nifikia alininongonezea maskioni mwangu kwamba natakiwa kuvaa vizuri,nguo yenye kufunika mwili,akaniambia nivae nguo ndefu yenye kufunika na mikono.Nikaona anazungukia na wengine akiwanongonezea maskioni mwao.Ni kweli tukutanikapo kanisani kumfanyia Bwana wetu huduma ,malaika wa Bwana wanakuja na kusaidiana natwe.Vile vile Paulo naye ametufahamisha kwamba malaika wanapendezwa sana mwanamke akivaa nguo nzuri bila kusahau kufunika kichwa.Malaika wa Bwana wanaonekana ni wenye adhabu nyingi.Wanapendezwa sana kila mwanamke avae kichwani eti dalili ya kumilikiwa na mumeo.
1Kor 11:10
”Kwa hiyo imempasa mwanamke awe na dalili ya kumilikiwa kichwani kwa ajili ya malaika.”
Ndugu mpendwa katika Bwana,hapa tunazungumzia ,jinsi ya muonekano mzuri tukiwa nyumbani mwa Bwana kumuabudu. Nimewasikia wakristo wengine wakisema kwamba Mungu huangalia moyo.Najiuliza ,je akiangalia moyo tu,mwili nao ni wanani? Je,si wake pia?Nimewahi pia kusikia mama moja akisema,..”nikienda kanisani,navaa nguo nzuri sana zenye bei kubwa,najipamba mwili wangu vizuri,na weka vizuri nywele zangu,nafanya hivyo,kwa maana najua Mungu ni mheshimiwa kuliko rais wa nchi.Kama najipamba nikialikwa kwa waheshimiwa wa nchi,je Mungu si zaidi?”Mama huyo alionyesha kwamba Mungu ni mheshimiwa ndiyo;lakini amesahau kujua kwamba Mungu si mwanadamu apendezwe wakati umevaa hii au ile,maana yeye anapendezwa na mioyo yetu ikiwa misafi bila dhambi.Mioyo iliopondeka,iliotakasika katika damu ya Yesu.Mapambo ya mwili,nguo za bei gani,mambo hayo ni ya wanadamu,wenye tamaa kama mimi na wewe,wenye majivuno,wenye mashindano,wenye kuhesabu waliye vaa vizuri au la,hayo ni mabo ya mwilini.Lakini,ukiwa msafi rohoni,ni vema na muonekano wako wa nje uwe mzuri.Si nguo za aibu,zenye kubana mwili,zenye kuacha mwili wazi.Vile ulivyo wewe ni mzuri sana.Bwana amekupa ngozi nyeusi kama mimi ,furahi.Ukiwa na ngozi nyeupe,furahi,vile vile.Nywele ndefu sawa,ziwe fupi furahi sana,maana yeye amatufanya apendavyo.Sisi tuliyemwamini Kristo Yesu tu wazuri sana.Miili yetu safi,mioyo yetu safi,ni utukufu kwa Bwana.
Ushuhuda.
Siku moja nimemuona mama mmoja akikaa nje ya nyumba yake akiwa amevuanguo zake na kujianika kwenye jua nikamuuliza vipi wewe mama?Kaniambia kwamba anataka kuwa na ngozi kama ya kwangu,ngozi nyeusi.Eti ngozi yake inawaka sana.Nikashamgaa kweli.Wakati nimetoka kwetu afrika,nilikuwa nimeona wanawake wakijipaka mafuta ya kubadilisha ngozi iwe kama ya wazungu.Kumbe na wao wanataka ngozi kama ya weusi.Nilipo kuwa shuleni,tulisoma pamoja na wazungu.Nywele zangu zilikuwa fupi na zao zilikuwa ndefu.Siku moja mama mmoja mzungu akaniambia,nyinyi mna nywele nzuri kuliko sisi.Maana nyie ni fupi haziwasumbui.Vile vile mkitaka ziwe ndefu mnaziweka!Nikajiuliza dunia hii ni hatali,watu hawajui kufurahia jinsi walivyo.Hapo shuleni kulikuwa na shule wanafundisha mambo ya salooni(kuhusu nywele).Niliona watu wengi sana wanaenda wanabadilisha rangi ya nywele.Nilikuwa naona mala hawa wana nywele zenye rangi ya njano,wengine nywele nyekundu,wengine nyeusi,wengine upande mmoja njano ,upande mwingine nyekundu.Siku moja mme wangu,akazungumza na mama mmoja mzungu,akamwambia ,unajua ni nani anaewaambia kwamba hampendezi,mala mkaweka rangi hii au hii?Huyo ni shetani.Hataki mfurahie uumbaji wa Mungu.Cha kushangaza zaidi,na sisi wakristo,tunashawishwa sana na mambo kama hayo.Jibu ni moja,shetani muongo,anatufanya tusione uzuri wetu,lakini ,ashukuliwe Mungu atusameheae makosa yetu.Tumekosa sana mbele zake,tumuombe Bwana aturehemu,afute uovu wetu wote machoni pake,tumwabudu katika roho na kweli,na utukufu wake utakuwa pamoja nasi.
Huduma
Kila mhudumu ni mtumishi wa Bwana.Wahudumu wamegawanyika kwenye makundi mengi.Kuna wahudumu wa Mbinguni(wanatoa ujumbe kutoka kwa Mungu na kutuletea) hao ni Malaika.Pia kuna wahudumu wanadamu kama mimi na wewe.Pia kuna wahudumu (wanyama ) kama tunavyosoma kwamba vitu vyote ni watumishi wa Bwana.
Zab 119:91.”Kwa hukumu zako vimesimama imara hata leo,maana vitu vyote ni watumishi wako.”
Wanyama, watumishi wa Mungu.
Neno la Mungu linasema kwamba,….vitu vyote ni watumishi wa Mungu.(zaburi 119:91) “kwa hukumu zako vimesimama imara hata leo,maana vitu vyote ni watumishi wako.”
Kwa neno hili vitu vyote ni pamoja na wanyama. Sasa tuangalie wanyama.
Kunguru,
1. kunguru kutumwa kumlisha Elia
(1waf 17:4)
“Itakuwa utakunywa maji ya kile kijito ;nami nimewaamuru kunguru wakulishe huko.”
Kwa hakili za kibinadamu ni vigumu kuelewa jinsi gani Mungu aliongea na kunguru,tena wengi ili wamuletee nyama na mikate jioni na asubuhi.Mpendwa kwa nini tusumbuke tukiwa ndani ya Yesu? Hitaji zetu zote zipo mikononi mwa Bwana. Tuombe Mungu awaagize watumishi wake watuletee hitaji zetu.
Mwanadamu si lahisi kufikilia kwamba myama anaweza kuleta nyama,sanasana kunguru,maana yeye anapenda sana nyama.Pia,si lahisi kuelewa jinsi gani hawa kunguru walikuwa wanapokezana ,wengine asubuhi,wengine mchana,wengine wanabeba mkate,wengine wanabeba nyama .Tena tunajua kunguru hana mikono alikuwa anabebea kwa kinywa chake.Lakini katika yote,kusudi la Mungu ni kumlisha mtumishi wake, Elia.
Sasa basi tuseme kwamba Roho wa Mungu alikuwa akitenda kazi ndani ya kunguru hizo?Inawezekana pia malaika wakawa walikuwa wanawaongoza wale kunguru kama walivyofanya kwa ile punda iliyokuwa inampeleka nabii Balaam? Njia za Mungu hazichunguzwi.Tunajifurahisha kutafakari lakini tunajuwa kabisa kwamba ufahamu wetu ni mdogo sana .Mungu ana uwezo wa kusemesha hata mawe akaongea lugha ya wanadamu.Si wajibu wetu kujuwa Mungu amefanyaje.Tunacho zungumzia hapa ni kwamba Bwana ana watumishi wengi sana.Anamtumia yeyote anayetaka haleluia.
2.Punda
Punda (munyama aliyetumika kuzuia kifo cha bwana wake,maana huyu alikuwa ameenda kinyume cha mapenzi ya Mungu)
Balaam aliombwa na mfalme Balaki ili aje amlaanie waisraeli
(Hesabu 22:11)
“Tazama kuna watu waliotoka Msri wanaufunika uso wa nchi ;basi njoo ukanilaanie watu hawa…..”
mst wa 12 unasema
“Mungu akamwambia usiende pamoja nao;wala usiwalaani watu hawa ,maana wamebarikiwa..”
Balaam ameshawishika akaenda lakini Mungu alikuwa amemkataza,
mst wa 22 unasema
“Hasira ya Mungu ikawaka kwa sababu alikwenda ;malaika wa Bwana akajiweka njiani ili kumpinga.Basi alikuwa amepanda punda wake na watumishi wake wawili walikuwa pamoja naye”
Tunasoma kwamba malaika huyo Balaam hakumuona ila punda alimuona .Punda alikatisha njia ili malaika asimpige na upanga lakini Balaam yeye akampiga punda eti anamuendesha vibaya.Alipofika mbele kuliko kuendelea punda akajilaza chini ya Balaam,ndipo Balaam akakasirika sana akampiga kwa fimbo.Bwana akamfumbuwa kinywa punda akongea na Balaam akimuuliza kwa nini anampiga .
Ndugu msomaji wa kitabu hiki ,Mungu alifumbuwa kinywa cha punda ili kitoe ujumbe kwa Balaam,kwamba anaona malaika mbele yake akimuzuia asiendelee na safari.Mungu akamfumbuwa macho akaona vizuri.Alipomuona ameinamisha kichwa na kuanguka kifudifudi ndipo malaika akasema;
“…Tazama nimekuja ili kukupinga,kwa sababu njia yako imepotoka mbele zangu,punda akaniona akageukia upande mbele zangu mara tatu kama asingejiepusha nami bila shaka ningekuua wewe,nikamuacha yeye hai.”(Hesabu 22:32-33).
Tumeona kwamba punda huu ameepusha kifo cha Balaam Mungu amemtumia kwa kumuonyesha yasiyeonekana kwa macho ya kawaida ,akamfumbua kinywa akaongea na bwana wake.Kweli Mungu ni muweza wa yote.
3.Samaki.
Vile vile tunasoma jinsi samaki amemhifadhi mtu wa Mungu Yona akawa ndani ya tumbo la samaki siku tatu
(Yona 1:17).
“Bwana akaweka tayari samaki mkubwa ili ammeze Yona ,naye Yona akawa ndani ya tumbo la samaki yule mda wa siku tatu,mchana na usiku.”
4.Simba.
Pia tunasoma jinsi simba walivyo mchunga mtumishi wa Mungu Daniel usiku kucha
(Daniel 6:22)
“Mungu wangu ametuma malaika wake naye ameyafumba makanwa ya simba nao hawakunidhuru;kwakuwa mbele zake mimi nilionekana sina hatia …”.
Usiseme simba hao labda walikuwa sio wakali hapana maan tunasoma pia jinsi hao hao wamewalaruwa wengine waliotupwa huko kesho yake
(Daniel 6: 24)
“Mfalme akamuru nao wakaleta wale waliomshitaki Daniel ,wakawatupa katika tundu la simba ,wao na watoto wao ,na wake zao ;na wale simba wakawashinda wakaivunja mifupa yao vipande vipande ,kabla hawajafika chini ya tundu.”
Bwana amewatumia simba kuua maadui wa Mungu,na kulinda vizuri mtumishi wake Daniel.
5.Mbweha
Tunasoma tena wanyama mbweha mia tatu .Aliwatumia Samsoni kujilipiza kisasi kwa kuharibu mashamba ya ngano za wafilisti kwa sababu wamemchukulia mkewe na kumuozesha kwa mwingine.
(Waamuzi 15:4)
“Samsoni akaenda akakamata mbweha mia tatu ;kisha akatwaa vienge vya moto akawafunga mbweha mkia kwa mkia,akatia kienge kati ya kila mikia miwili.Alipokwisha kuviwasha moto vile vienge ,akawaachia mbweha kati ya ngano ya wa filisti,akayateketeza matita,na ngano hata na mashamba ya mizeituni.”
6.Nyoka.
Pia tunasoma kwamba Mungu hutumia nyoka kufanya kusudi lake.
“Nao wajapojificha katika kilele cha Karneli,nitawatafuta na kuwatoa huko;na wajapositirika katika vilindi vya bahari nisiwaone,nitamwagiza nyoka huko naye atawauma.(Amosi 9:3).”
Bwana hutumia vitu visivyo na uhai.
Maji.
Kama maji,aliatumia kuangamiza kizazi cha kare kilichomuasi Mungu, kipindi cha Nuhu.Mwa6:17.
“Na tazama nitaleta gharika ya maji yuu ya nchi,niharibu kila kitu chenye mwili na pumzi ya uhai,kisiwepo chini ya mbingu,kila kilichoko duniani kitakufa”
Mwa7:22-23.
“Kila kitu chenye pumzi ya roho ya uhai puani mwake kikafa,kila kilichokuweko katika nchi kavu.kila kilicho hai juu ya uso w anchi kikafutiliwa mbali tangu mwanadamu hata mnyama wa kufugwa,na kitambaacho na ndege wa angani;vilifutiliwa mbali katika nchi,akabaki Nuhu tu na wale waliokuwa pamoja naye ndani ya safina.” tena alitumia upepo kukausha maji wakati gharika ilipo kawia kuishi.
Mwa7:12
”Nvua imenyesha siku 40,mchana na usiku”.
Mwa7:24.”Maji yakapata nguvu juu ya nchi siku 150.
Upepo
Mwa8:1
“Na Mungu akamkumbuka Nuhu,na kila kilicho hai,na wanyama wote waliokuwamo pamoja naye katika safina;Mungu akavumisha upepo juu ya nchi,maji yakapungua.Chemichemi za vilindi zikafungwa,pia na madirisha ya mbinguni,nvua kutoka mbinguni ikazuiliwa.”
Tena tunasoma jinsi Bwana hutumia wanyonge kufanya mambo makubwa.
Wenye ukoma
Wenye ukoma wanne wamefukuza jeshi kubwa la washami likakimbia kwa maana Bwana alikuwa amewasikizisha washami kishindo cha miendo ya magari,na kishindo cha farasi kama kishindo cha jeshi kubwa;Wakaambiana tazama mfalme wa Israeli amewaajiri wafalme wa Wahiti na wafalme wa Wamisri,waje wapigane nasi.Kwa hiyo wakaondoka wakakimbia kungali giza bado wakaziacha hema zao,na farasi zao,na punda zao na kimo chao vile vile kama kilivyo kuwa,wakakimbia wapate kuziponya nafsi zao.”(2Wafalme7:6-7).
Mungu wetu ni mkuu sana ,uweza wake hauna mipaka. Angalia, wenye ukoma ,hawana nguvu miguuni,wanatembea kwa shida,pia ni siku nyingi hawajala chakula,isitoshe ni wachache yaani wa nne tu,lakini Mungu alivyo mkuu,anawafanya waonekane kama jeshi kubwa likiendesha magari na mafarasi mpaka vikasababisha jeshi kubwa la washami kukimbia kwa hofu na kuacha kila kitu.
Mpendwa usijidharau,wewe ni chombo muhimu sana kwa Mungu.Kidogo ulichonacho,ni kikubwa kwa kutenda muujiza.Jinsi ulivyo,uwekilema au mzuri,ue tajili au maskini,ue umepungukiwa akili au kiongozi mkubwa wa nchi elewa kwamba wewe unatosha kwa Bwana kukutumia kutenda mambo makubwa ya kuokoa watu.
Tazama,wenye ukoma wanne,wameonekana kama jeshi la wa falme wa wahiti na jeshi la wafalme wa wamisri! Bwana Mungu wetu uweza wake hauna mfano!
Kumbuka jinsi Mungu alivyomtumia mjakazi wa Namani akamushuhudia akasababisha uponyaji wa ukoma wake.
Ushuhuda.
Sitasahau maishani mwangu jinsi Mungu alivyomtumia kaka mmoja tulipokutana mara ya kwanza kwenye eneo ya kuchapisha vitabu vyangu.Yeye nimemkuta huko akiwa mfanyakazi ndani ya ofisi hiyo ,akasoma vitabu vyangu akavipenda tukaanza kufahamiana hivyo.Kaka huyo aliniambia kwamba nikiwa na tatizo lolote kuhusu uhamiaji anaweza kunisaidia.Nilipomuona, kusema kweli nimeona kwamba hawezi kuwa msaada kwangu.Nimemuona ni mdogo hana marafiki wakubwa.Baadaye nilipata shida nikamwendea akanipeleka kwa rafiki yake akanisaidia na shida yangu ikaisha .Mambo Mungu alipomtumia huyo kijana ,ni makubwa sana kiasi kwamba nimeona kwamba si huyo kijana bali Mungu naona alituma malaika wake.Kweli kila mtu ni kifaa cha muujiza wa Bwana kwa watu wake!
Pia,tumeshasoma jinsi Mungu alivyotumia mjane mmoja kumlisha mtumishi wa Mungu kipindi cha miaka 2.Bwana ametenda miujiza kipindi cha njaa nyingi nchini Bwana alimulisha mtumishi wake kutumia mjane tena maskini.
(2Wafalme 17:9)
“Ondoka uende sarepta,ulio mji wa sidoni ,ukae huko .Tazama nimemwaagiza mwanamke mjane wa huko akulishe.”
Tumesoma vitu vyote ni watumishi wa Mungu.
Utajiri,umaskini,magonjwa,Upepo,maji.mawe,watu,wanyama,n.k.. Bwana anaweza kuvitumia kufanya kusudi lake.
Watumishi wa Mungu wanadamu.
Mtumishi wa Mungu halisi ni yule aliyesikia wito na kuitika.Biblia inatuonyesha kwamba Ibrahim alikuwa mmoja wapo aliposikia sauti ikimwagiza kuacha mji wake na nchi yake nakuenenda mpaka sehemu atakaye muonyesha ,Mungu.Vile vile Musa alisikia sauti ya Mungu ikimuagiza kuchunga wana wa israeli waliyekuwa wakiteswa na farao na kuwakomboa.kila mtu aliyetumwa na Mungu ,alisikia kwanza wito kutoka kwa Mungu.kama wewe ni mtumishi wa Mungu lazima unao shuhuda kuhusu wito wako. Mimi pia najua jinsi Mungu alivyo niita ,nilikuwa wapi,imekuaje ,nimejisikia je ,yote nayakumbuka mpaka leo.Shamba la Mungu ni pana mno. Wote tumeagizwa kufundisha watu habari za Bwana Yesu,ili dunia yote ifahamu kwamba wokovu ni katika yeye pekee.Yesu Kristo ndiye njia ya kweli itakaye tuongoza mpaka mbinguni. Yesu ametuagiza tufundishe wengine kushika amri zake na kuzi tii.Kila mtumishi wa Mungu,anafahamu kwamba ,ndani ya utumishi huo,ziko kazi nyingi.Iko kazi ya Mchungaji(kama ana kanisa),iko kazi ya Mwinjilisti(akizunguka duniya nzima,kanisani au kwenye mikutano ya injili),iko kazi ya Mitume(wakianzisha huduma mbali mbali kila mahali),iko kazi ya Mwalimu (akifundisha ndani ya kanisa,akifanya masemina mbali mbali.),iko kazi ya Nabii(akitoa unabii kanisani ,au sehemu yoyote Bwana anayemwerekeza).Wote hawa ni watumishi wa Mungu wenye karama za kufanya huduma hizo.Na karama hizi zinatoka kwa Bwana mwenyewe.Pia hawa maranyingi ni watumishi wenye wito.
Wapo wengine ,wanafanya kazi ya Mungu (kanisani) kama waimbaji, wenye maombi, mashemasi,na huduma zingine kama kuona wagonjwa ma hospitalini,na kazi zingine kama roho wa Bwana anavyo waagiza kufanya. Kazi hizi ,si lazima uwe na wito,ila unajisikia kupenda kufanya kazi hiyo. Ukijisikia kuimba,unaomba kujiunga na waimbaji fulani,hakuna kulazimishwa kufanya kazi hiyo.
Lakini wito,ni tofauti na kupenda au kujisikia;
Hapa unalazimishwa.Tena wengi wamekataa mpaka Mungu alipo waletea mapigo makali ndipo wakakubali.Kumbuka Musa alisema (mimi siwezi,mimi sijui kusema vizuri,tuma Haruni,n.k) Wengine wanasema (,mimi siwezi,sina elimu,mimi ni mdogo,n.k…) .
Wito unaogopesha,unatisha ! Lakini una raha ndani yake.Ukikubali wito wa Bwana ,unajisikia furaha,amani na utulivu kama vile kuwa kwenye sehemu sahihi.Kazi uliyeitiwa inaendana na kipaji au karama kutoka kwa Bwana.Hatutumiki kwa nguvu zetu au ujuzi wetu,ila kwa uwezo wa Bwana aliye tutuma.Katika kazi yote Bwana aliyekutuma ,ukimwamini yeye utaona kwamba atajidhihilisha kwa kazi yake,na watu watakapotambuwa uwepo wake na nguvu zake watamwamini Bwana,pia na wewe mtumishi wa Mungu utaheshimika.(Kut 14:31)
Watumishi,magugu.
Wapo wengine waliopandwa kama magugu ndani ya ngano.Watu hao, wamewekwa kwa kazi maalum ya mchungaji lakini sio wito wa Mungu kabisa.Wameajiliwa ili wawe kama jicho ya mchungaji ,awe mpelelezi huku akiingia kwenye maombi kumbe sio kuomba bali ni kujua fulani ameongea nini .Watu hao ni hatari kwa kazi ya Mungu,pia ni maadui kwa maendeleo ya kiroho ndani ya kanisa.Watu hao ndiyo wanaoongoza kanisa kwa siri ,maana ndiyo washauri wakubwa wa Mchungaji.Kumbuka hao hawana wito kwa kazi ya Bwana ,lakini sauti yao ndiyo inakubalika.Mungu atuhurumuye sana .Kwa maneno mengine ni wapagani viongozi,au ni watumishi wa shetani ndani ya kanisa la Mungu. Utawatambua kwa matendo yao,wao wako tayari kusema uongo ili mradi tu wasiende kinyume na yule aliyemtuma kazi hiyo. Ndugu mpendwa unayesoma kitabu hiki,usikubali kufanya kazi ya mtu chini ya mafuta ya kanisa.Bora uchaguwe uache kujifanya mtumishi wa Mungu huku ukijua wewe huna ushurika na Mungu wako.Bwana ametuita tumtumikie siyo kulinda uovu wa wachungaji au viongozi wa dini zetu.Wewe hata kama umewekewa mikono na watumishi kuwa mtumishi mwenzao,basi,badirisha fikra zako,ujue kwamba mikono hiyo haijakutuma kutetea uovu na kushindwa kusema kweli wakati wa kweli.
Kumbuka siku ya hukumu Mchungaji hatakutetea,pamoja na kukuonyesha anakupenda kwa sababu za msingi anazozijua yeye.Fikilia jinsi unavyosimama mbele za Mungu wako,fanya kazi ya Mungu kwa uaminifu ,sana sana Linda moyo wako kuliko vyeo vyako.Bwana ni mwaminifu ,ukimrudia na kuacha kutumikia miungu,atakupokea,na kukusamehe kabisa
Mtumishi wa Mungu popote ulipo,,unapaswa kusimama ndani ya kweli siyo kuegamia upande wa mume wako au wa mke wako.Maana sisi tunatakiwa kuwa washauri wa wenzetu “ndani ya kweli”,na kufanya kazi ya Bwana isonge mbele .Kiongozi yeyote,na aelewe kwamba kuwa kiongozi ni kusimamia.Muna shauriana na watumishi wenzako mufanye nini.Si kuendesha kanisa kama nyumba yako au familia yako.Maana vitu hivi viwili ni tofauti kidogo.Kwa familia yako ni wewe na mke wako na watoto,lakini kanisa ,ni wewe kama mchungaji wa kanisa hilo,na viongozi wengine .Lakini mara nyingi unakuta mke wa mchungaji ndiye anaye ongoza kanisa.Ukibahatika kuwa rafiki wa mke wa mchungaji na cheo unapata.Hayo yote ni upungufu mkubwa,unasababisha kanisha lisisonge mbele ,badala ya kuongozwa na Roho ,linaongozwa kimwili,kwasababu misingi ya utumishi ni mibovu.
Tunapata ufunuo wakuombea nyumba za watumishi ili wawe na nia moja katika kutimiza kusudi la Mungu.Mtumishi uwe macho,maana siyo wote wanayeonyesha wanakupenda ndiyo watumishi wazuri,hapana.Waache wakupende lakini Linda sana shamba la Mungu.Omba sana Mungu akuonyeshe ni nani anayestahili kuwekewa mikono? Lakini cha kwanza kabisa wewe mwenyewe kaa ndani ya Kristo,umtumikie kwa uaminifu,ndipo na Bwana atakuwa upande wako na kukuongoza.
Ushuhuda.
Tumeona kwamba vitu vyote ni watumishi wa Bwana.Pia watu wote Mungu anaweza kuwatumia kama chombo.Nimewahi kutumika ndani ya kanisa mmoja kule Afrika.Nchi ya Tanzania.Mimi ni mzaliwa wa Burundi,kule ni mara chache sana kuona mtumishi mwanamke.Unaweza kuwa mwimbaji,muombaji au shemasi.Lakini kuhubili ukiwa mchungaji ,au muinjilisti ,mwalimu ,sijawahi kuviona ndani ya kanisa langu la Burundi.Nilipofika Tanzania,nikaendelea kushirikiana na wengine kwenye ibada,kwenye vipindi vya maombi,na kuonyesha matunda mema ya mkristo.Bwana alikuwa ameniita nimtumikie,lakini kwetu kwa sababu wanawake huduma zao hazijakubalika bado kwetu,nilikuwa na tumika kwa ministri ya wanawake,hapo niliweza kufundisha chini ya kivuli cha ministri hiyo.Lakini ashukuliwe Bwana yeye anawatumishi wengi.Alimtumia mchungaji wa hapo Tanzania akaniteua kuwa mwalimu wa kanisa.Hapo nimemuona Bwana akinitoa kwenye kifungo cha wanawake kuhudumu madhabahuni tukihubili habali njema.Niliporudi kusalimia huko kwetu,wakawa wamejua kwamba mimi ni mwalimu wa kanisa,ndipo,wakanikaribisha vizuri kama mtumishi na kunipa jumapili moja nihubili habali njema.Bwana anazo njia.Anajua ni wapi amekuwekea malaika wa kukufungulia milango.
Utumishi sio ukristo.
Utumishi ni kazi ipatikanao kwa karama.Lakini ukristo ni hali ya mtu ndani ya maisha yake na mwenendo wake ,kulingana na neno la Mungu.Mkristo utamtambua kwa matendo yake.Utumishi kila mtu anaweza kutumika.Lakini si wote watumishi ni wakristo.Kuwa mkristo ni razima uwe umempokea kristo ,uwe umeokoka.Lakini utumishi,hatakama hujaokoka unaweza kutumika kama tulivyoona kwamba vyote ni watumishi wa Mungu.Pia neno la Bwana linasema kwamba hatatukikataa kutumika,Bwana ataamria mawe naye atatumika badala yetu.Kigezo cha ukristo si utumishi,kigezo cha ukristo ni matendo mema na imani katika Bwana Yesu.Lakini,kila mkristo anatakiwa kumtumikia Bwana Mungu.Kwanza kuokoka chapili huduma.
Ushauri wangu kwako Mtumishi.
Utumishi ni sehemu nzuri tuliye pewa na Mungu aliyetuita.Sasa basi kila moja ajiangalie mwenyewe alipofikia ndani ya kazi ya Mungu, na jinsi anavyoifanya.Ukiona umeshindwa,basi eleza watumishi wenzako watakushauri.Maana,wengi sana siku hizi wametoka kwenye sehemu ya wito wa Mungu,wako kwenye mashindano ya wingi wa waumini ,na majengo mazuri tu.Tumurudie Mungu na kunyenyekea,na kuanza upya.Bwana ni mwaminifu atakusaidia na kufufua roho yako na wito wako.Usijifariji mpendwa,Mtumishi wenzangu,Mtakatifu ni Mungu tu,asiyeshindwa ni Bwana peke yake,wewe si wakwanza kushindwa nakugeukia mali kuliko roho za watu,wako wengi sana .Wengi wamepigwa wamekufa hawako tena duniani,nakusii sana, wewe unaesikia maonyo haya ,usiwe na moyo mgumu,bali umgeukie Mungu ukubali makosa yako na ukubali kugeuka na kubadirika.Bwana akubaliki sana.
Tuombe,
Baba Mungu uliye Mbinguni,naja mbele zako nikimleta mtumishi wako huyu aliyesoma ujumbe huu.Mungu nakuomba umpe roho ya kunyenyekea na kukubali maonyo ili Baba, aweze kutubu kwa moyo wake wote, na kukuonyesha pale alipokukosea ,nawe Baba uweze kumrehemu na kumsamehe maovu yake yote.Baba Mungu wewe ni mwenye rehema,ukamrehemu sasa Baba,ukageuze moyo wake,umbadirishe kweli kweli,umrudishe kwenye ile hali aliyekuwa nayo wakati ulipomuita.Bwana mpake mafuta mapya ,ili aendelee kukutumikia kwa uaminifu.Baba asante kwa msamaha wako,na rehema zako. Baba nakuomba kwa uweza wako,wale wote waliyejiingiza kanisani nakujifanya wameokoka kumbe ni wana na watumishi wa ibilisi,Bwana ukawafichuwe ukawaweke wazi ,wasiendelee kuharibu mwili wa Kristo wakijifanya kondoo.Baba,ukawaondoe ,na kuwapa neema ya kukufuata wewe na kuwaokoa.Baba nakuomba,Mchungaji huu,ukamsaidie,umpe
watumishi wenye maarifa ili wasaidiane nae kwa kazi yako.Uwape kutumika katika umoja ,na kuongozwa na Roho
wakoMtakatifu.Baba,naomba pia ukarejeshe na kukarabati pale palipo bomoka (imani,maadili ya kikristo),na kurejesha vile vyote vilivyoibwa na ibilisi(uaminifu,upendo,umoja,utii,unyenyekevu,n,k…..).Naomba
hao katika jina la mwanao Yesu Kristo.Amen
Hasira ;chanzo cha dhambi nyingi.
Ushuda wa mchungaji na mshirika wake.
Mama mmoja alishuhudia kanisani jinsi Bwana Mungu alivyo mpiga kutokana na jeuri na chuki aliye onyesha juu ya kiongozi wake.Alisema hivi;
“Tulikuwa kanisani tukimwabudu Mungu,tulipo maliza mtumishi wa Mungu aliinuka kufundisha.Akaanza kusema kwamba tunatakiwa kupendana kanisani.Akanigeukia akanisogelea ,akanikazia macho na kusema:Ee,Ee mama wewe,nikainua macho nika muangalia maana nilikua nimeinama nasoma biblia.Akasema,(hata ujifanye wa kiroho sana kama humpendi nchungaji wako yote unayo fanya ni bure.Umesikia?)Akaendelea na kusema,nikaumia moyoni sana.Ndipo nikajiuliza nimemukosea nini,baba yangu?Nilitafakali sana juu ya hilo sikupata jibu.Kweli nikagunduwa kwamba alikuwa anamaanisha kwamba simpendi.Lakini mimi kwa sababu nilikuwa nampenda sina shida naye kabisa ,nilielewa kwamba yeye ndiye hanipendi.Basi tangu siku hiyo nikaanza kutompenda tena,nikaanza kumchukia kiasi kwamba nilikuwa natamani tusikutane tena. Namshukuru Mungu,nilipo msimlia mume wangu yaliyonikuta kanisani ,alihuzunika. lakini yeye aliendelea kuonyesha upendo kama kawaida.Alikuwa ananilazimisha kumsalimia na kuendelea kumpenda kama mwanzo lakini imeshindikana.Ndipo siku moja Bwana akanionyesha kwenye maono ya usiku kwamba mimi siko sawa mbele zake Mungu pamoja na mchungaji wangu. Nikauliza kwa nini Mungu?Bwana akasema ,kwa sababu umeingiza chuki na dharau juu ya kiongozi wako.Hapo nili ungama dhambi zangu nikaomba rehema mbele za Mungu. Bwana akanipiga pigo moja mwilini mwangu,liliniumiza siku tatu baada ya hapo Bwana akanirehemu.Nikamuuliza, sasa Bwana niambie,kiongozi wangu naye ametenda kosa gani? Akanipa jibu katika kitabu cha (Yobu 11:2-5)”Je huyu wingi wa maneno usijibiwe?Na mtu aliye jaa maneno Ahesabiwe kuwa na haki? Je,majivuno yako yawanyamanzishe watu wawe kimya?Nawe hapo ufanyapo dhihaka je hakuna mtu atakayekutahayarisha?Kwa kuwa wewe wasema mafunzo yangu ni safi nami ni safi machoni pako.Lakini,laiti Mungu angenena na kuifunua midomo yake juu yako.”
Ndugu mpendwa kulingana na ushuhuda huu wa mama,unaweza ukajitetea wewe ,lakini Bwana anaye ona ndani ya mtu anaelewa ni wapi umekosea. Sasa basi, hebu tujifunze kwa ushuhuda huu,si vema kujenga chuki moyoni mwako ,si vema kufanya dharau juu ya mtu yeyote.Sana sana juu ya kiongozi yeyote,maana neno la Mungu lina tushauri kuwa tii na kuwaheshimu na kuwanyenyekeea ili wafanye kazi ya Bwana kwa furaha.Kiongozi ni lazima apewe heshima zake kama kiongozi.Vile vile ni halali kila kondoo imuheshimu na kumu tii,la sivyo atapata ugumu sana katika kazi hiyo.Na wewe umeitiwa kumusaidia sio kumuwekea uzito na kumusababishia kushindwa katika kazi alioitiwa.
Tuombe
Ee Mungu uliye Mbinguni,tunanyenyekea mbele zako tukikuomba utusamehe makosa yote tuliowafanyia viongozi wetu na kuwasababishia kupata shida juu ya kazi yako.Mungu tufundishe zaidi tujue namna ya kuwasaidia ili kazi yako isonge mbele. Tunakushukuru tukiamini kwamba umetusamehe na utatuwezesha kuchukuliana na viongozi wetu na kufanya kazi kwa pamoja.Tunaomba yote hayo katika jina la mwanao Yesu Kristo.Amen.
Nawe mtumishi wa Mungu si vema utumie nafasi ulionayo kuwajeruhi watoto wako au viongozi wenzako,maana kila mtu ni wa thamani mbele za Mungu. Sisi ni mali ya Mungu mwenyewe.Kama ni kumuonya kwanini usimupeleke kando na kumushauri kwa upendo?Au kama mtu analeta mafundisho ya kupotosha imani ya kweli ya Kristo,hapo tunaruhusiwa kumukemea kabisa ili hiyo roho ya shetani isizae matunda kama alivyofanya Paulo alipokemea yule mchawi alikuwa anazuia liwali asipokee injili.
Tunaruhusiwa kumkemea pepo si wa Kristo wenzetu.Kwa wenzetu tunaingia na roho ya upendo sio kuwakazia macho na kuwazalilisha kanisani.
Yesu nawe alimkemea Roho chafu ilioingia ndani ya Petro .Roho hiyo ilionekana niya huruma lakini ilikuwa inazuia mpango wa Mungu.Yesu aliikemea akasema ;” rudi nyuma shetani maana huyawazi yaliyo ya Mungu bali ya wanadamu.”Kwakuwa mwanafunzi aliingiliwa na roho ya shetani ,Yesu alitambuwa moja kwa moja kwamba si Petro tena bali ni shetani,ndipo akasema (nenda nyuma yangu shetani.) Roho yeyote ya kishetani tuna ruhusiwa kuyikemea na kuyiangamiza maana hii ndio adui yetu
Mchawi huyu Paulo ali mulaani pia akamletea upofu juu yake.Kwa neno la Roho mtakatifu upofu ukamjia na yule liwali akaona ukuu wa Mungu akaamini akaokoka.(Tunasoma habari hiyo katika kitabu cha Mdo13:9-11). Si kila laana kutoka kwa mtumishi linafanikiwa,bali ni lile tu lililosukumwa na Roho mtakatifu ,maana Mungu ndiye anatambuwa ndani ya moyo wa mwanadamu.
Yohana aliandika katika barua yake ya pili
(2Yohana 1:10-11)
“ kwamba mtu akija kwenu naye haleti mafundisho hayo,msimkaribishe nyumbani mwenu,wala msimpe salamu.Maana yeye ampaye salamu azishiriki kazi zake mbovu”.
(2Yohana1:7)
“Kwa maana wadanganyifu wengi wametokea duniani wasio kiri kwamba Yesu Kristo yuaja katika mwili .Huyo ndiye mdanganyifu na mpinga Kristo”.
Kiongozi anatakiwa kuwa makini sana kwa mafundisho .Lakini kama ni mtu amekosea katika kufundisha akachanganya kidogo kwa kuelewa kwake kudogo,usimuseme mbele ya kanisa bali mweke pembeni umufundishe zaidi ,umufahamishe naye atafurahi.
Mtu akijiona kuwa ni nabii au mtu wa rohoni na ayatambuwe hayo niliyo waandikia,ya kwamba ni maagizo ya Bwana.Lakini mtu akiwa mjinga na awe mjinga.(1Korinto14:37-38)
Ndugu msomaji wa kitabu hiki, hasira ni kifaa kikubwa cha matengano,kama ulivyo ona ndani ya shuhuda hapo juu.Mchungaji kutengana na mshirika wake,sababu kubwa ni hasira.Baada ya hapo ilizaa chuki,jeuri n.k. Kilichohitajika kwa haraka ni (upatano) wa watu hao wawili,ili amani iwepo. Hapa njia ya upatanisho ililetwa na Mungu mwenyewe,kwa kumpiga yule mshirika na ugonjwa wa siku tatu,ili amfundishe kwamba anatakiwa kutubu
maana chuki ni dhambi maana ni uuaji,Biblia inasema.
Kupitia pigo hilo,alitubu kwa Mungu akasamehewa,amani ikarudi. Hasira ni mbaya sana inamadhara mengi sana kama tulivyoona.Hasira inapeleka mtu gehanamu,vile vile inauwa sana,wengi wamejinyonga kwa sababu ya hasira.Nakutakia ndugu mpendwa tunda la uvumilivu na upole,ndipo utakaposhinda hasira.Uvumilivu utakuzawadia unyenyekevu,hata ukionewa usivitie moyoni ,kumbuka kwamba Yesu
“ Alionewa lakini alinyenyekea.Wala hakufunua kinywa chake.kama mwana-kondoo apelekwaye machinjoni ,na kama vile kondoo anyamazavyo mbele yao wakatao manyoya yake;naam,hakufunua kinywa chake”.(Yesaya53:7)
Tuombe
Ee Mungu uliye hai,naja mbele zako nikiwaleta watumishi wako hawa waliosababisha kondoo kujeruhiwa na kuumizwa.Mungu nakusihi uwasamehe makosa yao yote walioyafanya kwa kujua kwa sababu ya hasira au walioyafanya bila kujua.Nakuomba Uwarehemu kwa kuwa wewe ni mwingi wa rehema.Nakushukuru kwamba umewasamehe ,naomba hayo kwa jina la mwanao Yesu Kristo,Bwana na Mwokozi wetu Amen.
Hasira ni mbaya sana na neno la Mungu linatushauri tuache kukasirika
Maana yeye aonaye hasira kwa upesi atatenda kwa ujinga(Mithali14:17)
Mtunga zaburi naye amesema (usikasirike mwishoe utatenda mabaya.(Zaburi 37:8)
Sulemani akaona kwamba asiye mwepesi wa hasira ni mwema kuliko shujaa;na mtu aitawalaye roho yake, ni mwema kuliko mtu atekae mji.(Mithali16:32).
Paulo naye anamwandikia Tito kwamba kiongozi wa dini anatakiwa kuwa si mwepesi wa hasira,au mgomvi au mlevi,bali awe mpenda wema,mwenye kiasi na mwenye haki,mtakatifu,mwenye kudhibiti nafsi yake.(Tito 1:7-8).
Yesu Kristo naye,anasema,kila mtu amuoneae ndugu yake hasira,itampasa hukumu,na mtu amfyoleae ndugu yake ,itampasa baraza,na mtu akimwapiza itampasa kwenda jehanamu ya moto.(Mathayo 5:22)
Yakobo naye anashauri watu wawe wepesi kusikia,bali si wepesi wa kusema ,wala kukasirika .Kwa maana hasira ya mwanadamu haitendi haki ya Mungu. (Yakobo 1:19-20) .
Ushauri kwa watu wote.
Nami nakushauri , ndugu msomaji uache hasira,ujipatie jina lenye sifa nzuri,maana usipo acha utaitwa (Hasira).
Kuna mfano mzuri aliye onyesha Stefano wakati walikuwa wakimpiga.Yeye alipigwa kwa mawe, lakini yeye,alipiga magoti yake na kuwaombea ili Mungu asihesabu dhambi hio,bali awasamehe.(Mdo 7:59-60).
Mfano mwingine,Bwana Yesu wakati walikuwa wanampiga mawe wayahudi,aliwambia,
“kazi njema niliwaonyesha zitokazo kwa Mungu,kwa lipi sasa mnataka kunitupia mawe? Wakajibu ,kwa sababu umejiita kwamba wewe ni Mungu.Naye akasema,ikiwa aliwaita miungu wale waliojiliwa na neno la Mungu;(na maandiko hayawezi kutanguka);je!yeye ambaye Baba alimtakasa,akamtuma ulimwenguni,ninyi mnamwambia unakufuru,kwa sababu nalisema mimi ni mwana wa Mungu?(Yohana 10:32-36)”
Yesu,hajakasirika,lakini aliwauliza kwa upole.
Stefano yeye hajauliza chochote bali aliwaombea tu.
Na wewe ujue kwamba Mungu atakutetea ukimtumaini .Bwana atawasha hasira zake kwa adui za wachaMungu.
“Bwana uondoke kwa hasira yako ;ujiinue juu ya jeuri ya watesi wangu;uamke kwa ajili yangu;umeamuru hukumu.”(Zab 7:6)
Bwana wetu ni mwema,tena ni mwenye nguvu.Atapigana na adui zetu atatushindia vita.Usikasirike,maana wewe una Mungu .Kwa kila jambo muonyeshe Bwana.Usipige kelele,bali mueleze Mungu atakusaidia.
Paulo naye anawaandikia waefeso eti
“ wawe na hasira lakini wasitende dhambi.Jua lisichwe na uchungu wenu bado haujawatoka;wala wasimpe ibilisi nafasi.”
Efeso 4:26-27,31&zab4:4
Ushauri
Nami nakuandikia mpendwa nikikukumbusha kwamba siku ya Bwana I karibu,wewe kama kiongozi wa kanisa ,jitahidi kuwa kiongozi mwema ili washirika wajivuniye uchungaji wako.Usiache kuwaonya tena kwa ukali ili waache dhambi zao.Ukilegeza msimamo wa injili utadaiwa wewe kama kiongozi.Usiwahurumie kwa kuficha ukweli ,wewe sema ukibaki na wachache basi lakini hakikisha wana msimamo mzuri ndani ya Kristo.Neno linasema
“Na yeyote atakayemkosesha mmoja wapo wa wadogo hawa waniaminio,afadhali afungiwe jiwe la kusagia shingoni mwake,na kutupwa baharini.Na mkono wako ukikukosesha,ukate;ni afadhali kuingia katika uzima u kigutu,kuliko kuwa na mikono miwili na kwenda zako jehanum,kwenye moto usiozimika.”(Marko 9:42-43).
Usikubali kitu chochote kinacho weza kukukosesha mbingu.Ukipinge kwa nguvu zote kabisa.
Nakukumbusha hivi,hakuna kitu cha thamani kuliko kuumaliza mwendo wako na huduma ile uliopokea kwa Bwana Yesu, kuishuhudia Habali njema ya neema ya Mungu.Kwa hiyo nawashuhudia wote siku hii ya leo ,ya kuwa mimi sina hatia kwa damu ya mtu awaye yote. Kwa maana sikujiepusha na kuwahubiria habari ya kusudi lote la Mungu.Sasa basi enyi watumishi wa Bwana ,Jitunzeni nafsi zenu,na lile kundi lote nalo,ambalo Roho mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi ndani yake mpate kulilisha kanisa lake Mungu,alilolinunua kwa damu yake mwenyewe.Amen (Matendo 20:24-28).
Kwa kuwa hao ni watumishi wangu ,niliowaleta watoke nchi ya Misri;wasiuzwe mfano wa watumwa.Usitawale juu yake kwa nguvu;ila umche Mungu wako ”.(Walawi 25:42-43).
Mungu akubariki mtumishi wa Mungu.
Sura ya2
Huduma ya Unabii.
Napenda tujifunze kidogo kwa watumishi wanadamu wafanyae kazi ya unabii.Watumishi hawa ni watu kama wewe na mimi,lakini wanatoa ujumbe kutoka kwa Bwana na kutuletea.Wanaweza wakatumika kanisani au popote Mungu anae watuma.
Hapa,tutazungumzia kuhusu Nabii,kama mtumishi wa Mungu.
Nabii ni mtu anayepeleka ujumbe wa Mungu kwa wanadamu.
Ni mtumishi wa Mungu kwa kanisa,kwa nchi,kwa familia au kwa mtu binafsi au kwa kundi la watu.
Nabii,ni mtu kama wengine lakini anawakilisha siri za Mungu kwa watu wake.Nabii ni mtu mwenye karama ya unabi.Na karama ni neema ya Mungu iliopo ndani ya roho mtakatifu.Ukipokea roho mtakatifu zipo karama mbali mbali Bwana anazotuwekea kulingana na mapenzi yake Bwana. Watu sasa wana karama tofauti,mfano,karama ya kuponya magonjwa,karama ya unabi,karama ya kufundisha ,n.k.
Hebu tuangalie kuhusu nabii.
Nabii mkuu wa wote ni “BWANA YESU KRISTO »Yeye alitumwa na MUNGU kwetu wanadamu. Alituletea unabii : « NENO LA MUNGU ».
Wapo manabii wengine tunawasoma katika kitabu cha Ufunuo wa Yohana 19 :10
« Nami nikaanguka mbele ya miguu yake,ili nimsujudie ;akaniambia,Angalia,usifanye hivi ;mimi ni mjoli wako na wa ndugu zako walio na ushuhuda wa Yesu.Msujudie Mungu.Kwa maana ushuhuda wa Yesu ndio roho ya unabii. »
« Ushuhuda wa Yesu, ndio roho ya unabii. »
sasa wote walio na ushuhuda huo ni : “manabii”.
wote walio na unabii ni manabii.Au kwa maneno mengine wote wanaye hubili habali njema ya Yesu hapo wanatoa “unabii”.Anayetoa unabii anaitwa nabii.Hapa tunazungumzia nabii au unabii wa Mungu. Anaye fundisha habari za mtu mwingine nje ya Bilia maandiko matakatifu ,huyo si nabii wa Mungu. Maana Biblia kitabu cha Neno la Mungu ndicho kimejaa “unabii wa Mungu.”
Soma Ufu 22:7 “Na tazama,naja upesi,heri yeye ayashikaye maneno ya unabii wa kitabu hiki.”
Mst 18 “Namshuhudia kila mtu ayasikiaye maneno ya unabii wa kitabu hiki,Mtu yeyote akiongeza,Mungu atamwongezea hayo mapigo yalioandikwa katika kitabu hiki.”Tunaruhusiwa kuchunguza unabii ili tuone kwamba haupingani na maandiko matakatifu.Biblia inatupa tahadhali kwamba;
“Na ma nabii wa uongo watatokea na kudanganya wengi.”Mathayo 24:11.
Mathayo 24:24 “Kwa maana watatokea makristo wa uongo,na manabii wa uongo,nao watatoa ishara kubwa na maajabu;wapate kuwapoteza,kama yamkini,hata walio wateule.Basi wakiwaambia yuko jangwani ,msitoke,yuko nyumbani ,msisadiki.Kwa maana kama vile umeme utokavyo mashariki ukaonekana hata magharibi,hivyo ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake mwana wa Adamu.”
Mfano,kama mtu akinijia na kuniambia kwamba Mungu amemtuma kwangu aniambie kwamba;( siku ya kuja kwake yesu ni kesho saa 3 usiku).Hapo moja kwamoja nitamkemea maana si kweli ,Neno la Mungu linasema kwamba atakuja
kama mwivi.Hakuna anayejua siku wala saa ya kuja kwake.
Lakini hatakama hatujui siku au saa tunaona dalili za kuja kwake
kama Biblia inavyo zitaja.
Mfano wa dalili ya kuja kwake Yesu
,Mathayo 24:6-14 “Nanyi mtasikia habari za vita na matetesi ya vita;angalieni msitishwe;maana hayo hayanabudi kutukia,lakini ule mwisho bado.Kwa maana taifa litaondoka kupigana na taifa,na ufalme kupigana na ufalme;kutakuwa na njaa,na matetemeko ya nchi mahali mahali.Hayo yote ndio mwanzo wa utungu”.
Mathayo 24:14 “Tena habari njema itahubiriwa katika ulimwengu wote,kuwa ushuhuda kwa mataifa yote;hapo ndipo ule mwisho utakapo kuja.”
Tumesema kwamba nabii,ni mtu au niseme mtumishi wa Mungu anyetumwa na Mungu kwa watu mbali mbali.
Ujumbe unatoka kwa Bwana.Unaweza ukawa ujumbe wenye kukufurahisha,mfano tumeuona pale malaika alipotumwa na Bwana kwa Zakaria kumwambia kwamba atapata mtoto wa kiume.Akaambiwa tena na kazi atakayeifanya. Mara nyingi ukipereka ujumbe mzuri wenye kufurahisha ,watu wanakupenda sana.
Nabii,akitumwa kumwambia mtu habari mbaya,anachukiwa kama vile ni yeye ameyafanya. Hapa tunapata mwaliko wa kuwaombea sana wenye karama hiyo.Maana Mungu anaweza akakutuma kwa watu kama alivyo mtuma Mussa kwa wana wa israeli eti Mungu amewaona kilio chao atawatowa kwa farao,Musa kweli aliwaendea na kuwafikishia ujumbe. Tena hata kwa farao alienda akasema kama vile Bwana alivyo muagiza. Musa alitazamia kuona farao akitetemeka na kuachilia wana wa israel waondoke. Badala ya kuwaachilia aliwaangamiza zaidi,na kuzidisha kazi zao ili wachoke .Farao aliona kwamba ni maneno ya uongo.
(Kutoka 5:6-9),
” Na siku ile Farao akawaamuru wasimamizi wa watu ,na wanyapara wao,akisema,msiwape watu tena majani ya kufanyia matofali,kama mlivyofanya tangu hapo;na waende watafute majani wenyewe.Lakini hesabu ya matofali waliokuwa wakifanya tokea hapo,wawekeeni hiyo hiyo msiipunguze hata kidogo,kwa maana ni wavivu hao;kwa hiyo wanapiga kelele wakisema tupe ruhusa tuende kumtolea Mungu dhabihu.Wapeeni watu kazi nzito zaidi,waitaabikie;wala wasiangalie maneno ya uongo.”
Musa alihuzunika kuona msimamo wa Farao.Alitazamia kuona mabadiliko mazuri,lakini anaona maangamizo makubwa.
Vile vile watu walimgeukia Musa na kumtukana sana.
(Kutoka 5 :20-21)
« Wakakutana na Musa na Haruni, waliokuwa wanasimama njiani,hapo walipotoka kwa farao ;wakawaambia ,Bwana awaangalie na kuamua ;kwa kuwa mmefanya harufu yetu kuwa chukizo mbele ya farao,na mbele ya watumishi wake,mkatia upanga mikononi mwao,watuue. »
Musa mtumishi wa Bwana akarudi kwa Mungu na kuuliza kwana nini mambo amekuwa mabaya zaidi.
Kutoka 5 :22.
« Musa akarudi kwa Bwana ,akasema,Bwana,mbona umewatenda mabaya watu hawa? Kwani kunituma mimi ? Kwamaana tangu nilipokwenda kwa farao, kusema naye kwa jina lako ,amewatenda mabaya watu hawa ; wala hukuwaokoa watu wako hata kidogo. »
Nabii yeyote akiona mambo anakwenda kinyume na ujumbe wake lazima aulize Mungu tena kwa nini. Kweli watu watakutukana eti wewe ni nabii wa uongo,watakushambulia na maneno kama walivyofanya kwa Musa,lakini wewe uliza Mungu nawewe ili akujulishe kwa nini imekuwa hivyo.
Mumgu alimjibu mtumishi wake.
Kutoka 6 :6
« Basi waambie wana wa israeli, mimi ni Yehova ,nami nitawaotoa ninyi mtoke chini ya mizigo ya wa misri,nami nitawaokoa na utumwa wao,nami nitawakomboa kwa mkono uliyonyoshwa na kwa hukumu kubwa.Nami nitawatwaeni kuwa watu wangu,nitakuwa Mungu kwenu ;nanyi mtajua kwamba mimi ni Jehova,Mungu wenu niwatoaye mtoke chini ya mizigo ya wa misri. »
Musa alipo rudisha ujumbe tena kwa watu,ulikuwa ujumbe mzito,wa kutia moyo nawa kufurahisha.Musa mwenyewe naamini alifurahi kusikia kwamba watakombolewa kwa mkono uliyenyoshwa na kwa hukumu kubwa. Musa alikuwa anajua kwamba Bwana atafanya hayo maana hasemi uongo hata siku moja. Chakushangaza alipo peleka ujumbe,mtamu namna hiyo,hawakusikiliza.
Kutoka 6 :9
« Musa akawambia wana wa israeli maneno haya ;lakini hawakumsikiliza Musa kwa ajili ya uchungu wa moyo, na kwa ajili ya utumwa mgumu. »
Mtumishi,kama wewe,ungekuwa Musa ungefanyaje tena ?
Siri ni moja tu,unarudi tena kwa Bwana ili akwambie ufanye nini tena.
Siku zote Bwana anatafuta mtu mwenye utayali moyoni mwake ili atende kazi yake.Nabii ni chombo cha Bwana ili Mungu akitumie kusema na watu,au kuwatendea makuu. Nabii yeye anatakiwa kufanya kama Bwana anavyomuagiza kufanya.
Musa aliagizwa tena arudi kwa Farao na kumwambia aachilie wana wa israeli. Jambo hilo lilikuwa gumu kwa Musa,kurudi kwa Farao,wakati alikumbuka jinsi alivyozidisha mateso kwao,aliposikia ujumbe tu. Tena alikumbuka jinsi wana wa israeli walivyokataa ujumbe kwa sababu ya uchungu wao mwingi.
Musa alipata shida sana kukubali. Hapa alionyesha kwamba ni mtu mwenye woga kama mimi na wewe. Lakini Bwana aliongea nae tena akamsisitia ili awaendee bila kuogopa ili Bwana aweze kutenda makuu.
Kutoka 6:13.
”Bwana akanena na Musa na Haruni,akawaagiza wawaendee wana wa israeli na Farao mfalme wa Misri,ili awatoe hao wana wa israeli katika nchi ya Misri”
Nabii anatakiwa kusema ili,Bwana afanye kitu. Nabii anaye funguo ,anatakiwa kutoogopa watu au vitishio vyo vyote bali amsikilize Mungu na kumtii.
Tangu zamani watu walikuwa wakiwaendea manabii ili wajuwe ufumbuzi wa shida zao. Mungu alikuwa anaongea na watu kupitia nabii. Zamani nabii alikuwa anaheshimika .
Mungu alimwambia Musa,
Kutoka 7:1
”Bwana akamwambia Musa,angalia nimekufanya wewe kuwa kama Mungu kwa Farao;na huyo ndugu yako Haruni atakuwa nabii wako.”
Ndugu,msomaji wa kitabu hiki, nabii ni mtumishi kama wewe na mimi,tuombeane ili kila mtu afanye kama alivyoagizwa na Bwana.
Wewe kama ni nabii,nakushauri,usitende kwa mazoea.Kila jambo muulize Bwana.Kama hajakujibu,subiri usije ukasema Bwana amesema kumbe hajasema nawewe kuhusu jambo hilo.!!
Lakini Mungu ni mwaminifu,kama anaona watu watakuja kuuliza jambo fulani,mara nyingi Bwana anakujulisha kabla.
Tuangalie jinsi nabii Elia alivyotenda maishani mwake ili tujifunze zaidi.
Nabii Elia.
1. Nabii Elia ni mtu wa kijiji cha Tislabe huko Gileadi.Ni nabii wa miaka 800 kabla ya Yesu Kristo.Alikua kati ya wale manabii walioondoka duniani kwa njia pekee( Enoko, mwanzo 5:24) Musa (Kumb 4:5-7) Elia (2 waf 2:11).
Pia Elia alitokea wakati wa Yesu kubadilika sura kule mlimani,hata mtume Petro alitaka wajenge vibanda 3,kimoja cha Musa ,cha pili cha Elia,na cha tatu cha Yesu(Luka 9:33)
2. Elia alitumikia sana siku za Ahabu mfalme wa Israel.Ahabu alikua anamjua Mungu wa kweli,lakini alioa mke(Yezebeli), huyu alikua anaabudu miungu.Alipo olewa na Ahabu,aliomba ajengewe hekalu la miungu yake.,hivyo vikamchukiza sana Mungu.Ndipo akatumwa sasa Elia kuleta ukame katika nchi yote.
(1 waf 17:1)
“Basi Elia wa mtishbi,wageni wa Gileadi,akamwambia Ahabu,kama Bwana,Mungu wa Israeli,aishivyo,ambaye ninasimama mbele zake,hakutakuwa na umande wala mvua miaka hii,ila kwa neno langu”.
Tafsili nyingine inasema,”Ninaapa kwa mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli alie hai…. Hakutakua na mvua mpaka nitakapo toa amri.Elia alikuwa nabii.Nabii tu mwenye kipawa cha unabii.
Paulo anasema tujitahidi kuwa na upendo,tufanye bidii kupata vipaji vingine vya kiroho,hasa kipaji cha kutangaza ujumbe wa Mungu.(1 kor 14:1)
Unabii ni kutangaza ujumbe wa Mungu iwe kwa kanisa,kwa mtu binafsi,kwa taifa .Elia alisema unabii kwa Ahabu wa kuleta ukame.Alisema mpaka nitakapo toa amri,alisema naapa kwa mwenyezi Mungu alie hai.
Haya maneno Elia anasema lakini ni maneno yake Mungu Mwenyewe.Ni kama mtu analeta ujumbe kutoka kwa mtu mwingine.Uzito wa ujumbe ni; kule unakotoka,na ujumbe wenyewe . Nabii ni kama mtumwa tu.
Elia alipotangaza ukame kwa nchi nzima yeye hajafikiria kwamba na yeye atahusika kukosa maji au tatizo hilo hajajua
kwamba nayeye litamkuta.Lakini Mungu kila wakati,anawasaidia watumishi wake.Mungu alimwambia aende akajifiche kwenye mto wa maji.
Unabii wa nabii Elia.
Mungu akamwambia Elia,Ondoka hapa uelekee mashariki ya mto Yordani.Itakuwa utakunywa maji ya kile kijito,nami nimemwamuru kunguru wakulishe hapo.(1waf 17:2-4).
Elia anatii ujumbe.Alienda kukaa pale peke yake akijua kwamba hayo ni mapenzi ya Mungu kwake .
Ujumbe huu unafurahisha.Tatizo la Elia alikuwa anahitaji maji, sana sana chakula.Alimwahidi atakula.Bwana akasema nimemwagiza.Kama Bwana amefanya hakuna wa kukataa.Tunapaswa kuamini maneno ya
unabii . Huo mji wa Sarepta,ulikuwa na tatizo la njaa sana Elia naye alikuwa na njaa na kiu.Alipoingia kwenye mji huo,akamkuta mwanamke huo wakasalimiana,wakapeana habari ndipo Elia akamwomba amletee maji.Pamoja na njaa ya mji huo,akamwagiza amletee na mkate maana alijua kwamba anaweza akawa na kitu kwa sababu alikuwa anaokota kuni.Alikuwa na unga kidogo lakini Mungu akamtumia sana akamlisha mtumishi wa Mungu.
Mtumishi akasema nifanyie kwanza mimi kisha mjifanyie ninyi.
(1 waf17:13).
Ukimtanguliza Mungu utabarikiwa,ukijitanguliza wewe utaishiwa.
Ukitoa fungu la kumi ,zilizobaki zitabarikiwa na Bwana.
Hii ni siri ya Mungu.
Mama mjane alisikiliza mtumishi akisema ,
« Kwa kuwa Bwana,Mungu wa Israel asema hivi,lile pipa la unga halitapunguka,wala lile chupa la mafuta halitaisha hata siku ile Bwana atakapoleta mvua juu ya nchi ».(1fal 17:14).
Utii
Mjane akatii na kukubali unabii.Hakika alishangaa sana kwa upendo wa Mungu kwake mstari wa 13, unasema « usiogope » yapo mambo mengi ya kuogopesha.Ukiambiwa, leta, wakati una kidogo, si utaogopa kwamba kidogo kitaisha ?Na hapo utakufa na njaa?
Mjane huyo alifurahia kusikia kwamba unga hautapunguka,na mafuta hayataisha.Ali tii,nakumfanyia mgeni chakula bila wasiwasi.Biblia inasema
(1Wafalme 17 :16)
« lile pipa la unga halikupunguka ,wala lile chupa la mafuta haikuisha ,sawasawa na neno la Bwana alilolinena kwa kinywa cha Eliya ».
Kutii maneno ya unabii vimemletea muujiza wa kupata chakula cha siku nyingi kinacho mtosheleza yeye na mtoto wake pamoja na mgeni wake.
Mstari wa 15 unasema
« Basi akaenda akafanya kama alivyosema Eliya ;na yeye mwenyewe ,na Eliya,na nyumba yake ,wakala siku nyingi. »
Bwana alicho sema atakitimiza,maana hasemi uongo.Tuamini unabii wa Mungu.Mungu anazungumza na wanawe kupitia njia nyingi sana sana unabii.
Mjane alikumbuka maneno haya ;
“usimuonee mgeni wala kumtendea jeuri.Kwa kuwa ninyi mlikua wageni katika nchi ya Misri.”
(Kutoka 22:21).
Pia,mjane huyu,ametimiza agizo la Bwana linalosema hivi;
“Msisahau kuwafadhili wageni.” (Hebr 13:2)
Eliya mtumishi wa Mungu, aliishi vizuri na mjane huo.Alizingatia sharti za kukaa na mjane.Alitimiza agizo la Bwana kuhusu namna ya ku kaa na wajane waliyefiwa na waume zao.Biblia inasema maneno haya :
“usimtese mjane yeyote aliyefiwa na mmewe; wala mtoto yatima.”
(kut 22:22).
Neno la Mungu linasema kwamba sisi ni vyombo vya Bwana.Mjane yeyote aliye okoka,ni tajili.Na Bwana anamletea wenye mahitaji wengi naye anawasaidia.Kwakuwa Bwana mwenyewe amejitambulisha kwamba ni mume wa wajane,pia ni Baba wa yatima.Na njia nzuri yenye baraka na mafanikio hapa duniani ni kuwekeza mali zako kwa kuwasaidia wajane na yatima kwenye mahitaji yao.
Biblia inasema;
“Heri amkumbukaye mnyonge;Bwana atamuokoa siku ya taabu.”Zaburi 41:1.
Dini iliyosafi,isiyo na taka mbele za Mungu,ni hii,kwenda kuwatazama yatima na wajane kwenye dhiki yao. Yakobo 1:27
Basi Elia alikaa kwa mjane huo miaka miwili . Mungu akamtuma tena arudi kwao akamuone mfalme Ahabu.Kama tulivyosema,nabii Elia alikuwa mtii sana kwa Mungu.Alikubali kurudi kumuona mfalme Ahabu.Hakuogopa kitu bali aliweka tumaini lake kwa neno la Mungu.Kama mtu yeyote hatii maneno ya unabii hawezi kuona mafanikio.Kutii ni muhimu sana.
Usiogope
Hili neno linaleta faraja sana.Linarudisha nguvu na matumaini.Kama vile Bwana amesema kwamba vitu vyote ni watumishi wake ,vile vile anavitia moyo vyote.(Wanyama wanaambiwa,watu ,nchi ,n.k)
Wanyama wanaambiwa wasiogope
(Yoeli 2:23)22)
“Msiogope enyi wanyama wa kondeni ,maana malisho ya jangwani yanatoa miche na huo mti unazaa matunda yake,mtini na mzabibu unatoa nguvu zake.”
Kuogopa ni matokeo ya kukata tamaa.Neno la unabii linaleta matumaini.Adamu na Hawa walivunja amri ya Mungu kisha wakaogopa
(Mwa 3:10).Matokeo ya dhambi wamekuwa uchi.
Mungu alimtokea Isaka akamwambia asiogope kwa kuwa Mungu yu pamoja naye.(Mwa 26:24).
Nchi inaambiwa isiogope
(Yoeli 2:21).
“Ee nchi usiogope;furahi na kushangilia;kwa kuwa Bwana ametenda mambo makuu.”
Bwana ndie anisaidiae sitaogopa kitu,Mwanadamu atanitenda nini?(Hebrania 13:6)
Ukarimu
Ukarimu wa mjane umemletea chakula cha siku nyingi.Amekaribisha mtumishi nyumbani mwake kama vile kumkaribisha Malaika wa Mungu
(Hebrania13:2).
« Msisahau kuwafadhili wageni,maana kwa jinsi hii wengine wamekaribisha Malaika pasipo kujua ».Mjane huyo,alitunza vizuri mtumishi wa Mungu Elia.
(Yakobo 4:17))
« .Basi yeye ajuaye kutenda mema wala hayatendi kwake huyu ni dhambi ».
Usimpotoshe mgeni asipate haki yake.(Malaki 3:5)
Tupende kuwasaidia wenye mahitaji na Bwana atashugulika na shida zetu.Kutunza wageni ni huduma,tufanye yote bila mang’uniko,usiku waja hatutaweza kufanya kazi tena.
Kifupi Nabii ni mtu kama wewe lakini amejaliwa kuwa na karama ya unabii.Karama haimanishi kwamba wewe ni mtakatifu kulikowengine.Vile vile nabii hajui vyote,anajua yale tu Mungu kamfunulia kwa manufaa ya wengine.Usiache kumhubilia nabii.Na yeye anahitaji kurekebishwa na kusaidiwa kama wengine.
Ushuhuda.
Siku moja,tumebahatika kutembelewa na nabii mmoja nyumbani kwetu.Mugeni huyo tulimuona kwamba ni mtu wa kawaida,kama watumishi wengine.Akatusomea neno la Mungu kidogo akaongea kuhusu neno hilo baada ya hapo tukaagana akaondoka.Yote aliyetwambia katika ujumbe wake kupitia neno hilo ,vimetimia masaha machache tu alipoachana nasi.Tukarudia kusoma yale yote aliyetwambia tukaona yote yametokea vile vile.Ndipo tukaamini kwamba kumbe alikuwa nabii wa Bwana.Siku nyingine alirudi kututembelea pamoja na mke wake,tukafurahi kumpa ushuhuda wa mambo jinsi alivyotokea kulingana na ujumbe wake.Nasi tukamshuhudia maisha ya ndoa jinsi mke na mme Bwana amewaweka wawe kitu kimoja tena waheshimiane.Ukitenda dhambi utubu ,ukitenda dhambi ya uzinzi ni lazima utubu kwa Mungu pia kwa mwenzako,maana umemkosea kwa kutoa mwili wake kwa wengine,ni kumdharau na kumuaibisha. Ni lazima utubu kwake pia.Nabii huyo,aliposikia hayo akakili kwamba alikuwa hajui jinsi ya kutubia dhambi hiyo,akamuita mke wake wakajiweka mbali nasi kidogo akatubu kwake wote wakaombana msamaha .Ndipo nilipo gundua kwamba nabii ni mtu wa kawaida kama sisi lakini mwenye karama ya unabi.
Biblia inatuonya kuhusu unabii .Tunapaswa kuuchunguza(kuangalia kwamba haupingane na neno la Mungu.),na kuwutii.Maana usipo tii,utaangamiya.Mungu anatuonya kutumia manabii,kutumia neno lake,kutumia ndoto n.k…lakini zaidi ya yote tutii yeye atuonyaye
Waebrania12 : 25
“ Angalieni msimkataye yeye anenaye,maana ikiwa hawakuokoka wale waliomkataa yeye aliye waonya juu ya nchi ,zaidi sana hatutaokoka sisi tukijiepusha na yeye atuonyaye kutoka mbinguni.”
Bira msaada wa Mungu ni vigumu mwanadamu kujitambua,maana,moyo wa mtu unamdanganya sana.Hata macho yetu hayaoni vizuri,maana ukitumia miwani ya dunia hii,unaona kama dunia inavyoona,lakini ukitumia miwani ya roho wa Mungu,utaona kama Bwana aonavyo.Sasa basi,ili tuone vizuri,inatupasa kuvaa miwani ya rohoni,maana yake,kuchunguza mienendo yetu kama tunaenda kama neno la Bwana linalosema.Tusiangalie,nchi yangu inafanyaje,au wanao nizunguka wanafanyaje.Bali niangalie ,kwa hili ,neno la Bwana linasema je?Maana hukumu ya Bwana itafanyika ikifuata sheria ya neno la Mungu na maagizo ya Mungu tuliyewekewa.Bwana atusaidie tutende sawasawa na neno lake.
Zaburi39:6
“Binadamu huenda huko na huko kama kivuli;hufanya ghasia tu kwa ajili ya ubatili ;huweka akiba wala hajui ninani atakayeichukua.”
Bali ,
“ Heri aliye mfanya Bwana kuwa tumaini lake,wala hakuwaelekea wenye kiburi,wala hao wanogeukia uongo.”Zaburi 40:4.
Kila siku utafute kumpendezesha Mungu wetu kwa kufanya mapenzi yake.
“Kuyafanya mapenzi yako Ee Mungu wangu ndio furaha yangu;Naam ,sheria yako imo moyoni mwangu.”Zaburi 40:8.
Sura3
Utoaji
Tuangalie huduma ya Utoaji.
Kwa nini tutoe?
Zipo sababu nyingi za kutufanya tumtolee Bwana aliyetukomboa.
· Kwa sababu Mungu ametubariki. “Na Mungu aweza kuwajaza kila neema kwa wingi,ili ninyi mukiwa na riziki za kila namna siku zote ,mpate kuzidi sana katika kila tendo jema.”2kor 9:8.
· Kwa sababu tunataka kuwatimizia riziki yao watumishi wa Bwana. “Maana utumishi wa huduma hii,hauwatimizii watakatifu riziki warizopungukiwa tu, bali huzidi sana kuwa na faida kwa shukrani nyingi apewazo Mungu.”2kor 9:12.
· Kwa sababu tuna upendo wa Mungu ndani yetu.
· Kwa sababu tuna roho ya huruma. “Ila neno moja tu walitutakia ,tuwakumbuke maskini;nami neno lilo hilo nalikuwa na bidii kulifanya.”Galatia 2:10., “Amhurumiaye maskini humkopesha Bwana;Naye atamlipa kwa tendo lake njema.”Mithali 19:17
· Kwa sababu tunataka Bwana atubariki zaidi.
“Na mlawi kwa kuwa hana fungu wala urithi pamoja nawe ,na mgeni na yatima ,na mjane aliyefiwa na mumewe,walio ndani ya malango yako,na waje wale na kushiba ;ili kwamba Bwana ,Mungu wako, akubarikie katika kazi yote ya mkono wako uifanyayo”.Kum 14:29.
“Mpe kwa kweli,wala moyo wako usisikitike utakapompa;kwa kuwa atakubarikia Bwana ,Mungu wako ,kwa neno hili katika kazi yako yote ,na katika kila utakalotia mkono wako.”kum 15:10.
Tutoe je ,sasa?
Tutoe kwa furaha,si kulazimishwa,wala kwa manung’niko.
“Kila mtu na atende kama alivyo kusudia moyoni mwake,si kwa huzuni,wala si kwa lazima;maana Mungu humpenda yeye atoae kwa moyo wa ukunjufu.”2kor 9:7
Unaweza pia ukatoa kwa ahadi.Maana inawezekana ukawa na nia ya kutoa,lakini ukawa huna kitu muda huo.unaonyesha kutaka,ukisubiria kutenda.Paulo anatukumbusha hivi:
“Lakini sasa ,timizeni kule kutenda nako,ili kama vile mlivyo tayari kutaka,vivyo hivyo mkawe tayari na kutimiza,kwa kadri mlivyo navyo.” 2kor 8:11.
Kwa kadri mlivyo navyo inamaanisha ,ukiwa na vingi toa vingi,ukiwa na uwezo mdogo usijilinganishe na wengine ili na wewe uonekane kwamba unaweza,hapana.Toa kulingana na uwezo wako,na Bwana atakubariki.
Pamoja na kwamba kutoa ni kwa hiari ,unaweza ukatenda dhambi kwa kutokuwa na upendo juu ya mtu.,ukamunyima msaada wako wakati wa uhitaji wake.Mtu huo akimulilia Mungu juu yako inakuwa dhambi kwako.Dhambi inatoka wapi wakati ni mali yako,pia unatoa kwa hiari yako si kwa lazima? Jibu ,ni hii,kwa nini umunyime,wakati unaweza?Na yeye amekuomba?kinacho sababisha umunyime si kingine,bali ni uovu wako au una neno moyoni mwako juu yake,humpendi.
Neno la Bwana linasema
“Jitunzeni msiwe na neno lisilofaa moyoni mwako ,kusema,umekaribia mwaka wa saba ,mwaka wa maachilio;jicho lako likawa ovu juu ya nduguyo usimpe kitu;naye akamlilia Bwana juu yako,ikawa ni dhambi kwako.”Kum15:9.
Agano jipya linatuonya kwamba kila siku,nisiku ya kuachilia ,siku ya amani na kila mtu,siku ya kusameheana na kuachiliana,kwa sababu tuna subiri siku ya kurudi kwake Yesu.Naye asipo tukuta tayari tuta achwa.Kuwa na neno la uovu juu ya mtu ni dhambi.Bwana atusamehe!
Sehemu ya utoaji ni sehemu ya upendo.
Mama moja alishuhudia kwamba ,sehemu ya utoaji ni sehemu ya upendo.Alisema hivi;
Siku moja nilikuwa na shughuri ya changizo kwa kazi ya Mungu ,nilialika watu wengi sana,nakuwashirikisha jambo hilo.Waliniitikiya, wakasema tutakusaidia ,maana tunataka kazi ya Mungu isonge mbele.Nililenga sanasana wale wenye pesa! Kusema kweli nilikuwa nimejitahidi kueleza kwa upana na urefu jinsi gani nina hitaji msaada kwao.Siku ilipofika,watu waliniletea udhuru ,mara huyu anasema hataweza kufika, mwingine akasema anakwenda kwenye kikao,mwingine hivi, mwingine hivi,.Basi nikatuliza mawazo nikainua macho yangu kwa Bwana ,nikijua kwamba nitafanikiwa tu,lakini sioni njia.Basi,wale niliona kwamba hawana uwezo mkubwa ,ndio wale Bwana aliye watumia kwa kutenda muujiza na kunifanikisha.Badaye Mungu akaniambia kwamba
“Ni heri kumkimbilia Bwana kuliko kuwatumainia wanadamu.”
Zab 118:8.
Mama huyo anasema kwamba kwa njia ya utoaji aliona wale wote wanaemchukia(wana neno la ovu juu yake) hawakuweza kushiriki pamoja naye.
Utoaji unaambatana na roho ya upendo.
Mungu kwa upendo wake mkuu,alipenda ulimwengu mpaka akamtoa mwanae wa pekee.Yohana3:16.
Tutoe kwa nani?
Tutoe kwa maskini,(Kum 15:11). kwa wageni au wapitaji,.kwa wa jane na yatima.(Kum 14:29).
Tutoe kwa watumishi wa Mungu,(2Kor 9:12)
Kutoa kuna faida gani?
Utoaji unamtukuza Mungu.Bwana anapewa shukrani nyingi na wenye kupokea.(2Kor 9:12)
Utoaji unaleta baraka nyingi kwa mwenye kutoa.(2Kor 9:10).
Utoaji unasababisha wale waliopokea wakuombee baraka kwa Mungu.(2Kor 9:14).
Biblia inalinganisha kutoa na kupanda mbegu. “Na yeye ampaye mbegu mwenye kupanda ,na mkate uwe chakula,atawapa mbegu za kupanda na kuzidisha,naye atawaongezea mazao ya haki yenu.”2Kor 9:10.
Kupanda mbegu,unaangalia je,ni kipindi cha kupanda?Unaangalia pia ni mbegu gani nipande hapa?Vile vile,kutoa unaangalia umpe nani? Umpe nini?na umpe lini?Kiasi gani?
Nani ?jibu ,mwenye uhitaji.
Nini?kile anacho hitaji.
Lini?Wakati anayekuomba,usichelewe,usije ukakuta msaada wako hauna maana tena.
Kiasi gani?Jibu,chenye kumtoshereza hitaji lake au chenye kumfurahisha.Maana ukizingatia haya yote utasababisha ,shukrani kwa Bwana,pia atakuombea baraka bila kukoma.
Cha namna gani?Kizuri,chenye kufurahisha moyo.
Ibrahim,wakati Bwana alipo mtokea kwa njia ya malaika wale malaika walivyomtokeya,aliwa sii sana wakubali awaandaliye maji kidogo wakanawe,pia awape chakula kidogo wale.Moyo huu,ni moyo wa utayari wa ukarimu.Walipo kubali,aliwaandalia chakula kingi na kizuri ;unga (unga vipimo 3 vya unga safi),na ndama wa ng’ombe(aliye laini,mzuri) .Walipo shiba na kufurahi wakasema (hakika nitakurudia wakati huu huu mwakani) Wakambariki vile vile(tazama Sara mkeo atapata mwana wa kiume). (Mwanzo 18:1-11).
Vivyo hivyo Biblia inasema kwamba, “mtu mwema atapata upendeleo kwa Bwana,bali mwenye hila atahukumiwa naye.”Mith 12:2.
“Nafsi ya mtu mkarimu itawandishwa,anyweshaye atanyweshwa mwenyewe.”Mith 11:25.
Onyo !
- Ukitoa utoe kwa moyo kama kwa Bwana.
-Kutoa kwako kuwe kama kipawa,isiwe kama kitolewacho kwa unyimivu.(2Kor 9:5).
-Mtolee Bwana matoleo ya kumridhisha. (Mwanzo 8:20-21) “Nuhu akamjengea Bwana madhabahu,akamtolea sadaka ya kuteketezwa ya wanyama walio safi,na ndege walio safi,na Bwana akasikia harufu ya kumridhisha,Bwana akasema moyoni mwake kwamba hatailaani nchi…”.
Kutoa ni kupanda.Utavuna kile ulichopanda.Kuna mbegu nyingi tena zinatofautiana kwa mazao.Mbegu nyigine unapanda na kuvuna vingi sana.Kuna mbegu nyingine hazizai zaidi ya kimoja`,kama karoti inazaa moja tu.
Nataka niongelee kuhusu mbegu inayozaa kuliko zingine ni utoaji.
Ukitoa fedha yako utabarikiwa kwa kupokea fedha.Kama wewe ni mchoyo wa kutoa fedha utakuwa ni mtu wa kusema “sina hela” kila anayekujia na kukuomba msaada unajikuta kila siku nyimbo yako ni “sina hera” tena si uongo hutakuwa nazo kwa sababu wewe kwenye hera hujafunguliwa bado.Ukitoa chakula kwa wenye mahitaji,Nyumba yako haitakosa chakula,maana mbegu uliopanda ni lazima izae .Ukipanda vifaa vya ujenzi ni lazima upate vifaa vizuri,vingi vya kujenga nyumba yako.Utavuna ulicho panda.Mbegu inayozaa kuliko zote ni “ Fungu la kumi” .Apandaye haba atavuna haba apandaye kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu(2 kol 9:6) Mungu umpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu,tena inatupasa kutoa kutoka moyoni si kwa lazima wala kwa huzuni.Utoaji unatoka kwa moyo wa mtu.
Ushuhuda,
Siku moja tumepeleka fungu la kumi kanisani nilipo fika nyumbani nilikuta ile bahasha ya fungu la kumi nimesahau kuyitoa ,badala yake imerudishwa nyumbani.Nikayificha ili mme wangu asiyione asije akafikiri kwamba nimeiacha makusudi.Nilisema moyoni kwamba nitayipeleka jumapili ijayo,ndipo nikatulia.kabla ya jumapili nikaota ndoto ikanipa hofu.Nilionyeshwa mtu ananiuliza,eti,ile mbegu umeipanda?Akaniuliza tena,ile mbegu umeipanda?Nikauliza mbegu gani?Huyo mtu akasema ile inao zaa sana.Ndipo nikaonyeshwa mti mkubwa wenye matunda mengi sana kama vile mti wa mnazi wenye matawi mengi,na kila tawi limejaa minazi.Nilipo ona mti huo,nimeamka asubuhi na mapema nikapeleka ile mbegu inao zaa sana.Sija subilia jumapili maana niligundua kwamba ukichelewa kupanda ,utachelewa pia kuvuna.
Ndugu mpendwa pamoja na kutoa vitu vingi na kusaidia wengi kumbuka mbegu inao zaa sana,usicheleweshe mbegu zako,na Mungu akubariki.
Onyo:
Usitumie pesa ulietenga kwa ajili ya Bwana.Inawezekana ukawa umepata hera ukakumbuka kabisa kutoa kikumi.Lakini unajikuta umekawia kukipeleka kanisani ,bado kimehifaziwa vizuri nyumbani.Hera zako zikikuishia unashawishika kujipatia kikumi kilichotengwa kwa ajili ya Bwana na kukitumia.Hii ni hatali sana kwako wewe uliye mtolea Bwana na kukitumia.Kinacherewesha muujiza wako.
USHUHUDA
Siku moja tulikubaliana na mwenzangu kumtembelea kikumi Mungu. Tumekiweka sehemu baada ya siku tumekitumia tukisema tutakirudisha na faida kama ilivyo andikwa katika Biblia.Usiku huyo tulipokitumia ,nilionyeshwa kwanba mgonjwa wangu amesogezewa siku za kuugua.Ameongezewa zaidi ya miezi mitatu. Mungu amelinganisha na wagonjwa wawili mmoja aningia kumuona dokta mwingine analipa pesa ya daktari akimtuma huyo mgonjwa aliye ingia wa kwanza.Nilionyeshwa nasema hivi kwa sababu tumelipa tutaanza kutibiwa baada ya siku 3.Nikasikia sauti nyingine inanijibu,mnaweza kucherewa mkasubiri siku nyingi zaidi ya miezi 3 maana hamjampa daktari mwenyewe.Huyu mliyempa hawajui jina pia anaweza akasahau.Nilipo amka nilipeleka kanisani kikumi hicho na faida juu tukaomba Bwana aturehemu kwa sababu tumekitumia. Pia nilikuwa na mgonjwa nyumbani nimeona kwamba kitendo hicho kimecherewesha muujiza wa uponyaji wake.
Usitumie kikumi kabla hakijafika sehemu husika ,tendo hilo linacherewesha muujiza ,au maombi yako kujibiwa!!!
Onyo la mwisho
Timiza ahadi yako.
Sikummoja tulikubaliana kwenda kumuona rafiki yetu alikuwa amejifunguwa.Tumkubaliana kilammoja wetu alete shillings2000 tu ili tununuwe zawadi.
Dada mmoja alitoa shillings 1000 akisema kwamba hajapata nyingine.Nikamuomba atafute shillings nyingine 1000 ili atimize shillings 2000.Kasema kwamba hawezi kuongeza kwa sababu hana.Tukamubembeleza akubali tumuongezee ili atimie 2000 atayalipa baadaye,akakataa.Nikakasirika nikamuambia na iyo 1000 hatuichukui kwa sababu unaonyesha hupendi.Akakasirika zaidi,kwasababu tumekataa kupokea mchango wake.
Je nani alikuwa ndani ya kweli?Kuchukulia kwamba ni mchango yule mama hana kosa,maana anatoa kulingana na moyo wake.Lakini kama ni makubaliano ya kuchanga kila mtu shilingi 2000,ukitoa sh1000 bado unadaiwa sh.1000 nyingine ili utimize.Ni sawasawa na ahadi.Tuombe Mungu atusaidie kutimiza malengo tuliyojiwekea.Makubaliano ni tofauti na sadaka.Sadaka unatoa kulingana na vile ulivyokusudia moyoni mwako bila kusukumwa wala kulazimishwa.Makubaliano nayafananisha na ahadi unatakiwa kutimiza.Lakini kwa kuwa wote tumekasirika,baadaye tumeombana msamaha kwa kuwa kugombana si vema.Kila mtu alikuwa anaonyesha ni mwenye haki.
Sharti za kutoa
1. Kutoa kwa Bwana(usifikilie kwamba mtu huo ulie mpa atakurudishia wema wako.Hapana,ila Mungu tu atakulipa kwa wakati wake.)
2. Kutoa na moyo mkunjufu(kuliko kutoa na moyo wa kulazimishwa,nibora uache,maana Mungu ana njia nyingi za kufanikisha hitaji lote ya mwanadamu sanasana mtumishi wake.Kama hatamfanikisha kwa mkono wako,atamfanikisha kwa mkono wa jirani yoko.)
3. Kutoa ukielekeza kwa mlengwa.(
Kama matoleo analenga wagonjwa wa Ukimwi,wapatie wale.Kama matoleo yenu analenga wasiyejiweza ,wapatie hao hao ,usije ukawapa na jamaa zako kwa upendeleo.)
4. Kutoa ndani ya makubaliano au mapatano.(Mukikubaliana kila mtu alete vitenge10 kwa ajili ya wajane ,na kilo25 za unga kwa ajili ya yatima wa kanisani,fanyeni kama mulivyokubaliana,asiwepo mtu wakutofanya,lakini timizeni kila moja kama mulivyokubaliana.)
5. .Ukitoa chochote kidogo au kikubwa ondoa roho ya majivuno,au roho yakutaka uonekane, maana Bwana anapendezwa na roho ya unyenyekevu na upole.Kutoa unapaswa pia kuangalia ,je nikitoa hiki anauhitaji nacho au la.Uombe Mungu utoe kulingaa na uhitaji wake ,ili usionekane hujafanya,maana hakuna shukrani kwa mwenye kupokea maana si faida kwake.
USHUHUDA
Ilikuwa ni siku ya kuwatunza wenye uhitaji.Umoja wa Akina mama wa kanisa letu(kule Tanzania)waliandaa sherehe ambayo ilikuwa inalenga kuwasaidia wasiyejiweza,au kuwatuza wenye uhitaji.Kamati yetu tulikaa na kuona vema tuhimize kanisa lote,lilete kila mtu nguo,viatu,sukari mchele,maharage ,chumvi,sabuni,chayi,n.k. Hapa ilikuwa fursa kwa kila mtu kumtolea Bwana.Wengi wameleta kulingana na hiari ya kila mtu.Wengine wametoa vingi,wengine ,vichache,wengi hawajatoa kabisa.Kamati ndio ilikuwa inagawa vitu hivyo.Ilionekana roho nyingi sana chafu ndani yetu,Bwana akaamua atufichuwe ili tujue namna ya kuomba na kuzing’owa roho hizo kabisa.
· Roho ya kiburi( kwa sababu nimetoa vingi nampa ninayempendelea.)Anaonekana anasauti kwasababu vitu hivyo ndiye aliyevitoa.Kwa hiyo anapendelea nguo yake ivaliwena Fulani siyo Fulani. Kumbuka ukisha toa wewe umemaliza huna mamlaka tena juu ya vile ulivyotoa.Ukifanya hivyo,ni dhambi kubwa.Hapo inaonekana pia roho ya upendeleo.
· Roho ya wizi,(kuwapatia wengine labda ni watoto wako au rafiki zako lakini siyo walengwa wa matoleo hayo.Unamunyima mlengwa,hiyo ni wizi. Usipo tubu na kurudisha ,ole kwako!.)
Ukitoa utoe kwa Bwana.Mwanadamu hana shukrani.hata kama unaonyesha kushukuru roho yake ina maswali mengine.
Mf.-kwa nini amenipa hiki? Mbona nguo hii niliyopewa si nzuri?
-Mboa nilipewa kidogo? na yeye ana uwezo wa kufanya makubwa?
-Kwa nini hajanipa kama cha Fulani?
-Izi hela zote alizotumia kuwapa wengine ,huu si lingine ni jeuri tu ya pesa!
-Kwa sababu amekosa wa kununua,ndio maana amenipa mimi?(Mama moja amechukuwa nguo nyingi sana dukani kwake akamtolea Bwana)
-Manung’uniko mengi anaweza kutokea wakati ni zawadi.Kwa kweli ukitoa mpe Mungu,utavuna kwa wakati wako.Na ukisikia lawama zozote kulingana na utoaji wako,shukuru Mungu tu.Usiogope,wala usihuzunike wala usiseme sitafanya tena bali zidisha kufanya mpaka adui akome ,Mugu ni mwenye haki,atakukumbuka na wewe kwenye mahitaji yako.AMEN.
kupitia utoaji niliweza kugunduwa roho zingine zinazosababisha kanisa kutofanikiwa.
Roho ya ubinafsi,wengi wanapenda kupokea lakini hawapendi kutoa.(hii ni ugonjwa wa nafsi.) Roho nyingine nimeona roho ya uchoyo.Niambie kweli unaweza kukosa hata chumvi?
Nilishangaa katika nguo zilizoletwa kulikuwemo nguo zilizochakaa kabisa.Nikasema kama hizi,hatuwezi kumpa mtu bora zitumike kudeki chooni! Nilipata aibu walipo nisimulia hivi:Zile nguo zililetwa na fulani ,zilikuwa sale zao za kwaya myiaka ya zamani!Nilishangaa sana maana hatakumtaja siwezi.Ana nguo nyingi sana,nzuri naamini hana pa kuweka zingine.Hii ni roho ya uchoyo.Bwana atusaidie sana
Sura ya 4
Ushuhuda,Kuhusu kanisa.
Siku moja,nilionyeshwa kwamba ndani ya kanisa tuko kwenye makundi ma 3.kundi lakwanza nila wachungaji na wazee wa kanisa.kundi la pili la wainjilisti na mashemasi na latatu la washirika wote.
——————————————————————————————–
1 2
Sauti yaMungu Nuru au Mwanga
Wachungaji na wazee
Wainjilisti.
——————————————————————————————–
3Washirika wote.
Wengine wako nje ya kanisa,wanasikiliza mahubiri ya mtu mwingine,alikuwa anaongea kama mtu wa Mungu na kuonyesha anataka kuamsha watu wamsikilize.Kwa sababu sauti itokayo kwa watumishi hawaisikii maana wako nje ya kanisa.
Sasa,
Wewe ukiwa katika kundi la kwanza ni sawa na kundi la pili au la tatu,yote ni mema tu kwa sababu Mungu ametuweka hapo kwa kusudi lake mwenyewe.
Cha msingi wote mko ndani ya kanisa.
Hapa tunaona kwamba taa au mwanga uko juu ya kundi la pili.
Je hao wa kundi la tatu au wa kundi la kwanza watawezaje kusoma neno la Mungu,wakati mwanga hauwafikii?
Hao wanatakiwa kuusogelea na kukaa chini ya ule mwanga ili waone maandiko na kuyaelewa.
Tunaona pia kwamba mhubiri anasimama mbele ya kundi la kwanza.
Je huyo aliye nyuma kabisa atasikia sauti?Atasikia ujumbe?wala walio huko nje watasikia mahubiri?
Wote wanatakiwa kuja kanisani na kusogea ili wasikie vizuri.
Mtumishi wa Mungu mahali popote ulipo mimi ni mtumishi wa Mungu mwenzako,nina kushauri,usiridhike na kuingia kanisani ridhika kwa kuwa una kaa chini ya nuru ya mbinguni(ukifunuliwa maandiko matakatifu)pia unasikia sauti ya Bwana (ikikuhubiria juu ya maisha yako na mwenendo wako wa kiroho)maana wengi wapo kanisani,na sauti ya Bwana iko mbali sana nao ,na hawawezi tena kusoma biblia maana hakuna mafunuo ya neno.
Ndani Ya biblia hawapati faida tena,ukiangalia huoni kosa ulilolifanya au dhambi ulioifanya lakini unajikuta huna hamu tena ya neno,kuomba ni kama desturi,kazi zote unafanya hazina utamu hii hali naifananisha na mtu anayeogelea baharini.
Mawimbi anampeleka polepole na baadaye anajikuta mbali sana na pale alipoanzia kuogelea ili arudi kule alipoanzia,anaamua tu kurudi huko.
Watumishi wa Mungu wanaweza kuchafua nguo zao bila kujua .Baada ya kazi nyingi wakajikuta nguo zimechafuka,kama ni hivyo zinatakiwa kufuliwa na sabuni.Yesaya ameshitakiwa na ibilisi kuwa nguo zake ni chafu,ndipo malaika akamvua akazifua akampatia zingine.
Kuna mwingine alionekana ana nguo nyeupe imechafuka kifuani,huyo alitakiwa kuifua hapo ilipochafuka.Nguo kawaida zinamaanisha kazi za Mungu tunazozifanya.(unaweza ukawa kiongozi katika kikundi cha kwaya mkagombana na wenzako hapo chuki,hasira,manung’uniko vinachafua nguo yako .
Nguo nyeupe inamaanisha wokovu,kama imechafuka kifuani ni swala la imani.umeingiza imani si ya kweli ndio maana nguo yako nyeupe imechafuka.Watumishi wenzangu chunguzeni nguo zenu kama ni safi,kama si safi mrudie Bwana awaoshe na kuwasafisha kabisa,maana yeye ndiye ajuaye mambo yetu yote.Kama wewe ni mumishi wa Mungu hakikisha uko chini ya uongozi wa roho mtakatifu au kwenye Nuru ili ujue maandiko.
Hakikisha unasikia sauti ya Mungu ikikujulisha kuhusu maisha yako ya kiroho au kukupa ushauri juu ya kanisa.
Je,wewe uko nje kabisa,nakushauri uingie maana sauti halisi ya Mungu iko kanisani.Wasikilize watumishi wa Mungu ,kwao utapata sauti ya Bwana.Usipo ingia wako wengine watakuhubilia mengine na utapotea.Ingia kanisani,uwasikilize watumishi,na uwaheshimu.
Soma neno na Nuru ya Bwana ikuangazie ujue mandiko.Na Mungu akubariki.
Tuko njiani tunakalibia kumaliza safari.
Ushuhuda.
Namshukuru Mungu ,usiku wa kuamkia tarehe 11/10/2008 Bwana amenionyesha yafuatayo:
1) wachungaji wawili,mmoja yuko mwanzo wa safari na mwngine yuko mwisho wa safari.
2) Safari yenyewe ni kuvuka kutoka feri ya kigamboni(Afrika,Tanzania,Dar es salaam) kuelekea ngambo nyingine.(kawaida tulikuwa tunavuka na pantoni lakini kwenye ndoto pantoni ilikuwa haipo)
3) Kulikuwa na mti mdogo tulikuwa tunawutumia kwa kuvuka bahari hiyo
Kazi ya kuvuka ilinipa shida sana,huu mti nilipoutumia ulienda kabla sijashuka,mti ukarudi kwenye maji,na kulikuwa na watu wengine pale ng’ambo nikawaomba wanivute,wakakataa wakaniambia tu kwamba kawaida mti huu unarudi kwenye maji kweli ukanirudisha baharini Ndipo mme wangu yeye alikuwa ameshavuka yupo pamoja na yule mchungaji wa ng’ambo akahuzunika sana akataka kuja kuniokoa lakini mimi sikuona shaka wala woga nilishika kwamba nitashikilia mti sana pia ninaamini nitafika
Hapo sasa ndipo nikajikuta nipo ndani ya daraja kubwa sana,imejengwa na simenti na kokoto,nikajikuta tuko watatu(mimi na mtoto wangu Billy na mme wangu),baada ya hapo nikajikuta tuko wawili(mimi na mtoto wangu)ndipo nikaona safari yangu ni salama sasa,ni kama kutembea barabarani.Nikafikiria kwamba dakika chache tu,nitafika.
Nikaanza kuangalia kama sina kasoro mwilini mwangu,maana nimekumbuka kuna mchungaji nitamkuta ananingojea.
Nilipojifikiria na kujiangalia nikakuta shati yangu imegeuzwa na vifungo vimefunguka vyote,nikaona aibu nikataka kuivua na kuivaa vizuri nikaona pia ina uchafu.ndipo nikatoka kwenye ndoto hizo.
Mtumishi mwenzangu kazi tunayo kweli ni lazima tuvuke, pantoni haipo,mti nao unasumbua,unahatarisha maisha yetu,lakini tunaye msaidizi naye yuko pamoja nasi nakututia nguvu(Roho mtakatifu) huyo,pia huko tukifika kuna Mungu anatusubiri ni lazima tujiangalie tutaonekanaje mbele zake.
Baada ya taabu nyingi za kutafuta kuvuka,angalia,nilikuwa sijawahi kujifikiria mwenyewe na kuangalia mavazi yangu yako vipi.
Shida,nyingine kama vazi langu limegeuzwa naweza mwenyewe kulivaa vizuri na kufunga vifungu mwenyewe,lakini mtatoa wapi maji ya kuifua?niko darajani nakaribia kufika?Bwana aturehemu na atuhurumiye.Uweza wake na nguvu zake zionekane.Kuna vitu vipo nje ya uwezo wetu.Kama huwezi kurudisha siku wala saa eti zisimame.Je hapo hapo nani anipe mavazi mazuri ya kunifanya nionekane vizuri mbele za Mungu?
Hapo hapo msaada utoke kwa nani?Jibu ni hakuna.Msaada ni kwa Mungu peke yake.Yeye mambo yote anaweza akayageuza kwa sekunde moja tu.Kinachotakiwa ,mpendwa,pamoja na kung’ang’ania kufika,tusisahau kumuomba Bwana,akuonyeshe jinsi gani utakavyoonekana mbele zake.vitakusaidia kwa kuomba,utajua umuombe Mungu nini.Bwana akiwasha taa yake,ni lazima utaona.Ukishaona,utatenda kwa utimilifu wa moyo.Haleluia!!!
Watu wengi sana,wamesahau kwamba tukimaliza safari yetu ya hapa duniani,tunangojewa huko,usipojifikiria utajikuta hauko salama mbele zake
(2Yoh 1:8).“jiangalieni nafsi zenu msiyapoteze mliyoyatenda,bali mpokee thawabu timilifu”
Neno la Bwana linatuonyesha pia kwamba,usipojiangalia,unaweza kuaibika mbele zake katika kuja kwake.
(1Yoh2:28) “na sasa watoto wadogo,kaeni ndani yake ili kusudi,atakapofunuliwa,muwe na ujasiri,wala msiaibike mbele zake katika kuja kwake”.
(1thess3:13) ”Apate kuifanya imara mioyo yenu iwe bila lawama katika utakatifu,mbele za Mungu Baba yetu,wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu pamoja na watakatifu wote.”
Bwana atusaidie sana,muda tulionao ni mfupi,lakini Bwana anaweza kutuweka sawa.Tumefanya huduma nyingi sana,kwa mateso makali,vitisho vya kifo,matusi,wengine wamewekwa magerezani kwa ajili ya injili,njaa,taabu nyingi,lakini tumevumilia.Kinachobaki ni kujiangalia sisi ili tuwe na ujasiri,tusiaibike mbele zake.Mungu atubariki sote,AMEN.
Hebu tujifunze kwa huyo mtoto wangu aliyekuwa pamoja nami akabaki nami,na ndiye aliyesababisha nifikirie kujiangalia,huyo si mwingine bali ni Roho mtakatifu na kazi yake ni kutusaidia,(yeye ni msaidizi)na kutukumbusha yanayotakiwa kufanyika.
Kuna mtu mwingine (mme wangu)alikuwa anakuja nikiwa na shida,akimaliza namuona anarudi pamoja na yule mchungaji wa ng’ambo.Yeye,alikuwa anakuja,ananisaidia halafu naona nabaki peke yangu huyo si mwingine ni Malaika wa Bwana.Kama tumefanya kwa nguvu zetu tukashindwa,anawatuma Malaika zake kuja kwetu na kutufanyia kazi maalum,kisha anarudi kwa Yesu,tukipatwa na shida tena anajitokeza na kutusaidia.
Mpendwa,usihofu kama vile uko peke yako,hapana!
Yupo roho mtakatifu anabaki na wewe kila sehemu,
pia yupo malaika wa Bwana anakuangalia na kukusaidia.
Kabla sijaanza kuvuka ile bahari,kuna mchungaji alikuwa ananikatisha tamaa,ili nisisubutu kuvuka eti nitakufa kwenye maji.Niliwaambia kwamba niko pamoja na mme wangu,hawezi kuniacha nizame na maji.
Huyo mchungaji,anafananishwa na viongozi wengi wanamtumikia Mungu,lakini hawana imani kwa Mungu,ni kama vile wafarisayo wanavyo fanya.
Paulo mwenyewe,aliwaona katika kazi ya Mungu,walimzuia asiseme na mataifa ili wapate kuokolewa,Biblia inasema hao ni wafuasi wa makanisa ya Mungu. watu kama hao,wakiitwa watumishi wanakuwa vizuizi katika maendeleo ya kiroho.
(1Thes 2:16) “huku wakituzuia tusiseme na mataifa wapate kuokolewa;ili watimize dhambi zao siku zote.lakini hasira imewafikia hata mwisho”.
Ukifanya hatua wanakufanyia kikao,wanaunda sheria kama ile waliomfanyia Danieli ili asiendelee kuomba Mungu wake.(Dan….)lakini kama wewe ni mteule wa Mungu,hujali,unasonga mbele.Hatuogopi vitisho,wala kufa,maana kufa itakuwa faida kwetu tukifia katika Kristo kama alivyosema mtume Paulo.Pia hatusahau kwamba,mateso ni chakula chetu au fungu letu.Kama walivyomchukia Mungu wetu na sisi ni hivyo hivyo.
“mtu asifadhaishwe na dhiki hizi maana ninyi wenyewe mnajua ya kuwa tumewekewa hizo”(1Thes3:3).
Yobu naye alisema kwamba,kama mwajiliwa anasubiria mwisho wa mwezi apate mshahara wake,naye ndipo anasubiri mateso yake kama mshahara.Anasema amewekewa miezi ya taabu kama mshahara.
Bwana Yesu naye alisema kwamba,yale yote yalioamriwa katika kitabu kile cha torati ya Musa,na manabii na zaburi,ni lazima ayapitiye,
(Luk24:44)“Kisha akawaamba,hayo ndiyo maneno yangu nilio waambia ya kwamba ni lazima yatimizwe yote nilioandikiwa katika torati ya Musa na manabii na zaburi.”
Sisi hatuogopi mateso kwa ajili ya Bwana wetu,maana ni sehemu ya furaha yetu.
Paulo naye anasema
“sasa nafurahia mateso nilio nayo kwa ajili yenu;tena nayatimiliza katika mwili wangu yale yaliopungua ya mateso ya Kristo,kwa ajili ya mwili wake yaani,kanisa lake.(Kol1:.4)”
Petro naye anaandika hivi
“Basi kwa kuwa Kristo aliteswa katika mwili wake,nanyi jivikeni silaha ya nia ile ile.Kwa maana yeye aliteswa kwa mwili wake ameachana na dhambi.(1Petro4:1)”
Mpendwa,safari yetu ina vikwazo vingi,ina hatari za kifo pia,yupo Roho mtakatifu hatuachi peke yetu,anatufariji,nasi tunasonga mbele.Wengi sana wakati wa mateso makali,wanakumbuka kuomba,maombi pia ni silaha ya kupigana na adui.Lakini kuomba kwetu lazima tuelekeze maombi yetu kwa Bwana Yesu,yeye ndiye mwenye uweza wa yote.Nguvu na mamlaka zina yeye.Haleluia!!!
Ndani ya maji niliwaita watu nilikuwa na waona lakini hawakunisaidia,wamesema kwamba
“kawaida huo mti unawarudisha nyuma ndani ya maji”
maana yake nini?kwa maana nimewaita watu(waliokufa) wanisaidie,imani yangu imeanguka,imerudi nyuma,wafu hawasaidii kitu,wale nao wanasubiri hukumu.usiombe msaada kwa watakatifu,au waganga,au wachawi,huko ni kuanguka kabisa
(Mdo4:12)” Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote ,kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.”
lakini Bwana wa majeshi alinitumia malaika kunisaidia na kunipeleka kwenye daraja,ndipo nikaona yule mtoto(Roho mtakatifu)na mme wangu(Malaika)wako pamoja nami.
Mpendwa,ugumu unaouona kwa kazi ya Bwana,karibu utaisha,maana siku zilizo baki ni chache sana.
Safari yetu inakaribia mwisho.Sasa basi leo hii unaweza ukaona hakuna shida,unaanza kusimulia jinsi maji yalivyo kuwa yanatisha,unakumbuka jinsi yule mchungaji alikuwa anakuzuia kuvuka na kukukatisha tamaa,na mambo mengine,unaona ni siku za raha na utulivu,siku za kicheko na mafanikio.
Umwambie Bwana ahsante kwa kukulinda na kukupigania,maana wengi sana wamepoteza uhai wao.
“Kinywa changu kitazinena sifa za Bwana;wote wenye mwili na walihimidi jina lake takatifu milele na milele.Zaburi145:1”
ukiishiwa nguvu,bado Bwana yupo.
“Bwana huwategemeza wote waangukao,huwainua wote walioinama chini Zaburi 145:14”
“Na ahimidiwe Bwana,mwamba wangu,anifundishae mikono yangu vita,vidole vyangu kupigana.zaburi144:1.”
Inawezekana vita vyako vilikuwa vikali mno,pasipo Bwana kukufundisha kupigana,hungeweza,lakini leo hii unafurahia,ukikumbuka jinsi Bwana alivyoonekana na kukushindia,
akakutoa katika maji mengi,katika mkono wa wageni,vinywa vyao vyasema visivyofaa,na mkono wao wa kuume ni mkono wa uongo.
Kama ilivyoandikwa katika kitabu cha Zaburi144:7-8.
Vita vikiisha,mpendwa kinachobaki ni kujiangalia ,kama unajeraha au kama mavazi yako yamechanika au hayaja chafuka.kipindi hiki ni kizuri sana.Tena ni cha muhimu.Hapa ndipo Mungu anaturuhusu kufanya“ubinafsi”macho yote mawili yanaelekea kwako,si kwa huduma,si kwa wengine bali kwako wewe,kwa nini sasa?Kwa sababu kila mtu atapelekwa mbele za Mwenyezi kutoa hesabu ya matendo yake.
“nao watatoa hesabu kwake yeye aliye tayari kuwahukumu walio hai na walio kufa:1Petro4:5”
Hapa,tumepata daraja imara,hatuna hofu tena ya kuvuka.Lakini hapa mawazo yetu yame hamishwa tunawaza jinsi tutakavyo onekana mbele zake.Tunapaswa kujitakasa nakufua nguo zetu ziwe safi na mili yetu pia.Neno la Mungu linatukumbusha,
“Mungu wa amani awatakase kabisa;nanyi nafsi zenu na roho zenu na miili yenu mhifadhiwe mwe kamili,bila lawama,wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo.Yeye ni mwaminifu awaita naye atafanya.1Thes5:23-24”
Kipindi hiki tunakimbizana na wakati.hizi ni siku za mwisho.Tuwe macho kabisa tusipoteze thawabu yetu.Tuombe sana Mungu atutakase ili tuhifadhiwe tukiwa kamili,bila lawama wakati wa kuja kwake Yesu.Paulo anakumbusha juu ya nyakati akisema,
“lakini ndugu,kwa habari ya nyakati na majira,hamna haja niwaandikie,maana ninyi wenyewe mnajua ya kuwa siku ya Bwana yaja kama mwivi ajavyo usiku(1Thes5:1-2.)
Tunasubiri kila mtu kuingia hukumuni,ndio maana inatupasa kujiweka sawa kila siku tukimngojea Bwana.
“yeye anahukumu kila mtu pasipo na upendeleo kwa kadiri ya kazi yake;enendeni kwa hofu katika wakati wenu wa kukaa humu kama wageni.(1petro1:17)”
Bwana atatuhukumu bila upendeleo,tuombe Mungu atufunulie yote yaliojificha ili tutubu maovu yote.Tusiwe watu wa kujiamini na kujihesabia haki.Tuombe Mungu aturehemu na kutuweka tayari tukiwa wakamilifu.Tuombe Roho wa Mungu atuamshe,tuwe macho tukikesha kwa maombi.
“Lakini mwisho wa mambo yote umekaribia;basi iweni na akili mkeshe katika sala.Zaidi ya yote iweni na juhudi nyingi katika kupendana,kwa sababu upendano unasitiri wingi wa dhambi.(1Petro4:7-8)”
MWISHO
Napenda sana kukumbusha,wewe mtumishi wa Mungu kwamba,mateso unayopitia,ni ya kitambo tu.Inawezekana Bwana yuko kazini kwa kukukamilisha;kwa kukupa uvumilivu na unyenyekevu.Vyovyote vile taabu ile unayopitia haitakuua.Bwana Yesu naye alitukanwa,alihuzunishwa lakini alivumilia yote.Watumishi wa zamani walitupwa kwenye moto,wengine wali uwawa.Nasisi leo hii tumeonewa,tunaumizwa kwa njia mbalimbali.Lakini zaidi ya yote,tuzidi kuwa washindi.Tushike sana kristo tusimuache.katika bahari,ule mti usiuache maana kwa huo tumeshikilia uhai wetu(nao si kingine ni imani na tumaini letu ni katika kristo)Ndugu usiache imani yako katika Kristo.Naye Bwana ataagiza Malaika atatutoa hapo na kutupeleka kwenye daraja,njia ya kweli na ya uhakika.
Njia hio si nyingine ni Kristo.Yeye ni njia ,na kweli na uzima.Hapa duniani tupo pamoja naye,tena tunasubiria timilifu ya ushindi wetu tukifika Mbinguni.Tukimaliza safari ya bahari(dunia) hii.Dunia hii ni bahari imemeza wengi sana,na sisi tumeponea chupuchupu maana tulikuwa miongoni mwao,lakini Bwana ametuhurumia na kutuonyesha njia sahihi.
Na sasa tunakaribia mwisho wa safari yetu.Tutafutwa machozi na taabu zote tulizozipata hapa duniani,tutafurahia kuwa pamoja na Bwana wetu,tunangojea kuvikwa taji ya utukufu ile isiyokauka.
Na mtume Petro alisema kwamba alikuwa shahidi wa mateso ya Kristo na mshirika wa utukufu utakaofunuliwa baadaye(1Petro5:1).
Watumishi wa Bwana,angaliani sasa kazi mliopewa na Bwana (kuchunga kundi la Bwana lililo kwenu)si kwa kulazimishwa bali ni kwa hiari kama Mungu atakavyo,si kwa kupenda fedha ya aibu bali kwa moyo.Wala msijifanye kama mabwana juu ya mitaa yao,bali kwa kujifanya kuwa kielelezo kwa lile kundi(1Petro5:2-4.)
Nanyi washirika,si vema nimalize bila kuwa kumbusha kwamba,ni vema kuwakumbuka wale wanaojitaabisha kwa ajili yenu na kuwasimamia ninyi katika Bwana na kuwaonya;mkawastahi sana katika upendo kwa ajili ya kazi zao.(1Thess5:12-13)
Kila mtu asimame kwa zamu yake.Ili Bwana atakaporudi,tusiaibike mbele zake.Tujue wale wote tuliohubiria wakaokoka hao ndio fahari yetu na utukufu wetu mbele za Bwana
(1Thess2:19)“maana tumaini letu,au furaha yetu,au taji ya kujionea fahari ni nini?Je! si ninyi ,mbele za Bwana wetu Yesu,wakati wa kuja kwake?Maana ninyi ndio utukufu wetu na furaha yetu.”
Nawakumbusha tena kwa ile habari ya lile kundi lililo ng’ambo ya bahari.wale ni wote waliomaliza safari yao ya hapa duniani.
“Lakini,ndugu hatutaki msijue habari zao waliolala mauti,msije mkahuzunika kama waliokosa matumaini.Maana ikiwa tunaamini kwamba Bwana alikufa na kufufuka,vivyo hivyo waliolala katika Kristo,Mungu atawaleta pamoja naye”(1Thes4:13-14)
wengi wanaamini kwamba waliokufa wamemaliza ,bado kabisa kwa sababu neno la Mungu linatuonyesha kwamba,wale waliolala katika Kristo ndio watakaookolewa na hukumu ya mwisho.
Ndugu unayesoma maono haya,usikimbilie kujiua eti ndipo utakapopumzika,hapana,kimbilia kwa Yesu utapona ugonjwa wako,huzuni zako zitaisha,hata ukifa,kuna matumaini ya baadaye utafufuka pamoja na Kristo.
“Kwa kuwa Mungu hakutuweka kwa hasira yake,bali upate wokovu,kwa Bwana wetu Yesu Kristo,ambaye alikufa kwa ajili yetu,ili tuishi pamoja naye kwamba twakesha au twalala.(1Thes5:9)
Ndugu msomaji wa kitabu hiki ninapenda kuchukua nafasi hii kukukumbusha kwamba safari yetu ya kuelekea Yerusalemu mpya inakaribia mwisho wake,hapa tunakumbushana kama ilivyo desturi ya wachaMungu.Nchi yetu ni mbinguni,tunatarajia kufunga harusi na mwana kondoo.(yaani Yesu kama bwana harusi na sisi kanisa la Mungu kama bibi harusi).
Tunavisoma katika kitabu cha ufunuo wa Yohana kwamba
“natufurahi,tukashangilie,tukampe utukufu wake,kwa kuwa arusi ya mwanakondoo imekuja na mkewe amejiweka tayari.”ufunuo 19:7.
Yohana alifunuliwa kwamba
“tutavikwa kitani nzuri,ing’arayo safi kwa maana kitani nzuri ni matendo ya haki ya watakatifu.ufunuo wa Yoh 19:8”
“Heri walioalikwa karamu ya harusi ya mwanakondoo.Maneno haya ni maneno ya kweli ya Mungu”ufunuo19:9.
Mwalikowa kuingia Yelusalemu mpya.
Ushuhuda.
Mpendwa nakusihi urudie mstari huo.unasemaMimi Francoise Habonayo,mwaka wa 1992 nilionyeshwa maono haya:
“Dada mmoja anajulikana kama mtoto wa baba yangu mdogo,nilionyeshwa kwenye ndoto hiyo ananiletea kadi nyingi za mwaliko wa harusi akaniagize niwapatie na wapendwa wengine,nikataka nimuulize unafunga harusi na nani?ni wapi?ni lini?lakini sikumuuliza hata swali moja.Maana nilisema moyoni kwamba majibu nitayapata nikisoma zile kadi alizonipa, naye akaniaga akaondoka.Nami nikaanza kuzipekuwa nikasoma ya kwanza,niliposoma,sikubahatika kujua ni lini maana lugha sikuweza kuisoma.(Na Biblia inasema si vyetu kujua siku wala saa Yesu ajapo)nilichobahatika kujua kusoma
Ni
“mahali pa sherehe :Yerusalemu” .
pia chini ya maneno hayo, kulikuwa na mstari wa Biblia
“Isaya61:10”
Ndipo nikapekua kadi ya pili,nikasoma
“Lieu de reception :Jerusalem. »
na mstali ; « Esai 61 :10 »
Kadi ya tatu nikasoma
« Urubanza ruzobera i Yerusalemu”
Yesaya 61:10.
nilipoendelea nikagundua kwamba ile kadi ni kwa mataifa mbalimbali na lugha mbalimbali(kama Yohana alivyoonyeshwa).
Ndugu mpendwa nimeagizwa nipeleke kadi hizo.Na wewe umebahatika kuipata ukiwa ni mteule wa Mungu.Kama umeoshwa dhambi zako kwa damu ya Yesu pokea kadi hiyo uitunze vizuri.Saa na siku ni siri ya Mungu mwenyewe.Ila mengine ameshatufunulia kupitia Yohana na mengine kupitia ufunuo huo.
Ndugu mpendwa soma vizuri fungu la Isaya61:10
“nitafurahi sana katika Bwana,nafsi yangu itashangilia katika Mungu wangu,maana amenivika mavazi ya wokovu,amenifunika vazi la haki,kama bwana arusi ajipambavyo kwa kilemba cha maua,na kama bibi arusi ajipambavyo kwa vyombo vya dhahabu”
siri kubwa ni hii“tutafurahi sana katika Bwana nafsi zetu zitashangilia katika Mungu wetu.”siku hiyo ni siku njema ya furaha kubwa mhubiri naye aliandika
“kwa ajili ya karamu kufanywa kwa ajili ya kicheko.” mhubiri 10:19
Bibi arusi anatakiwa kujiweka tayari kila dakika na kila sekunde,nakulinda sana vazi lako la wokovu lisiharibike wala lisichafuke,tuna vazi la haki pia.Bwana wetu ni mwema sana,anatufunulia ili tujue kwamba siku ya Bwana inakaribia.Ndugu mpenzi,kagua vizuri vazi lako.
Je umeoshwa kwa damu?ili upate vazi la wokovu?Je matendo yako ni mema mbele za Bwana?umemfanyia Bwana kazi?unahubiri?Unashuhudia,unawavuta wengine waje kwa Bwana?unaombea wengine ?unatoa mali zako kwa wajane na yatima na wenye mahitaji?Je unatoa sadaka na vikumi?Je kuna kazi Bwana amekupa hujaimaliza?ndugu nakuhimiza ufanye haraka,usije ukaonekana na aibu mbele zake.
Kadi za kualika zimeshasambazwa,je wewe umeshaipata?ingia kanisani,baba,mama,dada yangu na kaka yangu usichelewe.Tafuta msaada kwa watumishi wa Munngu watakueleza cha kufanya,basi kama uko mbali na kanisa fungua moyo wako nikusaidie,kama kweli unataka kupata mwaliko huo,fungua moyo wako urudie maneno haya.
“Bwana Yesu,nakuja kwako,na moyo mkunjufu naamini wewe ni mwana wa Mungu,wewe ni mtakatifu sana nakuomba unisamehe makosa yangu yote na dhambi zangu zote nilizofanya kwa kujua na zile nilizofanya kwa kutokujua.Futa jina langu kwenye kitabu cha hukumu,uliandike kwenye kile kitabu cha uzima.Leo hii nimeamua kukufuata wewe unishike mkono niwe wako siku zote.Ahsante Bwana Yesu kwa kunipokea,AMEN”
Ahsante ndugu mpendwa kwa kumpokea Bwana Yesu,awe kiongozi wa Maisha yako.Umefanya uamuzi wa busara,Mungu wangu akubariki sana .jiunge sasa na wengine ukashuhudie matendo makuu ya Mungu.Bwana yuko pamoja nawe popote,usiogope amekubariki na kukuosha,wewe ni kiumbe kipya.Upende kusoma Biblia(neno la Mungu)utaendelea kukua kiroho na kimwili.AMEN
“Naye akaniambia , Andika, Heri walioalikwa karamu ya arusi ya mwana-kondoo.Akaniambia maneno haya ni ya kweli ya Mungu.”Ufunuo 19:9.
“ Tazama naja kama mwivi,heri akeshaye na kuyatunza mavazi yake.” ufunuo16:15.
——————————————————————————————–